Eid Mubaarack. تقبل الله منا ومنكم

Eid Mubaarack. تقبل الله منا ومنكم

Muandamo wa mwezi ila ikitokea hujauona unafunga siku 30 kisha siku inayofuata unakula Idd, sawa kipenzi cocastic? Karibu Eid kesho Kigamboni.
Tunakubaliana kuwa EID inategemea muandamo wa mwezi, ila ikishindikana kuonekana na ikiwa siku ya 30, bas siku ya 31 watu wanakula Eid?

Ahsante nitakaribia, unipokee pale Ferry.
 
Kesho jumapili ya tarehe 30 march 2025 ni sikukuu ya Eid Al fitri kwa waislamu wote duniani.

Eid hii inakuja baada ya kuonekana mwezi wa shawwaal (mfungo Moshi ) ambao ni alama ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Taarifa za kuonekana mwezi wa shawwaali zimepatikana toka mataifa mbalimbali ya kiislamu ikiwa pamoja na Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Falme za kiarabu UAE.

Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم amesema: "fungeni kwa kuonekana mwezi, na fungueni kwa kuonekana mwezi, na mwezi ukifunikwa juu yenu(msiuone) kamilisheni siku thelathini)

Kunako majaliwa mimi nataraji kuswali swala ya Eid kesho asubuhi saa Moja na nusu katika uwanja wa Mandela mtaa wa Pasua manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro..

Namuomba Allaah azikubali ibada zetu za mwezi wa Ramadhani, na kwa rehema zake atupe uwezo na umri wa kuifikia Ramadhani ya mwaka ujao. Aammiyn.
Amina insha'Allah
 
Kwanza ni lini official huku kwetu? Na je ina siku 2?
 
.الحديث صحيح غير صريح.
SABABU YA IBNU ABBAAS KUUKATAA MWEZI WA SHAMU HAIKO WAZI.
Na kama unaijua sababu hiyo itaje halafu ujiandae kujibu maswali.

Hadithi hii ya Kuraibu ni maarufu sana lakini maana yake haiko wazi na kwahiyo siyo hoja juu ya jambo lolote katika masuala ya mwezi!
Katika hadithi hii hakuna hata sentensi moja inayosema kwamba KILA NCHI NA MWEZI WAKE!.
Ukisema hadithi hii ni ushahidi kuwa kila nchi ina mwezi wake tutakuuliza NINI MAANA YA NCHI?!
Ukisema nchi ni kama vile Tanzania na Kenya kwa maana ya eneo linalotawaliwa na serikali moja chini ya mtawala mmoja tunakuuliza Mbona Abdullaahi Ibni Abbaas aliukataa mwezi wa Shamu wakati Madina alipokuwa anaishi Ibnu Abbaas na Shamu alipokuwa anaishi Muawiya ibn Abii Sufyaan ilikuwa nchi moja , dola moja, chini ya mtawala mmoja ambaye alikuwa Muawiya ibn Abii Sufyaan mwenyewe na Mji wa Madina ulikuwa ni mkoa ( jimbo ) katika serikali ya Muawiya?!
Mji wa Madina alipokuwa akiishi Ibnu Abbaas na mji wa Damascas (Dimashqi ) aliokuwa akiishi Muawiya ni kama vile Ibnu Abbaas kuishi Daar es salaam na Muawiya akawa Dodoma makao makuu ya nchi, je inafaa kusema kuwa watu wa DSM wawe na mwezi wao na watu wa Dodoma wawe na mwezi wao?!
Hadithi ya Kuraibu ni sahihi kabisa haina utata juu ya usahihi wake lakini utata upo kwenye maana yake, INATUFUNDISHA NINI?!
Tuwe makini katika elimu ya mustwalahul hadithi.

Wanawazuoni wa mustwalahul hadithi wanasema: "swahaba akisema umirna yaani tumeamrishwa ama nuhina yaani tumekatazwa, huwa moja kwa moja inachukua hukumu ya hadithi ya kwamba ni Marfuu, yaani moja kwa moja ni kauli ya Mtume.

Yaani yale maneno moja kwa moja yanatoka kwa Mtume kwa sababu anayemuamrisha swahaba ni Mtume na anayemkataza sahaba ni Mtume.

