Ephraim Mrema na Ufisadi TANROADS

Ngereja

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
798
333
Nimeona ni vyema kuanzisha mada hii kwa ajili ya haya yaliyojiri bungeni kuhusu Afisa mtendaji mkuu wa TANROADS,Epharaim Mrema ilipostiwa mahali ambako nadhani isingepata attention inayostahili.

Je, hapa kuna ufisadi?Shadrack Sagati, Dodoma

HabariLeo; Ijumaa,July 04, 2008

MKURUGENZI Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads), Ephraem Mrema ameumbuliwa bungeni, kuwa amepewa wadhifa huo kinyume cha taratibu.

Mbunge wa Kasulu Magharibi, Kilontsi Mporogomyi (CCM) alisema Mrema hana taaluma ya uhandisi ujenzi, huku analipwa mamilioni ya fedha za Watanzania.

Mporogomyi ndiye aliyeweka hadharani habari za Mkurugenzi huyo kuingizwa kwenye madaraka hayo kupitia mlango wa nyuma; huku wataalamu ambao walipendekezwa na jopo la usaili wakiwekwa pembeni.

“Ninavyojua huyu Mrema hakuwa amependekezwa na jopo la usaili, hatujui alikotokea hadi akawekwa pale…naomba waziri useme juu ya ajira ya mkurugenzi huyu,” alisema wakati akichangia katika hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa.

Mporogomyi aliliambia Bunge kuwa sifa za mkurugenzi huyo ni kwamba ni mshauri wa mambo ya ununuzi na kabla ya kushika wadhifa huo, alikuwa anafanya shughuli zake visiwani Zanzibar.

Hata hivyo, Mrema mwenyewe alijitetea kuwa ana shahada ya kwanza ya ukandarasi uchumi (Construction Economics) na shahada ya pili ya Menejimenti ya miradi (Project Management) aliyoipata mwaka 1987. Hata hivyo, hakutaja vyuo alikopata shahada hizo.

Aliwataja wahandisi ambao walipendekezwa na jopo la usaili kuwa ni Boniface Nyiti, Venance Ndyamkama na mwingine aliyemtaja kwa jina la moja la Chacha. “Hawa ndiyo ambao walipendekezwa na ni wahandisi wa siku nyingi pale Tanroads; lakini huyu mkurugenzi alikotolewa na kuwekwa pale haijulikani.”

Mrema alichukua wadhifa wa mkurugenzi aliyekuwa anatokea Ghana ambaye alimaliza muda wake mwaka 2006. Mporogomyi alisema mkurugenzi wa sasa aliingizwa kwa misingi ya ufisadi.

Mbunge huyo aliongeza kuwa mara tu baada ya kupata wadhifa huo, alianza kuwanyanyasa wahandisi hao wenye sifa na akawahamishia wizarani ambako pia walirudishwa na wizara Tanroads. “Wizara ilisema hawa ni mawakala wa ujenzi wa barabara wakawarudisha.”

Alisema Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu wakati inawarejesha kwa Tanroads, ilishauri wapewe mikoa ya kuongoza, lakini kuwa tayari nafasi hizo zilishajazwa na watu wengine Mrema hakuweza kutekeleza agizo hilo.

Alisema alibaki nao makao makuu na wanalipwa fedha nyingi huku wakiwa hawana kazi za kufanya. Alisema kuwa mkurugenzi huyo baada ya kuona wahandisi hao ni tishio katika ajira yake, sasa ameingiza utaratibu mpya wa ajira za mikataba.

Mporogomyi alisema mpango huo mpya unafanywa na mkurugenzi huyo kwa nia ya kuwaengua wafanyakazi wote ambao anaona kama ni tishio kwake, hasa wale wahandisi wenye sifa za kushika wadhifa wake huo.

“Kibaya zaidi pamoja na kuingia kwa mlango wa nyuma, lakini ananyanyasa wafanyakazi,” alisema mbunge huyo huku akimtaka Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu amweleze namna mkurugenzi huyo alivyoingizwa kwenye nafasi hiyo nyeti na ikiwezekana aondolewe haraka.

Lakini pia alisema mkurugenzi huyo analipwa fedha nyingi kama vile ni mtaalamu ambaye ameajriwa kutoka nje ya nchi.

