Elimu imekusaidiaje?

Elimu imekusaidiaje?

Kwa upande wangu Technical education ni nzuri zaid na itamfaa yeyote compared to career education

nilitaka kusema hivyo hivyo pia,

elimu yetu ya secondary iwe flexible,

i just think kwanza, kungekua na wider choices,

masomo yaongezwe,

na pia kungekua na options mtu baada ya kumaliza la saba awe na choice either aende secondary au chuo asome vocational courses...

Mama Ndalichako kama unataka kuacha good legacy then jitahidi kujenga ma library mengi,ujaze vitabu,kila mtu mwenye kujua kusoma na kuandika asome vitabu,.....

Elimu Tanzania haina maana kama itabaki kuwa ya watu wachache waliofika chuo kikuu

wakati kuna limbi kubwa la watu uneducated.....

ivushe Tanzania kielimu...yes you can!

hata sijui naongea nini,lol…..mara napinga,mara nakubali...
 
Elimu si kwa ajili ya ajira tu. Jaribu kukaa na watu wasio na elimu ndio utajua umuhimu wake.

Hahahaaa!

Mchango wako umenichekesha sana aisee.

Hujaandika mengi ila nimekuelewa vizuri kabisa.

Hili suala la elimu ni pana sana.

Hebu ona tu jinsi ilivyo vigumu ku ‘reason’ na baadhi ya watu humu [ambao kwa kweli wengi wao sijui viwango vyao vya elimu ila naweza kusadiki kwamba wana walau ka ‘exposure’ flani kwa sababu wapo humu JF na ni wachangiaji wa mara kwa mara].

Saa ingine mtu unasoma michango yao unaishia kutikisa kichwa tu [emoji16].

Sasa mtu ambaye hana elimu iliyo rasmi na exposure hana, common sense aliyonayo nayo ni majanga....aisee ni shida sana.

Lakini pia, kuna watu hawana kiwango kikubwa cha elimu rasmi lakini ukiongea nao, ukijadiliana nao unaona kabisa ‘huyu mtu ana akili, ana uelewa mzuri, ana busara, n.k.

Labda ni vile tu hakupata fursa ya kupata elimu nzuri ya darasani au labda alipata lakini kwa sababu kadha wa kadha hakuweza kuendelea. Ila kama angepata basi angeweza kuelimika vizuri sana.

Vivyo hivyo, kuna watu wana elimu kubwa tu ya darasani lakini kila wafunguapo mdomo, kitokacho humo ni pumba tupu. Zaidi ya hiyo elimu yake ya darasani hana jingine kabisa.

Kwa hiyo, kwangu elimu ni suala lililo changamani kwa kiasi kikubwa.

Kwangu elimu ya darasani, hususan elimu ya juu [chuo kikuu na kadhalika], naichukulia kuwa ni dirisha ama mlango tu unaomfungulia mtu fursa au njia ya kufuta ujinga na kujifunza asiyoyajua.

Yanayofuata baada ya hiyo elimu ya juu ni juhudi tu za mtu mwenyewe katika kujifunza, kujiendeleza, na kujiboresha.
 
Watu wasiokuma na elimu wanadanganyana sana mambo obvious tuanze na magonjwa Kuna jiran yetu alipata kansa ya koo ila Sasa waswahili wakawa wanasema Chembe mara kimeo wakaangaika Sasa mzee wangu akamwambia bora uende muhimbili ukacheki shida ni nini.. kufika anakutwa na kansa imeshakomaa
Hapo sasa ukutane na watu wako katika jamii ya kuweka mbele imani za kishirikina.

Hata kansa utaambiwa mtu karogwa!
 
Elimu ipi maana elimu ni nyingi sana
Ipo ya darasani ambayo tunaita rasmi lakini isiyompa mtu nguvu ya kujiajiri, na hata akijiajiri wengi wao hufeli kwa kuwa hawana elimu ya kujiajiri Bali elimu ya kuajiriwa tu waliyotoka nayo mashuleni huko
 
nilitaka kusema hivyo hivyo pia,

elimu yetu ya secondary iwe flexible,

i just think kwanza, kungekua na wider choices,

masomo yaongezwe,

na pia kungekua na options mtu baada ya kumaliza la saba awe na choice either aende secondary au chuo asome vocational courses...

