Mrema: Lowassa aliimarisha CHADEMA kisiasa

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
"Mzee Lowasa kuhamia kwake Chadema kulibadilisha kabisa mwelekeo wa siasa mwaka 2015 kwenye nchi hii, kwa sababu alikuwa ni mtu ambaye ana ushawishi mkubwa, jamii ilikuwa inamuelewa, na aliweza kusaidia mageuzi ya nchi hii mwaka 2015 kwa mara ya kwanza majiji yote makubwa yakaongozwa na Chadema"

"Tuliongoza halmashauri nyingi, alikiwezesha chama kuwa na wabunge wengi, kuwa na madiwani wengi, na pia chama kiliimarika, kutokana na ujio wake"-John Mrema, Mkurugenzi wa Chadema, uenezi, mawasiliano, itifaki na mambo ya nje
 
Lowassa alipata uungwaji mkono mkubwa sana ambao haujawahi kutokea kwenye historia ya siasa za upinzani nchi hii, itatuchukua miaka mingi sana kuja kufikia kile kilele alichofika yule mzee.

Siku zote bado naamini na nitaendelea kuamini, kama chaguzi zetu zingekuwa huru na haki, mshindi wa uchaguzi mkuu 2015 alikuwa ni Marehemu E.N. Lowassa.

Na kwa ile rekodi aliyoiweka pale, imewaacha wengine bila matumaini tena, iweje mpinzani apate uungwaji mkono mkubwa vile bado asiingie ikulu?

Bado tuna safari ndefu sana, sio tu yakupata uungwaji mkono kama ule alioupata mzee Lowassa, lakini pia kutimiza lengo la upinzani kuingia ikulu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Siku zote bado naamini na nitaendelea kuamini, kama chaguzi zetu zingekuwa huru na haki, mshindi wa uchaguzi mkuu 2015 alikuwa ni Marehemu E.N. Lowassa.
Mimi naamini kwa chadema tuliyokuwa tumeijenga kuelekea 2015, hata mgombea urais angekuwa Mdude Nyagali angeshinda.

Lowasa angekuwa na hiyo nguvu mnayoinadi asingenunua ugombea chadema. Angekwenda kuibua moja ya vyama vidogo kama alivyofanya Mrema alipotoka nccr ndio kweli hiyo nguvu yake ingepimika.

Membe naye wapo waliodhani alikuwa na nguvu, alichoambulia act ni aibu. Fisadi lowasa alibebwa na nguvu aliyoikuta chadema.
 
"Mzee Lowasa kuhamia kwake Chadema kulibadilisha kabisa mwelekeo wa siasa mwaka 2015 kwenye nchi hii, kwa sababu alikuwa ni mtu ambaye ana ushawishi mkubwa, jamii ilikuwa...
Hivi yule Pressures mtoto wa kada wa chadema Mawazo alouawa Mwanza si alichukuliwa na Mzee lowasa
 
Back
Top Bottom