Ephraim Mrema na Ufisadi TANROADS

naona sasa bongo WIZI UMEHALALISHWA!tena umewekewa pambio zuri la neno''ufisadi''
 
75 Bilion anakula mtu mmoja du, sie wengine tukipata hiyo tunge wehuka na hata kuacha kazi tehetehe.
na labda unalewa na kufa kabisa kwikwikwikwi

ndiyo maana chenge alisema ile billion yake ni vijisent
 
Nina mashaka sana na maelezo ya aliyeanzisha thread hii. Kwanza, kwenye projects za TANROADS barabara hii haipo. Nenda kwenye website ya TANROADS ufungue "projects". Haimo. Pili, mchakato wa kupata tenda, kumuondoa mkandarasi na kumweka mwingine hauko rahisi kiasi ambacho mwanzishaji wa thread hii anataka tuelewe. Taratibu za tenda hazimruhusu Mrema pekee kufanya maamuzi kiasi hicho bila kushirikisha kamati ya tenda ya TANROADS. Sheria ya manunuzi inaeleza wazi namna ya kumuondoa, kumtangaza mkandarasi mpya na kadhalika. Sio rahisi kiasi hicho.
Hata kama kungekuwa na mabadiliko ya mkandarasi, tenda ingetangazwa upya na kuna uwezekano mkubwa washindani wapya wakatoa bei kubwa zaidi kwa sababu ya mabadiliko ya bei za vitu.
Kwa taratibu za tenda za sasa tenda huwa ni fixed (yaani fixed priced tender). Hakuna variations kama huyu bwana anavyotaka tuamini.
Hivyo basi hata kama kuna chuki kumhusu Bwana Mrema kuwe na ukweli kiasi fulani.
 
Last edited:
kama nilivyosema hii thread haina ukweli kabla hata sijaingia katika web ya tanroads,huyu mtuma thread seems anakisa chake kingine na mzee mrema,navojua tenda hizi zinaweza kuchukua hata 5yrs kuwekwa ktk action,sasa inabidi watu watoe ukweli ktk hii forum au kama haujui undani wa kitu uliza uambiwe km kuna mwenye uelewa tutajua hapahapa JF watu sio wachoyo
 
Inaeleka una insight ya taarifa za huo upande mwingine. Utatusaidia sana iwapo utazimwaga hapa
 
MKURUGENZI Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads), Ephraem Mrema ameumbuliwa bungeni, kuwa amepewa wadhifa huo kinyume cha taratibu.

Mbunge wa Kasulu Magharibi, Kilontsi Mporogomyi (CCM) alisema Mrema hana taaluma ya uhandisi ujenzi, huku analipwa mamilioni ya fedha za Watanzania.

Mporogomyi ndiye aliyeweka hadharani habari za Mkurugenzi huyo kuingizwa kwenye madaraka hayo kupitia mlango wa nyuma; huku wataalamu ambao walipendekezwa na jopo la usaili wakiwekwa pembeni.

“Ninavyojua huyu Mrema hakuwa amependekezwa na jopo la usaili, hatujui alikotokea hadi akawekwa pale…naomba waziri useme juu ya ajira ya mkurugenzi huyu,” alisema wakati akichangia katika hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa.

Mporogomyi aliliambia Bunge kuwa sifa za mkurugenzi huyo ni kwamba ni mshauri wa mambo ya ununuzi na kabla ya kushika wadhifa huo, alikuwa anafanya shughuli zake visiwani Zanzibar.

Hata hivyo, Mrema mwenyewe alijitetea kuwa ana shahada ya kwanza ya ukandarasi uchumi (Construction Economics) na shahada ya pili ya Menejimenti ya miradi (Project Management) aliyoipata mwaka 1987. Hata hivyo, hakutaja vyuo alikopata shahada hizo.

