Elimu imekusaidiaje?

Elimu imekusaidiaje?

Mazee nashukuru sana kwa heshima hii.

Moja ya kanuni zangu kubwa katika maisha yangu ni kwamba natafuta kujua mambo zaidi kuliko kuwajua watu.

Na kama lengo lako ni kubadilishana mawazo kuhusu mambo, sina tatizo.

Lakini ikiwa una lengo la kunijua mimi, hapo tutakuwa tunachepuka kwenda kwenye "cult of personality", tumjue huyu giant Kiranga yukoje.

Ingawa naelewa kwamba kuna kujifunza katika kujuana personally, nachelea kuhadaa umma, Kiranga ni ndugu yenu wa kila siku, yule mzungumzaji sana kwenye tafrija, yule ambaye heshi kutaka kujifunza, yule ambaye ana mapungufu yake mengi tu.

Mimi niko poa kwenye kujadili mambo.

Niko free zaidi weekends US Eastern time.
Hahahahah!!

Mkuu, wewe mwenyewe umeeleza kuwasoma wana sayansi kadhaa, maisha yao na andiko zao.

Mara kadhaa pia umekuwa ukiwaeleza hao wanasayansi / (hata viongozi) maisha yao.

Wote hao sidhani kama umeishi nao, bali kuwasoma kupitia kitabu, interview zao nk.

Au una waogopa wasiojulikana??[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Hahahahah!!

Mkuu, wewe mwenyewe umeeleza kuwasoma wana sayansi kadhaa, maisha yao na andiko zao.

Mara kadhaa pia umekuwa ukiwaeleza hao wanasayansi / (hata viongozi) maisha yao.

Wote hao sidhani kama umeishi nao, bali kuwasoma kupitia kitabu, interview zao nk.

Au una waogopa wasiojulikana??[emoji16][emoji16][emoji16]
Nimenyambulisha muktadha sawia, maongezi kwa minajili ya kuukabili mustakabala wetu vizuri kwa kuchambua mada na mambo sina pingamizi nayo.

Maongezi ya kuvunja faragha za watu au kutaka kumjenga mtu aweze kujifikiri yeye ni mwamba fulani wa ajabu, sina utashi nayo.

Wasiojulikana huwa nawatafuta mwenyewe kwenye simu halafu nawaambia wanavyoharibu, wenyewe wanakubali mambo yanaenda vibaya, ila wanatekeleza "amri kutoka juu" tu, hivyo, tayari wananijua, tena wa ngazi ya cabinet, wala sina haja ya kuwahofia.
 
Mkuu watake radhi darasa la saba maana najua kufika darasa la saba nayo ni elimu

Utofauti umakuja

Mmoja darasa la saba

Mwingine form four

Mwingine form six

Mwingine degree

Mwingine masters

Mwingine munaita PhD

Ukumbuke zote hizi ni elimu

Na kuna wengine hawajagusa hata darasa moja hapo
Hehehe last sentence!
 
Elimu ni pana hata kama hutoitumia kwenye ajira itakusaidia kwenye mambo mengine maishani.
Husomi kwa ajili ya ajira tuu bali kutoa ujinga na kujikomboa kifikra.
Halafu siku hizi hatuangalii vyeti bali talent.
 
Hapo ndipo utakapojua nguvu ya mazingira na utamaduni.

Mtu ana Ph.D lake, kasoma mpaka ulaya, anagombea ubunge, na yeye kaenda kwa mganga wa kienyeji amuoshee nyota.
Hao wasomi unawaonea mkuu kwa mfano huko ulaya hayo mambo ya giza ndio yametawala? kwa mfano marekani watu wake mashuhuri kama viongozi na wasanii wa musiki, wanafalsafa, wanajeshi ni freemason, illuminant na taasisi nyingine za giza? Ukitaja hizo jamii za giza matafia kama uingereza, italia na ufaransa utayaacha?

Bado naamini giza limetawala ulimwenguni wachawi, waganga, freemason, illuminant n.k wote ni agent wa shetani tu.
 
Hao wasomi unawaonea mkuu kwa mfano huko ulaya hayo mambo ya giza ndio yametawala? kwa mfano marekani watu wake mashuhuri kama viongozi na wasanii wa musiki, wanafalsafa, wanajeshi ni freemason, illuminant na taasisi nyingine za giza? Ukitaja hizo jamii za giza matafia kama uingereza, italia na ufaransa utayaacha?

