Eid Mubaarack. تقبل الله منا ومنكم

Eid Mubaarack. تقبل الله منا ومنكم

Wanao kula kesho eid ni cha 29,nasi cha 28,kwahiyo sie wa 28 lazima kesho tufunge cha 29 hlf tunacheki mwezi kama umeandama ni sawa eid na lau haukuandama basi tutafunga 30 jtatu na jnne ni sikukuu bila hata kuangalia mwezi

Ila jtatu inshallah itakuwa eid kwa sie wengine,Allah anajua zaidi

Asante
EID ni j3 au 4,? sitaki kuhusu kuandamwa kwa mwezi, mie nataka kuhesabu kwa chungu.
 
Sio mvurugano na hakuna wanachosema, kubalini ukweli kuwa EID hii ni KIVURUGE
Wewe huna ujualo ! Dini yako huijui halafu unajitia kukosoa dini za wengine?!
Mimi ni mwalimu wa dini ya kiislamu.
Na hadi kuwa Mwalimu usidhani nimesoma dini ya kiislamu tu!, nimesoma pia uyahudi, unaswara ( ukristu ) ubudha, uhindu na dini nyingine ambazo kwa hapa Tanzania hata hazijawa na hata mfuasi mmoja!
Zipo huko mashariki ya mbali!.
Isitoshe mimi mama yangu Allaah amrehemu alizaliwa kwenye ukristo na alhamdu lillaah amefia kwenye uislamu.
Wajomba zangu hadi leo bado ni wakristo na pia ninaishi mkoa wa Kilimanjaro ambao ni Moja ya mikoa yenye wakristo wengi hapa Tanzania.
Na Mimi huwa napatannafasi za kujadiliana na baadhi ya viongozi wa makanisa mbalimbali kwahiyo Mimi ukristo ninaujua vizuri zaidi ya unavyofikria.
Huenda pia nimikwambia kuwa BIBLIA YA KANISA KATOLIKI IMETAFAUTIANA NA BIBLIA YA MAKANISA MENGINE KWA VITABU SITA pia ukanibishia kwakuwa wewe ni mkristo jina ambaye huna muda wa kufuatilia mambo ya dini yako.
 
EID ni j3 au 4,? sitaki kuhusu kuandamwa kwa mwezi, mie nataka kuhesabu kwa chungu.
Uislamu unafuata lunar kalenda kwa maana kalenda ya mwezi,kwahiyo lazima ufuate tarehe kutokana na muandamo wa mwezi

Hayo unayotaka wewe ni maono yako binafsi

Nadhani nimefafanua vya kutosha

Asante na kwaheri
 
Shida mnayo nyie, huko kutofautiana kwa Eid,
Had mwenzi uonekane, je km siku 30 zimepita na hauonekani, inakuaje hapo? Lol
Fungeni kwa kuuona mwezi na fungueni kwa kuuona mwezi ama kwa kutimia siku 30. Dini hii sio ngumu unavyofikiri. Zikifika 30 kama mwezi hamjauona hairuhusiwi kuendelea kufunga.
 
Mfungo Moshi ni upo huo shekhe?
Baadhi ya miezi ya kiislamu waswahili waliipa majina ya kiswahili kama tafsiri yake saa nyingine ili waikumbuke vizuri katika namna ya kuihesabu wasipate tabu wakati wa kuihesabu.
Mwezi wa Shawwaali ambao unakuja baada ya Ramadhani wakauita Mfungo mosi, mwezi unaofuata (Dhulqiida au Dhul Qaad) wakauita Mfungo pili. basi waliendelea kuihesabu hivyohivyo hadi wakafika mwezi wa Jumaadal Akhiyr ( wengine huuita Jumaadal thaaniy ) wao waswahili wakauita mfungo tisa.
Miezi mitatu iliyofuata waliita majina ya kawaida kama inavyoitwa kwa kiarabu ambayo ni Rajabu, Shaaban na Ramadhani.
 
