Email from James - Jeddah

Email from James - Jeddah

Nimerudia tena kusoma na nimefurahishwa na uandikaji wako [@Kasinde] wa Kiswahili bila kuchanganya sana na Kiingereza.

Hapo kwenye 'breakfast' na 'lunch' ungetumia 'staftahi' na 'chakula cha mchana' basi ningekupa 98% kati ya 100% ambayo ni A+.

Kuna raha sana unapopata pongezi za dhati na kweli kutoka kwa umpendae. ..... ila kama ulikuwepo akilini mwangu, nilisema uzi huu sitaki kuongea kwa kiinglish na yale maneno niliyokosa kiswahili chake niliyawekea italic. Hayo maneno lunch na breakfast nilijisahau. Asante sana kwa pongezi mahabuba na kugundua nilichokuwa nimekimaanisha.🙂🙂🙂
Asante sweet pie wangu aka mahalat aka monkey pie😛😛😛
 
Ndugu Zako Umewaambia?
Waje Kuchukua Bloodless And Lifeless Body Of Yours Hapo Kempinski Should It Happen.
Kama Bado Basi Ungeanza Na Wao Ndo Uje Ku-Show Ofd Hapa.
KUDOS!
Nimeghairi nilichotaka kukiandika hapa.
 
Kuna raha sana unapopata pongezi za dhati na kweli kutoka kwa umpendae. ..... ila kama ulikuwepo akilini mwangu, nilisema uzi huu sitaki kuongea kwa kiinglish na yale maneno niliyokosa kiswahili chake niliyawekea italic. Hayo maneno lunch na breakfast nilijisahau. Asante sana kwa pongezi mahabuba na kugundua nilichokuwa nimekimaanisha.🙂🙂🙂
Asante sweet pie wangu aka mahalat aka monkey pie😛😛😛

Hahahaaa wewe hunitakii mema.

James Jeddah akipita hapa nitasalimika kweli?
 
Sisi ndo watu wako wa karibu? teh teh

Inawezekana wewe ukawa mmoja wa wana MMU lakini usiwe mtu wangu wa karibu. Wako ambao wako, hivo ondoa shaka sio wote wanipendao kama ninavyowapenda na pia wako wengi sana wanaonichukia sina la kufanya juu yao nasonga mbele. Kasie ni Kasie daima dumu.
Wale walio wangu utawasoma tuu.
 
Likitokea la kutokea nitarithi kile kibebi woka uliwahi sema unacho

Mie nilijua utasema unataka kurithi ID yangu maana hapo ndo ungepata kila kilichokuwa changu kiurahisi. Polee nimesalimika, mrejesho ntauleta baadae kidogo.
 
Kempiski kwa zaidi ya miaka miwili inaitwa Hyatt Regency

Hahahaa
Kuna vitu vingi sijavielezea kwenye hii habari walau nimejitahidi kuifupisha. Sasa kwa miaka miwili hiyo wako watu ambao hawana taarifa kuwa zamani kilimanjaro hotel imebadili majina kama mara tatu hivi. Hivo ili kufikisha ujumbe ilikuwa rahisi kutaja jina la zamani la hotel. Hujasikia hivi karibuni mtu akisema niko sheraton akimaanisha Serena?
Muhimu watu walelewe na wapate ujumbe wapi nilimaanisha.
 
umeshapajua jeddah
Sijapata nafasi ya kupatafuta kwenye ramani au mitandao ila kuna baadhi ya watu humu wamesema iko Saudi Arabia hivo ni nchi ya kiarabu. Naamini ni hivo.
 
Hivi Tanzania wana askari Jeddah SA....?

Sina hakika mie nime elezea nilichoambiwa na James yaweza kuwa kanidanganya na kumbe hana hata ajira ya askari au uanajeshi. Ndani ya muda kadhaa ntaufahamu ukweli na ntaweka mrejesho hapa. Kwa sasa niko salama hakukuwa na mbaya ilitokea.
 
Ndugu yangu na komredi wangu James,

Unakuja mjini hata hunistui?

Kweli Kasie kakukamata.....

Doho tabu!!

Hahahahaaa sasa wewe babu nawe unataka kumwaga mchele upenuni na kuku ndo hao wanadonoa donoa hehehehe
Kwani hujui kesho kuna tukio gani? Na haswa Daslam hiyo siku ya kesho inaadhimishwa mno kwa gharama kubwa kuwaweka wapendanao karibu........
Naibia siri..... sogea nikunong'oneze wengine wasisiskie. ..... James kaja mahsusi ili anipe mshangazo siku ya kesho hapa nilipo nimejiloweka kwenye jacuzzi kusubiria hiyo kesho 😛😛
Tena usiongee kwanguvu Magu akatoa tamko kuwa kesho atakayeonekana anaadhimisha siku hiyo anaswekwa ndani nikakosa mshangao kutoka kwa James.
 
Afu na bestman wa James niko tayari kusimamia show ya ndoa.

Isizidi October mwaka huu tafazali...

Hahahahaa kuolewa na mtu aliyeachana na mkewe kuna raha zake na karaha zake, hasa mke japo kaachika najua atanisumbua tuu maana James ni mcharoooo nahisi atakuwa anatamani kurudiana na James ila ndo hivoo .........
Halafu kwani babu wewe ulishasomea utabiri? Au James alikunong'oneza alichoniambia kuhusu oktoba? Mmmh umejuaje hii habari ya oktoba?
 
Hakuna mwanajeshi mtanzania wa jina la James anaweza kuwa jeshini Jeddah, Saudi Arabia. Labda awe na uraia wa USA na au awe ni mercenary.

Au sana sana kama yupo Jeddah ni korokoni wa shopping mall kwa kupitia njia za Mtemvu.

Changa la macho.

Okeee
 
Hahahaaa wewe hunitakii mema.

James Jeddah akipita hapa nitasalimika kweli?

Hahahahaaa ndo hapo sasa wewe ni mtamu ila James ni mcharoooo na mzani uko sawia hata nimechanganyikiwa......
Mnafanana kama ndizi kisukari khaaa
 
Back
Top Bottom