Aliwataja wahandisi ambao walipendekezwa na jopo la usaili kuwa ni Boniface Nyiti, Venance Ndyamkama na mwingine aliyemtaja kwa jina la moja la Chacha. “Hawa ndiyo ambao walipendekezwa na ni wahandisi wa siku nyingi pale Tanroads; lakini huyu mkurugenzi alikotolewa na kuwekwa pale haijulikani.”

Mrema alichukua wadhifa wa mkurugenzi aliyekuwa anatokea Ghana ambaye alimaliza muda wake mwaka 2006. Mporogomyi alisema mkurugenzi wa sasa aliingizwa kwa misingi ya ufisadi.

Mbunge huyo aliongeza kuwa mara tu baada ya kupata wadhifa huo, alianza kuwanyanyasa wahandisi hao wenye sifa na akawahamishia wizarani ambako pia walirudishwa na wizara Tanroads. “Wizara ilisema hawa ni mawakala wa ujenzi wa barabara wakawarudisha.”

Alisema Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu wakati inawarejesha kwa Tanroads, ilishauri wapewe mikoa ya kuongoza, lakini kuwa tayari nafasi hizo zilishajazwa na watu wengine Mrema hakuweza kutekeleza agizo hilo.

Alisema alibaki nao makao makuu na wanalipwa fedha nyingi huku wakiwa hawana kazi za kufanya. Alisema kuwa mkurugenzi huyo baada ya kuona wahandisi hao ni tishio katika ajira yake, sasa ameingiza utaratibu mpya wa ajira za mikataba.

Mporogomyi alisema mpango huo mpya unafanywa na mkurugenzi huyo kwa nia ya kuwaengua wafanyakazi wote ambao anaona kama ni tishio kwake, hasa wale wahandisi wenye sifa za kushika wadhifa wake huo.

“Kibaya zaidi pamoja na kuingia kwa mlango wa nyuma, lakini ananyanyasa wafanyakazi,” alisema mbunge huyo huku akimtaka Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu amweleze namna mkurugenzi huyo alivyoingizwa kwenye nafasi hiyo nyeti na ikiwezekana aondolewe haraka.

Lakini pia alisema mkurugenzi huyo analipwa fedha nyingi kama vile ni mtaalamu ambaye ameajriwa kutoka nje ya nchi.

Aliweka hadharani viwango hivyo kuwa Mrema alipoanza kazi alipewa posho ya kuanza (Commencement allowance) dola za Marekani 9,000 kwa siku 60 (sawa na Sh milioni 10.8), mshahara wake kwa mwezi ni dola za Marekani 8,500 (Sh milioni 10.2), posho ya nyumba kwa mwezi ni dola 2,200 (Sh milioni 2.6), posho ya matibabu dola 400 kwa mwezi (Sh 480,000), posho ya usafiri dola 500 (Sh 600,000).

Pia analipwa pensheni kwa mwaka kiasi cha dola za Marekani 10,200 (Sh milioni 12.4), akienda likizo analipwa dola 3,000 (Sh milioni 3.6), bonasi yake kwa mwaka analipwa dola 102,000 (Sh milioni 122.4) na mwisho wa mkataba wake analipwa dola 10,000 (Sh milioni 12) kama malipo ya kumaliza kazi.

Mporogomyi alisema pamoja na fedha nyingi anazolipwa mkurugenzi huyo; lakini bado anajihusisha na vitendo vya ufisadi zinavyosababisha wakati mwingine awanyanyase na kuwafukuza wafanyakazi ambao wanatenda haki.

Mbunge huyo alitoa mfano kuwa kuna mfanyakazi aliyemtaja kwa jina moja la Mabuye ambaye alikuwa anafanya kazi katika mizani ya Kibaha. Alisema siku moja mfanyakazi huyo alikamata malori ambayo yalikuwa yamezidisha uzito wa bidhaa walizobeba.

Alisema aliyazuia na kuwataka walipe faini ya Sh milioni 18, lakini matajiri wa yale malori walipoambiwa kukamatwa kwa magari yao walimpigia simu na yeye akaamuru Mabuye afukuzwe kazi.