Unachotakiwa kujua: Kutofautiana miandamo ya mwezi, hakuna mwanawachuoni anayekataa kuwa miandamo inatofautiana. Yaani mwezi una kituo! Yaani jana umeonekana Saudia na leo umeonekana Tz, wanawazuoni wote wamekubaliana kuwa miandamo inatofautiana.

Ikhtilafu ipo kwenye kuzingatia ama tusizingatie: Yaani je, tuzingatie kuwa mwezi unatofautiana katika miandamo yake au tusizingatie?

Wewe unadiriki kusema kuwa hii hadithi sababu ya ibn Abbas kuukataa mwezi wa Sham haiko wazi. Tuseme sawa! Haya turudi kwa maulamaa wa hadithi ambao ulimwengu wa kiislamu wanawategemea tuiangalie hii hadithi wameizungumziaje!

1)Ukirudi katika sahih ya Imam Muslim, utaipata hii Hadithi ipo chini ya Mlango unaosema: "Babu bayan Anna likulli baladin ru-uyatuhum wa annahu idhaa ru-iyal hilalu fi baladin laa yalzam hukumuhu Lima bauda anhu".

Ikiwa na maana: Mlango wa kubainisha kuwa kila maeneo yana mwandamo wao na kuwa mwezi ukionekana katika eneo fulani hawalazimiki waliyo mbali kuufuata mwezi ule.

Hii hadith ndivyo Imam Muslim alivyoielewa. Tunavyosema Sahih Muslim, yeye hii hadithi kaizungumzia hivi.

2)Imam Nisai ameiweka hadithi hii katika sunan yake kuwa watu waki ikhtalifiana katika mwandamo wafuate kama hadithi hii, yaani ni kama Kuraib na Ibn Abbas kilichotokea baina yao. Huyu ni Imam Nisai, ni kigogo wa hadithi huyu ulimwengu wa kiislamu unamtegemea, msimamo wake ndiyo huo kwenye hiyo hadithi.

3)Tazama na ufahamu wa wanawazuoni kama Imam Bayhaqi katika kitabu chake cha Assunanul Kubra. Hii hadithi kaifafanua kama maelezo ya Imam Muslim alivyoyaweka.

4)Imam Ibn Khuzayma, na wengine kama Abuu Dawuud katika kitabu chake sunan Abii Dawuud.

Hao wote ni aimma wa hadithi wakubwa wakubwa ambao wao wamemuelewa Ibn Abbas na kuielezea hiyo hadithi ina maana gani. Wewe unataka uelewa upewe na nani kama hao maulamaa wakubwa wa hadithi wameizungumzia hivyo?

5) Imam Attirmidhii katika Jami-i ya Imam Attirmidhii amesema " wal amalu ala hadhal hadithi in-da ahlil elimi anna likulli baladi ru uyatuhum."

Kwa maana: Kuifanyia kazi hadithi hii (ya Kuraib) kwa wenye elimu kuwa kila sehemu wana mwandamo wao.

Hao ni maulamaa wakubwa wa hadithi wanasema hivyo, na hiyo hadithi wameifafanua hivyo! Na ibn Abbas ndiyo kaielezea hivyo!

Vipi hao maulamaa wakubwa vigogo wa hadithi mbona maelezo yao na ufahamu wao unatofautiana na wa kwako?

adriz
 
Alhamdu lillaah.
Mji wa Moshi na vitongoji vyake vimekuwa na baraka ya mvua usiku mzima wa kumkia leo kuanzia saa 5 usiku hadi asubuhi .
Hadi muda huu bado mvua za rasharasha zinaendelea.
Kwa sababu hiyo waislamu wa Moshi mjini wameswali swala ya Eid Alfitri misikitini badala ya uwanja wa Mandela ambao ulikuwa umepangwa mwanzo kwamba hapo ndipo ingeswaliwa swala ya Eid Al fitri.
Mimi nimeswali swala ya Eid Alfitri katika msikiti wa Jundubu bin Junada unaopatikana kwenye makutano ya mtaa wa Mafuta na Kawawa manispaa ya Moshi.
Swala ya Eid imeswalishwa na imamu Ustaadh Abdul Rahman kutoka chuo cha IBNI TAIMIYYAH kilichopo Ponge JK ijini Tanga, na khutba ya Eid imetolewa na fadhiylatul Sheikh Abuu Nufaida Hussein Said Sembe.

