Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani | Page 22 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Discussion in 'Great Thinkers' started by Nguruvi3, Nov 7, 2016.

 1. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #1
  Nov 7, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  ELECTION NIGHT IN AMERICA

  Ref: Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

  H.CLINTON (DEM) VS D.TRUMP (GOP)

  Wanajamvi
  Miaka , miezi, siku na ni masaa machache tu uchaguzi wa Marekani utakamilika.

  Macho ya dunia yapo Marekani kujua nani atakuwa Rais ajaye wa Taifa hilo lenye nguvu

  Uchaguzi wa Marekani unaathari kubwa kwa dunia. Ni taifa lenye nguvu za kiuchumi, kijeshi, kisiasa na kijamii zinazoathiri mataifa mengine. Kwa hali yoyote ni tukio linalogusa dunia

  Hatua zote za uchaguzi zimefanyika na upigaji kura wa awali umeshamalizika

  Kesho ni siku ya kupiga kura ambapo state zilizokuwa na uchaguzi wa awali zitamalizia na zile zinazofanya kea siku moja zitamaliza.

  Itakapofika saa 3.0 usiku saa za Marekani sawa na saa 11 saa za Tanzania vituo vya mashariki vitafungwa. Vituo vya Marekani kati na magharibi vitafunga kwa muda huo kwa nyakati zao

  Kwa kuangalia ramani ya uchaguzi na umuhimu wa Mjaimbo, matokeo yanaweza kukamilika ikifika saa 4 au 5 za Marekani kama hakutakuwa na tatizo ambazo ni sawa na saa 12 au 1 za Tz

  Uzi huu utakuwa maalumu na endelevu ukiwaletea hali halisi ya matokeo kwa muda (real time)

  Kutakuwa na uchambuzi wa kila tukio linalohusiana na uchaguzi kwa wakati

  Nyote mnakaribishwa na uzi huu utakuwa 'active' kesho Jumanne saa 2 za usiku za Marekani sawa na saa 10 usiku Tz na kuendelea hadi matokeo ya mwisho

  Hadi wakati huo endelea kuwa nasi Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

  Kaa mkao wa habari
   
 2. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #421
  Jan 5, 2017
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Sijui una maana gani unaposema bado naamini Trump atakwama, nilichosema ni kwamba Trump atapata wakti mgumu kuliko aliowahi kupata hata huyo Obama aliyemtangulia.

  Tatizo ni kwamba wengi wenu mna-underestimate feeling iliyopo mtaani following Donald Trump win. Wengine wenu yawezekana mnaishi hata Marekani lakini nina wasi wasi kama kweli mnajua hisia za walio wengi na wanavyojuta kumpa mwanya huyo bwana.

  Tofauti ni kwamba huko Marekani, watu wanapokuwa disappointed hawakai kimya, watapaza sauti zao na wataonesha hisia zao kwa matendo.

  Nafikiri mnasahau Tea Party ya Republicans baada ya ushindi wa Obama lakini nawahakikishia safari hii mambo ni tofauti kidogo. Jamaa wanasubiri Trump aapishwe halafu naomba turudi hapa jamvini tupashane yanayojiri.
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #422
  Jan 6, 2017
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Keep betting against the Trumpster!
   
 4. El Jefe

  El Jefe JF-Expert Member

  #423
  Jan 6, 2017
  Joined: Sep 13, 2016
  Messages: 225
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 80
  Huo wakati mgumu aliopata Rais Obama ni baada ya kupoteza control ya House 2010 na haikurudi tena Democrat hadi leo (miaka 6). Na balaa lingine kupoteza control ya Senate 2014 hadi leo Senate control ipo chini ya Republicans.

  Lakini ukweli ambao hutaki kuzungumzia ni kuwa Rais Obama ni responsible kwa kiasi kikubwa kwa huo 'wakati mgumu' unaouzungumzia.

  Senate Majority na House Majority ni Republican, na performance ya Trump kwa miaka miwili hii na ijayo ndio moja ya sababu kubwa itakayo-determine sura ya Congress. Sasa sijui utasemaje elections za Class I Senators na MoHR 2018 zikija kuongeza Seats kwa Republicans?

  Usikae ukaamini kuwa Republicans wataenda kumuangusha Rais wa chama chao na kuwapa ahueni Democrats ambao wamekuwa na WH kwa miaka minane. Party politics kwenye Congress ni strong kuliko unavyodhani.

  Lakini ugumu anaoupata POTUS ni kutokana na suala na suala. Lindsey Graham na John McCain wanaweza kuwa na mawazo tofauti kuhusu Putin na Russia lakini wote wanasupport sera nyingi za Trump.

  Hizo hisia za walio wengi umezipimaje?

  Kweli, lakini pia kuna unafiki mwingi tu kwenye hayo mambo. Nadhani ulisikia kuwa waandamaji wengi tu walilipwa kuandamana kumpinga Trump na kuwashawishi Electors wa Rep wasimpigie kura Trump. Hadi Eectors walitishiwa kuuawa.

  Kuna waandamanaji walikuwa wakiandamana huku wakiwa hawajui wanachoandamania. Namaanisha kuna watu wengi tu walikuwa wakimpinga Trump kwa sababu waliambiwa ni racist, mysogynist, bigot, dictator, xenophobic n.k lakini wameanza kuona kuwa kumbe vyote vilikuwa uongo tu na wanajuta kutokumpigia kura.

  Inaeleweka kuwa Democrats wanapanga kumkwamisha Trump. Hivi baada ya Trump kuwaaibisha hao Team Hilary wakiongozwa na Marais wawili wa US unategemea watampa ushirikiano 100%?.

  Usije ukashangaa huo msimamo wa Democrats ukawacost kwenye uchaguzi wa 2018 na wakaendelea kupoteza seats.

  Je, unajua kuwa katika kipindi cha Rais Obama ndipo Democrats wamepoteza zaidi kuliko kipindi chochote katika historia ya US?
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #424
  Jan 6, 2017
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  El Jefe, either you are being disingeneuous or just acting plain dumb. Republicans waliapa kumkwamisha Obama toka siku ile anaapishwa na kuhakikisha hatapata awamu ya pili na ushahidi upo. Kilichotokea ni kwamba kwa miaka miwili toka 2008, Obama kwa kutojua (ni kweli alijidanganya) went out of his way to reach out akifukuza mirage, non-partisan support!

  Ajabu ni kwamba hata pale Obama alipounga mkono mambo yaliyopendekezwa na Republicans wenyewe, waliamua kumruka. Affordable Care Act ilikuwa ni blue print ya care act ya Republicans na si walichotaka Democrats hivyo wengi waliamua kukaa kando na kumwachia jukumu la kuinadi peke yake. Republicans walipoona hivyo nao wakaamua kuipinga na hicho ndicho kilichowafanya Democrats kuzinduka na kuipitisha bila Republican hata moja kuwaunga mkono.