Bado naamini giza limetawala ulimwenguni wachawi, waganga, freemason, illuminant n.k wote ni agent wa shetani tu.
Marekani wakila mavi, na wewe utakula mavi?
 
Suala la elimu ni pana sana na mara nyingi linaanza na sera utendaji na linashuka mpka ktk ngazi ya familia.
Hili la mwisho lina impact kubwa sana. Kwa mtazamo mdogo tuu unakuta hata ambao wanaonekana kuwa na uwezo mkubwa wa uelewa wa mambo investment yao ya kielimu na exposure inajengwa na strength ya familia ( sio wote lakini)
 
Tulowengi elimu yetu ni ya makaratasi yaani tunasoma ili kuhitimu na kupata vyeti vya kutaftia ajira hii inapelekea mtu akikosa ajira kwa vyeti kutafta kazi nje ya vitu alivyosomea ili kupata ugali wa kila siku.
Ila siku elimu yetu ikiwa content based tutakua mbal sana...
 
Umeeleweka.

Kwenye utamaduni wa kukariri na kulazimisha kukubaliana hapo kuna tabu sana.

One more story and then I am done for the day.

Nilipoanza chuo mwaka wa kwanza nilikuwa na kozi moja ya falsafa, elective.

Professor mzungu conservative anatoka upstate New York. Supporter wa George Bush. Republican. Judge. Mimi liberal, immigrant fresh off the plane from Bongo.

Darasa la introductory level philosophy, Western Philosophy, mainly pre-Socratic philosophy.

Basi nikataka kulianzisha siku ya kwanza kwa nini hawajaweka falsafa za sehemu nyingine. Lakini nikajirudi. Ukiwa mbishi kanuni ya kwanza ni kuusoma mchezo kabla ya kubisha.

Basi kutoka hapo, nikawa nabishana sana na Professor. Kila darasa ni ubishi. Halafu ubishi wa logic, arguments zangu Professor anazifahamu. Sibishi vitu ambavyo sijavisoma. Nabisha kwa kutumia hoja za wasomibwa falsafa ambazo hata Professor anazijua. Kwa hiyo nikibisha kwa point hii, Professor anajua hapo Locke, hapo John Stuart Mill, hapo Nietzche, hapo Aquinas, etc. Kuna wakati nikawa na dominate darasa mpaka nikaona imepita kiasi. Hususan topic za uwepo wa Mungu. Mpaka dada mmoja akaniuliza, vile unavyobisha unaamini kabisa au unafanya uzushi tu? Nikamwambia naamini hivyo.

Nikasema huyu Profesa atakuja kunifelisha. Kwa sababu nabishana naye sana, mtu mwingine anaweza kuona namvunjia heshima.

To cut a long story short, mwisho wa semester, professor aliniandikia email anasema usije kwenye mtihani wa mwisho wa semester. Nikaona tayari, Professor kashanifelisha kwa sababu ya ubishi wangu darasani. Nikamuuliza imekuwaje tena? Akaniambua hili darasa umeshapasi, umelionea sana. Zile arguments zako za darasani ni za graduate school level. Ni arguments za darasa la masters la falsafa. Hili darasa hata hukutakiwa kuwemo umelionea sana. Nakupa A+. Usije kwenye mtihani.

Nikasema mfumo wa elimu wa Marekani ni tofauti sana na Tanzania.

Nina hakika kama ingekuwa vyuo vyetu Profesa angenifelisha kwa kukosa nidhamu.

Wakati wenzetu Profesa anakubishia anaangalia umesoma na unaelewa nini. Akikuona unaweza kutetea arguments zako anakupitisha.

Kwa kweli yule Profesa alinitafuta sana urafiki akawa anataka niwe naenda kwenye mikutano yao ku network. Ila na mimi nikawa nina kazi zangu nyingi nikawa sina muda naye.

Kama unataka habari za kugezeana wote mseme sawa sehemu kama hiyo, hata kama una kipaji chako kiko tofauti, hakiwezi kuonekana.
Ulaya kinathaminiwa kipaji zaidi sio uwezo wa kukariri notes. Ukiwa na talent ni rahisi kuwa recognized na kupewa heshima unayostahili ila huku kwa ma shithole country ungeshadisko!
 
Back
Top Bottom