UJUMBE WA KHUTBA YA EID.
Sheikh baada ya kumhimidi Allaah na kumswalia mtume صلى الله عليه وآله وسلم
kafungua khutba kwa kuwapongeza waislamu kwa kuwafikishwa kuumaliza mwezi wa Ramadhani. Sheikh amebainisha kuwa siku ya Eid ni siku ya kufurahi kwa kula na kunywa vyakula na vinywaji vya halali na kufurahi kwa kumtaja Allaah سبحانه وتعالى .
Katika kubainisha msingi wa furaha ya Eid sheikh kaitaja hadithi ya mtume isemayo kwamba yule atakayefunga Ramadhani kwa imani na kutaraji malipo ya Allaah, Allaah atamsamehe madhambi yake yaliyotangulia.
Kisha akaitaja hadithi nyingine ambayo mtume kasema kwamba : "Mfungaji anazo furaha mbili:
Furaha ya kwanza ni wakati anapofungua na furaha nyingine ni siku atakapokutana na mola wake . (Siku ya qiyama).
Pia sheikh kawahimiza waislamu kuendelea kusimamisha swala tano na kujiweka mbali na madhambi na kuendelea kumtaja Allaah kwa wingi na kumuomba msamaha kama ilivyokuwa ndani ya mwezi wa Ramadhani.
Mwisho wa khutba sheikh alitoa mawaidha maalumu kwa ajili ya wanawake na akina mama ambapo kwanza kabisa amekemea tabia ya wanawake kulegeza sauti zao wanapozungumza na wanaume ambao sio waume zao kwakuwa tabia hii Allaah ameikataza kupitia Quran tukufu.
Pia kawahimiza wanawake kushikamana na vazi la hijabu na kuwataka wazipuuze kelele za makafiri wa kimagharibi na wanaharakati wapotevu wanaodai kwamba uislamu unamkandamiza mwanamke na kumnyima haki zake.
Pia kawataka wanawake kushirikiana na waume zao katika swala la malezi ya watoto na kwamba haitakiwi wazazi kuwaacha watoto wao wakizurura hovyo siku ya Eid kama mbuzi wasiokuwa na mchungaji.
Pia sheikh kawataka waislamu furaha yao ya Eid iwe katika mipaka aliyoiweka Allaah na mtume na kuwataka kutojiingiza katika mambo ambayo hayana uhusiano na mila na desturi za kiislamu kama madisko, matamasha na mabonanza yanayoandaliwa na makafiri na watu waovu kwa ajili ya kuwaingiza waislamu katika madhambi baada ya kumaliza funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kwa muhtasari huo ndio ujumbe uliotolewa katika khutba ya Eid Al fitri katika msikiti wa Jundubu bin Junada Moshi mjini.
Eid Mubaarack.
تقبل الله منا ومنكم.
 
Ndugu yetu @Chifu mkuu , anafunga msimamo wake na kuupambania kana kwamba ambao Wana msimamo wa pili wamepotoka wote kwa msimamo huo , wakati jambo hili ni lenye hitilafu kubwa hata Wanazuoni wakubwa wa zama zetu wakina Sheikh Ibn Uthaymeen, Ibn Baaz na Albani (Allaah awarehemu wote) wao wametolea ufafanuzi pia suala hili vizuri na kati ya hao hakuna hata mmoja aliyesoma ni makosa kusikia mwezi mahala Fulani (nchi nyingine) Kisha usifunge au kufungua , na wengine wameweka wazi kuwa msimamo wao kuwa kila watu wafuate mamlaka katika nchi Yao mahali walipo.
Sheikh ibn Baaz alisema ni "uwendawazimu dunia yote kufunga siku moja" kwa sababu maumbile ya dunia yenyewe yanakataa (yaani geography).

Msimamo wake ni kuwa kila eneo kufuata mwandamo wake.