Mporogomyi alisema Mrema alimpigia simu meneja wa Tanroads mkoa wa Pwani ili amfukuze na aliposita alimtishia kwa simu kuwa afanye hivyo haraka, kwani hataki kumwona huyo mfanyakazi akiendelea na kazi.

“Kama siyo ufisadi hiki nini, yaani mfanyakazi ambaye anafanya kazi kwa misingi ya sheria unamfukuza kazi, sababu ni nini hapa? Alihoji mbunge huyo na kusisitiza kutaka maelezo ya kina kutoka kwa Waziri wa Miundombinu.
 
Nina mashaka sana na maelezo ya aliyeanzisha thread hii. Kwanza, kwenye projects za TANROADS barabara hii haipo. Nenda kwenye website ya TANROADS ufungue "projects". Haimo. Pili, mchakato wa kupata tenda, kumuondoa mkandarasi na kumweka mwingine hauko rahisi kiasi ambacho mwanzishaji wa thread hii anataka tuelewe. Taratibu za tenda hazimruhusu Mrema pekee kufanya maamuzi kiasi hicho bila kushirikisha kamati ya tenda ya TANROADS. Sheria ya manunuzi inaeleza wazi namna ya kumuondoa, kumtangaza mkandarasi mpya na kadhalika. Sio rahisi kiasi hicho.
Hata kama kungekuwa na mabadiliko ya mkandarasi, tenda ingetangazwa upya na kuna uwezekano mkubwa washindani wapya wakatoa bei kubwa zaidi kwa sababu ya mabadiliko ya bei za vitu.
Kwa taratibu za tenda za sasa tenda huwa ni fixed (yaani fixed priced tender). Hakuna variations kama huyu bwana anavyotaka tuamini.
Hivyo basi hata kama kuna chuki kumhusu Bwana Mrema kuwe na ukweli kiasi fulani.

Congo,
Mashaka na taarifa hii ondoa! ILA mimi ndiye nina mashaka nawe....!

Unastaajabisha kuangalia taarifa kama hii kwenye mtandao wa TANROADS..! tangu lini TZ wakawa uptodate hivyo?

Kwa taarifa yako Mradi upo kutoka Kagera kuelekea Kigoma MUHUTWE - KAGOMA - KYAMRORWA - BIHARAMULO - LUSAHUNGA, hivyo ni vituo ndani ya mradi...UPO HAPO?

Kwani tulipomwajibisha LOWASA kwa Richimond yeye si ndo alikuwa kiongozi? Masha anavyotesa na vitambilisho vya uraia .. yeye si ndo kiongozi? list ndeeeefu, KWANINI usielewe kuwa MREMA kala yeye kwa ubabe wake? wa kufukuza wakandarasi na kuengage wengine aliokuwa karibu yao? au hujui wadanganyika tunavyodanganyika?

TAFUTA TAARIFA UTAPATA TAARIFA!
 
Kuna siku tunaweza kuvikimbia vivuli vyetu wenyewe kwa haya mambo tunayoyafanya. Mpaka lini tutaendelea kuihujumu nchi yetu?Watu wengi wanalalamika rushwa imekithiri kwenye utoaji wa tender za ujenzi.Ni kweli procedures zote za tender zinafuatwa ila kuna watu huwa wanaandaliwa with all inside information ambazo wakiziweka lazima watapata tender bila shida. Rushwa Rushwa Rushwa itatumaliza.Sishangai kuona tuhuma hizi kwa bosi wa Tanroad. Hii si mara ya kwanza. Zimesemwa sana shida zake tena mpaka bungeni
 
Contractors wengi wa KiChina walikuja /engaged wakati Magufuli ni Waziri wa Infrastructure. Performance yao imekuwa hovyo.(Barabara ya Mlimani, Ruvu Bridge, Shinyanga). Huwa wanaquote hela ndogo ukilinganisha na kazi yenyewe na ndiyo maana utakuta mikataba yao inavunjwa na kupewa wengine. Hii ndiyo "faida" ya lowest bidder.
 
Mi sijawahi ona. ERB na CRB wako wapi? au wao wanakazi nyingine.
 
Contractors wengi wa KiChina walikuja /engaged wakati Magufuli ni Waziri wa Infrastructure. Performance yao imekuwa hovyo.(Barabara ya Mlimani, Ruvu Bridge, Shinyanga). Huwa wanaquote hela ndogo ukilinganisha na kazi yenyewe na ndiyo maana utakuta mikataba yao inavunjwa na kupewa wengine. Hii ndiyo "faida" ya lowest bidder.

Bw. Heri,

Magufuli kakosa wapi hapa?

Je unajua kuwa mkandarasi aliyezawadiwa hiyo kazi kwa 192Bilion ya kujenga 100km ni MCHINA? anaitwa CHICO, kwani hizo zingine 50km zilishafanyika kwa kiwango kikubwa na mkandarasi wa awali?

Tafakari then leta hoja......tutafika kweli kwa kujenga 1km ya lami kwa 1.4Bilion? ...hayo mahesabu umeyafanya? Kwakweli huyo MREMA na watendaji wa juu MIUNDOMBINU akiwemo CHAMBO niwala rushwa wakubwa!!!!!
 
Hapo kaka suala si the lowest bidder, kamati za tender zinazokaa zinazingatia viwango husika vya mkandarasi bora ili kupata huduma bora, kilichopo kikubwa ni mkandarasi gani anaetoa asilimia kumi (10%) nzuri na bila mlolongo!

Kwa hivyo basi, kwa kuwa wachina ni watu waliozoea mambo ya milango ya nyuma na hawana shida katika kumwaga 10% basi unakuta wanashinda tender nyingi.

Kilichopo ni viongozi wetu kuwa makini na maamuzi ya mashirika yetu katika kuchagua wakandarasi, na ikibidi kuwe na ukaguzi wa kina wa wakandarasi husika kabla ya kuwapatia kazi.
 
Bhaghosha,

Ila iposiku wananchi watajichukulia sheria mkononi mtaja shangaaa wenyewe msi-washtue waacheni watakuja gundua kwamba twaja huko huko kuwata tandika bakora nadhani nyie mwajionea sasa serikali imeanza ule mchezo wa ruksaaaa kila mtu ale anavyo jua ati, nawambieni mtakuja shangaaeni wenyewe mwanya mkubwa kati ya matajiri na maskini utawaliza hao MAFISADI kweli mtu mmoja anakula 75 Billions kama ni kweli nikikuta anatandikwa njiani simwokoi ng'ooooo huwezi fanya mambo kama hayo hawaoni aibu jamani hii nchi mwataka ipeleka wapi kwenye vita au nadhani huko ndiko mwaatayarishia mazingira hayo watanzania itakuwa aibu kweli, UTAWALA WA SHERIA NA DEMOCRASIA SWAFI IKO WAPI jamani. Kama kweli we black africans twatendeana kwa hari hii sishangai wahindi wakija au kuajiliwa humu nchini mwetu na kutunyanyasa na kufanya hali iwe kama tuko enzi za Slavely,mifano mizuri nendeni mahotelini viwandani huko wahindi wameajiliwa kama njugu na wanapewa nafasi za juu ati wao ndio wanao aminiwa sana, duh iwapo kama huyu mtanzania mwenzetu anafanya mafyongo kama haya iweje hao wahindi wasitushangae na kututenda kama watakavyo??. kweli hiili ndilo latufanya tudharaulike au tudhalauriane nandio maana twatendeana haya, ila 2010 ndio majibu yatatoka subirini
 
Huu ufisadi sasa umekuwa ni kawaida, kila kona ya nchi kuna ufisadi. I wish tungekuwa na sheria kama za China makosa ya aina hii yapewe adhabu ya kifo. Hatuwezi kuendelea kuona watoto wa shule wanakaa chini, wagonjwa wanalala chini mahospitalini na dawa hakuna, maji safi tabu, umeme wa mgao, barabara mbovu halafu kikundi cha watu wachache wanajichukulia mamilioni hadi mabilioni ya watanzania kwa manufaa binafsi.

