Enai Na Abes Life
SEHEMU YA 1
. Enai aliishi maisha ya upweke na huzuni isiyoisha. Hakuwa na marafiki wa karibu isipokuwa Clara – mtu pekee aliyempa sababu ya kutabasamu. Lakini hata hivyo Clara alikuwa kama taa ndogo inayong’aa kwa mbali katika giza nene. Maisha ya Enai yalijaa kutengwa, fikra nyingi, na ndoto zisizo na amani.

. Alikuwa kijana mwenye miaka 23, asiyejua raha ya kuwa karibu na wengine. Wakati wake mwingi alitumia kutafakari kimya kimya, huku usiku wake ukiwa wa kupambana na mawazo na hisia zisizotulia. Dunia iliyokuwa nje ya dirisha lake ilimjia kama ndoto – kama maigizo ambayo hakuwa sehemu yake.

. Jioni moja ya baridi mwishoni mwa vuli, Enai aliamua kukutana na Clara juu ya paa la kiwanda cha zamani, kilichoachwa pembezoni mwa jiji. Mahali pale palikuwa kimya, kikubwa, na kimejaa huzuni – kama vile moyo wake mwenyewe.

. Clara alifika kwa kuchelewa kama kawaida. Alimtazama Enai kwa mashaka, lakini kwa tabasamu la pole.

"Enai, kuna nini?" aliuliza.

Enai alimtazama kwa macho yaliyokuwa na uzito wa maumivu.

"Najihisi vibaya sana, Clara. Kama niko ndani ya maisha ambayo si yangu."

. Clara alijaribu kumfariji, lakini alichoka na kurudia maneno yaleyale ya huzuni kila wakati. Enai alisogea karibu na ukingo wa paa, akatazama chini, huku akisema:

"Nadhani nisingekuwepo, mambo yangekuwa rahisi."

Clara alishtuka.

"Enai, tafadhali usifikirie hivyo. Bado una maisha ya kuishi!"

. Baada ya mazungumzo yao marefu juu ya paa la kiwanda cha zamani, Enai na Clara walianza kushuka taratibu na kuanza safari ya kurejea nyumbani. Usiku ulikuwa umetanda, baridi ikiwakaba mifupa, lakini kimya kati yao kilikuwa kizito kuliko upepo wa usiku.

. Wakiwa njiani, Wakati Clara alipokuwa bado anajaribu kumvuta kwa maneno huku wakitembea kando ya barabara ya vumbi iliyokuwa ikielekea kituoni, Clara alihisi kuwa Enai ametulizana kidogo. Alikuwa kimya, lakini hakuwa na machungu yale ya awali. Labda ile mazungumzo yalikuwa na faida.

. Ghafla, mwanga mkali wa taa ukang’aa mbele yao β€” gari lililokuja kwa kasi lisilokuwa na tahadhari wala honi.

β€œEnai!” Clara alipiga kelele kwa hofu.

. Lakini haikusaidia. Kwa sekunde moja tu, kila kitu kilibadilika.

. Gari lilimgonga Enai kwa nguvu. Mlio wa mwili kugonga chuma ulirindima. Enai alitupwa angani, kisha kuanguka vibaya barabarani. Hakutoa sauti. Mwili wake ulibaki kimya, ukitazama anga, macho yakiwa wazi bila maisha.

. Clara aliguswa na kioo cha gari upande wa kulia, akapigwa ubavuni, akaporomoka pembeni mwa barabara, na kuzimia hapohapo.

. Watu waliokuwa jirani walikusanyika haraka, wakazunguka miili yao kwa mshangao na hofu. Gari lililoteka maisha ya Enai lilikuwa tayari limetoweka gizani β€” ajali ya kukimbia.

. Clara alikimbizwa hospitalini akiwa hana fahamu, huku akiwa amejeruhiwa ubavuni na kichwani. Alilazwa chumba cha uangalizi maalum, siku zikapita β€” wiki moja, wiki mbili.

. Familia ya Enai, ilipopata taarifa, walienda hospitali kuchukua mwili wake. Kilio, simanzi, na maswali mengi yaliwazonga. Walimrudisha nyumbani kwa ajili ya maandalizi ya maziko, huku familia na majirani wakikusanyika kwa huzuni kubwa.

. Lakini hawakujua kuwa kifo cha Enai kilikuwa mwanzo tu wa safari nyingine ya ajabu β€” safari ya roho, ndani ya Abes, kule giza linalovuta waliopotea na wasiosahaulika... sauti ya ajabu na ya kutisha ilimwita

"Einai, umehukumiwa
 
Doh!πŸ˜’
 
Back
Top Bottom