Ester Bulaya akamatwa na Polisi jijini Mwanza

Ester Bulaya akamatwa na Polisi jijini Mwanza

Spika alipiga mtu kule jimboni kwake mpaka akazimia mbona hakukamatwa? Hizo amri za hovyo hovyo wazidhani zitawasaidia bali zinaongeza chuki kwa serikali.

Nakushukuru kama nawe umeuona udhaifu huu wa serikali na viongozi wao wanaojifanya ni wadogo zake mungu(miungu watu) Kwa kweli nami ninapoziangalia clip za aliyoyafanya Ndugai jimboni mwake na kwa mwanasiasa mwenzake na msomi mzuri tu na asichukuliwe hatua yoyote nakata tamaa na uongozi wa kiafrika.Bwana aliechapwa fimbo za kichwa na huyu Ndugai alizimia na kulazwa kwa kipindi hospitalini.Ratiba ya kikao ilivurugika na bado uchaguzi ukafanyika muathirika akiwa bado wodini na bado wananchi wakamchagua mtembeza bakora kama mbunge wao. Sasa taarifa nilizozipata ni kuwa Bulaya yupo safarini kurudi Mwz kuungana tena na wenzie kwenye vikao vya halimashauri kuu vinavyoendelea. Ndiyo maana nikasema kama ni dhamana hata ofisi ya polisi Mwz ingeweza kuelekezwa na makao makuu kuchukua maelezo yake na kumpa dhamana kama walivyofanya Dsm. Sasa watupe sisi walipa kodi gharama za kukodi hiyo ndege na kuwarudisha Mwz askari waliomsindikiza Bulaya.Vinginevyo tuambiwe hiyo dhamana hutolewa na nani mwenye cheo kipi ambacho hakipo Mwz au ni utaalamu upi wa kuchukua maelezo na kuyatuma Dsm ki-elektroniki ambao haupo Mwz. Raisi nakuonea huruma kama juhudi zako za kusaka mapato na kuziba mianya matumizi yake yatakuwa hivi.
 
Nimemsikia mtumishi mmoja wa serikali akilalamika kuwa alikuwa na swala muhimu la kikazi mikoani lakini kutokana na sera ya kupunguza matumizi hata gharama za kufika huko kwa basi ilishindikana.
Najiuliza fungu la kulipia ndege ya dharula kumfikisha 'mtuhumiwa' Dar es Salaam liliidhinishwa na nani!
Kweli ukitaka kujua uhalisia na ujinga wa Mwafrika ni pale anapopate uongozi, ndipo hapo utaelewa kuwa 99.5% yetu ni nusu binadamu!
 
Wangepungukiwa weledi, hapo ndiyo wametumia weledi
Hizi ni mbinu za kizamani sana,kuna watu ndani ya serikali bado wanatumia mbinu za Karne ya Kanu kuwanyamazisha upinzani.
Haya yote yanatokana na poor thinking capacity ya hao watu,there are many ways to deal with a mp ,sio mpaka mkamkamate,na mabunduki yenu na maland rover ..
Hivi police wangle m sermon bulaya aende central mwanza au Banda au Dar wangepungukiwa nini? Kwa I bulaya Ana murder case mpaka akamatwe usiku?
Nchi za wenzetu police wanapo deal na wabunge hasa wa upinzani,huwa Wana waita kituoni au CID for grilling ,Ili isije onekana anaonewa.
Wito Wangu kwa Jes la police,tumieni njia na mbinu za kisasa..mnawapa hao wabunge sifa na popularity zaid Mnavyo zidi kuwafrastrate .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 329145

Mbunge wa jimbo la Bunda,Ester Bulaya amekamatwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza na kulazimika kulala rumande baada ya kunyimwa dhamana.

Polisi walivamia Hoteli aliyofikia mbunge huyo na kumkamata majira ya saa 7 usiku na kisha kumpeleka kituo cha kati cha Jijini Mwanza akiwa ameambatana na Mhe. Halima Mdee (Mb) , Joyce Sokombe (Mb) pamoja na Wakili John Malya.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Justus Kamugisha amesema hati ya kukamatwa kwake imetoka ofisi ya Bunge na kwamba Mbunge huyo anashikiliwa kama mtuhumiwa ambaye anatakiwa kusafirishwa kwenda Dar es Salaam.

Wabunge hawa pamoja na uongozi wa juu wa CHADEMA Wako jijini Mwanza kwa ajili ya kikao cha Baraza Kuu la chama hicho kinachofanyika leo katika Hotel ya Gold Crest.
Mungu akuvike moyo wa amani na roho ya ujasi** Easter
 
Kwa hiyo kwa akili yako unadhani kuwa kilichompa ushindi Sugu ni ile mihemko ya bungeni? Subiri 2020 jinsi wabunge wako watakavyosombwa na maji
Uko sahihi kwa hili. Nilidhani umelaza jumla ubongo kumbe una ufahamu kidogo.
Si uchaguzi wa 2020 tu ambako ushindi kwa chama chetu mahiri cha m/kiti mchapakazi unatarajiwa kupatikana kwa msaada wa tume na usimamizi mzuri na wa haki wa vyombo vya ulinzi na usalama, bali hata chaguzi zote zilizopita pia ulipatikana kwa staili hiyohiyo: matukio na matokeo ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni ni mfano mzuri na unathibitisha hilo.
Chama na uongozi wake wanaaminika, wana mahaba ya wananchi, na kuungwa mkono nao kwa kutimiza kauli mbiu ya "hapa kazi tu" na kasi ya kuwaletea maendeleo ya viwanda na uchumi wa kati.
Wabunge na madiwani kuvihama vyama vyao kwa hiari yao wenyewe kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za rais ni mfano bayana kuwa misingi ya utawala bora wa sheria na demokrasia nchini vinakuwa chini ya utawala mahiri wa awamu ya 5.
Chama oyeee . . .!
 
Back
Top Bottom