TANZIA Ephraim R. Mwansasu, Nguli wa Nyimbo za Injili Afariki Dunia

Baraka Mina

JF-Expert Member
Sep 3, 2020
581
574
Mwimbaji mkongwe wa nyimbo za injili na Askofu wa Hossana Assemblies of God Ephraim R. Mwansasu amefariki dunia usiku wa kuamkia leo (29/08/2021). Mwasasu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu, kwa sasa msiba upo Kimara Mwisho.

Mwansasu atakumbukwa kwa nyimbo zake nyingi alizoziimba kwa mvuto wa aina yake na kutoa ujumbe mzuri kwa kila aliyesikiliza na kuona video za nyimbo hizo zilizopendwa na kupata umaarufu Tanzania na nje ya Tanzania.

Baadhi ya nyimbo za Mwasasu ni:
  1. Siku nikilala mauti.
  2. Nangojea wakati.
  3. Kutesa kwa zamu.
  4. Dunia inapita.
  5. Tukimaliza kazi.
  6. Kiama.
  7. Heri wenye moyo safi.
  8. Tutatesa milele.
  9. Wosia wa baba.
  10. Watoto wachanga.
  11. Wanawake.
  12. Maumivu ya Yesu.

Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina Lake Lihimidiwe, Pumzika kwa amani nguli wa nyimbo za injili Askofu Ephraim R. Mwansasu.

FB_IMG_1630244542837.jpg


 
Growing up nyimbo zake ni miongoni mwa nyingi nilizosikia ...

.. maombolezo,

Nikilala

Na vilio,

Wengi watalia sana,

Maombolezo,

Na vilio.
Nyimbo zake zilikuwa zinagusa sana. Katika nyimbo ya siku nikilala aliimba na kusema siku akilala mauti hakuna atayeweza kumwamsha.

Akaongezea katika wimbo wa nangojea wakati kuwa anangojea wakati utakapotimilika na atafika angani kituo cha watakatifu.
 
Back
Top Bottom