Kibaya zaidi haya mafisadi yanatumia pesa waliyotuibia kufunga miradi na sisi wananchi tunawapongeza kwa kuinvest nyumbani ebo hii pesa si yetu kwa nini wasifilisiwe ikatumika kuleta maendeleo ya nchi.
 
haya ndio maisha ya kibongo na watendaji wetu, maana unakuta mtu kasomea engineering ankwenda kuwa counter wa bank, so hilo sioni hatari
 
Bosi wa Tanroads aitunishia serikali msuli

Na Restuta James

13th November 2009

email.png

B-pepe

printer.png

Chapa

comment_bubble.png

Maoni

headline_bullet.jpg
Awabandua wakurugenzi watatu
headline_bullet.jpg
Wamo mameneja watatu wa mikoa

Tanroad%282%29.jpg

Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads).

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Ephraem Mrema, ameitunishia misuli bodi ya wakurugenzi ya taasisi hiyo na Wizara ya Miundombinu kwa kupuuza maagizo halali yaliyotolewa kwake.
Kinyume cha maelekezo ya wakuu wake kwamba asiwafukuze kazi wakurugenzi na mameneja wa mikoa bila kufuata taratibu za utumishi serikalini, Mrema ambaye awali alitii agizo hilo na kusitisha uamuzi wake, baadaye aligeuka tena na kuendelea na maamuzi yake ambayo sasa yameamsha taharuki kubwa ndani ya taasisi hiyo yenye dhima ya kujenga na kusimamia matunzo ya barabara kuu nchini.
Sakata hili ambalo sasa linaonekana kama ni mapambano ya kimamlaka kati ya Mrema, Bodi ya Tanroads na Wizara mama, lilianza Oktoba 30, mwaka huu, baada ya kiongozi huyo kuitisha kikao cha wafanyakazi na kutangaza kuwafukuza kazi baadhi ya watendaji waandamizi ambao ni Mkurugenzi wa Matengenezo ya Barabara, Thomas Mosso; Mkurugenzi wa Mipango, Jason Rwiza na mameneja wa mikoa mitatu ya Dodoma, Gerson Lwenge; Morogoro, Charles Madinda na wa Ruvuma, Abraham Kissimbo. Pia kwenye orodha hiyo yupo William Shilla ambaye ni mhandisi makao makuu Tanroads.
Habari zilisema kwamba watendaji hao waandamizi walionyesha wazi kukataa kukubaliana na hatua hizo kwa sababu zilikuwa ni kinyume cha taratibu na hivyo wakakata rufaa wizarani.
Baada ya mamlaka hizo kupata kilio cha watendaji hao, zilitengua maamuzi ya Mrema kwa kuwa hayakuzingatia taratibu za Tanroads.
Kwa mujibu wa nyaraka za Mrema juu ya suala hilo ambazo Nipashe imeziona, kiongozi huyo
Novemba 6, mwaka huu aliwaandikia wafanyakazi wote waraka wa kutangaza kusitisha utekelezaji wa tangazo la kikao chake na wafanyakazi cha Oktoba 30, 2009 kwa kuwa alikuwa amepata maagizo kutoka Serikalini ya kusitisha tangazo lake.
"Napenda kuwajulisheni kwamba nimepata agizo la Serikali kwamba uteuzi wa wakurugenzi na viongozi wengine wa Tanroads umesitishwa, aidha," sehemu ya waraka huo inasomeka na kuongea kuwa:
"Serikali imeagiza kuwa mchakato wa uteuzi wa viongozi hao utatakiwa kufuata kanuni za ‘Executive agencies' kwa kuzingatia usawa, uwazi na ushindani…kutokana na hayo, napenda kukujulisheni kwamba mawasiliano hivi sasa yanaendelea na mamlaka husika jinsi ya kutekeleza agizo hili kulingana na muundo wa Tanroads ulioidhinishwa."
Hata hivyo, siku tatu baadaye yaani Novemba 9, Mrema aliandika waraka mwingine wa kutengua ule wa Novemba 6, akidai kuwa ulikuwa umesambazwa kwa wafanyakazi kimakosa ijapokuwa ulikuwa na saini yake.
Badala yake alisema kwamba maofisa waandamizi waliokuwa wamefutwa kazi maamuzi yake yanaendelea kama alivyokuwa ameamua na kutangaza kwa wafanyakazi wote Oktoba 30, mwaka huu, kwani alikuwa amepata baraka za mamlaka za juu.
"Nasikitika kuwajulisheni kwamba taarifa ya kusitisha utekelezaji wa waraka wa terehe 30 Oktoba 2009 ilitumwa kwenu kimakosa kabla ya kupata kibali cha mtendaji mkuu kwa hiyo waraka huu unafuta waraka wa kusitisha utekelezaji wa waraka wa Mtendaji Mkuu wa Novemba 6 na unawajulisha kwamba uteuzi wa uongozi uliotajwa Oktoba 30 umeanza kazi rasmi Novemba 1, 2009 na umepelekwa katika ngazi husika kupata baraka za mwisho," alisema Mrema katika waraka huo.
Katika waraka huo, Mrema alitangaza kusitisha mikataba ya wahandisi waandamizi sita, yaani Mosso, Rwiza, Shilla, Lwenge, Madinda na Kissimbo.
Kwa mujibu wa waraka huo, tayari nafasi za mameneja hao zinashikiliwa na wahandisi wengine ambapo Mkoa wa Dodoma unashikiliwa na Dorothy Mtenga; Morogoro, Obrien Machange, wakati Yusuph Mazana amepelekwa Ruvuma.
Hata hivyo, taarifa nyingine zinaonyesha kuwa mikataba ya wahandisi waliofukuzwa kazi ilikuwa haijamalizika wala hawakuwa wametimiza umri wa kustaafu.
Wafanyakazi ambao hawakupenda majina yao yaandikwe gazetini, waliliambia gazeti hili kuwa Mrema amekuwa akitamba kwa wafanyakazi kuwa mabadiliko yote anayofanya ndani ya wakala huo ni utekelezaji wa ahadi yake alipokuwa akipewa ajira.
Walisema awali, kila baada ya miezi mitatu, wakuu wa idara na mameneja wa Tanroads wa mikoa walikuwa na utaratibu wa kukutana katika vikao kwa ajili ya kuangalia utendaji wa wakala huo, lakini Mtendaji huyo aliufuta utaratibu huo na kueleza kuwa Tanroads haiwezi kuendeshwa kwa vikao.
Mfanyakazi mmoja wa wakala huo alidokeza kuwa kwa miaka miwili mfululizo, Mrema amekuwa akifanya mabadiliko makubwa ndani ya Tanroads na anapoulizwa anasema anadhani huo ndio utendaji bora.
Mwandishi wa habari hizi alipoomba kukutana na Mrema jana, alielezwa kuwa yupo kwenye kikao nje ya ofisi na kwamba asingeweza kurudi ofisini mapema.
Gazeti hili lilipomtafuta Mwenyekiti wa Bodi ya Tanroads, Abel Mwaisumo, ili kuzungumzia madai hayo, lilielezwa kuwa yupo nje ya nchi kwa matitabu.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dk. Samwel Nyantahe, alithibitisha kuwa na taarifa ya Mrema kupindisha maagizo ya bodi na kusema kuwa bodi na Wizara zinakutana leo jijini Dar es Salaam kujadili suala hilo.
"Bodi imekwishapokea ‘allegations' (madai) yote kutoka kwa wafanyakazi na sisi tunayafanyia kazi, tulikutana Jumatatu tulijadiliana na kesho (leo) tutakutana tena, hii yote ni kuhakikisha kuwa tunayapatia ufumbuzi matatizo haya," alisema Dk. Nyantahe.