Aliweka hadharani viwango hivyo kuwa Mrema alipoanza kazi alipewa posho ya kuanza (Commencement allowance) dola za Marekani 9,000 kwa siku 60 (sawa na Sh milioni 10.8), mshahara wake kwa mwezi ni dola za Marekani 8,500 (Sh milioni 10.2), posho ya nyumba kwa mwezi ni dola 2,200 (Sh milioni 2.6), posho ya matibabu dola 400 kwa mwezi (Sh 480,000), posho ya usafiri dola 500 (Sh 600,000).

Pia analipwa pensheni kwa mwaka kiasi cha dola za Marekani 10,200 (Sh milioni 12.4), akienda likizo analipwa dola 3,000 (Sh milioni 3.6), bonasi yake kwa mwaka analipwa dola 102,000 (Sh milioni 122.4) na mwisho wa mkataba wake analipwa dola 10,000 (Sh milioni 12) kama malipo ya kumaliza kazi.

Mporogomyi alisema pamoja na fedha nyingi anazolipwa mkurugenzi huyo; lakini bado anajihusisha na vitendo vya ufisadi zinavyosababisha wakati mwingine awanyanyase na kuwafukuza wafanyakazi ambao wanatenda haki.

Mbunge huyo alitoa mfano kuwa kuna mfanyakazi aliyemtaja kwa jina moja la Mabuye ambaye alikuwa anafanya kazi katika mizani ya Kibaha. Alisema siku moja mfanyakazi huyo alikamata malori ambayo yalikuwa yamezidisha uzito wa bidhaa walizobeba.

Alisema aliyazuia na kuwataka walipe faini ya Sh milioni 18, lakini matajiri wa yale malori walipoambiwa kukamatwa kwa magari yao walimpigia simu na yeye akaamuru Mabuye afukuzwe kazi.

Mporogomyi alisema Mrema alimpigia simu meneja wa Tanroads mkoa wa Pwani ili amfukuze na aliposita alimtishia kwa simu kuwa afanye hivyo haraka, kwani hataki kumwona huyo mfanyakazi akiendelea na kazi.

“Kama siyo ufisadi hiki nini, yaani mfanyakazi ambaye anafanya kazi kwa misingi ya sheria unamfukuza kazi, sababu ni nini hapa? Alihoji mbunge huyo na kusisitiza kutaka maelezo ya kina kutoka kwa Waziri wa Miundombinu.
 
wala sishangai tena nimekataa!
Kwa hiyo ndio kusema kwamba mshahara hausaidii mtu kufanya kazi kwa uwajibikaji?
au tusemeje?
manake Tanroads siku hizi ni kama kijiwe fulani hivi.
Mishahara mikubwa barabara hakuna.
mie sijali sana mishahara, ila kwanini alipwe dola?
pia kwa nini hafanyi basi kazi?
 
Nimeona ni vyema kuanzisha mada hii kwa ajili ya haya yaliyojiri bungeni kuhusu Afisa mtendaji mkuu wa TANROADS,Epharaim Mrema ilipostiwa mahali ambako nadhani isingepata attention inayostahili.

Je, hapa kuna ufisadi?

mmh haya makubwa madogo yana nafuu,ila nachofurahi hapa tukianza kusemana bila woga hivi nchi itapiga hatua
 
Suala la package linakuwepo wakati wa kutafuta mtu wa kufanya kazi yoyote, ili kupata washindani wa kutosha huwa inakuwepo package ya kuvutia. Hivyo suala la malipo 'makubwa' ya CEO wa TANROADS (au taasisi nyingine yoyote) sio kosa la CEO.

Suala alilosema Mhe. Mporogomnyi kwamba anatishia watu wanaofanya kazi zao ipasavyo naliona ni suala kubwa linastahili uchunguzi na maamuzi yafanyike kwa kuzingatia uchunguzi huo.

Kuna mwana JF anajua mchakato wa kumpata huyu CEO wa TANROADS ulivyokua? Kwamba tangazo lilitolewa lini na wapi? Vilitakiwa vigozo gani? Kina nani waliomba? Waliopitishwa kwenye usahili?
 
shaloom wandugu,

Hayo ya Kilaza Mrema yalishasemwa sana hapa, na jinsi alivyoifanya tanroads mali ya wachagga!

Kwakweli ana maamuzi ya kimangimangi hasa tena wakati mwingine ya kitoto!

Lakini hayo yote ni kwakuwa alipata hiyo chance kwa mgogo wa LOWASSA, akisaidiwa na CHENGE, bila kumsahau kakayake ambaye ni rafiki wa lowasa MREMA WA NGURUDOTO ARUSHA.

Kaanguka Lowassa, Chenge, Sasa zamu yake Mrema!
 
