England National Football Team (Three Lions), Special Thread

Page 94

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
5,205
15,162
Huu uzi ni mahususi kwa ajili ya matukio yote yanayoihusu timu ya mpira wa Miguu ya Uingereza.

Timu hii inajulikana kwa jina la Utani la Three Lions, yaani Simba Watatu. Jina hili limechochewa zaidi na nembo ya timu hiyo yenye alama ya Simba watatu (tazama picha)

England_national_football_team_crest.svg.png

Timu hii ipo chini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Uingereza, The FA.

Timu hii imekuwa ikiiwakilisha Uingereza katika mashindano mbalimbali tangu mwaka 1872. Timu hii huvaa jezi za rangi nyeupe na nyekundu.

Simba watatu wameshiriki katika mashindano ya kimtaifa ikiwepo Kombe la Dunia na Michuano ya bara Ulaya.

Kwa kombe la dunia, Uingereza imewahi kuwa mabingwa mwaka 1966. Huku ikiwa imeshiriki mara 16 katika mashindano hayo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1950. Mwaka huo wa 1966, Uingereza ilikuwa Mwenyeji wa Mashindano hayo na kulibakiza kombe nyumbani.

Kwa michuano ya Ulaya, timu hii imeshiriki mara 10. Mafanikio mazuri zaidi ni kuishia nafasi ya pili mwaka 2021.

Timu hii inautumia uwanja wa Wembley uliopo jijini London kama uwanja wake wa nyumbani. Uwanja huu una uwezo wa kubeba idadi ya watazamaji tisini elfu (90,000).

Mchezaji mwenye magoli mengi zaidi katika timu ya taifa ya Uingereza ni Wayne Rooney (Wazza) mwenye magoli 53. Huku mchezaji aliyeichezea michezo mingi zaidi ni Peter Shilton, alicheza mechi 125.

Kwa sasa timu ipo chini ya kocha Gareth Southgate na nahodha wa kikosi hicho ni mchezaji nguli wa Tottenham Hotspurs, Harry Kane.

Kwa Mwaka 2022, katika mashindano ya kombe la dunia yanayofanyikia nchini Qatar, uingereza ipo kwenye kundi B. Timu zingine ni Marekani, Wales na Iran.

Katika mchezo wa kwanza, Uingereza ilianza kwa kuichabanga bila huruma timu ya Iran kwa mabao 6-2.

Timu hii inapewa nafasi ya kufanya vizuri katika mashindano haya. Ina vijana waliojawa na vipaji vya hali na juu na uchu wa kufanya vema.

Ukurasa huu utatumika kwa updates mbalimbali kuhusu Timu ya soka ya Taifa la Uingereza.

Karibuni.
 
Hawa ni nyota waliopo nchini Qatar kwa ajili ya kuiwakilisha Uingereza kwenye Kombe la dunia 2022.

Magolikipa:
  • GK: Jordan Pickford
  • GK: Nick Pope
  • GK: Aaron Ramsdale
Walinzi:
  • DF: Trent Alexander-Arnold
  • DF: Conor Coady
  • DF: Eric Dier
  • DF: Harry Maguire
  • DF: Luke Shaw
  • DF: John Stones
  • DF: Kieran Trippier
  • DF: Kyle Walker
  • DF: Ben White
Viungo:
  • MF: Jude Bellingham
  • MF: Conor Gallagher
  • MF: Jordan Henderson
  • MF: Mason Mount
  • MF: Kalvin Phillips
  • MF: Declan Rice
Washambuliaji:
  • FW: Phil Foden
  • FW: Jack Grealish
  • FW: Harry Kane
  • FW: James Maddison
  • FW: Marcus Rashford
  • FW: Bukayo Saka
  • FW: Raheem Sterling
  • FW: Callum Wilson
 
Kikosi cha Leo dhidi ya USA:
.Jordan Pickford
.Kieran Trippier
.Luke Shaw
.John Stones
.Harry Maguire
.Declan Rice
.Jude Bellingham
.Bukayo Saka
.Mason Mount
.Raheem Sterling
.Harry Kane
 
England akifanikiwa kumtoa France njia ni nyeupe kutwaa ubingwa.
 
Back
Top Bottom