Anza wewe mimi nitamalizia!
Wewe dini umeisomea wapi?!
Kwa sababu yawezekana ikawa mtu anayeniuliza nilikosomea dini yeye hajaisoma kabisa!.
Nieleze wewe dini umeisomea wapi na kwa kiwango gani, Je kiwango chako ni Rawdhwa, Ibtidaaiy, Ii'daadiy, Thaanawiy au Jaamiah, Maajisteer au Douktouraah?
Eleza tafadhali wewe umeisomea wapi na elimu yako ni kiwango gani?!
Al Imaami Al shaafiy katika maneno yake alisema:
"ما جادلت جاهلا إلا غلبني وما جادلت عالما إلا غلبته'"
Naomba tafsiri ya maneno hayo ili nijue nazungumza na mtu wa kiwango gani!
"Sikuwahi kubishana na mjinga ila alinishinda, na sikuwahi kubishana na mjuzi ila nikamshinda."
--------------
Sahih Muslim (Kitabu cha Swawm, Hadithi Na. 1087).

Maelezo ya Hadithi

Kuraib anasimulia:

"Nilitumwa na Ummu Fadhw’l binti Al-Harith kwenda kwa Mu’awiyah (aliyekuwa katika mji wa Shaam). Nilipomaliza kazi yangu huko, nilikuwa Shaam, na nikaona mwezi wa Ramadhan siku ya Ijumaa jioni. Kisha nikarudi Madina mwishoni mwa mwezi. Ibn Abbas akaniuliza: 'Je, mliona lini mwezi wa Ramadhan?' Nikajibu: 'Tuliona siku ya Ijumaa jioni.' Akaniuliza: 'Je, Mu’awiyah na watu wa Shaam walifunga siku hiyo?' Nikasema: 'Ndio.'

Ibn Abbas akasema: 'Lakini sisi tuliuona siku ya Jumamosi, kwa hiyo hatutaacha kufunga hadi tutakapomaliza siku 30 au tuuone mwezi mpya.'

Kuraib akasema: 'Je, haitoshi kwenu mwandamo wa mwezi huko Shaam na kufuata siku za kufunga za Mu’awiyah?'

Ibn Abbas akajibu: 'Hapana. Hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume ﷺ.'"

Unaielewaje hii Hadithi, unaifafanuaje?
 
Ni wapi Quran imesema kuwa lazima mwezi uonekane kwenye nchi yako ndio ufunge?!
Halafu bila simu,TV na radio wafuasi wa bakwata waliopo huko Kibondo vijijini mkoani Kigoma watapataje taarifa ya mufti wao aliyepo Dar Salam kuwajulisha kuwa mwezi umeandama au haujaandama?!
Ikiwa inaruhusiwa kwa muislamu wa huko wilayani Ngara mkoani Kagera kupokea taarifa za mwezi toka Dar es salaam Tanzania kupitia simu,tv na radio kuna ubaya gani Mimi mtu wa Dar es salaam kutumia simu,tv na radio kupokea taarifa toka kwa ndugu zetu waislamu waliopo pande mbalimbali za dunia?!
Wewe dini umesomea wapi?

Mbona unapotosha?
 
Usiseme pande mbali mbali za dunia sema Nchi za Kiarabu.
Toka lini taarifa ikapokewa kutoka marekani ama Thailand?
Anasimamia mambo ambayo hayapo katika dini. Imam Suyutwi anasema "hii dini ni elimu, na hii elimu ndiyo dini yenyewe".

Chifu mkuu kwa bahati mbaya hasimamii katika misingi ya elimu, bali anasimamia katika misingi ya itikadi.

Na anakosea.

Kama yeye kesho inshaallah yupo kwenye Eid basi ni kheri, na kama wengineo siku ya kesho kutwa ama mtondogoo watakuwa na Eid basi kwao ni kheri pia.
 
Ila waislamu wana kazi na hii EID, mara wengine ni kesho, wengine keshokutwa, wengine mtondogoo.