Kwani TANROADS kuna Biashara nyingine wanayofanya ili kuwaingizia kipato? au ni hizi fedha zetu (kodi) za kila mwezi pamoja na za wahisani za kuchangia kile kilichopungua kwenye hizi hela zetu ??? Naomba jibu waungwana kabla sijaanza kujadili hili swala...... maana naona mwili unaanza kuchemka na kutetemeka......
 
Nafikiri itatusaidia kwenye discussion ya hii thread kama tukizingatia mambo machache ya msingi:

1. Huyu Bwana Ephraem Mrema hakuamua mwenyewe kujilipa mshahara huu - ni lazima kulikuwa na kikao ambacho kiliamua hivyo based perhaps on salary history yake na mishahara wanayolipwa maCEO wengine kama wale wa TCRA; TBC; TRA; TMA; ATC; THA; TPB etc. Let us be informed how much these other CEOs are paid before starting to jump into conclusions.

2. Katika ku decide on who to employ as CEO wa TANROADS naamini kabisa kuwa huyu Bwana alikuwa interviewed pamoja na shortlisted applicants wenzake. Qualifications ni only one aspect ya selection criteria. Katika ngazi kama hii ya CEO experience carries more weight than qualifications. Nafikiri tungepewa pia experience ya huyu Bwana Mrema na aliipatia wapi pamoja na zile za hao applicants wenzake. Ikiwa kama selection criteria ilikuwa based only on basic qualifications then maprofessor wa Civil Engineering UDSM would have been given the post automatically.

3. Swala la kama Bwana Mrema ni mchagga au mnyamwezi au mnyaturu ni irrelevant - kwa mawazo yangu hiyo ni village mentality. Kwa nini mchagga hana haki ya ku apply kwa kazi kama hiyo? Tuacheni Unduli na U-fascist!

4. Pia sijui kama huyu Ephraem Mrema ana uhusiano wowote ule wa kindugu na Mrema wa Ngurdoto. The mere fact they are both called Mrema does not mean they are related. Why not link him with Mrema wa TLP? Na pili sielewi reason ya kuingiza urafiki wa Mrema wa Ngurdoto na Lowassa? Besides is it a sin in Tanzania kuwa rafiki wa Lowassa? Tuacheni Unduli.

5. Let us be objective and avoid parochialism! Ahsanteni.
 
Kudi shauri,

All in all kuna kaharufu ka ufisadi tu hapo....hizo porojo nyingine ni kujazia kurasa tu but we really need Ngereja atueleze kilichotokea nadhani ana mandate ya kuisafisha Tanroads na wizara yake au we unasemaje?? We are tired of these rubbish..
 
Mshahara siyo kitu kinachoniumiza kichwa bali ni utendaji wa mtu huyo. Habari kama hii haitakiwi kuachwa hivi hivi, inabidi ipigiwe kelele ili kitu cha maana kifanyike.
Suala la kabila nalo halinipi shida kwani ni uadilifu una-matter na si kabila la mtu.
Mtu kulipwa mshahara mkubwa ni kama msukumo wa kufanya kazi kwa bidii, sasa kama mtu analipwa kiasi chote hicho na bado ale rushwa atakuwa hafai hata kwa shetani.

Ombi langu ni kwamba uchunguzi ufanyike juu ya huyu ndugu kufukuza wafanyakazi wanaolinda sheria za nchi ili kuwanufaisha wanyonyaji. Kama akigundulika kutumia madaraka yake vibaya basi afukuzwe kazi na afilisiwe mali zake ili iwe fundisho kwa wanaotumia madaraka yao vibaya.
 
Bonus Sh 122,000,000/= ?????? lol! imekua vodacom sasa hii.....halafu mtu kama huyu utakuta bado haridhiki na hapo..anafanya na ufisadi juu.!! Hii ndio TZ
 
Huyu ndugu mbunge alikuwa wapi siku zote ? CEO wengi wa Tanzania wanalipwa vizuri. Huyu Mrema hayuko related na Mrema wa Ngurudoto.
Track record ya Mrema ni nzuri sana. He has worked for London Underground and for some World Bank Projects in Tanzania. Ndugu mbunge anatumiwa na mmoja wa hao waliokosa hiyo position
 
Bonus Sh 122,000,000/= ?????? lol! imekua vodacom sasa hii.....halafu mtu kama huyu utakuta bado haridhiki na hapo..anafanya na ufisadi juu.!! Hii ndio TZ


System iliyopo ya uongozi ni uozo mtupu na ndio maana haya yanatokea wanauhakika kuwa hakuna lolote litakalofanywa dhidi ya ufisadi wao...Tutapigwa mabao sana kwa mtindo huu....Waziri mwenye dhamana hapa ndio mahali pa kutupa upande wa pili wa picha ya hii habari sio kuleta siasa zao hapa. Kila siku wanaibuka na mbinu mpya ya kutuibia...
 