Sheikh Al-Uthaymeen alikuwa na msimamo kama Ibn Baaz, kwamba kila nchi inapaswa kufuata mwandamo wake, mradi wanazingatia ushahidi wa kisharia. Alisema kwamba kutokana na tofauti za maeneo na vipindi vya kuonekana kwa mwezi, si lazima nchi zote zifuate mwandamo mmoja.

Dalili alizozitumia ni pamoja na kauli ya Ibn Abbas (Radhiya Allahu Anhu) alipokataa kufuata mwandamo wa Muawiyah (Radhiya Allahu Anhu) kwa sababu mwezi haukuwa umeonekana katika mji wake. Hadithi hii inapatikana katika Sahih Muslim.

Hadithi ambayo huyu ndugu yetu Chifu mkuu anasema haipo wazi!

Ukifika Makka kwenye vibanda vya fatawa unaruhusiwa kuuliza swali tena ni bure bila gharama yoyote. Chifu mkuu aende akaulize hilo swali kule aangalie atapatiwa jawabu gani!

Hii ndiyo inaitwa kushibishwa itikadi. Yaani anashibishwa itikadi bila ya elimu, ni hatari hii.

Na ikiwa mhusika ana itakidi hivi, tumuulize; kama mwezi ni mmoja, Korea ya Kusini maghribi ikiingia yeye aliyepo huku Tz anaweza akafuturu? Kwamba Alhamdulillah mwezi ni mmoja duniani Korea ya kusini sasa hivi magharibi imeingia ngoja nifungulie!
 
Para ya 3 huyo mwenzako jana aliikataa, alisema ni funga ni siku 30, hakuna 28, au 29, ni 30 tyuh, na sio hiyo 31.

Ndo maana niliendelea na mjadala, nilicho kigundua, nyie wenyewe wahusika hamjui nini kinatakiwa kifuatwe, aidha siku timilifu za mfungo, au muandamo wa mwezi.

Naomba unijibu hili, EID inategemea siku timilifu za mfungo, au muandamo wa mwezi?
Mwezi kuonekana kwa mzunguko wake ni siku 29 au 30.

Ina maanisha kuwa mwezi unaweza kuonekana kwa mzunguko wa siku 29 au 30 na si zaidi ya hapo. Kama ikitokea siku 28 basi nao huo utakuwa ni mzunguko wake pia.

Unachotakiwa kuelewa: Ibada ya kiislamu inaenda na maumbile ya dunia na uhalisia wa maisha ya binadamu.

Mwenyezi Mungu ameufanya mfumo wa jua na mwezi kuwa thabiti: Kama mzunguko wa dunia na kuleta mabadiliko ya siku na watu wengine wakatenga kwamba siku hizi kwetu ni muhimu na za kuabudiwa, kwa upande wa kiislamu nyakati zao hazipimwi kwa mabadiliko ya siku pekee kwenye ibada zao, halikadhalika na zile nyakati zilizomo kwenye mzunguko wa dunia. Hivyo masaa yao na calendar yao na mahesabu yao yanafuata kanuni za kiasili za kiulimwengu.

Jua na mwezi haviwezi kubadilishwa na binadamu, hivyo mfumo wa Kiislamu hauwezi kuharibiwa na mabadiliko ya kisiasa au teknolojia.

Kalenda ya Kiislamu haitegemei taratibu za wanadamu bali ni za kiasili, zinazodumu milele.

Hitimisho:
Uislamu ni dini ya kimaumbile na nyakati za ibada zinaendana na mzunguko wa jua na mwezi kwa sababu ni mfumo wa Mungu uliowekwa kwa faida ya wanadamu. Mfumo huu ni rahisi, wa asili, wa uhakika, na unadumu milele.
 
Sheikh ibn Baaz alisema ni "uwendawazimu dunia yote kufunga siku moja" kwa sababu maumbile ya dunia yenyewe yanakataa (yaani geography).

Msimamo wake ni kuwa kila eneo kufuata mwandamo wake.

Sheikh Al-Uthaymeen alikuwa na msimamo kama Ibn Baaz, kwamba kila nchi inapaswa kufuata mwandamo wake, mradi wanazingatia ushahidi wa kisharia. Alisema kwamba kutokana na tofauti za maeneo na vipindi vya kuonekana kwa mwezi, si lazima nchi zote zifuate mwandamo mmoja.