Mama Ndalichako kama unataka kuacha good legacy then jitahidi kujenga ma library mengi,ujaze vitabu,kila mtu mwenye kujua kusoma na kuandika asome vitabu,.....

Elimu Tanzania haina maana kama itabaki kuwa ya watu wachache waliofika chuo kikuu

wakati kuna limbi kubwa la watu uneducated.....

ivushe Tanzania kielimu...yes you can!

hata sijui naongea nini,lol…..mara napinga,mara nakubali...
Hili la technical education lishaongelewa sana, Nyerere kaandika vitabu lundo, sijui hata kama watu wanasoma.

Mwaka juzi nilikuwa namsikiliza Aung San Suu Kyi naye anasisitiza hilo hilo kwao huko.

daily11-july16-2016-akk01.jpg

Suu Kyi lauds vocational education | Eleven Myanmar

State Counsellor Aung San Suu Kyi addresses the technical and vocational education and training forum in Nay Pyi Taw.
The development of national vocational education will promote living standards, according to State Counsellor Aung San Suu Kyi.

Speaking to the technical and vocational education and training forum at MICC-2 in Nay Pyi Taw, she said: "I had a burning desire to develop vocational training. Education qualifies us to embrace and overcome challenges.

"Around the globe, the role of vocational education is increasing. Our country usually values university education rather than vocational training. Vocational education is regarded as second-class,” she said.

"Graduates find it difficult to get jobs. This has gone on for years. We need to place special emphasis on creating jobs for graduates," she added.

"Our educational standards are low but all citizens are urged to have big ambitions. We need to learn from countries with successful vocational education. It is very simple to judge whether vocational education is successful.

"Ideally the young will pick courses that suit their hobbies. There is no better educational system. A person whose job is also their hobby is the luckiest. The education ministry opens vocational training schools but parents regard them as second-rate and only use them if their children fail to get a university place. I value them. Vocational education will develop only when all citizens accept and value it," Suu Kyi said.
 
Mimi elimu ya darasani imenisaidia kwa 100% kuufanya ubongo wangu uweze kuhandle vitu vya huu ulimwengu shule imenifanya niweze kujisomea mwenyewe bila msaada wa professor na kufanya vizuri katika mitihani. Kwa kupenda kujisomea nimejiongeza ujuzi kwenye sheria za kodi, investment management and acquisitions stocks trading, future and trade commodities. Apart from that it has influenced on pursuing PhD in bioinformatics in 2 years to come and I think I will mainly focus on malaria combat since I believe it is about time African we handle our own problem. Also I am good in history and economic development of East Asia why Japan n Korea succeed and malaysia failed. And the last book I read opened my eyes ya Kuwa in this society hakuna right or wrong it depends on the culture same as religions kuwa hizi ni imaginary orders kutufanya tuwe controlled. Mtu akitaka hiko kitabu Ani pm angalizo mtu anatakiwa awe na akili iliyotulia vinginevyo anaweza akaharibikiwa kabisa maana inachallenge our fundamental belief
 
I just think tungekua na na vyuo vingi vya serikali kama VETA,

ambavyo viko regulated kutoa quality education,

tungepiga hatua kubwa kielimu,

huu msululu wa vyuo kama utitiri uangaliwe

.pia,hakuna haja ya kutoa mikopo kwa watu kukariri huko chuo,badala yake tu invest huku level za chini,watu wote wapate elimu……

.kwenda chuo iwe option ya mtu kutaka kuwa more professional ,

kungekua na utaratibu wa kusoma vitabu pia ingekuwa kama tool kufanya informed decisions about what to study further....sio kama sasa hivi, unaenda chuo huko ulikopangiwa ukikuta course ngumu and not enjoyable...unalo hilo,.. LOL
 
Elimu imenisaidia saana japo siwezi sema kiasi cha asilimia ila kwa namna maisha yangu yalivo na ninavo ishi , elimu imenitengeneza katika namna ya kitofauti, mathalani katika kuangalia baadhi ya mambo na kuchanganua ,kama vile mambo ya kiajamii, kisiasa, kiuchumi n.k,

Mbali na kuangalia kuwa kip ulikisomeaa na namna gani unanufaika nacho Moja Kwa Moja, Bali Kwa kuangalia mjumuisho wa elimu katinga angle mbali mbali umeleta tija kwangu ...
 
