SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,129
- 7,898
Wakati kuna katimu kanajifanya kana "besi" la kusema mashindano ya kombe la mapinduzi hayana maana na kwamba yana gundu, Simba haikusikia kelele za vyura hao na badala yake imeyapa mashindano ya Kombe la Mapinduzi heshima inayostahili. Ukiacha kombe itakalobeba leo na zawadi za pesa, nadhani klabu ya Simba inastahili tuzo maalumu kutoka SMZ.
Ushauri wangu kwa SMZ na Kamati ya mashindano, kabla ya mashindano yajayo wakae chini na uongozi wa Simba ili waone ni jinsi gani wanaweza kuyafanya mashindano haya yakawa bora zaidi. Simba ina ushawishi wa kuvutia timu kubwa zije kushiriki na kuachana na hawa viroboto wanaodhani bila wao mambo hayawezi kwenda.
Ukipata jumla ya timu 8, tatu za Z'bar na zinazobaki kutoka kanda tofauti za Africa, wacheze makundi mawili, ondoa robo fainali itapunguza uchovu wa mechi kuwa nyingi ndani ya muda mfupi. Hadi fainali, timu zitakuwa zimecheza mechi 5 tu. Mashindano haya yanaweza kusaidia timu kuboresha vikosi vyao kipindi cha likizo fupi ila bila kukamiana.
Wale wanaoona mashindano haya hayana maana wawekwe pembeni kwanza hadi watakapojitambua.