Elimu imekusaidiaje?

Elimu imekusaidiaje?

Kwa uelewa wako huu sidhani kama ulipata shida kwa mitaala yetu hapa bongo.....

Na kama ulisoma arts na uhakika ulifanya vizuri mno.....

Nikupe tu Hongera yako wewe jamaa unajiamini kinouma halafu kama unakifahamu kitu bhasi unakielezea vizuri tena chote bila kuacha kitu hata bongo lala yoyote ataelewa na hakutokuwa na maswali kabisa.....

Na imani ungezaliwa kwa wazungu huko sasa hivi tungekuwa tunakusoma kwa articles mbalimbali za uvumbuzi....
Daah,

Mazee ina maana kuzaliwa Madongokuinama Mbombongaaf ndo kumenikosehsa Nobel Prize in Physics?

Enough about me.

Ume raise point moja nzuri sana.

Napenda sana kusoma historia ya Physics. Huwa siku nyingine nawasoma maisha yao kina George Gamow, Georges Lemaitre, Edwin Hubble, Murray-Gell Mann, Paul Dirac, Enrico Fermi, Albert Einstein, Niels Bohr, Wolfgang Pauli, Warner Heisenberg, J. Robert Oppenheimer, Richard Feynman, Kip Thorne, Stephen Hawking, Roger Penrose, etc halafu najiuliza sana.

Hivi hawa magwiji mbona wote watu wa Ulaya na Marekani tu, sanasana utapata wachache wa Asia.

Huku kwetu Africa ina maana hakuna watu wenye akili kama hawa? Au hatujajiwekea mifumo tu ya kuwezeshana?
 
Nikiitafakari Africa napataga maumvu fulani moyoni mwangu , yani aise wazungu wametushinda kila kitu hata mpira tu, hata kuimba, hata kuigiza, hata kwenye kujiamini, hata kwenye kujithamimi, nk

Dada zetu ndo wanafanya tudharaulike zaidi kwa kutumia vitu vyao vya kijinga jinga tu.

Hahaa,

Dada zetu wamefanya nini tena mkuu?
 
Hahaa,

Dada zetu wamefanya nini tena mkuu?

Wanatudhalisha sana na madubwasha wanayonunua kwa wazungu na kuyapachika kichwani

Wanafanya dharau zinazidi kwa kutaka weupe wa wazungu

Baadhi ya dada na mama zetu usoni wamekuwa kama nguruwe iliyomwagiwa maji kwa ajili ya kuchunwa, wengine wamekuwa kama kidonda kibichi hivi

Pasipo shaka wanafanya tuendele kudharaulika na ulimwengu wa kwanza Mkuu.

Inauma sana, Inasikitisha sana na kuacha mdomo wazi Mkuu.
 
Dada yangu Rebeca 83 asante kwa mada nzuri sana hii.

Kwanza elimu unayoelekea kujikita nayo ni elimu rasmi, hili si jambo baya, elimu rasmi imewekewa viwango na mifumo ya kupima vitu.

Lakini elimu ni pana kuliko elimu rasmi.

Ndiyo maana unaweza kuwa na Ph.D yako ya geology, ukaenda misitu ya Congo kufanya uchunguzi wa sehemu za kuchimba madini ya coltran yanayotumika kutengeneza sehemu za simu za mkononi, ukaumwa na nyoka wakali wa misitu ya Congo, halafu wenyeji wa hapo wenye elimu ya asili ya kukabiliana na mazingira yao wakajua tiba, wakaweka kijiwe fulani sehemu uliyoumwa na nyoka, kijiwe kile kikanyonya sumu yote na kukunusuru maisha yako ("Sara's Notebook" anyone?).

Binafsi, naamini sana katika kujisomea mwenyewe nje ya mitaala ya elimu rasmi.

Na tabia hii imenifanya niweze kujua mbivu na mbichi sehemu nyingi, na kila mtu anapotaka kunidanganya kwa uongo mdogo mdogo, naweza kutambua na kukataa habari hizo.

