Ephraim Mrema na Ufisadi TANROADS

Nimeona ni vyema kuanzisha mada hii kwa ajili ya haya yaliyojiri bungeni kuhusu Afisa mtendaji mkuu wa TANROADS,Epharaim Mrema ilipostiwa mahali ambako nadhani isingepata attention inayostahili.

Je, hapa kuna ufisadi?



Shadrack Sagati, Dodoma

HabariLeo; Ijumaa,July 04, 2008

MKURUGENZI Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads), Ephraem Mrema ameumbuliwa bungeni, kuwa amepewa wadhifa huo kinyume cha taratibu.

Mbunge wa Kasulu Magharibi, Kilontsi Mporogomyi (CCM) alisema Mrema hana taaluma ya uhandisi ujenzi, huku analipwa mamilioni ya fedha za Watanzania.

Mporogomyi ndiye aliyeweka hadharani habari za Mkurugenzi huyo kuingizwa kwenye madaraka hayo kupitia mlango wa nyuma; huku wataalamu ambao walipendekezwa na jopo la usaili wakiwekwa pembeni.

“Ninavyojua huyu Mrema hakuwa amependekezwa na jopo la usaili, hatujui alikotokea hadi akawekwa pale…naomba waziri useme juu ya ajira ya mkurugenzi huyu,” alisema wakati akichangia katika hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa.

Mporogomyi aliliambia Bunge kuwa sifa za mkurugenzi huyo ni kwamba ni mshauri wa mambo ya ununuzi na kabla ya kushika wadhifa huo, alikuwa anafanya shughuli zake visiwani Zanzibar.

Hata hivyo, Mrema mwenyewe alijitetea kuwa ana shahada ya kwanza ya ukandarasi uchumi (Construction Economics) na shahada ya pili ya Menejimenti ya miradi (Project Management) aliyoipata mwaka 1987. Hata hivyo, hakutaja vyuo alikopata shahada hizo.

Aliwataja wahandisi ambao walipendekezwa na jopo la usaili kuwa ni Boniface Nyiti, Venance Ndyamkama na mwingine aliyemtaja kwa jina la moja la Chacha. “Hawa ndiyo ambao walipendekezwa na ni wahandisi wa siku nyingi pale Tanroads; lakini huyu mkurugenzi alikotolewa na kuwekwa pale haijulikani.”

Mrema alichukua wadhifa wa mkurugenzi aliyekuwa anatokea Ghana ambaye alimaliza muda wake mwaka 2006. Mporogomyi alisema mkurugenzi wa sasa aliingizwa kwa misingi ya ufisadi.

Mbunge huyo aliongeza kuwa mara tu baada ya kupata wadhifa huo, alianza kuwanyanyasa wahandisi hao wenye sifa na akawahamishia wizarani ambako pia walirudishwa na wizara Tanroads. “Wizara ilisema hawa ni mawakala wa ujenzi wa barabara wakawarudisha.”

Alisema Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu wakati inawarejesha kwa Tanroads, ilishauri wapewe mikoa ya kuongoza, lakini kuwa tayari nafasi hizo zilishajazwa na watu wengine Mrema hakuweza kutekeleza agizo hilo.

Alisema alibaki nao makao makuu na wanalipwa fedha nyingi huku wakiwa hawana kazi za kufanya. Alisema kuwa mkurugenzi huyo baada ya kuona wahandisi hao ni tishio katika ajira yake, sasa ameingiza utaratibu mpya wa ajira za mikataba.

Mporogomyi alisema mpango huo mpya unafanywa na mkurugenzi huyo kwa nia ya kuwaengua wafanyakazi wote ambao anaona kama ni tishio kwake, hasa wale wahandisi wenye sifa za kushika wadhifa wake huo.

“Kibaya zaidi pamoja na kuingia kwa mlango wa nyuma, lakini ananyanyasa wafanyakazi,” alisema mbunge huyo huku akimtaka Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu amweleze namna mkurugenzi huyo alivyoingizwa kwenye nafasi hiyo nyeti na ikiwezekana aondolewe haraka.

Lakini pia alisema mkurugenzi huyo analipwa fedha nyingi kama vile ni mtaalamu ambaye ameajriwa kutoka nje ya nchi.

