Enzi zangu mie Karucee

Enzi zangu mie Karucee

Unapenda ujiko sana
Hakuna binadamu asiyependa ujiko nakupa mfano mmoja tu

CHRISTIANO RONALDO kila siku anaonekana kwenye luninga lakini cha ajabu akiwa kwenye gemu kila wakati au naweza sema mara mara macho yote kwenye luninga la uwanjani akianguka kidogo macho yote luningani

Na umaarufu wote ule
 
Hahahaaa..tena nilikuwa na sura danganyifu wewe.... Yaani ilikua nikikutwa kwenye adhabu walimu wangu wananitetea.. ''huyu hausiki au unasikia wanasema hata huyu? (kimoyomoyo nilikua naumia wanaposema hata wewe?) Sasa mkong'oto ukianza pengine natumwa viboko nikirudi wenzangu wameshakula vyao. Back then I had such an innocent look aisee. Ila siku hizi mtoto mdogo akiniangalia usoni kama hajajipanga lazima alie tu!!
lols. Sweetheart ulikuwa mtundu kimya kimya.
 
Hahahahaa Acha kabisa hii mambo. Hahaahahahaaa. mlikoma aiseee!!

Form one hio hio akaja mwalimu flani wa kike bhana akakuta darasa lina kelele balaa. akauliza ''Is this a class or Kisambo market'' (kisambo ni soko moja maarufu mitaa hio) basi bana wakatokea wachache ''Kisambooo'' My goodness... tukasagwa nje mitaa ya saa tano hivi tukapelekwa kiwanjani, ni mwendo wa pushup, kichura chura, mwendo wa bata, kusimama na mguu mmoja huku umeshika wa mtu wa mbele afu mnaruka... mnakaa mkao wa pushapu ila usijiguse.. ukijigusa tu wako na wewe.. kuchuchumaa nusu mlingoti... kuita mvua kwa mikono n.k n.k

Baba ilikua balaa... yaani hapo nilisikia kila aina ya harufu chafu unayoijua, sio vijambo sio chafya sio makohozi sio makamasi yaani Kila aina ya kilio na majasho yalitutoka; na mishati yetu meupe ilikuwa ya vumbi tu siku hio. Yaani mkuu wiki nzima watu tunatembea kwa kuchechemea.. wasichana ndio walikua hawajiwezi kabisaaaa.... hapana ile siku ipo kwenye diary yangu sitaisahau.
CC Mr Rocky na Karucee wenenu yametukutaga haya


Ha ha haa hiyo kama haijakukuta huwezi jua nini inafanya mkuu yaani jamaa alikuwa anatukimbiza mlimani asee mkifika sehemu moja kulikuwa na tank kubwa sana la maji hapo ndio mnapumzika sasa na hiyo pumzika ndio hiyo mwendo wa bata na mwendo wa mamba, mi push ups kibao!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom