Ephraim Mrema na Ufisadi TANROADS

TANROADS katika mgogoro mpya

lC.gif
rC.jpg

bul2.gif
Bagamoyo-Msata yatafuna mabilioni
MRADI wa Ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia-Msata, ambao umepewa jina la 'ng'ombe wa maziwa' umeingia katika mgogoro mpya baada ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kumfuta mkandarasi aliyeshinda na mwenye gharama nafuu na kuchukua kampuni iliyoshindwa kwa tofauti ya zaidi ya Sh bilioni 20.
Habari za ndani ya TANROADS zimethibitisha kwamba kampuni ya China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) imeenguliwa Julai mwaka huu na kuchukuliwa kampuni ya Estim Construction Co. Ltd yenye mahusiano na mfanyabiashara maarufu familia ya Subash Patel.
Pamoja na kushinda katika vigezo vingine, kampuni ya CHICO ilikuwa ndiyo iliyokuwa na gharama nafuu kwa kupanga kutumia Sh 84, 176, 440, 756.96 wakati Estim wamepewa kwa Sh 105, 604, 611,700.00 pamoja na kuwa walishindwa katika zabuni ya awali.
Huu ni mgogro wa pili kuhusiana na barabara hiyo baada ya TANROADS kuingia katika mgogoro na kampuni ya Korea ya TAKOPA Construction Ltd ambayo Serikali iliilipa Sh bilioni 15 za awali (advance payment) lakini ikaitimua kutokana na kudaiwa kushindwa kazi bila kurejeshwa kwa fedha zilizotolewa kwa kampuni hiyo.
Zabuni hiyo ya 2009/2010 ilitolewa kwa kampuni hiyo ya CHICO ya China baada ya kuondolewa kwa TAKOPA kabla ya uongozi wa TANROADS chini ya Mtendaji wake Mkuu, Ephraem Mrema kuingilia kati na kuvuruga taratibu za zabuni zilizoipa ushindi CHICO.
Raia Mwema imefahamishwa kwamba hata Sheria ya Manunuzi ya Umma haikufuatwa katika kuing’oa kampuni ya CHICO na kuiparua Estim inayodaiwa kuwa karibu zaidi na watu walio karibu na uongozi wa juu wa serikali.
Tayari TANROADS imeisababisha Serikali hasara ya mabilioni ya shilingi ikiwa ni pamoja na fedha zilizolipwa kutokana na kesi mbalimbali zilizofunguliwa na wawekezaji baada uongozi wa wakala kukiuka mikataba na sheria ya manunuzi.
Kwa mujibu wa nyaraka ambazo Raia Mwema imezipata pamoja na habari za ndani ya TANROADS, baadhi ya mikataba imekatishwa kutokana na sababu zinazoweza kutajwa kuwa ni mizengwe ama maslahi binafsi.
Tayari wakandarasi hao, baadhi wakiwa wa kimataifa, wamewasilisha mashitaka yao katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (Arbitration Court) Paris, Ufaransa na London, Uingereza. Mashitaka mengine yamo kwenye mahakama za usuluhishi Tanzania.
Miongoni mwa migogogro inayotajwa ni pamoja na unaohusu barabara ya Marangu-Rombo-Mkuu na Mwika-Kilalacha ambako TANROADS iliingia mkataba wa Sh bilioni 23.4, lakini baadaye mkandarasi akafukuzwa kwenye eneo la ujenzi akidaiwa kushindwa kutimiza wajibu wake.
Mgogoro mwingine ni kati ya TANROADS na kampuni ya PRISMO-BADR, ulioko katika Mahakama Kuu ya Tanzania, ukihusisha madai ya malipo ya awali na udhamini.
Mgogoro mwingine unahusisha Shirika la China Estate Construction Eng. (CSCEC), ukihusu kuboresha kiwango cha barabara ya Kigoma-Lusahunga, deni likiwa Sh bilioni 46.8.
Eneo jingine ni la mkataba wa Sh bilioni 1.39 kati ya kampuni ya Norconsult AS dhidi ya TANROADS, ukihusu utoaji huduma ya usimamizi kwa ajili ya kuinua kiwango cha barabara ya Geita-Sengerema na Sengerema-Usagara.
Kampuni nyingine katika mgogoro na TANROADS ni pamoja na Roughton International, Kundasingh, Shabbirdin & Associate na Grineker-LTA Ltd.
Kampuni nyingine ni Konoike iliyoingia mkataba wa Sh bilioni 103.47 na TANROADS. Mkataba huo ulihusu kubuni na kujenga barabara ya Dodoma-Manyoni.
Shauri la kampuni ya Konoike na TANROADS kwa sasa liko katika Mahakama ya Usuluhishi jijini London, Uingereza, na kampuni hiyo inatajwa kufukuzwa kwenye eneo la ujenzi kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya mkataba.
Mrema, ambaye hata uteuzi wake kuongoza TANROADS ulihojiwa ndani ya Bunge, amekuwa katika dimbwi la tuhuma kadhaa; huku mwenyewe akihaha kujaribu kuzima tuhuma hizo kwa njia mbalimbali.
Baadhi ya tuhuma zinazomuelekea ni pamoja na kuingia mikataba na kampuni za ujenzi; hata kabla ya Serikali kuu kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara husika na hivyo kuisababishia Serikali hasara ya kulipa fidia kwa kampuni husika ambazo zimejikusanya bila kazi.
Imeelezwa kwamba kutokana na hali hiyo, Mtendaji huyo mkuu wa TANROADS amejikuta akishindwa kuelewana hata na wasaidizi wake wakuu ambao amewaona kama tishio kwa ajira yake; huku akijiweka karibu na viongozi wa juu wa serikali na vyombo vya dola.
Mrema ambaye uteuzi wake umekuwa na utata mkubwa ameelezwa kuwa baada ya muda wake wa ajira uliotajwa kuwa miaka mitatu kutofautiana na mkataba aliongia na Wizara ya Miundombinu wakati Andrew Chenge akiwa Waziri ambao unampa miaka mitano.
Ndani ya Bunge tayari Serikali imekiri kuingia hasara ya Sh bilioni 300 kutokana na Mrema kuingia mikataba tata ambayo imeilazimu Serikali kulipa fedha hizo kama fidia. Tuhuma hizo kwa sasa zinachunguzwa na vyombo vya dola kwa mujibu wa taarifa ya serikali bungeni.
Hata hivyo, Wizara ya Miundombinu imepata kigugumizi kuchukua hatua pamoja na kushauriwa kufanya hivyo na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi (PPRA) baada
 