Nitaongea mambo kiujumla zaidi (kwa mfano siwezi kukutajia jinsi elimu ilivyoweza kunifanya niweze kujaza hela benki za Uswizi, joking)

Ukisoma mambo kama logic, computer programming na falsafa, unaweza kuangalia maisha kama a set of propositions, a sort of branching tree, hata maamuzi ya nisome nini, nifanye kazi gani, niishi wapi, nimuoe nani, nichukue risk gani, nisaidie kipi, nijiendeleze wapi etc ni maswali ambayo yanahitaji elimu.

Pia, elimu imenisaida kuweza kufanya utabiri mzuri wa mambo yanayokuja kwa kuangalia yaliyopita na yaliyopo. Ni vigumu kutabiri yanayokuja kama huna elimu inayotakiwa kuweza kuunganisha mambo. Ndiyo maana mtu anaweza kufanya kitu leo kikaonekana cha kijinga (kanunua kiwanja kikubwa Gezaulole shamba huko mwaka 1990, kule atakuja kukaa nani mbona porini?) kumbe baada ya miaka 25 panakuwa mjini na viwanja vinapanda bei sana.

Elimu ya kweli pia inasaidia mtu kuwa mtu bora zaidi. Kuona maana ya kusaidia wengine hata bila ya kujali zawadi ya mbingu wala kuogopa moto (kwa watu tusioamini kuwepo kwa Mungu kama sisi). Mtu unaishi bila woga, lakini kinyume na mategemeo ya wengi kwamba usipoamini Mungu utakuwa valuvalu, elimu yako ya kuweza kuishi na watu, usomi wa dini mbalimbali na jitihada za kufanya mema kwa sababu unapenda kufanya mema tu, zinakufanya uishi vizuri na watu.

Elimu inakupa confidence ya kuwa comfortable katika mazingira tofauti. Miaka kama 15 iliyopita nilialikwa na Warusi fulani kufanya interview World Trade Center. Warusi wana mkwanja sana, walikuwa wanatafuta mtu wa kuangalia systems zao. Nilivyofika chumba cha interview nilikuwa nimekamilisha kuwa na majibu ya maswali ya kazi niliyokuwa naitaka. Nikawekwa chumba cha interview, nilikuwa free vibaya sana, ikatokea mwanzo wa interview tu sijui kukawa na nini nikaongea habari za Stephen Hawking na theoretical physics, basi yule Mrusi interviewer akawa kama kasahau kabisa maswali ya interview ya ile kazi, akawa so interested kujua ninajua nini kuhusu theoretical physics. Badaye, nikaja kugundua kwamba yule Mrusi anatoka katika utamaduni ambao unathamini sana watu wanaoweza kujua mambo kama theoretical physics, watu hawa wanatukuzwa sana kwao kama ma genius (partly due to the Cold War/arms race), kwa hiyo kwake, mtu anayeweza kujielezea kwa kupitia habari za theoretical physics confidently ana uelewa mpana sana na hiyo kazi aliyotaka kunipa nitaielewa kirahisi tu.

Mfano mwingine elimu inakupa confidence katika awkward situation ulinitokea high school. Mwalimu wetu mmoja wa General Studies aliingia darasani wiki fulani na kutoa assignment watu wakae makundi, ya watu watatu mpaka watano, waandae presentation, halafu kipindi kinachofuata, kila kikundi kimtaje mtu mmoja aende mbele ya darasa na kufanya presentation. Alisema hajali topic, anataka kuona public speaking and presentation skills.

Basi, kama kawaida yetu wahuni tunadharau General Studies. Mimi na genge langu hatukuwepo darasani siku hiyo. Na kibaya zaidi, tulivyorudi kutoka mizunguko yetu, hata hatukuulizia wenzetu wamefundishwa nini.

Basi kipindi kilichofuata, mwalimu kaja darasani. Anauliza "Mshajiandaa? Nataka muanze kuja mbele hapa mtoe presentations zenu". Kila mtu anakaa na kikundi chake, wanaanza kwenda mbele. Mimi na wahuni wangu tunang'aa macho, tunauliza, nini kinaendelea hapa?