Dalili alizozitumia ni pamoja na kauli ya Ibn Abbas (Radhiya Allahu Anhu) alipokataa kufuata mwandamo wa Muawiyah (Radhiya Allahu Anhu) kwa sababu mwezi haukuwa umeonekana katika mji wake. Hadithi hii inapatikana katika Sahih Muslim.

Hadithi ambayo huyu ndugu yetu Chifu mkuu anasema haipo wazi!

Ukifika Makka kwenye vibanda vya fatawa unaruhusiwa kuuliza swali tena ni bure bila gharama yoyote. Chifu mkuu aende akaulize hilo swali kule aangalie atapatiwa jawabu gani!

Hii ndiyo inaitwa kushibishwa itikadi. Yaani anashibishwa itikadi bila ya elimu, ni hatari hii.

Na ikiwa mhusika ana itakidi hivi, tumuulize; kama mwezi ni mmoja, Korea ya Kusini maghribi ikiingia yeye aliyepo huku Tz anaweza akafuturu? Kwamba Alhamdulillah mwezi ni mmoja duniani Korea ya kusini sasa hivi magharibi imeingia ngoja nifungulie!
Hoja zenu zote zinajibika kirahisi ila kwa Sasa ni muda wa chai na naona mvua inapungua ngoja nikanywe chai kisha narudi kizijibu hoja zenu zote.
Lakini nina maswali ambayo nitakuulizeni na nitahitaji majibu ya kielimu na sio ubabaishaji!.
 
Halikadhalika na kwako pia ujibu maswali yetu, tena kwa ufahamu wa kielimu na wala si kwa rai yako.
 
Hoja zenu zote zinajibika kirahisi ila kwa Sasa ni muda wa chai na naona mvua inapungua ngoja nikanywe chai kisha narudi kizijibu hoja zenu zote.
Lakini nina maswali ambayo nitakuulizeni na nitahitaji majibu ya kielimu na sio ubabaishaji!.
Kheri mkuu , utaendelea na Hammaz kwa upande wangu Elimu yangu ndogo bado najitafuta na sijafikia uwezo wa kufanya mijadala ya kielimu na Wasomi.

Mimi kwenye hilo sijachagua upande Fulani upo sawa wala kusema upande fulani wana msimamo batili , ila niliposimamia ni kwamba jambo ambalo lina hitilafu kubwa na pande zote zina hoja na makundi ya Maulamaa wanaojulikana tena wakubwa wakispoti si vyema mtu ambaye kachagua upande mmoja kuwaona wenzake wapo kwenye batili tena bora awaone wapo kwenye batili maana inaweza litakotekea kwenye nafsi ya mtu naturally baada ya kupata Elimu ila kuwatangazia hadharani kwamba mko kwenye batili na wangu ndio sahihi wakati na unaodai wapo kwenye batili wana waliowatangulia wanavyuoni wakubwa katika msimamo wao.

Kwa hiyo najitoa kwenye majadiliano na sababu nyingine ni kwamba sijaweka wazi Mimi nipo upande upi .
 
Binafsi nilishtushwa sana na kauli ya ndugu yetu kwamba dunia nzima tunapaswa kufuata mwezi mmoja na akasema yeye ni msomi

Sasa wakati mwezi unaandama sehemu fulani ya dunia,sehemu nyingine watu ni usiku wamelaa,sasa wakipambazukiwa na siku ya funga na wao hawajatia nia usiku kwa kuwa hawakuwa na taarifa za mwandamo kabla hawajalala,je watafunga kwa nia ipi ?

Maana ili funga ijuzu basi yampasa mtu alale na nia usiku wa kuamkia mfungo

Tusifuate itikadi bali tufuate dalili za kielimu

Ntabakia kuwa msomaji kwa yatakayo endelea
 
Ewaaa!

Wasomi ndiyo wanakuwa hivyo ndugu yangu kama wewe ulivyofanya.

Wanawazuoni wametofautiana uelewa, maswahaba wenyewe wametofautiana uelewa. Hii, inampaasa aelewe kwa namna hiyo.

Tunajaribu kumuonyesha kuwa upande mwengine wa ufahamu upo hivi, hivyo akimuona mwenzake anafuata mwandamo wa eneo lake basi asimuone ya kuwa ni mjinga au yumo kwenye makosa makubwa mnoo!

