Kwanini siku hizi wasanii wa nyimbo za Injili hawaimbi kukemea maovu kama zamani?

Apr 28, 2018
36
32
Kama kichwa cha Habari kinavyo jieleza hapo juu, miaka ya hivi karibuni wasanii wa nyimbo za injili wamekuwa wakitoa nyimbo nyingi zakusifu mazuri, kama vile maisha mazuri na pesa n.k, tofauti na Miaka ya zamani wasanii wengi walikuwa wakitoa nyimbo za maonyo, nyimbo zakukemea dhambi, nyimbo ya kuwafanya watu tuwe na hofu ya Mwenyezi Mungu.

Lakini saiz hali imekuwa tofauti sanaaaa. Kwa sasa wasanii wachache Sana wa injili wanakemea dhambi
 
Ni baadhi sio wote.

Wapo ambao wanajua kabisa kuwa uimbaji ni uinjilisti kwahiyo wanakemea uovu.

Lakini pia wimbo unaweza kuwa haukemei uovu lakini unamsifu Mungu au kuelezea uzuri wa Yesu, uzuri wa mbingu n.k

Kwa mfano wimbo unaweza usikuambie kuwa ''Acha uzinzi'' lakini ukakuambia ''Mungu ni mwema kwako au Mungu anakupenda''

Ilimradi ni Ujumbe wa Mungu kwa watu wake.
 
Ulimwengu wa sasa dhambi imetawala matendo mengi yanaonekana nadra sana.

Kwaya au waimba gospel wakiimba kuhusu dhambi wasikilizaji watahisi kushambuliwa wengi hawatasikiliza hizo nyimbo wala kuvutiwa nazo.

Ila wasikilizaji wanataka nyimbo za faraja na kupeana moyo ili waendelee kufarijika huku wakiendelea kuishi katika ulimwengu wa dhambi.

Imagine leo ukimwambia binti na kijana katika umri wa miaka 20 kuwa mfunge ndoa ndipo muishi pamoja Jamii nzima italipuka na kukushambulia. Ila hawa hawa vijana wakiishi kisela hata jamii ikatazama hawatawaambia chochote.

Watawekana ujauzito, watatoa, watafanya zinaa zote hakuna atae sema.

So tunaishi katika nyakati ambazo wanadamu wamechagua kuishi nje ya misingi ya maagizo ya MUNGU na ndio maana ujumbe wa MUNGU hauwapi hamasa bali unawapa hofu ya kukimbia kabisa mazingira ambayo kuna uwepo wa MUNGU au ujumbe wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tambua kuwa sikuhizi kuna "wasanii WA nyimbo za injili" hawa ni watu WA kuigiza Tu Kwa MUNGU Ila hawana roho mtakatifu wala hawana MUNGU ndani ya mioyo Yao.

Alafu kuna "waimbaji WA nyimbo za injili" hawa ndiyo wale waliokuwa wanaimba katika roho na kweli pia hata kabla ya kutunga nyimbo walikuwa wanafunga na kuomba Kwanza ili roho WA MUNGU apate kuhusika kwenye tungo zao, takataka za sikuhizi huwa sisikilizi hata kidogo kwasababu hazina ujumbe ndani yake WA kimungu

Kama kichwa Cha Habari kinavyo jieleza hapo juu,Miaka ya hivi karibuni wasanii wa nyimbo za injili wamekuwa wakitoa nyimbo nyingi zakusifu mazuri,Kama vile maisha mazuri na pesa n.k,tofauti na Miaka ya zamani wasanii wengi walikuwa wakitoa nyimbo za maonyo,nyimbo zakukemea dhambi,nyimbo yakuwafanya watu tuwe na hofu ya Mwenyezi Mungu......

Lakini saiz Hali imekuwa tofauti sanaaaa.Kwasasa wasanii wachache Sana wa injili wanakemea dhambi
Kwa sababu wale ni wasanii tu wanaocheza na hisia za watu kwa kusingizia dini
 
Ulimwengu wa sasa dhambi imetawala matendo mengi yanaonekana nadra sana.

Kwaya au waimba gospel wakiimba kuhusu dhambi wasikilizaji watahisi kushambuliwa wengi hawatasikiliza hizo nyimbo wala kuvutiwa nazo.

Ila wasikilizaji wanataka nyimbo za faraja na kupeana moyo ili waendelee kufarijika huku wakiendelea kuishi katika ulimwengu wa dhambi.

Imagine leo ukimwambia binti na kijana katika umri wa miaka 20 kuwa mfunge ndoa ndipo muishi pamoja Jamii nzima italipuka na kukushambulia. Ila hawa hawa vijana wakiishi kisela hata jamii ikatazama hawatawaambia chochote.

Watawekana ujauzito, watatoa, watafanya zinaa zote hakuna atae sema.

