Kwenye historia ya vita na mahusiano ya kimataifa, kuna nadharia inaitwa “Thucydides Trap” ambayo utumika kuelezea ulazima wa kutokea mgogoro au vita endapo taifa linalochipukia linapotishia kulizidi nguvu na ushawishi taifa lenye nguvu.
Kama wewe ni msomaji wa siasa za Nicollo Machiavelli, utakumbuka kuwa msingi wa nadharia zake ni kuwa kiongozi akihodhi madaraka na mamlaka, hawezi kutengeneza muhimili mwingine wa kisiasa wenye nguvu na ushawishi kama wake. Ndiyo maana marais ushauriwa wasiwateue wagombea wenza au mawaziri wakuu wenye nguvu au ushawishi wa kisiasa kuliko wao.
Bado hatujui sababu za Rais Samia kumteua Makonda lakini tunajua kuwa Makonda alimhadaa Magufuli kiasi kwamba “aliogopa” kumuondoa kwenye nafasi ya mkuu wa mkoa licha ya kukabiliwa na tuhuma nzito. Tulichokiona wiki iliyopita wakati wa ziara za Makonda kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa ni kutumia mbinu zile zile alizozitumia kwa Magufuli kumhadaa Rais Samia; anaonekana kama vile anampigia kampeni Rais Samia wakati huohuo anasafisha jina lake na kuandaa mtaji wake wa kisiasa wa huko mbeleni.
Mwanasiasa yoyote mkongwe hawezi kuamini maneno ya Makonda kutokana na historia yake na ukweli kwamba anachokiwaza kichwani mwake ni tofauti na matendo yake.
Kufanikiwa kwake kisiasa kumetokana na kuwahadaa watu, kuwadhalilisha wana CCM, wapinzani na viongozi washaafu. Hawezi kushidwa kumfanyia vitendo kama hivyo Raisa Samia hata kama amekula kiapo cha utii kwake. Kwahiyo ni wazi kuwa Makonda anazitumia ziara hizi kujenga taswira kuwa serikali ipo chini yake kwa kutoa maelekezo kwa mawaziri na viongozi waandamizi wa serikali.
Kumruhusu aendelee kufanya hivyo ni kurudia makosa aliyoyafanya Rais Mkapa kwa kumjenga Magufuli kisiasa. Natumaini Rais Samia amewaza kwa undani na kupokea ushauri wa watu wake wa karibu kabla ya kufikia uamuzi huu.
Kama hakufanya hivyo, atajikuta anamuandaa mshindani wake kwenye uchaguzi ujao au anamtengeneza mwanasiasa atayeiingiza nchi kwenye matatizo baada ya kuondoka kwake madarakani. Hapo ndipo dhana ya “Thucydides Trap” itakapodhibitika.
c&p
Thucydides's Trap refers to the natural, inevitable discombobulation that occurs when a rising power threatens to displace a ruling power...[and] when a rising power threatens to displace a ruling power, the resulting structural stress makes a violent clash the rule, not the exception
Tunao memo huu: Mgema akisifiwa, tembo hulitia maji