  Republicans baada ya ACA kupitishwa na kuona inaanza kupendwa waliamua kufanya jitihada za kuihujumu kwa lengo la kuikwamisha. Mbinu moja waliyoitumia na ikafanikiwa miongoni mwa watu wenye uelewa mdogo ni kuibatiza jina la Obama Care Act na kujaribu kuonesha kuwa ni tofauti na Affordable Care Act. Kwa kitendo hiki Republicans wakafanikiwa kuwachanganya wengi wakiamini hivi ni vitu viwili tofauti...wako waliopenda ACA na si Obama Care.
  Ndiyo hiyo ni kweli, Obama alisababisha hali hiyo kwani alijikita katika kutafuta muafaka ambao hangeupata kwa watu walioapa toka awali kumkwamisha. Kwa kufanya hivyo ili kutimiza ndoto yake kama unifier akawasahau Democrats ambao nao kwa upande wao wakaamua kuwa kama watazamaji tu!
  Ni kweli Trump ana Senate na House majority lakini sidhani kama anamfikia Obama mwaka 2008. Njia pekee aliyo nayo tofauti na alichofanya Obama ni kuvitumia hivyo vyombo viwili kusukuma ajenda zake, partisan politics, bila kujali wapinzani wake wanasemaje. Tatizo alilo nalo ni kwamba kwanza, anaingia White House na idadi ndogo ya Wamarekani. La pili ni kwamba hana total support ndani ya chama chake na positively zero support nje ya chama chake.
  Nadhani kwa hiyo sentensi ya pili umejijibu na juzi tu tumeshuhudia Republicans wakianza kwa kujikwaa.
  Nazipima kwa kura karibu milioni tatu za Democrats dhidi ya Republicans.
  Nitajie uongo moja tu aliopandikiziwa Donald Trump. Ninavyojua watu wengi wanajuta si kwa kutompigia kura Trump bali kwa kumpuuzia na hivyo kutokujitokeza kupiga kura dhidi yake!
  Huo mpango uliusikia wapi? Na hata kama ingekuwa kweli...au ni yale yale ya mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu uchungu.
  Kama msimamo kama huo wa Republicans kumkwamisha Obama uliwanufaisha kwenye uchaguzi wa 2010 kwa nini iwe tofauti kwa Democrats? Unaona unavyoongozwa na mihemuko!
  Lakini bado wakampa Obama kipindi cha pili mwaka 2012 na sasa anauacha Urais akiwa anapendwa kwa zaidi ya asilia 50% ya Wamarekani. Subiri shujaa wako Trump aapishwe baadaye mwezi huu...weka tu akiba ya maneno.
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #425
  Jan 7, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Mitch McConnell alisema. Kwamba, Obama awe one term president
  Na hapa ndipo wengi hawana ufahamu.

  GOP hawana affordable care. Wanachokifanya ni kutengeneza mbadala wa Obamacare.
  Hawakuwa na sera bali kushambulia Obama care bila kitu mbadala.

  Repubican hawakuwa na detailed act kwasababu Obamacare originally ni yao

  Hili lina maana, Watu walipiga kura dhidi ya Obamacare bila kujua ACA ya Republican

  Kitakachotokea sasa hivi baada ya watu kujiunga zaidi
  1. Kufuta Obamacare na kuleta tatizo katika uchumi kama wanvyoonyesha wasomi
  2. Kubakiza Obamacare katika baadhi ya vifungu na hiyo itabaki kuwa Obamacare

  Nimesoma WSJ kwamba inawezekana siku 100 za kwanza hiyo act isiwe tayari
  Na kwamba tayari kuna mgawanyiko Republican

  Mgawanyiko unatokana na ukweli wengi waliona nafuu ya Obamacare hata kama kuna premiums zimeongezeka.Dem wanakiri , wanachosema suluhu si kubomoa ni kukarabati

  Affordable care inaonekana katika mtazamo wa 'build the wall''.

  Jana Trump kasema ataomba congress wasaidie kujenga ukuta tofauti na kauli yake ukuta utajengwa na Mexico. Ugumu wa ukuta ni kutokana na mandate aliyo nayo.

  Kama ilivyo ACA , ukuta utasababisha matatizo yale yale kuwa sehemu ya jamii itakuwa na nguvu za kumpinga. Kupeleka ukuta congress ni kuwataka walipa kodi walipie.

  Unaweza kuona jinsi mambo alivyoanza kuwa tofauti na ilivyotarajiwa.
  Kwa maneno mengine ACA na ukuta anaikabidhi kwa house na senate

  Yote mawili yatahitaji pesa zisizoainishwa zitapatikana wapi.

  Tatizo hapa ni kuongezeka kwa deni kinyume na msingi wa GOP wa fiscal discipline

  Kampeni yote national debt haikuwa 'agenda' ya Trump.

  Swali , kwa gharama zinazoonekana ataweza kushawishi Republican 'spending spree'?