Full tafrani. Eid yaleta kizaa zaa. 😂😂😂😂
Wanatuchanganya hawa. Wengine jumapili wengine jumatatu wengine wanasema sijui waarabu wanawahi kwa sababu wanafuata mwezi wa kimataifa, unabaki kushangaa kwamba kuna mwezi wa kitaifa na mwezi wa kimataifa
 
M
Wewe huna ujualo ! Dini yako huijui halafu unajitia kukosoa dini za wengine?!
Mimi ni mwalimu wa dini ya kiislamu.
Na hadi kuwa Mwalimu usidhani nimesoma dini ya kiislamu tu!, nimesoma pia uyahudi, unaswara ( ukristu ) ubudha, uhindu na dini nyingine ambazo kwa hapa Tanzania hata hazijawa na hata mfuasi mmoja!
Zipo huko mashariki ya mbali!.
Isitoshe mimi mama yangu Allaah amrehemu alizaliwa kwenye ukristo na alhamdu lillaah amefia kwenye uislamu.
Wajomba zangu hadi leo bado ni wakristo na pia ninaishi mkoa wa Kilimanjaro ambao ni Moja ya mikoa yenye wakristo wengi hapa Tanzania.
Na Mimi huwa napatannafasi za kujadiliana na baadhi ya viongozi wa makanisa mbalimbali kwahiyo Mimi ukristo ninaujua vizuri zaidi ya unavyofikria.
Huenda pia nimikwambia kuwa BIBLIA YA KANISA KATOLIKI IMETAFAUTIANA NA BIBLIA YA MAKANISA MENGINE KWA VITABU SITA pia ukanibishia kwakuwa wewe ni mkristo jina ambaye huna muda wa kufuatilia mambo ya dini yako.
Mbona umejitetea sana mkuu, kwani kuna mtu amekutisha?
 
Itakuwa changamoto za kisiasa
Ni mwaka gani ambao mwezi uliandama
Usiseme pande mbali mbali za dunia sema Nchi za Kiarabu.
Toka lini taarifa ikapokewa kutoka marekani ama Thailand?
Kilichopo ni kwamba America na Thailand , Japani au Indonezia hawajawahi tangaza kuona mwezi kabla ya nchi za kiarabu kama unavyosema.
Lakini ikitokea wao waislamu waliopo huko Amerika au sehemu yoyote duniani wakatangaza kuonekana mwezi kabla ya Suudia sisi tunafunga na kufungua na hatutangoja Saudi Arabia au nchi yoyote ya kiarabu.
Msimamo wetu ni kwamba mwezi ukionekana popote duniani ambapo tunazotaarifa kuwa waliotoa taarifa hizo ni waislamu na kwamba waislamu waliopo katika nchi hiyo wanafunga na kufungua kwa kutegemea kuonekana mwezi na hawategemei kalenda basi sisi tunafunga na kufungua pamoja nao.
Saa nyingine kuna sababu za kijiografia zinazofanya kuwa mara nyingi watu wanaoona mwezi mapema ni nchi za mashariki ya kati.
 
Wanatuchanganya hawa. Wengine jumapili wengine jumatatu wengine wanasema sijui waarabu wanawahi kwa sababu wanafuata mwezi wa kimataifa, unabaki kushangaa kwamba kuna mwezi wa kitaifa na mwezi wa kimataifa
Kwani huko kwenu Kuna krismas ya kitaifa na krismas ya kimataifa?!
Je ulishasikia jumapili ya kitaifa na jumapili ya kimataifa?!
Hata ijumaa ulishasikia ijumaa ya kitaifa na ijumaa ya kimataifa.
Kilichopo mwezi wa kweli ni mmoja!
Na ilitakiwa waislamu dunia nzima wafunge na kufungua siku moja kama vile ambavyo wakristu husherehekea sikukuu zao siku moja!
Hakuna kusema wakristo wa Tanzania Wana pasaka yao na wakristo wa India wana pasaka yao.
Wakristo dunia nzima sikukuu zao huwa ni ndani ya siku moja ila wanapishana masaa tu kwasababu inapokuwa wakristo wakienda kanisani asubuhi kuna wakristo wengine ambao kwao bado ni usiku mwingi tu lakini wakiamka wataelekea kanisani ndani ya siku hiyohiyo!
Hii habari ya kusema kuna mwezi wa kitaifa na kimataifa ipo kwa waislamu tu pamoja na kwamba wanajua ya kwamba inapokuwa yupo ndani ya siku ya ijumaa dunia nzima ni ijumaa ila tunapishana masaa kadhaa tu.
Inapokuwa hapa Tanzania tunaswali ijumaa kuna maeneo mengine bado ni asubuhi ila baadae wataswali ijumaa ndani ya siku hiyohiyo.
Ilitakiwa hata kufunga Ramadhani na kufungua iwe hivyohivyo!.
 