I just think tungekua na na vyuo vingi vya serikali kama VETA,

ambavyo viko regulated kutoa quality education,

tungepiga hatua kubwa kielimu,

huu msululu wa vyuo kama utitiri uangaliwe

.pia,hakuna haja ya kutoa mikopo kwa watu kukariri huko chuo,badala yake tu invest huku level za chini,watu wote wapate elimu……

.kwenda chuo iwe option ya mtu kutaka kuwa more professional ,

kungekua na utaratibu wa kusoma vitabu pia ingekuwa kama tool kufanya informed decisions about what to study further....sio kama sasa hivi, unaenda chuo huko ulikopangiwa ukikuta course ngumu and not enjoyable...unalo hilo,.. LOL
Shida sio utitiri WA vyuo Germany inavyuo zaidi ya 100 Sasa sisi 26 sijui ndo tunaita utitiri shida ni mitaala ya kikoloni tunatumia ambayo haina manufaa tena Sasa we mtu anajifunza to calculate distance from the sun kweli ili agundue nini
 
Nilitoka familia masikini sana lakini baada ya kuhitimu elimu yangu ya chuo kikiuu nikagundua water table ipo karibu kijijini kwetu . Nilibuni project nzuri ya kuchimba maji na sasa kijijini taabu ya maji imeisha . Hiyo ndiyo elimu ama kweli elimu ni ufunguo wa maisha.
 
Shida sio utitiri WA vyuo Germany inavyuo zaidi ya 100 Sasa sisi 26 sijui ndo tunaita utitiri shida ni mitaala ya kikoloni tunatumia ambayo haina manufaa tena Sasa we mtu anajifunza to calculate distance from the sun kweli ili agundue nini

😀😀😀😀😀😀😀
 
Hapo sasa ukutane na watu wako katika jamii ya kuweka mbele imani za kishirikina.

Hata kansa utaambiwa mtu karogwa!

Hapo hapo kuna waganga wa jadi huwa wanajitangaza kuwa wanazo dawa za kuongeza akili za darasani, wana uwezo wa kufanya ushinde kesi mahakamani, wana uwezo wa kukupatia pesa za majini [jini mapesa], yaani kwa kifupi wana uwezo wa kufanya mengi.

Na kuna watu wanawaamini kabisa hao waganga. Na wapo watu na elimu zao za juu wanaowaamini hao waganga!

Hapo ndo ujue kuwa elimu tu ya darasani si kila kitu!

Maana unaweza ukawa na mashahada yako kibao na bado ukawa mjinga mjinga tu pengine kushinda hata ambao hawana hiyo elimu uliyonayo wewe.
 
Elimu si kwa ajili ya ajira tu. Jaribu kukaa na watu wasio na elimu ndio utajua umuhimu wake.

Mama ntilie anaangalia mazingira anaona jinsi ya kupata pesa siku zote kusaidia familia yake, watoto wake.

Mmachinga hana elimu yoyote anajitahidi kupata kipato ili kuishi.

Form six, graduates wanakaa nyumbani miaka kibao kulalamika kila siku.

Elimu ni kwa ajiri gani? Si kwa ajiri ya kusoma mazingira, kujua jinsi ya kuyatumia mazingira yetu vizuri, uwezo wa kusoma mazingira. Kuyatumia mazingira ya nchi kupata kipato?

Au elimu ni vyeti?
 
Hapo hapo kuna waganga wa jadi huwa wanajitangaza kuwa wanazo dawa za kuongeza akili za darasani, wana uwezo wa kufanya ushinde kesi mahakamani, wana uwezo wa kukupatia pesa za majini [jini mapesa], yaani kwa kifupi wana uwezo wa kufanya mengi.

Na kuna watu wanawaamini kabisa hao waganga. Na wapo watu na elimu zao za juu wanaowaamini hao waganga!

Hapo ndo ujue kuwa elimu tu ya darasani si kila kitu!

Maana unaweza ukawa na mashahada yako kibao na bado ukawa mjinga mjinga tu pengine kushinda hata ambao hawana hiyo elimu uliyonayo wewe.
Hapo ndipo utakapojua nguvu ya mazingira na utamaduni.

Mtu ana Ph.D lake, kasoma mpaka ulaya, anagombea ubunge, na yeye kaenda kwa mganga wa kienyeji amuoshee nyota.
 