  Hili litawagawa Republican, kuna program ya infrastructure na tax cut kama walivyoahidi

  Kufanyia ACA marekebisho ni kudumisha Obamacare kitu Republican wasichokitaka
   
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #426
  Jan 7, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  TAARIFA YA 'INTEL COMMUNITY'

  Rais mteule Trump amekutana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama 'intelligence community'
  Ni baada ya wiki takribani moja ya 'kuvisema' hadharani vyombo hivyo kwa tweets

  HIilo limeumiza IC na kusema ni haki kwa Trump kukosoa,si vema kudharau(disparage)

  Kauli imekuja baada ya Trump kusema ana taarifa wengi wasio nazo angezito J5 au Alhm

  Trump aliyasema kwa jitihada za kitisha IC kama pre-preemptive strategy
  IC ilishikilia msimamo hakukuwa na kuahirishwa kwa mkutano bali ulipangwa Ijumaa

  Wiki nzima habari ikawa Russia, Trump akatumia mbinu kuondoa watu katika hoja
  Kwanza, alitoa taarifa ya kupunguza mamlaka ya NSA akitaraji ingechukua uzito

  Pili, zikaja 'tetesi' atabadili mabalozi waliochaguliwa na Obama, halikubadili majadiliano

  Tatu, akaja na tweets akimlaumu Shwatzniger kwa rating ndogo ya apprentice
  Yote aliyafanya kupunguza mjadala unaomhusu yeye na IC na jinsi alivyowadharau

  Dharau kubwa ni kusema J. Assenge amesema Russia haikuhusika.
  Wengi walihoji Rais wa US kusimama na Assenge na Russia dhidi ya IC yake

  Hatimaye IC imekutana naye na kutoa taarifa ambayo baadhi ya maeneo ni 'classified'
  Habari classified ni wanazohisi ni muhimu kuendelea kufanyia kazi na si kwa umma

  Taarifa ime eleza mengi, kwamba, Russia na Putin wamehusika.
  Vyama vyote vilifanyiwa hacking, kulikuwa na lengo la kumdhuru Clinton(unfair)

  IC inasema wana uhakika. IC ikasema Russia walihusika ingawa impact yake kisiasa hawakufanya kwasababu si kazi yao kufuatilia mienendo ya siasa

  IC imesema wazi hakukuwa na kuingiliwa kwa mfumo wa upigaji kura kwa namna yoyote

  Trump ametoa taarifa Russia haikuathiri matokeo yaliyopo kwa namna nyingine yoyote

  Taarifa ya mteule haikuvisema vyombo vya ulinzi ikiwa ni dalili ya kukubaliana na taarifa
  Trump anasema, ataunda tume kwa ajili ya kuangalia cyber security

  Kwa mnaofuatilia mjadala, kuna mambo tuliyasema ambayo sasa yanazidi kujitokeza
  Tweets za Trump ni za ku divert attention, na inaonekana media imelitambua hilo

  Pili, hakuna namna uchaguzi wa US ambao ni local unaweza kuwa hacked kwa ujumla
  Na kwamba, tatizo linaloonekana si ushindi, bali namna uchaguzi ulivyoingiliwa

  Mwisho tukasema tweets na ugomvi na IC za US hautakuwa na mwisho mzuri kwa DT

  IC, inaonekana transition team imekubaliana na suala moja, Russia walihusika

  Walihusika kiasi gani na impact yake ni ipi, ni suala jingine

  Tusemezane
   
 8. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #427
  Jan 8, 2017
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Uzuri wa Marekani ni kwamba hakuna mwenye uwezo wa kuzima uchunguzi unaotarajiwa kufanyika hata akiwa Rais na haijalishi huo uchunguzi unachukua muda gani. Kuhusika kwa Russia si swali tena bali impact yake katika zoezi zima la uchaguzi na bahati nzuri ushahidi wa maneno na video upo.

  Transition team ya Trump inajitahidi kweli kweli kujaribu kupunguza makali ya ripoti ya IC ingawa wengi wao hawajui kwa undani kilichopo kwenye Classified Report. Kwanza Trump mwenyewe hawezi kuwapa hizo taarifa alizopewa, hivyo kwa kiwango fulani ni kwamba wanajitahidi kutetea wasichokijua.

  Hata hivyo muhtasari wa Declassified report yenye kurasa 6 ambayo sasa iko mtandaoni imeweka wazi wikileaks walikuwa wanapata ripoti zao kutoka wapi. Hii ndiyo sababu hata pale ilipozimiwa mtandao bado ripoti ziliendelea kutoka na swali litakalohitaji majibu ni uhusiano wa Trump team na wikileaks.

