Eid Mubaarack. تقبل الله منا ومنكم

Eid Mubaarack. تقبل الله منا ومنكم

Kesho jumapili ya tarehe 30 march 2025 ni sikukuu ya Eid Al fitri kwa waislamu wote duniani.

Eid hii inakuja baada ya kuonekana mwezi wa shawwaal (mfungo Moshi ) ambao ni alama ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Taarifa za kuonekana mwezi wa shawwaali zimepatikana toka mataifa mbalimbali ya kiislamu ikiwa pamoja na Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Falme za kiarabu UAE.

Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم amesema: "fungeni kwa kuonekana mwezi, na fungueni kwa kuonekana mwezi, na mwezi ukifunikwa juu yenu(msiuone) kamilisheni siku thelathini)

Kunako majaliwa mimi nataraji kuswali swala ya Eid kesho asubuhi saa Moja na nusu katika uwanja wa Mandela mtaa wa Pasua manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro..

Namuomba Allaah azikubali ibada zetu za mwezi wa Ramadhani, na kwa rehema zake atupe uwezo na umri wa kuifikia Ramadhani ya mwaka ujao. Aammiyn.
Hii ni Pre Eid.
 
Waislamu wa dunia nzima wote ni ndugu.
Waislamu waliopo mashariki mwa Dunia na waliopo magharibi, kusini na kaskazini wote ni ndugu.
Mungu wao ni mmoja, mtume wao ni mmoja, kitabu chao ( Qurani ) ni kimoja na kibla Chao ni kimoja.
Ni jambo jema wakifunga na kufungua pamoja.
Mipaka kati ya nchi moja na nyingine imewekewa na wanasiasa kwa faida na maslahi ya kisiasa .( Nchi nyingi barani Afrika mipaka yake imewekwa na wakoloni)
Na mipaka hii hubafilika mara kwa mara kwa maslahi na faida za kisiasa.
Kwa msimamo wa kwamba KILA NCHI NA MWEZI WAKE! hadi tarehe 25 April 1964 waislamu wa Tanganyika walikuwa na mwezi wao na waislamu wa Zanzibar walikuwa na mwezi wao.
Mara baada ya muungano April 26 , 1964 mwezi mmoja ukazamishwa baharini ukapotea ( sina uhakika kama mwezi uliopotea ni ule wa Tanganyika au mwezi wa Zanzibar ndio uliopotea!)
Hadi mwaka 2010 waislamu wa Sudani ya kusini na kaskazini walikuwa wanafunga kwa mwezi mmoja kwa kuwa Sudani ilikuwa moja tu bila kujali kwamba kuna kusini na kaskazini.
Kutokana na migogoro ya kisiasa mwaka 2011 Sudani ya kusini ikajitenga toka Sudani ya kaskazini.
Kwa msimamo wa KILA NCHI NA MWEZI WAKE waislamu wa Sudani kusini ikabidi watafute mwezi wao kwakuwa hawawezi kufunga kwa mwezi ulioandama Sudani ya kaskazini wakati hiyo ni nchi tafauti.
Kwa maslahi na faida za WANASIASA yaliyotokea Sudani siku moja yaweza yakatokea Tanzania.
Kwa maslahi na faida za WANASIASA haitashangaza siku moja kuwa na Tanzania ya mashariki na Tanzania ya magharibi, au Tanzania ya kusini na Tanzania ya kaskazini . Je itakuwa kila nchi zikitengana tunatafuta mwezi mpya na zikiungana mwezi mmoja tunauzika?!
Chifu mkuu samahani kama nitakukwaza hivi mkuu darasani achana na madrasa umeingia kweli ?

Kwamba mwezi mmoja ulipotelea baharini 😂😂😂😂kuwa serious basi mkuu
 
Chifu mkuu samahani kama nitakukwaza hivi mkuu darasani achana na madrasa umeingia kweli ?

Kwamba mwezi mmoja ulipotelea baharini 😂😂😂😂kuwa serious basi mkuu
Sasa palikuwa na mwezi wa Tanganyika na mwezi wa Zanzibar, Baada ya muungano tukabaki na mwezi mmoja! Sasa wewe uliyeenda darasani na madrassa unaweza kunisaidia kujua mwezi mmoja ulienda wapi baada ya muungano?!
Na je huu mwezi unaotangazwa na bakwata kwa Sasa ni ule wa Zanzibar au ni wa Tanganyika?!
 
Idd ni jumatatu na Jumanne tusiharibu utaratibu
😀 😀 😀 😀 😀 ngoja waje

FROM GOOGLE

Sunni and Shia Islam are the two main branches of Islam, differing primarily on the issue of succession to the Prophet Muhammad, with Sunnis believing in a council-elected caliph and Shias believing in a divinely appointed leader from Muhammad's family.

Here's a more detailed breakdown:
Key Differences:
  • Succession:
    • Sunni: Believes the leadership of the Muslim community (caliphate) should be determined by a council of the community (Sunna) and not necessarily by bloodline.

    • Shia: Believes that the leadership should be passed down through Muhammad's family, specifically his cousin and son-in-law, Ali, and his descendants (Imams).
    • Religious Authority:
        • Sunni: Emphasizes the "Sunnah" (the Prophet's example and teachings) and the consensus of the Muslim community (Ijma).
        • Shia: Places emphasis on the teachings and guidance of the Imams, whom they believe to be infallible and divinely guided.
    • Legal Traditions:
        • Sunni: Follows different schools of legal thought (Hanafism, Shafi'ism, etc.) that strive to apply the Sunnah to daily life.
        • Shia: Follows Shia jurisprudence, which emphasizes the role of reason and the teachings of the Imams in interpreting Islamic law.
    • Historical Events:
        • Sunni: Views the first four caliphs (Abu Bakr, Umar, Uthman, and Ali) as "rightly-guided".
        • Shia: Only recognizes Ali as the rightful successor and considers the other three caliphs as usurpers.
    • Prophetic Household:
        • Shia: Shia Muslims revere the ahl al-bayt, the family of Muhammad, maintaining that they possess divine knowledge.
        • Sunni: Sunnis also admire the prophetic household, but Shia Muslims see them as authority figures when it comes to gaining knowledge and spirituality.
Similarities:
    • Both Sunnis and Shias share the core tenets of Islam, including belief in one God (Allah), the Prophet Muhammad, the Quran, and the Five Pillars of Islam (faith, prayer, charity, fasting, and pilgrimage).
    • Both groups adhere to Islamic law (Sharia), although they may interpret it differently.
Global Distribution:
    • Approximately 80-90% of Muslims worldwide are Sunni.
    • Shia Muslims are concentrated in countries like Iran, Iraq, Azerbaijan, and Lebanon, with significant communities in other parts of the Middle East and Asia.
 
Wewe dini umesomea wapi?

Mbona unapotosha?
Ndugu yetu Chifu mkuu , anafunga msimamo wake na kuupambania kana kwamba ambao Wana msimamo wa pili wamepotoka wote kwa msimamo huo , wakati jambo hili ni lenye hitilafu kubwa hata Wanazuoni wakubwa wa zama zetu wakina Sheikh Ibn Uthaymeen, Ibn Baaz na Albani (Allaah awarehemu wote) wao wametolea ufafanuzi pia suala hili vizuri na kati ya hao hakuna hata mmoja aliyesoma ni makosa kusikia mwezi mahala Fulani (nchi nyingine) Kisha usifunge au kufungua , na wengine wameweka wazi kuwa msimamo wao kuwa kila watu wafuate mamlaka katika nchi Yao mahali walipo.

Albaniy yeye msimamo wake mwezi popote lakini ana maelezo mazuri kuhusiana na Hilo na akahitimisha kutokana na hali za sasa watu wafuate mamlaka za nchini mwao.

Suala likiwa Lina hitilafu kubwa na zenye hoja na kila kundi Lina Wanazuoni wakubwa wanaosimamia msimamo huo , ni Bora usimamie msimamo wako bila kufunga milango kuwa wewe ndio Top uko 💯 sahihi na wengine wapo katika msimamo batili.
 
Hata hizo nchi zilizotangaza kuuona mwezi zina mamufti Tena wenye elimu kushinda hawa mashehe ubwabwa wa hapa Tanzania.
Mwezi umeonekana Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Falme za kiarabu.
Hapo kuna mamufti watatu wenye elimu za kutosha ambao wamethibitisha mwezi umeonekana , Sasa Mimi niache kuwasikiliza mamufti watatu wa nchi za kiislamu ningoje ngonjera za mufti wa bakwata ?!

Kwani unaishi UAE(Qatar,Saudia)? Kwa TZ bado haujaandama ngoja tusikilizie leo.
 
Uislamu unafuata lunar kalenda kwa maana kalenda ya mwezi,kwahiyo lazima ufuate tarehe kutokana na muandamo wa mwezi

Hayo unayotaka wewe ni maono yako binafsi

Nadhani nimefafanua vya kutosha

Asante na kwaheri
Ona sasa ndo unazidi kuchanganya, nyie mnafuata siku 30 za mfungo, au mwandamo wa mwezi?

Hii EID kivuruge, ni hatari. 😂😂😂😂
 
Kesho jumapili ya tarehe 30 march 2025 ni sikukuu ya Eid Al fitri kwa waislamu wote duniani.

Eid hii inakuja baada ya kuonekana mwezi wa shawwaal (mfungo Moshi ) ambao ni alama ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Taarifa za kuonekana mwezi wa shawwaali zimepatikana toka mataifa mbalimbali ya kiislamu ikiwa pamoja na Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Falme za kiarabu UAE.

Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم amesema: "fungeni kwa kuonekana mwezi, na fungueni kwa kuonekana mwezi, na mwezi ukifunikwa juu yenu(msiuone) kamilisheni siku thelathini)

Kunako majaliwa mimi nataraji kuswali swala ya Eid kesho asubuhi saa Moja na nusu katika uwanja wa Mandela mtaa wa Pasua manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro..

Namuomba Allaah azikubali ibada zetu za mwezi wa Ramadhani, na kwa rehema zake atupe uwezo na umri wa kuifikia Ramadhani ya mwaka ujao. Aammiyn.
Haya mamlaka ya kutangaza kumalizika kwa mwezi mtukufu umeyatoa wapi?
 
Mnafungua kwa kuuona mwezi, au timizo la siku 30? Mbna mnachanganya waja. Lol
Kuna mdau amekuelezea hapo na mimi pia nimejararibu kukuelezea ila naona hujaelewa so nimeconclude kwamba unasoma ili ujibu na sio unasoma ili uelewe.

Ngoja niiweke namna hii tunafunga kwa kutegemea kufunga na kufungua kwa kuuona mwezi. Mwezi unaweza kuwa mzunguko wa siku 29, 30 au 31 ni kama unavyoona February ina siku 29, Jan siku 31 na June siku 30 huwa hujiulizi kwanini??

Sasa kwenye kuuona mwezi kunaweza kuwa na changamoto mbalimbali hivyo ikitokea imefika siku 30 za kufunga hupaswi kuendelea tena. Kama utakuwa una nia ya kuelewa utakuwa umeelewa sasa ila kama ni nia ya kukosoa na kukashifu hutaweza kuelewa
 
Para ya 3 huyo mwenzako jana aliikataa, alisema ni funga ni siku 30, hakuna 28, au 29, ni 30 tyuh, na sio hiyo 31.

Ndo maana niliendelea na mjadala, nilicho kigundua, nyie wenyewe wahusika hamjui nini kinatakiwa kifuatwe, aidha siku timilifu za mfungo, au muandamo wa mwezi.

Naomba unijibu hili, EID inategemea siku timilifu za mfungo, au muandamo wa mwezi?
 
Muandamo wa mwezi ila ikitokea hujauona unafunga siku 30 kisha siku inayofuata unakula Idd, sawa kipenzi cocastic? Karibu Eid kesho Kigamboni.
 
Back
Top Bottom