Maadamu kwa wengine leo ni Eid basi tunawatakia Eid mubaraka. Na wengineo wanaweza wakawa kesho ama kesho kutwa, basi nao tutawatakia Eid mubaraka.
 
Naaam! Naam! Naam!

Tujaribu kumpindulia upande wa pili wa sarafu.

Kama mwezi ni mmoja anaweza akafungulia mwezi wa Japan?

Japan imetuzidi Tanzania mbele kwa masaa 6. Ikiwa kwetu ni saa 6 mchana basi Japan ni saa 12 ya jioni.

Anaweza kufunga ama kufungulia mwezi wa Japan ambao wametuzidi masaa 6 mbele?

Burj Khalifa, jengo refu zaidi Dubai. Masheikh walishatoa fatwa kuwa waliyojuu ya jengo zaidi na waliyo chini muda wao wa kufuturu ni tofauti.

Aliye chini kwake yeye jua linawahi kuzama hivyo anatangulia kufuturu. Aliye juu zaidi kwake jua litachelewa kuzama hivyo asubiri lizame ndipo afuturu.
 
Sasa palikuwa na mwezi wa Tanganyika na mwezi wa Zanzibar, Baada ya muungano tukabaki na mwezi mmoja! Sasa wewe uliyeenda darasani na madrassa unaweza kunisaidia kujua mwezi mmoja ulienda wapi baada ya muungano?!
Na je huu mwezi unaotangazwa na bakwata kwa Sasa ni ule wa Zanzibar au ni wa Tanganyika?!
Kabla hatujaenda kwenye hoja zingine tuanzie kwanza hapa

Twende taratibu mkuu kwamba Tanganyika kulikua na mwezi wao na Zanzibar nao walikua n mwezi wao halafu mmoja ukatumbukia baharini ?

Chifu mkuu hizi taarifa unazitoa wapi ?
 
Ewaaa!

Wasomi ndiyo wanakuwa hivyo ndugu yangu kama wewe ulivyofanya.

Wanawazuoni wametofautiana uelewa, maswahaba wenyewe wametofautiana uelewa. Hii, inampaasa aelewe kwa namna hiyo.

Tunajaribu kumuonyesha kuwa upande mwengine wa ufahamu upo hivi, hivyo akimuona mwenzake anafuata mwandamo wa eneo lake basi asimuone ya kuwa ni mjinga au yumo kwenye makosa makubwa mnoo!

Maadamu kwa wengine leo ni Eid basi tunawatakia Eid mubaraka. Na wengineo wanaweza wakawa kesho ama kesho kutwa, basi nao tutawatakia Eid mubaraka.
Baarakallaahu fiykum.
Ninakupendeni kwa ajili ya Allaah.
Nyinyi ni ndugu zangu hasa!
Mungu wetu ni mmoja.
Mtume wetu ni mmoja.
Kitabu cheti (Quran ) ni kimoja.
Na kibla cheti ni kimoja.
Kupendana ni lazima hata kama tunapishana uelewa katika baadhi ya mambo.
Mimi bado sikukuu imenishughulisha lakini nataraji baadae nitapata nafasi ya kufafanua kwa yale ambayo hamjanielewa au mmenielewa tafauti na nilivyokusudia.
Jambo ambalo nasisitiza ni kwamba mwanzo wa uzi huu hapakuwa na nukta ya kuwakosoa wenye msimamo wa mwezi wa kitaifa.
Nilianza kujenga hoja kutetea msimamo wetu na kuonyesha dosari zilizopo katika msimamo wa wenzetu baada ya wachangiaji kuanza kukosoa msimamo wa wale walioswali Eid siku ya leo.
Pamoja na yote hayo hapajaharibika neno Bado nafasi ya kuendelea kuonyeshana hoja za kila upande ipo na haimaanishi kwamba ni ugomvi.
Kwasababu naona kuna baadhi ya maeneo nimeeleweka vibaya nitakapokuwa tayari nitaanza kuzungumzia msimamo wetu juu ya ikhtilafu za wanachuoni inshaa Allaah.
Eid Mubaarack.
تقبل الله منا ومنكم.
 
Back
Top Bottom