  Kwa nini Donald Trump alikuwa anakataa uhusika na Russia lakini alikuwa mwepesi sana kukiri uhusika wa wikileaks huku akiidondoa na kuisifu kwa kazi nzuri. Pamoja na kukataa uhusika wa Russia yuko kwenye rekodi akiiomba Russia ku hack na kuweka wazi Email za mpinzani wake Hillary Clinton.
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #428
  Jan 8, 2017
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mimi sikubali kwamba hiyo inayodaiwa kuwa ndo hacking ya Russia imemsaidia Trump.

  Kwa nini nasema hivyo?

  Nasema hivyo kwa sababu ukilinganisha hizo emails ambazo inadaiwa zilipatikana kutokana na hiyo hacking halafu ukazilinganisha na mambo alokuwa anayasema na kuyafanya Trump kwenye campaign trail, hizo email zina pale in comparison.

  Hizo emails ukizilinganisha na ile tape ya Trump ya ku grab them by the pussy, utaona kuwa haziko damning kabisa kama hiyo tape.

  Ile tape ilipovuja ni nani ambaye hakudhani kuwa huo ndo ulikuwa msumari wa mwisho kwenye jeneza la Trump?

  Trump alisema na kufanya mengi mno ambayo yako damning dhidi yake kuliko hizo emails zilizodukuliwa.

  Ni kitu gani au jambo gani kwenye hizo emails ambalo hata linaweza hata kukaribiana na hiyo tape ya Trump au kile kitendo chake cha kumkejeli yule mwandishi mlemavu?

  Sasa iweje emails ambazo hazikuwa damning kabisa ukizilinganisha na matendo na kauli za Trump ndo ziwe sababu ya Hillary kushindwa?

  Haiwezekani hata kidogo. Hillary kashindwa kihalali kabisa na kuilaumu Urusi ni jaribio tu la kuhamisha lawama.

  Hillary hakuwa mgombea mzuri. Hata mwaka 2008 yeye ndo alikuwa favorite wa kupata nomination lakini akashindwa na Obama.

  Mwaka huu nao kama isingekuwa figisu za vigogo wa chama chake basi mzee Bernie Sanders alikuwa anaibuka kidedea.

  Lakini kwa vile vigogo wa Democrats walikuwa wanamtaka Hillary basi ikabidi wafanye figisu ili aipate hiyo nomination.

  Licha ya figisu zote dhidi ya Bernie, mzee alimchachafya kweli huyo bibi.

  Kwa hiyo naamini kabisa kuwa hiyo hacking inayodaiwa, kama ni kweli ilitokea, haikuwa na athari zozote zile katika kushinda kwa Trump na kushindwa kwa Hillary.
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #429
  Jan 8, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Juzi ali tweet,wasiotaka uhusiano mzuri wa US na Russia ni 'stupid'. Hili litamsumbua sana katika uongozi

  Kwanza, Republican kama akina McCain na Graham kama viongozi wanazidi kukereka
  Nao wataonyesha misuli yao wakati wakiwa na 'kisu' hasa kupitisha sera

  Pili, kuendeleza malumbano na IC ambao wamempa ushahidi ni kutafuta mengine

  Uhusiano wake na Russia utakuwa kisiasa tu. Kiulinzi , usalama na kiuchumi vitakavyohitaji mkono wa congress vitakutana na vikwazo kwasababu tayari kuna shaka juu yake na Russia

  Uhusiano mbaya kati yake na IC utafungua matatizo mengine.
  IC, obvious wanachukizwa na Trump kumuamini Putin na Assange watataka ku prove him wrong.

  Itachukua muda lakini lazima interest za Trump Russia zitawekwa wazi.
  IC wana uwezo huo, hawataweka kama wao bali wataziacha tu zizagae au wanaweza ku leak

  By the way alisema anajua mengi atayaweka wazi Jumatano au alhamisi, hakuyaweka

  MKUTANO

  Jumatano Trump atakuwa na mkutano na waandishi.

  Kwa kumbu kumbu, utakuwa mkutano wake rasmi kwa zaidi ya siku 160, mara ya mwisho ikiwa ni July

  Trump amepanga mkutano huo Jumatano, wakati Obama ana farewell speech Jumanne jioni

  Hapa kuna mambo mawili
  1. Kwanza, ili apate nafasi ya kujibu hoja za Obama kama itabidi.