TANROADS katika mgogoro mpya

lC.gif
rC.jpg

bul2.gif
Bagamoyo-Msata yatafuna mabilioni
MRADI wa Ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia-Msata, ambao umepewa jina la 'ng'ombe wa maziwa' umeingia katika mgogoro mpya baada ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kumfuta mkandarasi aliyeshinda na mwenye gharama nafuu na kuchukua kampuni iliyoshindwa kwa tofauti ya zaidi ya Sh bilioni 20.
Habari za ndani ya TANROADS zimethibitisha kwamba kampuni ya China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) imeenguliwa Julai mwaka huu na kuchukuliwa kampuni ya Estim Construction Co. Ltd yenye mahusiano na mfanyabiashara maarufu familia ya Subash Patel.
Pamoja na kushinda katika vigezo vingine, kampuni ya CHICO ilikuwa ndiyo iliyokuwa na gharama nafuu kwa kupanga kutumia Sh 84, 176, 440, 756.96 wakati Estim wamepewa kwa Sh 105, 604, 611,700.00 pamoja na kuwa walishindwa katika zabuni ya awali.
Huu ni mgogro wa pili kuhusiana na barabara hiyo baada ya TANROADS kuingia katika mgogoro na kampuni ya Korea ya TAKOPA Construction Ltd ambayo Serikali iliilipa Sh bilioni 15 za awali (advance payment) lakini ikaitimua kutokana na kudaiwa kushindwa kazi bila kurejeshwa kwa fedha zilizotolewa kwa kampuni hiyo.
Zabuni hiyo ya 2009/2010 ilitolewa kwa kampuni hiyo ya CHICO ya China baada ya kuondolewa kwa TAKOPA kabla ya uongozi wa TANROADS chini ya Mtendaji wake Mkuu, Ephraem Mrema kuingilia kati na kuvuruga taratibu za zabuni zilizoipa ushindi CHICO.
Raia Mwema imefahamishwa kwamba hata Sheria ya Manunuzi ya Umma haikufuatwa katika kuing'oa kampuni ya CHICO na kuiparua Estim inayodaiwa kuwa karibu zaidi na watu walio karibu na uongozi wa juu wa serikali.
Tayari TANROADS imeisababisha Serikali hasara ya mabilioni ya shilingi ikiwa ni pamoja na fedha zilizolipwa kutokana na kesi mbalimbali zilizofunguliwa na wawekezaji baada uongozi wa wakala kukiuka mikataba na sheria ya manunuzi.
Kwa mujibu wa nyaraka ambazo Raia Mwema imezipata pamoja na habari za ndani ya TANROADS, baadhi ya mikataba imekatishwa kutokana na sababu zinazoweza kutajwa kuwa ni mizengwe ama maslahi binafsi.
Tayari wakandarasi hao, baadhi wakiwa wa kimataifa, wamewasilisha mashitaka yao katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (Arbitration Court) Paris, Ufaransa na London, Uingereza. Mashitaka mengine yamo kwenye mahakama za usuluhishi Tanzania.
Miongoni mwa migogogro inayotajwa ni pamoja na unaohusu barabara ya Marangu-Rombo-Mkuu na Mwika-Kilalacha ambako TANROADS iliingia mkataba wa Sh bilioni 23.4, lakini baadaye mkandarasi akafukuzwa kwenye eneo la ujenzi akidaiwa kushindwa kutimiza wajibu wake.