Aliweka hadharani viwango hivyo kuwa Mrema alipoanza kazi alipewa posho ya kuanza (Commencement allowance) dola za Marekani 9,000 kwa siku 60 (sawa na Sh milioni 10.8), mshahara wake kwa mwezi ni dola za Marekani 8,500 (Sh milioni 10.2), posho ya nyumba kwa mwezi ni dola 2,200 (Sh milioni 2.6), posho ya matibabu dola 400 kwa mwezi (Sh 480,000), posho ya usafiri dola 500 (Sh 600,000).

Pia analipwa pensheni kwa mwaka kiasi cha dola za Marekani 10,200 (Sh milioni 12.4), akienda likizo analipwa dola 3,000 (Sh milioni 3.6), bonasi yake kwa mwaka analipwa dola 102,000 (Sh milioni 122.4) na mwisho wa mkataba wake analipwa dola 10,000 (Sh milioni 12) kama malipo ya kumaliza kazi.

Mporogomyi alisema pamoja na fedha nyingi anazolipwa mkurugenzi huyo; lakini bado anajihusisha na vitendo vya ufisadi zinavyosababisha wakati mwingine awanyanyase na kuwafukuza wafanyakazi ambao wanatenda haki.

Mbunge huyo alitoa mfano kuwa kuna mfanyakazi aliyemtaja kwa jina moja la Mabuye ambaye alikuwa anafanya kazi katika mizani ya Kibaha. Alisema siku moja mfanyakazi huyo alikamata malori ambayo yalikuwa yamezidisha uzito wa bidhaa walizobeba.

Alisema aliyazuia na kuwataka walipe faini ya Sh milioni 18, lakini matajiri wa yale malori walipoambiwa kukamatwa kwa magari yao walimpigia simu na yeye akaamuru Mabuye afukuzwe kazi.

Mporogomyi alisema Mrema alimpigia simu meneja wa Tanroads mkoa wa Pwani ili amfukuze na aliposita alimtishia kwa simu kuwa afanye hivyo haraka, kwani hataki kumwona huyo mfanyakazi akiendelea na kazi.

“Kama siyo ufisadi hiki nini, yaani mfanyakazi ambaye anafanya kazi kwa misingi ya sheria unamfukuza kazi, sababu ni nini hapa? Alihoji mbunge huyo na kusisitiza kutaka maelezo ya kina kutoka kwa Waziri wa Miundombinu.

Hii kitu si ishawahi kujadiliwa humu ama?Kwani huyu muheshimiwa bado suala lake halijashughulikiwa?Mafisadi kweli wana nguvu sana...
 
Na Restuta James
13th November 2009


headline_bullet.jpg
Awabandua wakurugenzi watatu
headline_bullet.jpg
Wamo mameneja watatu wa mikoa


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Ephraem Mrema, ameitunishia misuli bodi ya wakurugenzi ya taasisi hiyo na Wizara ya Miundombinu kwa kupuuza maagizo halali yaliyotolewa kwake.

Kinyume cha maelekezo ya wakuu wake kwamba asiwafukuze kazi wakurugenzi na mameneja wa mikoa bila kufuata taratibu za utumishi serikalini, Mrema ambaye awali alitii agizo hilo na kusitisha uamuzi wake, baadaye aligeuka tena na kuendelea na maamuzi yake ambayo sasa yameamsha taharuki kubwa ndani ya taasisi hiyo yenye dhima ya kujenga na kusimamia matunzo ya barabara kuu nchini.

Sakata hili ambalo sasa linaonekana kama ni mapambano ya kimamlaka kati ya Mrema, Bodi ya Tanroads na Wizara mama, lilianza Oktoba 30, mwaka huu, baada ya kiongozi huyo kuitisha kikao cha wafanyakazi na kutangaza kuwafukuza kazi baadhi ya watendaji waandamizi ambao ni Mkurugenzi wa Matengenezo ya Barabara, Thomas Mosso; Mkurugenzi wa Mipango, Jason Rwiza na mameneja wa mikoa mitatu ya Dodoma, Gerson Lwenge; Morogoro, Charles Madinda na wa Ruvuma, Abraham Kissimbo. Pia kwenye orodha hiyo yupo William Shilla ambaye ni mhandisi makao makuu Tanroads.