Huyu jamaa mimi nilihisi sana hasa kwenye maamuzi yake, ila acha kwanza nione hii itafika wapi, kama yataiva sana nitaleta ushahidi humu ndani.
 
shaloom wandugu,

Hayo ya Kilaza Mrema yalishasemwa sana hapa, na jinsi alivyoifanya tanroads mali ya wachagga!

Kwakweli ana maamuzi ya kimangimangi hasa tena wakati mwingine ya kitoto!

Lakini hayo yote ni kwakuwa alipata hiyo chance kwa mgogo wa LOWASSA, akisaidiwa na CHENGE, bila kumsahau kakayake ambaye ni rafiki wa lowasa MREMA WA NGURUDOTO ARUSHA.

Kaanguka Lowassa, Chenge, Sasa zamu yake Mrema!

Huyu mtu inabidi Bunge limchunguze yeye kuhusiana na uhalali wa ajira yake pamoja na mwenendo mzima wa utendaji wa kazi zake.

Inabidi pia kuchunguza kama kweli anafanya upendeleo wa ajira kwa wachaga wenzake kwani tanroads ni ya watanzania wote.
 
5. Let us be objective and avoid parochialism! Ahsanteni.

Mzee mbona unaongea kama vile wewe ndiye Mrema wa tanroads?????????!!!!!!!!! Mbona unajitetea sana??!! Au wamekupatia kwa njia moja au nyingine?! Please let's know your relationship with both Mremas of tanroads and ngurudoto.
 
''Anger is a condition in which the tongue works faster than the mind''

Huyu Mbunge alikuwa na hasira kweli. Hata hivyo hajajiuliza anayepanga na kupitisha policy za hiyo Tanroads ni nani. Mishahara na maslahi ya shirika kama Tanroads sio specific kwa mtu bali kwa nafasi.Mrema alikuta haya tokea kwa mtangulizi wake.

Niliwahi kusikia siku za nyuma kuwa wafanyakazi wa Tanroads ndio the highly paid workers in Tanzania. mbunge angetuambia pia mishahara ya Tanroads iko vipi na sio kumchachamalia CEO kama vile yeye ndiyo Tanroads. Think about the role of the Board Of Directors Mr Mp and stop political bla blas.
 
Kudi shauri,

All in all kuna kaharufu ka ufisadi tu hapo....hizo porojo nyingine ni kujazia kurasa tu but we really need Ngereja atueleze kilichotokea nadhani ana mandate ya kuisafisha Tanroads na wizara yake au we unasemaje?? We are tired of these rubbish..

Ngereja?! Hivi naye anahusika na tanroads?! Au ni ngereja mwingine??
 
Huyu ndugu mbunge alikuwa wapi siku zote ? CEO wengi wa Tanzania wanalipwa vizuri. Huyu Mrema hayuko related na Mrema wa Ngurudoto.
Track record ya Mrema ni nzuri sana. He has worked for London Underground and for some World Bank Projects in Tanzania. Ndugu mbunge anatumiwa na mmoja wa hao waliokosa hiyo position


Tafadhali thibitisha maneno yako!
 
Mshahara siyo kitu kinachoniumiza kichwa

That is because you are not the experienced graduate engineer, being paid tsh 350.000 gross, from the same pot as Mrema!

Hata hivyo, Mporogomyi alikuwa akihoji zaidi jinsi ambavyo Mrema alifanikiwa kunyakua nafasi hiyo ambayo kutokana na mchujo ulivyofanyika, yeye hakuwa miongoni mwa best 4. Kama nilimuelewa vyema, badala ya mmoja kati ya hao best 4, Mrema alinyakua kazi kwa staili kama ile ya Richmond kunyakua mradi fukarishi wa umeme wa dharula.

Mporogomyi alisema, Mrema aliambiwa (na wizara?) kuwa wale best 4 awapangie kazi kama kama maofisa wa TANROADS wa mikoa jambo ambalo hakulifanya kwa kuwaona hao maofisa kama threat kwani hakulingana kabisa na taaluma zao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom