Mama wawilii
Senior Member
- May 10, 2012
- 149
- 124
Mimi Mama wawili (naamini na wengine wengi) nina nia sana ya kujifunza na kuboresha uwezo wangu wa kutumia Lugha ya Kiingereza. Nimeomba ushauri na nimepata jibu kuwa kuna washiriki wengi hapa JF wana uwezo wa kunikuza katika hii lugha ngeni ambayo kwangu ni Mtihani katika kuweza kuitumia. Naomba ushauri wenu lakini zaidi naomba kujifunza. Kila ambae anaona anaweza kuwa ni Mwalimu naomba niwe mwanafunzi wake katika hili.
Nitajitahidi sana post zinazofuata nitumie Kiingereza ambacho nina hakika kabisa kuwa kitapinda; na hapo ndipo najikabidhi kwenu ili kiwe kinyoofu. Nitakuwa huru sijali kukosea sababu najua ndio njia pekee naweza tambua ni kwa kiasi gani nakosea hasa nikitegemea masahihisho toka kwenu.
Natanguliza shukrani kwa washiriki wote wataoweza nisaidia katika mapungufu yangu ya lugha hii ya Kiingereza.
Mama Wawili.

Last edited by a moderator: