Dada yangu
Rebeca 83 kwanza elimu unayoelekea kujikita nayo ni elimu rasmi, hili si jambo baya, elimu rasmi imewekewa viwango na mifumoya kupima vitu.
Lakini elimu nipana kuliko elimu rasmi.
Ndiyo maana unaweza kuwa na Ph.D yako ya geology, ukaenda misitu ya Congo kufanya uchunguzi wa sehemu za kuchimba madini ya coltran yanayotumika kutengeneza sehemu za simu za mkononi, ukaumwa na nyoka wakaliwa misitu ya Congo, halafu wenyeji wa hapo wenye elimu ya asili ya kukabiliana na mazingira yao wakajua tiba, wakaweka kijiwe fulani sehemu uliyoumwa na nyoka, kijiwe kile kikanyonya sumu yote na kukunusuru maisha yako ("Sara's Notebook" anyone?).
Binafsi, naamini sana katika kujisomea mwenyewe nje ya mitaala ya elimu rasmi.
Na tabia hii imenifanya niweze kujua mbivu na mbichi sehemu nyingi, na kila mtu anapotaka kunidanganya kwa uongo mdogo mdogo, naweza kutambua na kukataa habari hizo.
Nitaongea mambo kiujumla zaidi (kwa mfano siwezi kukutajia jinsi elimu ilivyoweza kunifanya niweze kujaza hela benki za Uswizi, joking)
Ukisoma mambo kama logic, computer programming na falsafa, unaweza kuangalia maisha kama a set of propositions, a sort of branching tree, hata maamuzi ya nisome nini, nifanye kazi gani, niishi wapi, nimuoe nani, nichukue risk gani, nisaidie kipi, nijiendeleze wapi etc ni maswali ambayo yanahitaji elimu.
Pia, elimu imenisaida kuweza kufanya utabiri mzuri wa mambo yanayokuja kwa kuangalia yaliyopita na yaliyopo. Ni vigumukutabiri yanayokuja kama huna elimu inayotakiwa kuweza kuunganisha mambo. Ndiyo maana mtu anaweza kufanya kitu leo kikaonekana cha kijinga (kanunua kiwanja kikubwa Gezaulole shamba huko mwaka 1990, kule atakuja kukaa nani mbona porini?0 kumbe baada ya miaka 25 panakuwa mjini na viwanja vinapanda bei sana.
Elimu ya kweli pia inasaidia mtu kuwa mtu bora zaidi. Kuona maana ya kusaidia wengine hata bila ya kujali zawadi ya mbinmgu wala kuogopa moto (kwa watu tusioamini kuwepo kwa Mungu kama sisi). mtu unaishi bila woga, lakini kinyume na mategemeo ya wengi kwamba usipoamini Mungu utakuwa valuvalu, elimu yako ya kuweza kuishi na watu, usomiwa dini mbalimbali na jitihada za kufanya mema kwa sababu unapenda kufanya mema tu, zinakufanya uishi vizuri na watu.
Elimu inakupa confidence ya kuwa comfortable katika mazingira tofauti. Miaka kama 15 iliyopita nilialikwana Warusi fulanikufanya interview World Trade Center. Warusi wana mkwanja sana, walikuwa wanatafuta mtu wa kuangalia systems zao.Nilivyofika chumba cha interview nilikuwa nimekamilisha kuwa na majibu ya maswali ya kazi niliyokuwa naitaka.Nikawekwa chumba cha interview, nilikuwa free vibaya sana, ikatokea mwanzo wa interview tu sijui kukawa na nini nikaongea habari za Stephen Hawkings na theoretical physics, basi yule Mrusi interviewer akawa kama kasahau kabisa maswali ya interview ya ile kazi, akawa so interested kujua ninajua nini kuhusu theoretical physics. Badaye, nikaja kugundua kwamba yule Mrusi anatoka katika utamaduni ambao unathamini sana watu wanaoweza kujua mambo kama theoretical physics,watu hawa wanatukuzwa sana kwao kama ma genius (partly due to the old war/arms race), kwa hiyo kwake, mtu anayeweza kujielezea kwa kupitia habari za theoretical physics confidently ana uelewa mpana sana na hiyo kazi aliyotaka kunipa nitaielewa kirahisi tu.
