Lung'wecha
JF-Expert Member
- Aug 20, 2014
- 927
- 574
kwenye lugha yoyote kuna stadi kuu nne yaani kuongea(speaking) kuandika(writing) kusikiliza (listening) na kusoma(reading)! sisi wengi wetu tuna tatizo katika kusikiliza na kuongea ipasavyo hata kama tunakimudu vipi kiingereza,katika kuongea ukiwa na tabia ya kufanya mazoezi hata ukiwa peke yako ndani au na watu wa karibu inasaidia sana kulainisha matamshi! kuwa na maneno mapya kila siku ni utajiri mwingine katika lugha.