Usiseme pande mbali mbali za dunia sema Nchi za Kiarabu.
Toka lini taarifa ikapokewa kutoka marekani ama Thailand?
Kwani kuna mwaka waislamu waliopo Thailand na Amerika walitoa taarifa ya kuonekana mwezi tukaikataa?!
 
Wewe dini umesomea wapi?

Mbona unapotosha?
Umejibu maswali niliyouliza ?!
Ukishanijibu nieleze na wewe dini umeisomea wapi?!
Ukiniambia uliposomea na Mimi nitakueleza nilikosomea ili twende pamoja.
 
"Sikuwahi kubishana na mjinga ila alinishinda, na sikuwahi kubishana na mjuzi ila nikamshinda."
--------------
Sahih Muslim (Kitabu cha Swawm, Hadithi Na. 1087).

Maelezo ya Hadithi

Kuraib anasimulia:

"Nilitumwa na Ummu Fadhw’l binti Al-Harith kwenda kwa Mu’awiyah (aliyekuwa katika mji wa Shaam). Nilipomaliza kazi yangu huko, nilikuwa Shaam, na nikaona mwezi wa Ramadhan siku ya Ijumaa jioni. Kisha nikarudi Madina mwishoni mwa mwezi. Ibn Abbas akaniuliza: 'Je, mliona lini mwezi wa Ramadhan?' Nikajibu: 'Tuliona siku ya Ijumaa jioni.' Akaniuliza: 'Je, Mu’awiyah na watu wa Shaam walifunga siku hiyo?' Nikasema: 'Ndio.'

Ibn Abbas akasema: 'Lakini sisi tuliuona siku ya Jumamosi, kwa hiyo hatutaacha kufunga hadi tutakapomaliza siku 30 au tuuone mwezi mpya.'

Kuraib akasema: 'Je, haitoshi kwenu mwandamo wa mwezi huko Shaam na kufuata siku za kufunga za Mu’awiyah?'

Ibn Abbas akajibu: 'Hapana. Hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume ﷺ.'"

Unaielewaje hii Hadithi, unaifafanuaje?
.الحديث صحيح غير صريح.
SABABU YA IBNU ABBAAS KUUKATAA MWEZI WA SHAMU HAIKO WAZI.
Na kama unaijua sababu hiyo itaje halafu ujiandae kujibu maswali.

Hadithi hii ya Kuraibu ni maarufu sana lakini maana yake haiko wazi na kwahiyo siyo hoja juu ya jambo lolote katika masuala ya mwezi!
Katika hadithi hii hakuna hata sentensi moja inayosema kwamba KILA NCHI NA MWEZI WAKE!.
Ukisema hadithi hii ni ushahidi kuwa kila nchi ina mwezi wake tutakuuliza NINI MAANA YA NCHI?!
Ukisema nchi ni kama vile Tanzania na Kenya kwa maana ya eneo linalotawaliwa na serikali moja chini ya mtawala mmoja tunakuuliza Mbona Abdullaahi Ibni Abbaas aliukataa mwezi wa Shamu wakati Madina alipokuwa anaishi Ibnu Abbaas na Shamu alipokuwa anaishi Muawiya ibn Abii Sufyaan ilikuwa nchi moja , dola moja, chini ya mtawala mmoja ambaye alikuwa Muawiya ibn Abii Sufyaan mwenyewe na Mji wa Madina ulikuwa ni mkoa ( jimbo ) katika serikali ya Muawiya?!
Mji wa Madina alipokuwa akiishi Ibnu Abbaas na mji wa Damascas (Dimashqi ) aliokuwa akiishi Muawiya ni kama vile Ibnu Abbaas kuishi Daar es salaam na Muawiya akawa Dodoma makao makuu ya nchi, je inafaa kusema kuwa watu wa DSM wawe na mwezi wao na watu wa Dodoma wawe na mwezi wao?!
Hadithi ya Kuraibu ni sahihi kabisa haina utata juu ya usahihi wake lakini utata upo kwenye maana yake, INATUFUNDISHA NINI?!
 
Back
Top Bottom