Mfano mwingine elimu inakupa confidence katika awkward sitiation ulinitokea high school. Mwalimu wetu mmoja wa General Studies aliingia darasani wiki fulani na kutoa assignment watu wakae makundi, ya watu watatu mpaka watano, waandae presentation, halafu kipindi kinachofuata, kila kikundi kimtaje mtu mmoja aende mbele ya darasa na kufanya presentation. Alisemahajali topic, anatakakuona public speaking and presentation skills.
Basi, kama kawaida yetu wahuni tunadharau General Studies. Mimi na genge langu hatukuwepodarasani siku hiyo. Na kibaya zaidi, tulivyorudi kutoka mizunguko yetu, hata hatukuulizia mmefundishwa nini.
Basi kipindi kilichofuata, mwalimu kaja darasani. ANauliza mshajiandaa? Nataka muanze kujambele hapa mtoe presentations zenu. Kila mtu anakaa na kikundi chake, wanaanza kwenda mbele. Mimi na wahuni wangu tnang'aa macho, tunauliza, nini kinaendeleahapa?
Basiwakaanza kutoa presentations mara za Geography, mara za Economisc, mara za Statistics. Kila mtu akianza kusema, maswali kibao (hayo ni masomo ambayo kila mtu aliyajua sana).
Basi ikawa watu wa mwisho ni mimi nawahuni wangu wanne, ambao tuliform a natural group ya watu wasiona group.
Jamaa wakasema wewe Kiranga lazima uende kutuwakilisha. Mimi nikapinga,wakaniambia usipoteze muda, jambo hili halina mjadala. Wewe ndiye msemaji sana, huishi stories, wewe ndiye unajua maneno ya ajabu ya Kiingereza, wewe ndiye mtu unayeweza ku perform in front of a crowd, nenda tu.
Sasa mimi najiuliza, niende nitasema nini? Sijajiandaa kwa lolote. Basi ikawa kama inataka kutokea scene pale, watu wanatuangalia. Sasa kaka yako unajua sipendi kutegeana, sipendi scene, sehemu yoyote yenye kutegeana nataka kumaliza mjadala. Nikainuka.
Naanza kuinuka kwenye desk, sijui nitaongea nini.
Napiga hatua kwenda mbele darasani, sijui nitaongea nini.
Nafika karibu na mbele darasani, sijui nitaongea nini.
Nimefika mbele darasani, sijui nitaongea nini.
Nageuka kuliangalia darasa (actually madarasa mawili yaliwekwa pamoja), naona watu wote wananiangalia mimi.
Sijui nitaongea nini.
Naanza kufungua mdomo niongee, sijui nitaongea nini.
Naanza kuongea, "Today I am going to talk ab..."
Sijui nitaongea nini.
Then I make a split second decision "about cosmogony".
Then I hear the entirety of the two classes going like "huuuh" ? "Cosmology" "Cosmetics" ?
Nikasema "Cosmogony is teh science of the beginning of the universe".
Nikawapelekesha kwenye singularity, nikawapelekesha kwenye inflation, Alan Guth's papers, formation of lower atoms, stars and nuclear processes to forge higher atoms, the arrow of time and the second law of thermodynamics, nikaelezea mambo mengi niliyokuwa nasoma wakatihuo USIS library Peugeot House. Nikaongea sana habari za "A Brief History of Time:From The Big Bang To Black Holes".
Mpaka namaliza, hakuna swali hata moja.
Mwalimu wa General Studies akasema "Kwakweli hata mimi sina swali, kwa sababu hizi habari zote ndiyokwanza nazisikia leo".
Nikaona hapa kujisomea kumeniepusha na aibu ya kwamba nilikuwa sijajitayarisha kwa presentation hii.
Kuanzia siku hiyo watu walipenda sana nifanye presentations na nikafanya mbili zaidi, moja ya kuhusu the effects of ChloroFluoroCarbons on depleting the ozone layer and global warming, na nyingine ni kuhusu antibiotics zinavyoleta tatizo la drug resistance kwa bacteria.
Mifano ya jinsi gani elimu inasaidia ni mingi sana. Katika maisha yangu ya kila siku ninaweza kuzungumza na mtu kidogo tu, mtu akapata kuona mvuto wa kipekee kutokana na upana wa mawazo.
Kuhitimisha niseme,elimu inasaidia kupanuamawazo na kumuweeksha mtu kupambana na mazingira yake katika hali tofauti, ndiyo maana hata kama hakuna ajira, kupata elimu kunaweza kumsaidia mtu kujiajiri.