Email from James - Jeddah

Email from James - Jeddah

Habari za mwisho wa wiki mabibi na mabwana wa MMU,

Leo nawasimulia kisa kilichonitokea kuanzia wiki iliyopita………….

Jumanne iliyopita ya tarehe 2/02.2016 saa nne asubuhi, Kasie nilipokea barua pepe kutoka kwa mwanajeshi aliyejitambulisha kwa jina la James kuwa yeye ni mtanzania anayeishi Jeddah (sijajua vizuri Jeddah ni nchi ya kiarabu au laah hata sikujisumbua kuitafuta kwenye mtandao (gugo).

Alikuwa ananiuliza habari za kikazi maana mie asili ya kazi ninazofanya ni kuhudumia wateja, baada ya kumalizana na kumhudumia kwa njia ya barua pepe nikajua vimeishia pale maana huwa nahudumia wateja wengi. Kwenye barua pepe yangu nimeweka saini ya jina langu, anuani, na namba ya simu ya mkononi na ya mezani ya ofisini. James kumbe akaihifadhi namba ya ngu ya simu ya mkononi na kuanza kuniangalia kupitia mtandao wa whattsapp. Kumbuka shida yake iliisha siku ile ile jumanne ya tarehe 2 kwasababu alijibu name nikajibu hadi tulipoelewana na kuridhika kuwa shida yake imeisha.

Alhamisi jioni nikapokea simu iliwa haina namba wala jina na hata ile application ya caller identity haikufanya kazi kuniletea jina kuwa huyu ni flani. Nilipokea simu ile na sauti ilikuwa uuuuuh maashaalaaaah!!!!

Mazungumzo yakaanza na alijitambulisha kwangu na moja kwa moja akasema shida yake anaomba urafiki na mimi. Nikamjibu nina mpenzi wangu akasema sihitaji kuwa mpenzi wako naomba urafiki na wewe. Nikaguna akasema najua hunielewi ila naomba uniruhusu niwe rafki yako na hutojutia.

Kwakuwa sikuwa na mpango nae nikamwambia sawa ili niachane nae, ijumaa asubuhi ya tarehe 5.02.2016 akaanza mawasiliano ya whattsapp mmmmmmmmmmmmmhhhhhhhhh, ………………………………. Hadi sasa hivi nilichokigundua ni kuwa kuna vitu sio vya kujaribu maana ukiingia huwezi kutoka hata uwe mgumu vipii.

Hapa nilipo leo nimetoka kupata breakfast na James Kempisk na Lunch pia tulipata hapo hapo Kempisk Hotel zamani Kilimanjaro Hotel. James amekuja jana na amefikia hotel hiyo yaani mtihani nilionao ni weekend hii ntapona kweli…………………………..

James ni mwanajeshi yuko Jeddah kikazi na anaishi huko, alioa na akaachana na mkewe na wana watoto 2 ambao wanaishi na mama yao. Sijelewi hadi dakika hii kuwa itakuwa ni CRUSH kama crush nyingine zilizopita, one night stand au ndo nimetumbukia tundu bovu……………………..

Hapa ndo najiandaa kutoka kazini maana kasema dinner pia kwake hapo hapo Kempisk ila nikamwambia ntarudi kulala kwangu lakini hata sijui kitakuweje.

Nawapenda sana MMU hata sielewi elewi naogopa hata kunywa wine………

HINT: James ni msukuma…………..

Ntawataarifu kilichojiri mkiona kimya mjue nimekuwa terrorized au nimenyoywa damu na mumiani James. Ikitokea sitatokea tena hapa jukwaani mjue kuwa nawapenda sana na laah sina la kusema. Sina mume, wala mtoto wala shosti wa kunisindikiza ila nyie ndo watu wangu wa karubu nimeona niwaelezee ili mkisikia loote muwe na pa kuanzia.

Nawapenda mnooo wana MMU,


Kasie.

Ina maana sisi ni watu wako wa karibu kuliko boyfriend wako? Boyfriend wako analijua hili?Kwa nini unataka kumsaliti boyfriend wako very easily?unataka kuniambia kuwa mapenzi ya siku hizi yamefikia hapo???
 
It's me.

Really me.

James...James Jeddah.

Halafu pole eeh..

Asante James...... nshapoa, yamebaki majeraha tuu...

I feel uuuhhhh ......thanks for coming darling.....

I really adores you, I feel you, and I am smelling you.....

Mmmmuuuahhhh! !

Kasie J. J.
 
EBU NIELEWESHENI HUYU MDADA UWAGA STORY ZAKE ANATUNGA AU? MANA STORI ZAKE NI ZA KUPENDWA TU NA WALIOMATAWISJAWAI ONA KALETA STORY YA MUUZA GENGE
 
EBU NIELEWESHENI HUYU MDADA UWAGA STORY ZAKE ANATUNGA AU? MANA STORI ZAKE NI ZA KUPENDWA TU NA WALIOMATAWISJAWAI ONA KALETA STORY YA MUUZA GENGE

Hahahahahahahaaa kuna habari ya ukweli iliyonitokea zamani wakati wa uschana wangu, kichwa cha uzi ni mama ntilie..... utafute huo uzi uusome utakuwa umepata majibu ya maswali yako.

Mi sio mtunzi maana sina ujuzi huo, mara zote nasimulia matukio yaliyonitokea mimi Kasinde.

Kuhusu kupendwa na watu matawi sina jibu lake maana hata nami najikuta tuu imekuwa hivyo.
 
Hahahahahahahaaa kuna habari ya ukweli iliyonitokea zamani wakati wa uschana wangu, kichwa cha uzi ni mama ntilie..... utafute huo uzi uusome utakuwa umepata majibu ya maswali yako.

Mi sio mtunzi maana sina ujuzi huo, mara zote nasimulia matukio yaliyonitokea mimi Kasinde.

Kuhusu kupendwa na watu matawi sina jibu lake maana hata nami najikuta tuu imekuwa hivyo.
Acha kamba.
 
Hakuna mwanajeshi Mtanzania wa jina la James anaweza kuwa jeshini Jeddah, Saudi Arabia. Labda awe na uraia wa USA na awe jeshi la USA lililopo Saudi Arabia tenaa jeshi la USA halipo Jeddah au awe ni mercenary, na mercenary hata siku moja hawezi kujijulisha kuwa yeye ni jeshi.

Au sana sana kama yupo Jeddah ni korokoni wa shopping mall kwa kupitia njia za Abbas Mtemvu.

Changa la macho.
Huyu ndo Bi Faiza Foxy bhana.. AkA The google.com.
 
Back
Top Bottom