Mgogoro mwingine ni kati ya TANROADS na kampuni ya PRISMO-BADR, ulioko katika Mahakama Kuu ya Tanzania, ukihusisha madai ya malipo ya awali na udhamini.
Mgogoro mwingine unahusisha Shirika la China Estate Construction Eng. (CSCEC), ukihusu kuboresha kiwango cha barabara ya Kigoma-Lusahunga, deni likiwa Sh bilioni 46.8.
Eneo jingine ni la mkataba wa Sh bilioni 1.39 kati ya kampuni ya Norconsult AS dhidi ya TANROADS, ukihusu utoaji huduma ya usimamizi kwa ajili ya kuinua kiwango cha barabara ya Geita-Sengerema na Sengerema-Usagara.
Kampuni nyingine katika mgogoro na TANROADS ni pamoja na Roughton International, Kundasingh, Shabbirdin & Associate na Grineker-LTA Ltd.
Kampuni nyingine ni Konoike iliyoingia mkataba wa Sh bilioni 103.47 na TANROADS. Mkataba huo ulihusu kubuni na kujenga barabara ya Dodoma-Manyoni.
Shauri la kampuni ya Konoike na TANROADS kwa sasa liko katika Mahakama ya Usuluhishi jijini London, Uingereza, na kampuni hiyo inatajwa kufukuzwa kwenye eneo la ujenzi kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya mkataba.
Mrema, ambaye hata uteuzi wake kuongoza TANROADS ulihojiwa ndani ya Bunge, amekuwa katika dimbwi la tuhuma kadhaa; huku mwenyewe akihaha kujaribu kuzima tuhuma hizo kwa njia mbalimbali.
Baadhi ya tuhuma zinazomuelekea ni pamoja na kuingia mikataba na kampuni za ujenzi; hata kabla ya Serikali kuu kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara husika na hivyo kuisababishia Serikali hasara ya kulipa fidia kwa kampuni husika ambazo zimejikusanya bila kazi.
Imeelezwa kwamba kutokana na hali hiyo, Mtendaji huyo mkuu wa TANROADS amejikuta akishindwa kuelewana hata na wasaidizi wake wakuu ambao amewaona kama tishio kwa ajira yake; huku akijiweka karibu na viongozi wa juu wa serikali na vyombo vya dola.
Mrema ambaye uteuzi wake umekuwa na utata mkubwa ameelezwa kuwa baada ya muda wake wa ajira uliotajwa kuwa miaka mitatu kutofautiana na mkataba aliongia na Wizara ya Miundombinu wakati Andrew Chenge akiwa Waziri ambao unampa miaka mitano.
Ndani ya Bunge tayari Serikali imekiri kuingia hasara ya Sh bilioni 300 kutokana na Mrema kuingia mikataba tata ambayo imeilazimu Serikali kulipa fedha hizo kama fidia. Tuhuma hizo kwa sasa zinachunguzwa na vyombo vya dola kwa mujibu wa taarifa ya serikali bungeni.
Hata hivyo, Wizara ya Miundombinu imepata kigugumizi kuchukua hatua pamoja na kushauriwa kufanya hivyo na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi (PPRA) baada

Si lazima kwa Owner/Client Kumlazim kumpa mkataba the lowest Bidder/Tenderer................labda kama Instructions to Bidders/Tenderers........which is one the standard document kwenye procurement..............imekuwa amended...............