Habari zilisema kwamba watendaji hao waandamizi walionyesha wazi kukataa kukubaliana na hatua hizo kwa sababu zilikuwa ni kinyume cha taratibu na hivyo wakakata rufaa wizarani.

Baada ya mamlaka hizo kupata kilio cha watendaji hao, zilitengua maamuzi ya Mrema kwa kuwa hayakuzingatia taratibu za Tanroads.

Kwa mujibu wa nyaraka za Mrema juu ya suala hilo ambazo Nipashe imeziona, kiongozi huyo

Novemba 6, mwaka huu aliwaandikia wafanyakazi wote waraka wa kutangaza kusitisha utekelezaji wa tangazo la kikao chake na wafanyakazi cha Oktoba 30, 2009 kwa kuwa alikuwa amepata maagizo kutoka Serikalini ya kusitisha tangazo lake.

“Napenda kuwajulisheni kwamba nimepata agizo la Serikali kwamba uteuzi wa wakurugenzi na viongozi wengine wa Tanroads umesitishwa, aidha,” sehemu ya waraka huo inasomeka na kuongea kuwa:

“Serikali imeagiza kuwa mchakato wa uteuzi wa viongozi hao utatakiwa kufuata kanuni za ‘Executive agencies’ kwa kuzingatia usawa, uwazi na ushindani…kutokana na hayo, napenda kukujulisheni kwamba mawasiliano hivi sasa yanaendelea na mamlaka husika jinsi ya kutekeleza agizo hili kulingana na muundo wa Tanroads ulioidhinishwa.”

Hata hivyo, siku tatu baadaye yaani Novemba 9, Mrema aliandika waraka mwingine wa kutengua ule wa Novemba 6, akidai kuwa ulikuwa umesambazwa kwa wafanyakazi kimakosa ijapokuwa ulikuwa na saini yake.

Badala yake alisema kwamba maofisa waandamizi waliokuwa wamefutwa kazi maamuzi yake yanaendelea kama alivyokuwa ameamua na kutangaza kwa wafanyakazi wote Oktoba 30, mwaka huu, kwani alikuwa amepata baraka za mamlaka za juu.

“Nasikitika kuwajulisheni kwamba taarifa ya kusitisha utekelezaji wa waraka wa terehe 30 Oktoba 2009 ilitumwa kwenu kimakosa kabla ya kupata kibali cha mtendaji mkuu kwa hiyo waraka huu unafuta waraka wa kusitisha utekelezaji wa waraka wa Mtendaji Mkuu wa Novemba 6 na unawajulisha kwamba uteuzi wa uongozi uliotajwa Oktoba 30 umeanza kazi rasmi Novemba 1, 2009 na umepelekwa katika ngazi husika kupata baraka za mwisho,” alisema Mrema katika waraka huo.

Katika waraka huo, Mrema alitangaza kusitisha mikataba ya wahandisi waandamizi sita, yaani Mosso, Rwiza, Shilla, Lwenge, Madinda na Kissimbo.

Kwa mujibu wa waraka huo, tayari nafasi za mameneja hao zinashikiliwa na wahandisi wengine ambapo Mkoa wa Dodoma unashikiliwa na Dorothy Mtenga; Morogoro, Obrien Machange, wakati Yusuph Mazana amepelekwa Ruvuma.

Hata hivyo, taarifa nyingine zinaonyesha kuwa mikataba ya wahandisi waliofukuzwa kazi ilikuwa haijamalizika wala hawakuwa wametimiza umri wa kustaafu.

Wafanyakazi ambao hawakupenda majina yao yaandikwe gazetini, waliliambia gazeti hili kuwa Mrema amekuwa akitamba kwa wafanyakazi kuwa mabadiliko yote anayofanya ndani ya wakala huo ni utekelezaji wa ahadi yake alipokuwa akipewa ajira.

Walisema awali, kila baada ya miezi mitatu, wakuu wa idara na mameneja wa Tanroads wa mikoa walikuwa na utaratibu wa kukutana katika vikao kwa ajili ya kuangalia utendaji wa wakala huo, lakini Mtendaji huyo aliufuta utaratibu huo na kueleza kuwa Tanroads haiwezi kuendeshwa kwa vikao.

Mfanyakazi mmoja wa wakala huo alidokeza kuwa kwa miaka miwili mfululizo, Mrema amekuwa akifanya mabadiliko makubwa ndani ya Tanroads na anapoulizwa anasema anadhani huo ndio utendaji bora.

Mwandishi wa habari hizi alipoomba kukutana na Mrema jana, alielezwa kuwa yupo kwenye kikao nje ya ofisi na kwamba asingeweza kurudi ofisini mapema.

Gazeti hili lilipomtafuta Mwenyekiti wa Bodi ya Tanroads, Abel Mwaisumo, ili kuzungumzia madai hayo, lilielezwa kuwa yupo nje ya nchi kwa matitabu.

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dk. Samwel Nyantahe, alithibitisha kuwa na taarifa ya Mrema kupindisha maagizo ya bodi na kusema kuwa bodi na Wizara zinakutana leo jijini Dar es Salaam kujadili suala hilo.

“Bodi imekwishapokea ‘allegations’ (madai) yote kutoka kwa wafanyakazi na sisi tunayafanyia kazi, tulikutana Jumatatu tulijadiliana na kesho (leo) tutakutana tena, hii yote ni kuhakikisha kuwa tunayapatia ufumbuzi matatizo haya,” alisema Dk. Nyantahe.

CHANZO: NIPASHE
 
Nafikiri itatusaidia kwenye discussion ya hii thread kama tukizingatia mambo machache ya msingi:

1. Huyu Bwana Ephraem Mrema hakuamua mwenyewe kujilipa mshahara huu - ni lazima kulikuwa na kikao ambacho kiliamua hivyo based perhaps on salary history yake na mishahara wanayolipwa maCEO wengine kama wale wa TCRA; TBC; TRA; TMA; ATC; THA; TPB etc. Let us be informed how much these other CEOs are paid before starting to jump into conclusions.

2. Katika ku decide on who to employ as CEO wa TANROADS naamini kabisa kuwa huyu Bwana alikuwa interviewed pamoja na shortlisted applicants wenzake. Qualifications ni only one aspect ya selection criteria. Katika ngazi kama hii ya CEO experience carries more weight than qualifications. Nafikiri tungepewa pia experience ya huyu Bwana Mrema na aliipatia wapi pamoja na zile za hao applicants wenzake. Ikiwa kama selection criteria ilikuwa based only on basic qualifications then maprofessor wa Civil Engineering UDSM would have been given the post automatically.

3. Swala la kama Bwana Mrema ni mchagga au mnyamwezi au mnyaturu ni irrelevant - kwa mawazo yangu hiyo ni village mentality. Kwa nini mchagga hana haki ya ku apply kwa kazi kama hiyo? Tuacheni Unduli na U-fascist!

4. Pia sijui kama huyu Ephraem Mrema ana uhusiano wowote ule wa kindugu na Mrema wa Ngurdoto. The mere fact they are both called Mrema does not mean they are related. Why not link him with Mrema wa TLP? Na pili sielewi reason ya kuingiza urafiki wa Mrema wa Ngurdoto na Lowassa? Besides is it a sin in Tanzania kuwa rafiki wa Lowassa? Tuacheni Unduli.

5. Let us be objective and avoid parochialism! Ahsanteni.

mmh ... wewe?! we umejuaje yote haya?? mbona watetea hivi ....
 
Mamlaka ya kuteua nani awe CEO wa Tanroad yako kwa waziri na halazimiki kufuata ushauri wa mtu yeyote.

Amandla......
 
Bw. Heri,

Magufuli kakosa wapi hapa?

Je unajua kuwa mkandarasi aliyezawadiwa hiyo kazi kwa 192Bilion ya kujenga 100km ni MCHINA? anaitwa CHICO, kwani hizo zingine 50km zilishafanyika kwa kiwango kikubwa na mkandarasi wa awali?

Tafakari then leta hoja......tutafika kweli kwa kujenga 1km ya lami kwa 1.4Bilion? ...hayo mahesabu umeyafanya? Kwakweli huyo MREMA na watendaji wa juu MIUNDOMBINU akiwemo CHAMBO niwala rushwa wakubwa!!!!!
Naungana na wewe huyu jamaa hafai kabisa hizo ulizotaja hapo cha mtoto sasa hivi kuna kampuni moja ya wahindi E ambayo konoike amenyag'wanywa kazi ikapewa hiyo kampuni kwa mabilioni ya pesa kulinganisha na pesa ambazo konoike ilikuwa inaomba kama extra hii ni hatari kampuni hiyo hiyo ndo imepewa kandarasi zote zile zenye pesa hapa Dar huku kapuni za kizalendo kama skoll, delmonte,seekv,tena na zingine zikikosa Kama mac wakiwa hawana kazi, huyu mtu anakula yeye pamoja na mjamba mtu
 
rev. Kishoka,

interviews za tanzania ziko tofauti na hasa hizo zinazoendeshwa na wizara.

Pia kwenye mambo ya technical, ukiachia maswali ya jumla kama uliyoyaandika, kuna kampuni wanaingia deep kwenye nyanja husika.

Huku west sasa wameacha kwenda ndani kwenye nyanja husika na badala yake wanauliza maswali genaral kwasababu wanaamini kwenye uwezo wa mtu ku cope kwenye mazingira mbalimbali, tanzania na afrika, tunaamini kwenye ukipanga, uwezo wa kukokotoa majibu kama yalivyo kwenye vitabu vya wasomi.

Sisemi mrema alipewa maswali, ila nataka kutofautisha tu juu ya interviews ambazo zinaendeshwa na makampuni ya uajiri na zile za wizarani.

Aidha ukiaangalia matatizo mengi ya tanzania utakuta kinachokosekana ni management skills na wala sio hizo technical skills. Nafasi kama ya ceo inatakiwa skills zaidi ya zile za ujenzi barabara. Ukiwa fundi ujenzi ni added value lakini muhimu zaidi ni management skills.

Huyo mrema ni mwakilishi tu wa kundi kubwa amblo mimi huwa naliita middle class ya tanzania ambao ni mzigo kwa maendeleo ya nchi yetu. Wanapata pesa nyingi lakini utendaji wao mbovu, wanapiga vita watanzania wenzao, wanakula rushwa, wana ukabila nk.
hrm wako ustawi wa jamii wanajua sana mambo ya mgnt
 
Haki ya nani vile................yaani Wazalendo tutapochukua hii nchi........y'all (Mrema et al) gonna answer.......wallahi tena....
 
Siyo lazima lkn hapa kincho wauma watu ni jinsi anavyo tafuna kupitia wachina na wahindi na kubagua wataalam wenzie
Kuna siku historia itatuhukumu kwa haya magonjwa tunayoendelea kuyalea.Tanroad kuna tatizo kubwa la uongozi. Time will tell...mfano mdogo tu ni huu wakutoa kibali kwa makampuni matatu tu ya mabango ya matangazo bila kutoa utaratibu wa wengine wote kuufuata.Wamepeleka kesi kwenye fair competition commision.
Au Na wao wana CEO decree ambazo hazina taratibu? Pengine sijalielewa tatizo lilipo minifahamishe
 
Hakuna wa kumgusa Mrema!

Ameteuliwa toka Ikulu na hakuwepo kwenye Interview. Ukiangalia maamuzi yake mengi ni tata! He cant make engineering judgement lakini nani amuguse?

Dr. Kawambwa alitulia kama amelowa na mvua kwani hawezi kumugusa Mrema..... amewekwa na mzee kwa kazi maalum!
 
Hakuna wa kumgusa Mrema!

Ameteuliwa toka Ikulu na hakuwepo kwenye Interview. Ukiangalia maamuzi yake mengi ni tata! He cant make engineering judgement lakini nani amuguse?
Dr. Kawambwa alitulia kama amelowa na mvua kwani hawezi kumugusa Mrema..... amewekwa na mzee kwa kazi maalum!
Kazi maalumu zinasomewa wapi? Maana uzoefu wangu unaonyesha wengi wanaopewa madaraka ili kufanya kazi maalumu wanaharibu big time!! Kama mtu anayeongoza Tanroad hajui umuhimu wake itakuwa hasara yetu.Kwa mfano ile barabara ya Dodoma, manyoni Singida ilianza kujengwa 2004 mpaka leo hii haijakamilika. Chico walijenga hii Sam Nujoma kwa takribani miaka mitatu ndo wameweza kukamilisha.

Lakini Grinekers ya SA ilijenga ile barabara ya kutoka Mpaka wa Mwanza hadi Isaka na Nzega kwa miaka miwili ikakamilika.

Delays kama hizo katika project zina effect kubwa in its critical path which eventually end up increasing the cost of building the roads.
Hii ni hasara ya nani?
 
Hakuna wa kumgusa Mrema!

Ameteuliwa toka Ikulu na hakuwepo kwenye Interview. Ukiangalia maamuzi yake mengi ni tata! He cant make engineering judgement lakini nani amuguse?
Dr. Kawambwa alitulia kama amelowa na mvua kwani hawezi kumugusa Mrema..... amewekwa na mzee kwa kazi maalum!
Wateuliwa wa Aina ya Ephraim Mrema ni wote unaowaona wanongoza hizi Agencies na hakuna hata mmoja alipatikana kwa staili nyingine. It depends ni nani mwenye kuhusika na hiyo Mamlaka. Kumtoa Mrema kafara tutakuwa hatutendi haki mbona kule TANESCO aliteuliwa Dr. IDRIS RASHID kuwa Mkurugenzi Mkuu wakati katika Tangazo sifa kubwa alitakiwa awe Mhandisi na hatujasema aondolewe na amepeta na Uchumi wake mpaka makataba umekwisha na IKULU kwa kupitia kwa Swahiba wameagiza aongezewe mkataba for another three years .

Naomba mnitajie taasisi hata moja ambyo CEO wake alipatikana kwan njia ya machakato wa Wazi.Sidanganyiki they are all birds of the same feathers. Tanzania ni kama nyama ya Tembo na kwa sisi wawindaji anayekula Maini ya Tembo ni mwenye kisu tena kikali. Kama huna connections it means huna kisu kwa hiyo kula maini ya tembo Tanzania itabakia kuwa ndoto ya mchana. Akiondolewa Mrema na wengine wote including akina Salva waondoke!!!
 
Mamlaka ya kuteua nani awe CEO wa Tanroad yako kwa waziri na halazimiki kufuata ushauri wa mtu yeyote.

Amandla......
Ni Rais anateua CEO baada ya kuletewa majina matatu na Waziri mwenye dhamana husika.Mtu akishapewa utendaji kumuondoa then sharti sheria za kazi zifuatwe na ndo maana mwaka 1996 Rais Mkapa alipowaondoa kazini Police Commisioners kadhaa kwa kilichoitwa 'manufaa ya umma' jamaa walikwenda mahakamani na kushinda na kulipwa fidia,nadhani walikuwa ni kina Kamanda HS Rashid na wenzake. Kumuajiri mtu,kama ilivyo kufunga ndoa ni rahisi,kumuondoa kama ilivyo talaka ni kimbembe maana sheria za ajira kama zilivyo za ndoa ni ngumu na zina tend kumlinda mwajiriwa.
 
Ni Rais anateua CEO baada ya kuletewa majina matatu na Waziri mwenye dhamana husika.Mtu akishapewa utendaji kumuondoa then sharti sheria za kazi zifuatwe na ndo maana mwaka 1996 Rais Mkapa alipowaondoa kazini Police Commisioners kadhaa kwa kilichoitwa 'manufaa ya umma' jamaa walikwenda mahakamani na kushinda na kulipwa fidia,nadhani walikuwa ni kina Kamanda HS Rashid na wenzake. Kumuajiri mtu,kama ilivyo kufunga ndoa ni rahisi,kumuondoa kama ilivyo talaka ni kimbembe maana sheria za ajira kama zilivyo za ndoa ni ngumu na zina tend kumlinda mwajiriwa.

Sio kwenye Executive Agencies. Hawa sio Presidential appointees. Hizi ni matunda ya Civil Service Reform na zililetwa ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi. CEs wa EA wanakuwa kwenye contract na kuwaondoa si vigumu kama ilivyo kwa civil servants. Ni kufuata taratibu tuu zilizomo au kungoja mkataba wake uishe ( ambao si wa muda mrefu) na kukataa ni kuuongeza.

Amandla........
 
Kama tunadhamiria kwa dhati kuimarisha hata Civil Service tungebadilisha Sheria ili Mkuu wa Idara au Wizara awe na contract ya miaka mitano, itakayokuwa renewable. Napendekeza miaka mitano ili Rais mpya aweze kuwa na uhuru na uwezo wa kuwa na wasaidizi atakaoweza kufanya kazi nao bila matatizo.

Kwa sasa inaonekana tunajiingiza katika kuwafanya maafisa waandamizi ambao Rais mpya hawataki, kuwa mabalozi au wakuu wa mashirika ya umma, ambapo wateule hao sio fani zao. Matokeo ni kuboronga etc.
 
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, kupitia ofisi ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo, ametaka kupewa maelezo ya kina kuhusu uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kupoteza mwelekeo na kushuka kwa kiwango cha ufanisi, ikiwa ni siku kadhaa baada ya gazeti hili kufichua pamoja na mambo mengine, hasara iliyosababishwa kutokana na kuyumba kwa wakala huo.

Kwa mujibu wa nakala ya barua yenye kumbukumbu namba CEA.388/389/01/28, ya Machi 31, mwaka huu, kwenda Wizara ya Miundombinu, ofisi ya Waziri Mkuu inamtaka Katibu Mkuu wa Miundombinu kutoa taarifa kuhusu hatua zilizochukuliwa na wizara hiyo ili kuliokoa Taifa na kile kilichoelezwa kuwa hasara kubwa.

TANROADS inaongozwa na Ephraim Mrema kama Mkurugenzi Mtendaji, ambaye amekuwa akiandamwa na tuhuma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutumia majina ya viongozi wa juu serikalini na wanasiasa katika kutishia watu wanaofichua maovu ndani ya taasisi yake.

Imebainika kuwa mbali na gazeti hili kuripoti utendaji mbovu katika TANROADS katika toleo lake namba 126, la Machi 24, mwaka huu, wafanyakazi wa wakala huo pia waliandika malalamiko yao kwenda kwa Waziri Mkuu, kupitia barua yenye kumbukumbu namba TMC/TRD/HQ ya Machi 22, mwaka huu.

Kutokana na barua ya wafanyakazi hayo na taarifa za gazeti hili, barua ya Katibu Mkuu wa ofisi ya Waziri Mkuu kwenda kwa Katibu wa Wizara ya Miundombinu inasomeka; “Ni dhahiri kwamba kama hali ya utendaji kazi ndani ya Wakala wa Barabara kama ilivyoelezwa na uongozi wa Chama Cha Wafanyakazi haitarekebishwa, Taifa linaweza kupata hasara kubwa ikizingatiwa kuwa kiasi kikubwa cha fedha kimetengwa kwa ajili ya shughuli za wakala huo.”

Barua hiyo iliyosainiwa na Fanuel Mbonde Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu kwa niaba ya Katibu Mkuu, inasomeka zaidi kwamba; “Ofisi hii itapenda kupata taarifa ya hatua zinazochukuliwa na Wizara yako (Miundombinu) kuhusu shutuma zilizoelezwa na Chama Cha Wafanyakazi na mapendekezo yao ya hali ya uongozi wa Wakala wa Barabara ili Mheshimiwa Waziri Mkuu ajulishwe ipasavyo.”

Kutokana na hatua hiyo ya ofisi ya Waziri Mkuu, inaelezwa kuwa viongozi waandamizi wa Wizara ya Miundombinu hivi karibuni wamelazimika kukutana kujadili suala hilo na hasa utendaji unaodaiwa kuwa mbovu wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANROADS, Ephraim Mrema, pamoja na kuwapo taarifa za kulindana na baadhi ya watu kuelezwa kumuogopa mtendaji huyo.

Katika gazeti la Raia Mwema la Machi 24, mwaka huu, iliripotiwa kuwa uongozi wa Mrema umeibua migogoro ambayo baadhi imefikishwa mahakamani ikiwa ni kati ya TANROADS na kampuni mbalimbali za ujenzi zilizopangwa kujenga barabara katika mikoa tofauti nchini.