Daah,

Mazee ina maana kuzaliwa Madongokuinama Mbombongaaf ndo kumenikosehsa Nobel Prize in Physics?

Enough about me.

Ume raise point moja nzuri sana.

Napenda sana kusoma historia ya Physics. Huwa siku nyingine nawasoma maisha yao kina George Gamow, Georges Lemaitre, Edwin Hubble, Murray-Gell Mann, Paul Dirac, Enrico Fermi, Albert Einstein, Niels Bohr, Wolfgang Pauli, Warner Heisenberg, J. Robert Oppenheimer, Richard Feynman, Kip Thorne, Stephen Hawking, Roger Penrose, etc halafu najiuliza sana.

Hivi hawa magwiji mbona wote watu wa Ulaya na Marekani tu, sanasana utapata wachache wa Asia.

Huku kwetu Africa ina maana hakuna watu wenye akili kama hawa? Au hatujajiwekea mifumo tu ya kuwezeshana?
Kwetu wapo wenye akili zaidi ya hao, ina tegemea akili una idifaini vp.

Hayo yote ulio ongelea sio utamaduni wetu, na huu mfumo wa maisha tunaoishi sasa sio mfumo wetu.

Sisi ilitosha kuishi misituni, kutafuta kitoweo basi.

Sasa tumeingizwa kwenye ulimwengu usio wetu, wenye utamaduni usio wetu. Ndio maana unatupa sana tabu.

Kwahiyo nikiona hivi vitwimbwi vya viongozi wa Kiafrika na Wananchi wenyewe mwishoni na concludi kwamba, Huu mfumo wa kizungu ndio unatuvuruga, hatuja uzoea, itahitaji miaka mingi kuja kuendana nao sawa.

Watu enzi hizo walikuwa na mfalme wao, waliishi maisha yao na kuridhika. Sasa kaja mtu anasema huo utawala sio mzuri, kwanini ufalme uwe ni wa familia moja?
Ina maana nyie hamtaki kupiga kura na kuchagua yoyote?

Hapo ndipo vurugu zilipo anza Africa. Maisha tunayo ishi sio yetu, itatuhitaji miaka mingi kuendana na mfumo huu.

Si kwamba hatuna akili, akili tunazo ila si hizi za kizungu.
 
Haaa, mkuu, kuna watu wengine ukiendelea sana wanakuona show off na wao nawapa nafasi nisiwakwaze.

Hahaa.

Mimi hii kitu ipo kwenye damu, hata mshua wangu ni mtu wa "personal stories and testifying anecdotes".

Halafu nishapata vindication kwa bosi wangu mmoja, nilikuwa nafanya global project moja, basi yeye kila siku ananiambia anapenda sana ninavyoandika, ananiambia "paint a picture, tell a story".

Yani kuelezea vitu bila hata anecdotal stories naona kama sijakamilisha mambo vile.
Mkuu Kiranga, naomba nikufanyie live interview hapa JF, kuna vitu kibao watu wanahitaji kujua kuhusu wewe.
 
Mkuu Kiranga, naomba nikufanyie live interview hapa JF, kuna vitu kibao watu wanahitaji kujua kuhusu wewe.
Mazee kwanza kabisa nashukuru sana kwa heshima hii.

Siichukulii kwa urahisi rahisi heshima hii.

Moja ya kanuni zangu kubwa katika maisha yangu ni kwamba natafuta kujua mambo zaidi kuliko kuwajua watu. Kama hali itaruhusu kulingana na ulazima. Ingawa pia, nakubali kuna kujua mambo kwa kujua watu, na kujua watu kuna raha ya vielelezo vya pekee, ndiyo maana historia imejaa habari za watu fulani.

Na kama lengo lako ni kubadilishana mawazo kuhusu mambo, sina tatizo.

Lakini ikiwa una lengo la kunijua mimi, hapo tutakuwa tunachepuka kwenda kwenye "cult of personality", tumjue huyu giant Kiranga yukoje.

Ingawa naelewa kwamba kuna kujifunza katika kujuana personally, nachelea kuhadaa umma, Kiranga ni ndugu yenu wa kila siku, yule mzungumzaji sana kwenye tafrija, yule ambaye heshi kutaka kujifunza, yule ambaye ana mapungufu yake mengi tu.

Mimi niko poa kwenye kujadili mambo.

Niko free zaidi weekends US Eastern time.
 
Back
Top Bottom