CHANZO: NIPASHE

0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni

adlog.php

Habari Zaidi
Articles

CCM yamruka Sophia Simba

Chiligati: Sijawahi kumbeza Sitta

Marekani yawapongeza Seif, Karume

Lori laparamia nyumba, laua watu watano Iringa

Lipumba awasindikiza washtakiwa kortini

Walimu wasitisha mgomo, baadhi wasusia

Mitambo zaidi ya IPTL yashindikana kuwashwa

Waingereza waadhimisha miaka 10 kifo cha Nyerere
 
Bosi wa Tanroads aitunishia serikali msuli

Na Restuta James

13th November 2009

headline_bullet.jpg
Awabandua wakurugenzi watatu
headline_bullet.jpg
Wamo mameneja watatu

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Ephraem Mrema, ameitunishia misuli bodi ya wakurugenzi ya taasisi hiyo na Wizara ya Miundombinu kwa kupuuza maagizo halali yaliyotolewa kwake.
Kinyume cha maelekezo ya wakuu wake kwamba asiwafukuze kazi wakurugenzi na mameneja wa mikoa bila kufuata taratibu za utumishi serikalini, Mrema ambaye awali alitii agizo hilo na kusitisha uamuzi wake, baadaye aligeuka tena na kuendelea na maamuzi yake ambayo sasa yameamsha taharuki kubwa ndani ya taasisi hiyo yenye dhima ya kujenga na kusimamia matunzo ya barabara kuu nchini.
Sakata hili ambalo sasa linaonekana kama ni mapambano ya kimamlaka kati ya Mrema, Bodi ya Tanroads na Wizara mama, lilianza Oktoba 30, mwaka huu, baada ya kiongozi huyo kuitisha kikao cha wafanyakazi na kutangaza kuwafukuza kazi baadhi ya watendaji waandamizi ambao ni Mkurugenzi wa Matengenezo ya Barabara, Thomas Mosso; Mkurugenzi wa Mipango, Jason Rwiza na mameneja wa mikoa mitatu ya Dodoma, Gerson Lwenge; Morogoro, Charles Madinda na wa Ruvuma, Abraham Kissimbo. Pia kwenye orodha hiyo yupo William Shilla ambaye ni mhandisi makao makuu Tanroads.
Habari zilisema kwamba watendaji hao waandamizi walionyesha wazi kukataa kukubaliana na hatua hizo kwa sababu zilikuwa ni kinyume cha taratibu na hivyo wakakata rufaa wizarani.
Baada ya mamlaka hizo kupata kilio cha watendaji hao, zilitengua maamuzi ya Mrema kwa kuwa hayakuzingatia taratibu za Tanroads.
Kwa mujibu wa nyaraka za Mrema juu ya suala hilo ambazo Nipashe imeziona, kiongozi huyo
Novemba 6, mwaka huu aliwaandikia wafanyakazi wote waraka wa kutangaza kusitisha utekelezaji wa tangazo la kikao chake na wafanyakazi cha Oktoba 30, 2009 kwa kuwa alikuwa amepata maagizo kutoka Serikalini ya kusitisha tangazo lake.
"Napenda kuwajulisheni kwamba nimepata agizo la Serikali kwamba uteuzi wa wakurugenzi na viongozi wengine wa Tanroads umesitishwa, aidha," sehemu ya waraka huo inasomeka na kuongea kuwa:
"Serikali imeagiza kuwa mchakato wa uteuzi wa viongozi hao utatakiwa kufuata kanuni za ‘Executive agencies' kwa kuzingatia usawa, uwazi na ushindani…kutokana na hayo, napenda kukujulisheni kwamba mawasiliano hivi sasa yanaendelea na mamlaka husika jinsi ya kutekeleza agizo hili kulingana na muundo wa Tanroads ulioidhinishwa."