Kutokana na vielelezo mbalimbali, gazeti hili liliripoti kuwa hasara inayotarajiwa kulikabili Taifa kutokana na mazingira hayo ya uongozi unaotajwa kuwa mbovu ni takriban Sh bilioni 250, na chanzo cha hali hiyo ni kukatisha au kusimamisha miradi kadhaa ya barabara kinyume cha taratibu.

Kwa mujibu wa habari hiyo, kiwango hicho cha fedha kinatarajiwa kulipwa kwa wakandarasi waliongia mikataba ya uhandisi (consultancy services) na mikataba ya ujenzi wa barabara.

Kwa mujibu wa nyaraka, baadhi ya mikataba imekatishwa kutokana na sababu zinazoweza kutajwa kuwa ni mizengwe ama maslahi binafsi. Tayari wakandarasi hao, baadhi wakiwa wa kimataifa, wamewasilisha mashitaka yao katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (Arbitration Court) katika nchi za Ufaransa, jijini Paris na Uingereza, jijini London. Mashitaka mengine yamo kwenye mahakama za usuluhishi Tanzania.

Uchambuzi wa awali wa wataalamu unabainisha kuwa TANROADS italazimika kuwalipa wakandarasi na watalaamu washauri (consultancy) wenye mgogoro nao kiasi cha Sh bilioni 250.

Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa barabara zinazohusishwa kuibua hasara hiyo ni pamoja na ile ya Marangu-Rombo Mkuu na Mwika-Kilacha ambako TANROADS iliingia mkataba wa Sh bilioni 23.4.

Mgogoro uliopo katika ujenzi huo wa kuboresha barabara hiyo unatokana na mkandarasi kufukuzwa kwenye eneo la ujenzi akidaiwa kushindwa kutimiza wajibu wake.

Mgogoro mwingine ni kati ya TANROADS na kampuni ya PRISMO-BADR, ulioko katika Mahakama Kuu ya Tanzania, ukihusisha madai ya malipo ya awali na udhamini.

Orodha ya migogoro pia inahusisha Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na TANROADS, mgogoro huo kwa sasa upo kwenye Mahakama ya Biashara na TANROADS inadai kurejeshewa malipo ya awali na dhamana kutoka benki hiyo. Hapa, Tanroad inadai Sh bilioni 6.3.

Mgogoro mwingine unahusisha Shirika la China Estate Construction Eng. (CSCEC), ukihusisha kuboresha kiwango cha barabara ya Kigoma-Lusahunga, deni likiwa Sh bilioni 46.8.

Eneo jingine ni la mkataba wa Sh bilioni 1.39 kati ya kampuni ya Norconsult AS dhidi ya TANROADS, ukihusu utoaji huduma ya usimamizi kwa ajili ya kuinua kiwango cha barabara ya Geita-Sengerema na Sengerema-Usagara.

Kampuni nyingine katika mgogoro na TANROADS ni pamoja na Roughton International, Kundasingh, Shabbirdin & Associate na Grineker-LTA Ltd.

Kampuni nyingine ni Konoike iliyoingia mkataba wa Sh bilioni 103.47 na TANROADS. Mkataba huo ulihusu kubuni na kujenga barabara ya Dodoma-Manyoni.

Shauri la kampuni ya Konoike na TANROADS kwa sasa liko katika Mahakama ya Usuluhishi jijini London, Uingereza, na kampuni hiyo inatajwa kufukuzwa kwenye eneo la ujenzi kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya mkataba.
 
Sasa ndio mna amka! Loss of that scale unaamshwa na taarifa za magazeti! That means ulikuwa huoni ubabaishaji uliokuwa unaeendelea! Kasi ya ujenzi wa barabara virtualy ilisimama punde mhe alikabidhiwa nchi! and you just cant see something was very wrong? Mbona wengine wanafanya na kazi zao zinaonekana? Wakati wa Dr Pombe kazi zilikuwa zinaenda!

Kweli viongozi wetu ni vipofu kiasi hiki?
 
Back
Top Bottom