Eid Mubaarack. تقبل الله منا ومنكم

Eid Mubaarack. تقبل الله منا ومنكم

Baarakallaahu fiykum.
Ninakupendeni kwa ajili ya Allaah.
Nyinyi ni ndugu zangu hasa!
Mungu wetu ni mmoja.
Mtume wetu ni mmoja.
Kitabu cheti (Quran ) ni kimoja.
Na kibla cheti ni kimoja.
Kupendana ni lazima hata kama tunapishana uelewa katika baadhi ya mambo.
Mimi bado sikukuu imenishughulisha lakini nataraji baadae nitapata nafasi ya kufafanua kwa yale ambayo hamjanielewa au mmenielewa tafauti na nilivyokusudia.
Jambo ambalo nasisitiza ni kwamba mwanzo wa uzi huu hapakuwa na nukta ya kuwakosoa wenye msimamo wa mwezi wa kitaifa.
Nilianza kujenga hoja kutetea msimamo wetu na kuonyesha dosari zilizopo katika msimamo wa wenzetu baada ya wachangiaji kuanza kukosoa msimamo wa wale walioswali Eid siku ya leo.
Pamoja na yote hayo hapajaharibika neno Bado nafasi ya kuendelea kuonyeshana hoja za kila upande ipo na haimaanishi kwamba ni ugomvi.
Kwasababu naona kuna baadhi ya maeneo nimeeleweka vibaya nitakapokuwa tayari nitaanza kuzungumzia msimamo wetu juu ya ikhtilafu za wanachuoni inshaa Allaah.
Eid Mubaarack.
تقبل الله منا ومنكم.
Uwe na amani ndugu yetu, tunakupenda vilevile kwa ajili ya Allah. Mapenzi baina yetu ni haki.

Ikiwa kama kuna sehemu yoyote kwenye mjadala nilikukwaza unisamehe. Kwa upande wangu hukunikwaza, hivyo natanguliza kuomba radhi kama niliteleza popote kwa bahati mbaya kama nilikukwaza ndugu yangu unisamehe.

Mungu wetu ni mmoja,
Mtume wetu ni mmoja,
Kitabu chetu ni kimoja,
Na kibla chetu ni kimoja.

Naam, umesema kweli, kupendana kwetu ni lazima hata kama tunatofautiana katika baadhi ya mambo.

Eid Mubaraka na kwako pia na kwa familia yako na kwa waislamu wote kwa ujumla ambao leo wanasheherekea sikukuu ya Eid.
 
Kabla hatujaenda kwenye hoja zingine tuanzie kwanza hapa

Twende taratibu mkuu kwamba Tanganyika kulikua na mwezi wao na Zanzibar nao walikua n mwezi wao halafu mmoja ukatumbukia baharini ?

Chifu mkuu hizi taarifa unazitoa wapi ?
Swala la kutumbukia baharini au kupotelea msituni ni lugha tu ambayo maana yake ni kwamba baada ya muungano mwezi mmoja ulipotelea kusipojilikana.
Kama umewahi kusoma balagha mlango علم البيان huwezi sumbuka kwa Mimi kutumia lugha ya aina hiyo!
 
Swala la kutumbukia baharini au kupotelea msituni ni lugha tu ambayo maana yake ni kwamba baada ya muungano mwezi mmoja ulipotelea kusipojilikana.
Kama umewahi kusoma balagha mlango علم البيان huwezi sumbuka kwa Mimi kutumia lugha ya aina hiyo!
Aisee hizi dini hizi 😂😂😂😂kwamba mwezi mmoja ulipotelea kusiko julikana ?

Kuna umuhimu mkubwa wa watu kufundishwa elimu ya darasani ili wawe na uwezo wa ku-logic mambo katika mafundisho ya dini
 
Sio kweli.
1000094487.jpg
 
Kesho jumapili ya tarehe 30 march 2025 ni sikukuu ya Eid Al fitri kwa waislamu wote duniani.