Basi wakaanza kutoa presentations mara za Geography, mara za Economics, mara za Statistics. Kila mtu akianza kusema, maswali kibao (hayo ni masomo ambayo kila mtu aliyajua sana).

Kifupi, licha ya kujiandaa kwa wiki nzima, kwa lughaya kisasa, "walipata taabu sana".

Basi ikawa watu wa mwisho ni mimi na wahuni wangu wanne, ambao tuliform a natural group ya watu wasio na group.

Jamaa wakasema wewe Kiranga lazima uende kutuwakilisha. Mimi nikapinga, wakaniambia usipoteze muda, jambo hili halina mjadala. Wewe ndiye msemaji sana, huishi stories, wewe ndiye unajua maneno ya ajabu ya Kiingereza, wewe ndiye mtu unayeweza ku perform in front of a crowd, nenda tu.

Sasa mimi najiuliza, niende nitasema nini? Sijajiandaa kwa lolote. Basi ikawa kama inataka kutokea scene pale, watu wanatuangalia. Sasa kaka yako unajua sipendi kutegeana, sipendi scene, sehemu yoyote yenye kutegeana nataka kumaliza mjadala. Nikainuka.

Naanza kuinuka kwenye desk, sijui nitaongea nini.

Napiga hatua kwenda mbele darasani, sijui nitaongea nini.

Nafika karibu na mbele darasani, sijui nitaongea nini.

Nimefika mbele darasani, sijui nitaongea nini.

Nageuka kuliangalia darasa (actually madarasa mawili yaliwekwa pamoja), naona watu wote wananiangalia mimi.

Sijui nitaongea nini.

Naanza kufungua mdomo niongee, sijui nitaongea nini.

Naanza kuongea, "Today I am going to talk ab..."

Sijui nitaongea nini.

Then I make a split second decision "about cosmogony".

Then I hear the entirety of the two classes going like "huuuh" ? "Cosmology?" "Cosmetics?"

Nikasema "Cosmogony is the science of the beginning of the universe".

Nikawapelekesha kwenye singularity, nikawapelekesha kwenye inflation, Alan Guth's papers, formation of lower atoms, stars and nuclear processes to forge higher atoms, the arrow of time and the second law of thermodynamics, nikaelezea mambo mengi niliyokuwa nasoma wakatihuo USIS library Peugeot House. Nikaongea sana habari za "A Brief History of Time:From The Big Bang To Black Holes".

Mpaka namaliza, hakuna swali hata moja.

Mwalimu wa General Studies akasema "Kwakweli hata mimi sina swali, kwa sababu hizi habari zote ndiyo kwanza nazisikia leo".

Nikaona hapa kujisomea kumeniepusha na aibu ya kwamba nilikuwa sijajitayarisha kwa presentation hii.

Kuanzia siku hiyo watu walipenda sana nifanye presentations na nikafanya mbili zaidi, moja ya kuhusu the effects of ChloroFluoroCarbons on depleting the ozone layer and global warming, na nyingine ni kuhusu antibiotics zinavyoleta tatizo la drug resistance kwa bacteria.

Mifano ya jinsi gani elimu inasaidia ni mingi sana. Katika maisha yangu ya kila siku ninaweza kuzungumza na mtu kidogo tu, mtu akapata kuona mvuto wa kipekee kutokana na upana wa mawazo.

Kuhitimisha niseme,elimu inasaidia kupanuamawazo na kumuweeksha mtu kupambana na mazingira yake katika hali tofauti, ndiyo maana hata kama hakuna ajira, kupata elimu kunaweza kumsaidia mtu kujiajiri.
You are a smartest man in any room
 
Wanatudhalisha sana na madubwasha wanayonunua kwa wazungu na kuyapachika kichwani

Wanafanya dharau zinazidi kwa kutaka weupe wa wazungu

Baadhi ya dada na mama zetu usoni wamekuwa kama nguruwe iliyomwagiwa maji kwa ajili ya kuchunwa, wengine wamekuwa kama kidonda kibichi hivi

Pasipo shaka wanafanya tuendele kudharaulika na ulimwengu wa kwanza Mkuu.

Inauma sana, Inasikitisha sana na kuacha mdomo wazi Mkuu.
Mimi falsafa yangu ni kumuachia Ngoswe ya Ngoswe.

Hususan kama hao wanaofanya nisiyopenda ni watu wazima, wanafanya hivyo kwa hiyari yao bila kulazimishwa, na hawajaniingilia maisha yangu.

Ukiamua kuhamanika kwa kila mtu anayeishi usivyotaka wewe dunia hii utahamanika kwa mangapi ndugu yangu?
 
ulipata shida gani mkuu ulivyokaa na watu wasio na elimu?lol
Watu wasiokuma na elimu wanadanganyana sana mambo obvious tuanze na magonjwa Kuna jiran yetu alipata kansa ya koo ila Sasa waswahili wakawa wanasema Chembe mara kimeo wakaangaika Sasa mzee wangu akamwambia bora uende muhimbili ukacheki shida ni nini.. kufika anakutwa na kansa imeshakomaa
 
Nimekuta watu wanabishana kijiweni nami nikachangia hoja. Hakuna anaenijua pale ila wakaambiana "Sikiliza point za msomi"
Elimu inakupa exposure na knowledge then uko free kufanya chochote na maisha yako.
 
kansa ya koo lazima itakuwa na dalili,

kama hakwenda hospitali kuchekiwa then sio kosa la mtu yeyote..

.au unataka kila mwanajamii wajifunze utabibu kujua on spot kwamba hii ni kansa?,

hospitali madaktari watafanya nini sasa?
 
Nimekuta watu wanabishana kijiweni nami nikachangia hoja. Hakuna anaenijua pale ila wakaambiana "Sikiliza point za msomi"
Elimu inakupa exposure na knowledge then uko free kufanya chochote na maisha yako.

knowledge iko kwenye vitabu,sio kwenye majengo ya shule……sijakataa kuwa tuwe na basic education,ila hii ya kukariri kuwa Msomi ni yule aliyepata Masters or PhD ni wrong,Msomi ni yule aliyesoma vitabu vingi…...LOL ….msinipopoe this is what I believe...
 
Elimu si kwa ajili ya ajira tu. Jaribu kukaa na watu wasio na elimu ndio utajua umuhimu wake.
Somehow kuna ukweli ila wasomi wengi sku hizi ndo akili hawana na ndio wanaoiharibu jamii kwa kujua kwingi
Wapo wengi nimewashuhudia wamesoma sana lakin ni hopeless
 
Somehow kuna ukweli ila wasomi wengi sku hizi ndo akili hawana na ndio wanaoiharibu jamii kwa kujua kwingi
Wapo wengi nimewashuhudia wamesoma sana lakin ni hopeless
Kuna kusoma na kuelimika. Hao hawajaelimika.
 
Ni kweli tunapaswa tuweke vichwani mwetu yanayotuhusu tu.

Jaza kichwa chako na mambo yanayokuhusu

Mimi falsafa yangu ni kumuachia Ngoswe ya Ngoswe.

Hususan kama hao wanaofanya nisiyopenda ni watu wazima, wanafanya hivyo kwa hiyari yao bila kulazimishwa, na hawajaniingilia maisha yangu.

Ukiamua kuhamanika kwa kila mtu anayeishi usivyotaka wewe dunia hii utahamanika kwa mangapi ndugu yangu?
 
Kwa upande wangu Technical education ni nzuri zaid na itamfaa yeyote compared to career education
 
Mimi falsafa yangu ni kumuachia Ngoswe ya Ngoswe.

Hususan kama hao wanaofanya nisiyopenda ni watu wazima, wanafanya hivyo kwa hiyari yao bila kulazimishwa, na hawajaniingilia maisha yangu.

Ukiamua kuhamanika kwa kila mtu anayeishi usivyotaka wewe dunia hii utahamanika kwa mangapi ndugu yangu?

Mkuu naomba nikuone PM
 
Back
Top Bottom