Kukitolewa sababu za msingi (ambazo si lazima kuzi-justify) moja wapo ikiwa ni historia ya performance ya kampuni........inaweza ukaipiga chini..........ni uamuzi wa Owner/Client at the end................

Clause 36 :procuring Entity Right to Accept any Bid and to Reject any or all Bids of Instruction to Bidders i.e. ITB (from PPRA Standard Document) inasema hivi...................

Sub-Clause 36.1: Notwithstanding ITB Clause 34, the Procuring Entity (i.e. Owner/Client in this Case.....hii blue ni yangu kwa ufafanuzi) reserves the right to accept or reject any bid, and to cancel the bidding process and reject all bids, at any time prior to the award of Contract, without thereby incurring any liability to the affected Bidder or Bidders or any obligation to inform the affected Bidder or Bidders.

Furthermore.........Sub-Clause 36.3....inasema hivi...........
The Procuring Entity shall upon request communicate to any Bidder the grounds for its rejection of its bids, but is not required to justify those grounds................

Kwa hiyo kuenguliwa kwa hiyo kampuni ya Kichina si kitu cha ajabu...............

......Hivi Mrema bado ni CEO wa TANROADS?
 
Hivi jamani huyu Subash si ndiye anayejenga kijiji cha JK pale Msoga Chalinze au nimepitiwa? sasa bado tunashangaa nini tena ktk hili? Wachina kama wachina sio wabaya lakini pia wapo wachina wachache na vikampuni vyao wenyewe ni wazuri sana kwenye madili kama haya, kumbukeni jinsi mzee wa vijisenti alivyoiongezea pesa kwa siri kampuni moja ya kichina iliyokuwa inajenga barabara ya Singida-Dodoma halafu baadaye ikajafukuzwa wakati wamechota billions zetu....kuna njia nyingi wanazo za kujichotea pesa na mwisho tunapigwa changa la macho kuwa Contractor kashindwa kazi, ninavyojua mimi miaka yote wizara hii ya Miundo mbinu ndio kinara wa kutoa pesa za serikali na kuwapa Viongozi wetu kwa mzunguko kupitia kwa tender ambazo ni feki
 
Mporogomyi ndiye aliyeweka hadharani habari za Mkurugenzi huyo kuingizwa kwenye madaraka hayo kupitia mlango wa nyuma; huku wataalamu ambao walipendekezwa na jopo la usaili wakiwekwa pembeni.

“Ninavyojua huyu Mrema hakuwa amependekezwa na jopo la usaili, hatujui alikotokea hadi akawekwa pale…naomba waziri useme juu ya ajira ya mkurugenzi huyu,” alisema wakati akichangia katika hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa.

La ajabu huyu mtu bado anatamba sana huko TANROADS hadi leo na huku muda wake umekwisha kwa ghiliba ya JK na CCM yake. Huu uozo mwisho wake ni Oktoba 31st
 
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ameanza kazi kwa kufanya maamuzi magumu kwa kumfukuza kazi Mtendaji Mkuu (Ceo) wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Ephraim Mrema.

Habari za uhakika ambazo NIPASHE limezipata kutoka vyanzo vya kuaminika zinaeleza kuwa Dk. Magufuli alifanya uamuzi huo jana.

Vyanzo hivyo havikueleza sababu za kumtimua Mrema, zaidi ya kusema kuwa uamuzi huo unaanza mara moja.
source:Nipashe
 
Huyu Mrema contract yake ya ajira ilikwisha na alichofanya Waziri ni kutomuongezea muda wa mkataba huo.
 
Sasa tunasemaje TZ ni maskini huku kodi zetu zikilipa madeni kwa mabilioni bila pesa. Hivi Serkali ya CCM na JK wake wanaweza kujustify mambo haya namna gani? Ni kutuuaa watanzania. Ninakuwa na shaka kwa nini alimweka Shukuru PhD pale na akimess up bila kumchukulia hatua yeye na hata huyo Mrema na wengineo.
 
Jamani mbona Tanzania kuna package za ajabu? Package hizo za Mrema hupati hata huku tuliko Ulaya. Kwa mara ya kwanza nasikia kitu commencement allowance. Kuuuuuuuumbe ndiyo maana nchi haiendelei. Maana hiyo package yake ya mwezi tu yaweza kujenga kilomita mbili za barabara mjini Moshi!
 
Anayetoa mshahara ni mwajiri, na kwa siku hizi mshahara mnajadiliana kama hujaridhika unaanza mbele ama mwajiriwa au mwajiri.
 
Back
Top Bottom