BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,283
Hongera zenu Watanzania mnaokaa na wazee, mnaobeba mabox kwa kuamua kufuata njia halali ili kujiingizia vipato vyenu. Ni rahisi mno kuamua kutumia short cut za kujiuza miili yenu, kubeba unga au hata kuwa wanyang'anyi wa kutumia silaha. Lakini mmeamua kutumia njia halali ili kutimiza malengo yenu. Wengi mmejisomesha na kujipatia elimu nzuri sana, mmesomesha watoto wenu, mmesomesha ndugu zenu, mmejenga nyumba za maana Tanzania au kufungua biashara au kununua nyumba huko mliko. Haya maneno ya wakosaji wala yasiwakatishe tamaa kabisa mradi mnajua nini malengo yenu. Watanzania walio nje ambao ni wasomi wengi wao wanakazi nzuri sana pamoja na kulalamika kulipa kodi kubwa lakini unaona matunda ya kodi hizo katika huduma mbali mbali muhimu za kijamii tofautu na kwetu ambako matatizi yetu ni yale yale miaka nenda miaka rudi, Hakuna maji safi, umeme siku zote ni wa shida, Wanafunzi hawana madawati au madarasa na walimu pia, Hospitali hazina madawa, vitanda au vifaa muhimu. Matatizo ambayo kwa maoni yangu yako ndani ya uwezo wetu, lakini kwa kuwa hakuna anayejali basi yapo plae miaka nenda miaka rudi.
Kwa mara nyingi tena hongera kwa Watanzania wote ambao mmeamua kujiingizia vipato vyenu kwa kutumia njia halali badala ya kutafuta njia rahisi ambazo ni haramu na kujiingiza kwenye matatizo.
Kwa mara nyingi tena hongera kwa Watanzania wote ambao mmeamua kujiingizia vipato vyenu kwa kutumia njia halali badala ya kutafuta njia rahisi ambazo ni haramu na kujiingiza kwenye matatizo.