Erick Mwijage alimwambia Djigui Diarra upande atakaopiga penati katika mchezo wa Yanga na Kagera sugar jana

Execute

JF-Expert Member
Sep 21, 2022
3,000
7,291
Ushahidi wa picha unaonesha Diarra akienda na kuinama kisha Mwijage naye akainama pale wakanong'onezana.

Diarra alipangua penati ile nyepesi.

Screenshot_20221114-175042.jpg
 
Ufikie wakati tukue kiakili ya ushabiki sio kuleta hisia za kishabiki. Haya embu leta clip ikionesha mdomo wa Diarra au mchezaji wa Kagera ukiwa unacheza cheza hapo alipokuwa ameinama. Tusiende mbali kuwa kaongea nini bali tuone tu kama kuna maneno kayaongea.

Mimi nimeitaza hiyo kipande ni kwamba Diarra alitoka golini kwake kwa lengo la kuuchukua mpira aushike shike nadhani tunaona ni tabia za makipa wengi tu, ikitokea penati huwa wanajisikia raha kwenda kuuchukua mpira na kuumbatia au kuushika shika. Bila shaka lengo ni kuutoa hofu kwake na kumtisha mpinzani anayepiga penati

Saaa Diarra alienda kwa hilo lengo ila mchezaji wa Kagera akauwahi kuukamata ule mpira, Diarra akabakia kuinama. Kuinama kati ya Diarra na mchezaji wa Kagera haikufukisha hata sekunde tano hivyo hakukuwa na majadiliano yoyote ila Diarra ndiye aliyeinama kwa muda mrefu. Imetokea coincidence ya wote kuonekana wameinama kwavile lengo la Diarra limestukiwa na mchezaji wa Kagera.

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
 
Haya maelezo yako hapa ni aibu tupu. Pale hakwenda kujadili bali aliinama ili aambiwe upande. Majadiliano yalishafanyika kabla ya mchezo.

Wewe huoni kwamba kilichotokea pale ni kitu cha ajabu sana?

Yaani mpira awe nao mchezaji wa kagera lakini Diarra ainame palepale.
 
Unastahili kupewa pole kwa maumivu unayopitia.
Naona ume edit lugha ya kukera uliyoitumia mwanzoni, hongera, huo ndio uungwana.

Wewe huoni kwamba kilichotokea pale ni kitu cha ajabu sana?

Yaani mpira awe nao mchezaji wa kagera lakini Diarra ainame palepale.
 
Haya maelezo yako hapa ni aibu tupu. Pale hakwenda kujadili bali aliinama ili aambiwe upande. Majadiliano yalishafanyika kabla ya mchezo.

Wewe huoni kwamba kilichotokea pale ni kitu cha ajabu sana? Yaani mpira awe nao mchezaji wa kagera lakini Diarra ainame palepale.
Una akili timamu za kujibishana kwa hoja na mimi? Nijibu ndio kisha tujadiliane kwa hoja na uwe unajibu nitapikuwa nakuuliza swali

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
 
Naona ume edit lugha ya kukera uliyoitumia mwanzoni, hongera, huo ndio uungwana.

Wewe huoni kwamba kilichotokea pale ni kitu cha ajabu sana? Yaani mpira awe nao mchezaji wa kagera lakini Diarra ainame palepale.
Wala haikuwa lugha ya kukera. Ilikuwa ni lugha sahihi kabisa. Siku zote wazazi hujivunia kuwa na watoto werevu, na siyo watoto wenye akili za kipopoma kama hizi za kwako!

Na ni watu wapumbavu pekee ndiyo wataamini hicho ulicho kielezea hapo juu.
 
Back
Top Bottom