Effects of knowing a person outside jf............prefer anonymuos

Effects of knowing a person outside jf............prefer anonymuos


mi sio muoga ila msumbufu
bibi anaweza kukuliza huyu mjukuu
wa leo umemtoa wapi ukakosa jibu babu!!

Ataniulizaje wakati anaongea na wewe?

Kwani hajui kuwa tuna wajukuu wengi kama majani??

Labda kama maswali yako yatakuwa hayana adabu...jambo ambalo yeye mwenyewe anajua adhabu ya kukugaia..lol!!

Babu DC!!
 
Ataniulizaje wakati anaongea na wewe?

Kwani hajui kuwa tuna wajukuu wengi kama majani??

Labda kama maswali yako yatakuwa hayana adabu...jambo ambalo yeye mwenyewe anajua adhabu ya kukugaia..lol!!

Babu DC!!

sawa babu tiririka macontact ya
bibi nijimwage hewani mie!!
 
Mimi niseme tu kwamba kuna baadhi yetu tunadhani JF is a dating site...HAPANA!

Na ndio kisa na maana watu wanalalamika..ukimsoma sakapal kwa undani utagundua tu kwamba hao aliokutana nao walidhani wanaenda kwenye ahadi ya ngono.

Tusisahaunkuwa japp JF ni internet forum bado inabaki kuwa ina watu halisi wenye tabia zao halisi na ambazo hazijifichi kama mkionana

Lakini mashuhuda wa undugu, urafiki, uchumba, ndoa, kufarijiana kwen misiba....kupeana michongo ya kazi...kupeana deal za biashara...
Kwa hiyo kukutaba kupo na faida zipo nyingi wameshazisema wengine na hasara zipo pia kama tukitumia fursa hii vibaya.


Baada ya kusema hayo.naomba hawa wafuatao waione hii useful post (kimoyo moyo mnaikubali eeh?)
AshaDii gfsonwin cacico snowhite FP amu Asprin Filipo marejesho KOKUTONA Arabela marejesho Arushaone Mzee wa Rula Highlander Husninyo Lady doctor Mamndenyi Bishanga Mr Rocky Invisible Paw Madame B Paloma Mtambuzi Ruttashobolwa MwanajamiiOne Ritz chama Rejao

Hakika nimeipata hii copy Kaizer.Binafsi sijawai kujuta kukutana na wana jf, wamekuwa na mchango mkubwa katika maisha yangu.
 
Last edited by a moderator:
Sijawahi mpenzi kila dakika ina thamani tangu uingie kwenye maisha yangu... You know what, I will always love you...

Good wife! I'll love you forever!

"Apataye mke apata kitu chema, naye ajipatia kibali kwa Bwana... (Mit 19:22).
Unywe maji ya birika lako mwenyewe, na maji yenye kububujika katika kisima chako...(Mit 5:15)"


Copy: Kaizer, Arushaone, PakaJimmy, Baba V, Bishanga and "many others"
 
sosoliso nawe zako zipo zote?
bombom watu wamepata masaibu kwa kutaka kujua the person behind avatar. wengine "wameng'olewa kucha" na "kukatwa kabisa vidole" imagine unaishije sasa kama sio kuwa fukara.
Ooh I didn't know your highness, I'm sorry, but its just bcause I respect u. Tell Sosoliso that I normally fear nobody on earth.
 
I Salute all MMU members!!!!!

Habari zenyu wapendwa, hope mko vizuri kakitka kusaka shekeli, me too am fine, get well soon kwa wote wanaogonjweka.
Ni hivi tangu niingie JF April 2011 ndo niliji register kama member but before was browsing kama guest it was since late 2010 na kilichonofanya nijiunge ni kuwa kuna mada zilikuwa hot hasa kwenye jokes nikitamani kuchangia naambiwa sina ruhusa hadi niji-register.

Sasa tangu nimeingia humu nimekuwa na marafiki wengi wa kike kwa wa kiume na wengine tunachat fresh tuu ila kuna watu humu kutokana na mtu anavyojipresent humu wanawish au wanakuwa na hamu ya kumuona huyu mtu ouyside jf bila kujali nini madhara yake.

Kwa mtazamo wangu finyu na kutokana na uzoefu nilioupata humu binafsi imetokea nikakutana nje ya JF na watu wawili ambao kabla sijakutana nao tulikuwa marafiki wazuri sana na tulikuwa tunachat sana ila baada tu ya kuamua kukutana nje ya jf na kujua ok kumbe sakapa ndo huyu baaas ikawa ndo mwisho wa habari, hadi hapa nilipo mitamboni mawasiliano yamekatika kabisaaaaa.

Moral of the story (according to my thinking capacity) its better and good to remain anonymous here in JF and chat and be free with everyone, kuliko kutaka kuonana na kila unayezoeana naye humu urafiki unaisha na wengine ndo wanahama kabisa JF wakati mwanzo walikuwa wahudhuriaji/wachangiaji wazuri.

Pia tabia hii imewafanya baadhi ya member humu jamvini kuja na ID mpya kila leo kwasababu tuu huko nje ya JF alishajitambulisha na akajulikana kama sakapal sasa kutokana na watu wanavomjua huko nje anajikuta anashindwa kuchangia vitu flani flani au kuwa huru humu jamvini. Binafsi sipendi tabia ya mtu kutumia ID mpya kila leo huku wana ID zao za zamani, better be urself members!!

Kuna mtu huku jamvini leo kareport mtu na bosi wake wamekutana humu jf na kupanga kukutana ile kuonana kila mtu aibu na macho yakawatoka sasa anajiuliza aache kazi au la!! hiyo inaonesha kuwa ni moja ya side effect, licha ya kuwa na perception ya matarajio ya kukutana na bonge la mtu kumbe unakutana na mbilikimo si kuja kufedheheshana huku kama alivolalama retired sister.

Sasa mfano mie sakapal tangu niingie humu ID yangu ndo hii hii sijaibadili na wala sitaanzisha nyingine ili kumkwepa mtu au ili niulize au nichangie jambo flani, hii inanifanya niwe mgumu sana kukutana na watu nje ya JF as sitaki kuwa dormant maana hapa ndo kijiwe changu nikiwa idle or bored. Ukizingatia kule FB nilishahama kitambo now ni JF kwa kwenda mbele.

Mnisamehe wote ambao nitakuwa nimewakwaza kwa mitazamo yangu finyu ni mawazo yangu tuu na uzoefu wangu wa humu jamvini.

NOTE: If you prefer sakapal as a friend, goodfriendship is here in JF outside there ni michosho na mastress tuu.

Ever remaining,

sakapal.

Haya maneno ni ya maana sana. Hata ikitokea ikalazimu kuonana si vyema ukawatajia ile ID yako ya JF. Ni hapo tu utabaki kuwa huru na salama milele hapa JF.

Lingine ni kwamba watu wengine wanapokutana na watu wanajaribu kujilinganisha na from nowhere wanaanza kuwa na chuki ambazo kwa namna nyingine zinakuja kufika mbali na kuleta madhara flani. Usipende mtu akufahamu kile unafanya na vile ulivyo. Jitahidi sana kuendelea kuwa anonymous kwani hii itapunguza mengi sana.
 
Back
Top Bottom