So tunaishi katika nyakati ambazo wanadamu wamechagua kuishi nje ya misingi ya maagizo ya MUNGU na ndio maana ujumbe wa MUNGU hauwapi hamasa bali unawapa hofu ya kukimbia kabisa mazingira ambayo kuna uwepo wa MUNGU au ujumbe wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Daah umenena Sawa Sawa
 
Kama kichwa Cha Habari kinavyo jieleza hapo juu,Miaka ya hivi karibuni wasanii wa nyimbo za injili wamekuwa wakitoa nyimbo nyingi zakusifu mazuri,Kama vile maisha mazuri na pesa n.k,tofauti na Miaka ya zamani wasanii wengi walikuwa wakitoa nyimbo za maonyo,nyimbo zakukemea dhambi,nyimbo yakuwafanya watu tuwe na hofu ya Mwenyezi Mungu......

Lakini saiz Hali imekuwa tofauti sanaaaa.Kwasasa wasanii wachache Sana wa injili wanakemea dhambi
Haki mimi nimekua na masikitiko makubwa sana kwani hao hao wasanii wa injili ukifatilia mienendo yao ya maisha imekua na taswira njema mbele za watu lakini ukifuatilia nyuma ya macho ya watu aseeee utasikitika wasanii wengi sikuizi wanamambo makubwa na magumu yasiyoelezeka asee wengine ni wanachama wa upinde wa mvua na bado wako katika kuimba injili ni masikitiko sana..
 
Duh mbn hatariii
 
Ni baadhi sio wote.

Wapo ambao wanajua kabisa kuwa uimbaji ni uinjilisti kwahiyo wanakemea uovu.

Lakini pia wimbo unaweza kuwa haukemei uovu lakini unamsifu Mungu au kuelezea uzuri wa Yesu, uzuri wa mbingu n.k

Kwa mfano wimbo unaweza usikuambie kuwa ''Acha uzinzi'' lakini ukakuambia ''Mungu ni mwema kwako au Mungu anakupenda''

Ilimradi ni Ujumbe wa Mungu kwa watu wake.
Huyo Mungu ni wa kwenu au wa wazungu? Africa tubadilike, tunaamini mambo ya kuletewa na kuacha asili yetu
 
Kama kichwa cha Habari kinavyo jieleza hapo juu, miaka ya hivi karibuni wasanii wa nyimbo za injili wamekuwa wakitoa nyimbo nyingi zakusifu mazuri, kama vile maisha mazuri na pesa n.k, tofauti na Miaka ya zamani wasanii wengi walikuwa wakitoa nyimbo za maonyo, nyimbo zakukemea dhambi, nyimbo ya kuwafanya watu tuwe na hofu ya Mwenyezi Mungu.

Lakini saiz hali imekuwa tofauti sanaaaa. Kwa sasa wasanii wachache Sana wa injili wanakemea dhambi
wanaimba za kuburudisha kama bongo flavour wapate ugali na kuuza.
 
Kama kichwa cha Habari kinavyo jieleza hapo juu, miaka ya hivi karibuni wasanii wa nyimbo za injili wamekuwa wakitoa nyimbo nyingi zakusifu mazuri, kama vile maisha mazuri na pesa n.k, tofauti na Miaka ya zamani wasanii wengi walikuwa wakitoa nyimbo za maonyo, nyimbo zakukemea dhambi, nyimbo ya kuwafanya watu tuwe na hofu ya Mwenyezi Mungu.

Lakini saiz hali imekuwa tofauti sanaaaa. Kwa sasa wasanii wachache Sana wa injili wanakemea dhambi
Siku kuna insipiration songs hata sio injili. Ni muda tu mkuu hata nyimbo za gospel za miaka 1800 bila shaka hazifanani na za miaka 1990
 
Kama kichwa cha Habari kinavyo jieleza hapo juu, miaka ya hivi karibuni wasanii wa nyimbo za injili wamekuwa wakitoa nyimbo nyingi zakusifu mazuri, kama vile maisha mazuri na pesa n.k, tofauti na Miaka ya zamani wasanii wengi walikuwa wakitoa nyimbo za maonyo, nyimbo zakukemea dhambi, nyimbo ya kuwafanya watu tuwe na hofu ya Mwenyezi Mungu.

Lakini saiz hali imekuwa tofauti sanaaaa. Kwa sasa wasanii wachache Sana wa injili wanakemea dhambi
Mimi mwenyewe binafsi siwezi kukaa nikasikiliza wimbo wa kukemea unywaji wa pombe wakati ndo starehe yangu! Hakuna mtu anaekubari kupondwa kwa tabia yake zama hizi!

Ila nikisikiliza wimbo wa Mercy Masika Mwema, hata nikiurequest ukapigwa kwenye spika za bar, naona ushindi tu! Maake naona ni kwa jinsi gani sir God kanijalia nimepata pesa mpaka nakuja kurefresh mind sehemu kama hizo!!
 
Back
Top Bottom