Hata hivyo, siku tatu baadaye yaani Novemba 9, Mrema aliandika waraka mwingine wa kutengua ule wa Novemba 6, akidai kuwa ulikuwa umesambazwa kwa wafanyakazi kimakosa ijapokuwa ulikuwa na saini yake.
Badala yake alisema kwamba maofisa waandamizi waliokuwa wamefutwa kazi maamuzi yake yanaendelea kama alivyokuwa ameamua na kutangaza kwa wafanyakazi wote Oktoba 30, mwaka huu, kwani alikuwa amepata baraka za mamlaka za juu.
"Nasikitika kuwajulisheni kwamba taarifa ya kusitisha utekelezaji wa waraka wa terehe 30 Oktoba 2009 ilitumwa kwenu kimakosa kabla ya kupata kibali cha mtendaji mkuu kwa hiyo waraka huu unafuta waraka wa kusitisha utekelezaji wa waraka wa Mtendaji Mkuu wa Novemba 6 na unawajulisha kwamba uteuzi wa uongozi uliotajwa Oktoba 30 umeanza kazi rasmi Novemba 1, 2009 na umepelekwa katika ngazi husika kupata baraka za mwisho," alisema Mrema katika waraka huo.
Katika waraka huo, Mrema alitangaza kusitisha mikataba ya wahandisi waandamizi sita, yaani Mosso, Rwiza, Shilla, Lwenge, Madinda na Kissimbo.
Kwa mujibu wa waraka huo, tayari nafasi za mameneja hao zinashikiliwa na wahandisi wengine ambapo Mkoa wa Dodoma unashikiliwa na Dorothy Mtenga; Morogoro, Obrien Machange, wakati Yusuph Mazana amepelekwa Ruvuma.
Hata hivyo, taarifa nyingine zinaonyesha kuwa mikataba ya wahandisi waliofukuzwa kazi ilikuwa haijamalizika wala hawakuwa wametimiza umri wa kustaafu.
Wafanyakazi ambao hawakupenda majina yao yaandikwe gazetini, waliliambia gazeti hili kuwa Mrema amekuwa akitamba kwa wafanyakazi kuwa mabadiliko yote anayofanya ndani ya wakala huo ni utekelezaji wa ahadi yake alipokuwa akipewa ajira.
Walisema awali, kila baada ya miezi mitatu, wakuu wa idara na mameneja wa Tanroads wa mikoa walikuwa na utaratibu wa kukutana katika vikao kwa ajili ya kuangalia utendaji wa wakala huo, lakini Mtendaji huyo aliufuta utaratibu huo na kueleza kuwa Tanroads haiwezi kuendeshwa kwa vikao.
Mfanyakazi mmoja wa wakala huo alidokeza kuwa kwa miaka miwili mfululizo, Mrema amekuwa akifanya mabadiliko makubwa ndani ya Tanroads na anapoulizwa anasema anadhani huo ndio utendaji bora.
Mwandishi wa habari hizi alipoomba kukutana na Mrema jana, alielezwa kuwa yupo kwenye kikao nje ya ofisi na kwamba asingeweza kurudi ofisini mapema.
Gazeti hili lilipomtafuta Mwenyekiti wa Bodi ya Tanroads, Abel Mwaisumo, ili kuzungumzia madai hayo, lilielezwa kuwa yupo nje ya nchi kwa matitabu.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dk. Samwel Nyantahe, alithibitisha kuwa na taarifa ya Mrema kupindisha maagizo ya bodi na kusema kuwa bodi na Wizara zinakutana leo jijini Dar es Salaam kujadili suala hilo.
"Bodi imekwishapokea ‘allegations' (madai) yote kutoka kwa wafanyakazi na sisi tunayafanyia kazi, tulikutana Jumatatu tulijadiliana na kesho (leo) tutakutana tena, hii yote ni kuhakikisha kuwa tunayapatia ufumbuzi matatizo haya," alisema Dk. Nyantahe.

CHANZO: NIPASHE

http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=9728
 
Back
Top Bottom