Eid hii inakuja baada ya kuonekana mwezi wa shawwaal (mfungo Moshi ) ambao ni alama ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Taarifa za kuonekana mwezi wa shawwaali zimepatikana toka mataifa mbalimbali ya kiislamu ikiwa pamoja na Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Falme za kiarabu UAE.

Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم amesema: "fungeni kwa kuonekana mwezi, na fungueni kwa kuonekana mwezi, na mwezi ukifunikwa juu yenu(msiuone) kamilisheni siku thelathini)

Kunako majaliwa mimi nataraji kuswali swala ya Eid kesho asubuhi saa Moja na nusu katika uwanja wa Mandela mtaa wa Pasua manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro..

Namuomba Allaah azikubali ibada zetu za mwezi wa Ramadhani, na kwa rehema zake atupe uwezo na umri wa kuifikia Ramadhani ya mwaka ujao. Aammiyn.
Kabla ya simu, internet na njia zingine za mawasiliano, mlikuwa mnafanyaje kwani?
 
Aisee hizi dini hizi 😂😂😂😂kwamba mwezi mmoja ulipotelea kusiko julikana ?

Kuna umuhimu mkubwa wa watu kufundishwa elimu ya darasani ili wawe na uwezo wa ku-logic mambo katika mafundisho ya dini


Sasa "Profesa", mbona kaeleweka tu ndugu yangu huyo? Au wewe na elimu yako kubwa na akili kubwa uliyonayo, hukusoma Kiswahili sekondari mambo ya tamathali za semi?
 
Sheikh ibn Baaz alisema ni "uwendawazimu dunia yote kufunga siku moja" kwa sababu maumbile ya dunia yenyewe yanakataa (yaani geography).

Msimamo wake ni kuwa kila eneo kufuata mwandamo wake.

Sheikh Al-Uthaymeen alikuwa na msimamo kama Ibn Baaz, kwamba kila nchi inapaswa kufuata mwandamo wake, mradi wanazingatia ushahidi wa kisharia. Alisema kwamba kutokana na tofauti za maeneo na vipindi vya kuonekana kwa mwezi, si lazima nchi zote zifuate mwandamo mmoja.

Dalili alizozitumia ni pamoja na kauli ya Ibn Abbas (Radhiya Allahu Anhu) alipokataa kufuata mwandamo wa Muawiyah (Radhiya Allahu Anhu) kwa sababu mwezi haukuwa umeonekana katika mji wake. Hadithi hii inapatikana katika Sahih Muslim.

Hadithi ambayo huyu ndugu yetu Chifu mkuu anasema haipo wazi!

Ukifika Makka kwenye vibanda vya fatawa unaruhusiwa kuuliza swali tena ni bure bila gharama yoyote. Chifu mkuu aende akaulize hilo swali kule aangalie atapatiwa jawabu gani!

Hii ndiyo inaitwa kushibishwa itikadi. Yaani anashibishwa itikadi bila ya elimu, ni hatari hii.

Na ikiwa mhusika ana itakidi hivi, tumuulize; kama mwezi ni mmoja, Korea ya Kusini maghribi ikiingia yeye aliyepo huku Tz anaweza akafuturu? Kwamba Alhamdulillah mwezi ni mmoja duniani Korea ya kusini sasa hivi magharibi imeingia ngoja nifungulie!
Faidika na fatwa mbalimbali za masheikh wakubwa wa Kisunni kama vile:

Sheikh Al-Albani

Sheikh Ibn Baaz

Sheikh Ibn Uthaymiyn

Sheikh Muqbil

Sheikh Fawzan

Fatwa hizi zipo katika mfumo wa video na zimewekewa maandiko ya Kiswahili (subtitles) ili kueleweka kwa urahisi zaidi.
Tembelea kupitia link hii


Unaweza kushare pia ili na wengine wafaidike
 
Back
Top Bottom