  Kwa weledi wa Obama haitarajiwi ataeleza lolote lenye utata zaidi ya kuweka rekodi yake sawa.

  Hili litaleta ugumu katika kumjibu au kumshambulia.

  2. Trump anataka habari za farewell speech zisivume katika media.
  Njia rahisi ni kufanya mkutano baada ya hapo ili habari zake zifunike

  Trump anaweza kufanikiwa kufunika habari za Obama
  Tatizo ni kuwa atakutana na waandishi akiwa president elect, the stake is too high.

  Maswali atakayokutana nayo hayata reflect hotuba ya Obama bali tweets zake

  Ataulizwa kuhusu mambo ya dunia kwa ujumla, na mwelekeo wa serikali yake
   
 11. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #430
  Jan 9, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Hii ni sehemu moja ya suala zima. Sehemu ya hacking inahusu Russia kuingilia uchaguzi wa Marekani.

  IC na zile za Poland na Ujerumani zimeeleza hali kama hiyo. Hivyo, hoja si kama ameshinda au la, ni involvement ya Russia na kwamba kuna interest gani.
  Tape ilikuwa na mtazamo wa jamii ambao sehemu kubwa walikuwa wanawake.

  Emails zilikuwa kwa mtazamo wa Democrats ambao ziliumiza Dem 'within'

  Kama utakumbuka uzi wa primaries tulijadili,Trump atashinda hata GOP wakiungana

  Trump alikuwa anashinda katika wastani wa 30% wengine wakigawana.

  Hii maana yake alikuwa na base ya 30% isiyojali nini kinatokea bali Trump

  Katikati kulikuwa na independents ambao ni 'tie breaker' ilivyo wa US

  Ndani ya Democrats kuliwa na timbwili la Bernie Sanders na Clinton.

  Bernie alikuwa millennial wengi waliomuunga mkono. Ilifikia mahali na kama ulivyosema ilionekana DNC walikuwa wana favour Clinton

  Hiyo ilibaki 'speculation' ikiwa ina doubts miongoni mwa Millennials.

  Kuvuja kwa emails kuliamsha hisia na kuonyesha mengine ambayo hayakupaswa kuwa wazi kwa public

  Hapo ndipo effects ya leaking emails inapoonkena. Ddamning effects ilikuwa ndani ya Democrats na si nje. Hivyo millennial walioegemea Dem hawakupiga kura kwasababu hawakumpenda Trump, na hakupiga kura kwasababu ya hasira zao dhidi ya Clinton iliyotokana na uchaguzi ndani ya Democrats

  Kwa msingi huo, Trump haku gain chochote kutoka kwa millenial wa Dem, lakini Clinton ali loose kwa millennial waliotegemea kumpa boost kama ilivyokuwa kwa Obama.

  Kama utakumbuka Obama aliombwa sana kusaidia kuamsha hamasa ya Millennial kutokana na hilo

  Uchaguzi ukahamia kwa independents ambapo tayari mmoja alisha lose camp mwingine hakuathirika

  Kwa hesabu mmoja alipoteza na mwingine hakupata lakini hakupoteza
  Athari si kwa Trump kwasababu katika makundi, alikuwa na kundi lisilojali amefanya nini. Walioathirika na aliyofanya ni Republican ambao siyo necessary kuwa walipigia Dem
  Independents walikuwa na uwezo wa kupima athari za wote, kauli, matendo na emails
  Democrats wali 'suppress' wapiga kura wao waliokuwa na shaka kuhusu process, emails zika confirm na hivyo hawakupiga kura kwa GOP na Dem, lakini aliyeathirika ni Dem
  Kashindwa perfect and square, lakini si hoja ya hacking
  IC imesema hakuna ballot box yoyote iliyoathirika na hacking.

  Kuna hoja labda tujiulize. Kwanza, tusahau na to assume hakuna impact yoyote katika uchaguzi
  1. Je, Russia wali hack uchaguzi?
  2. Je, wali hack vyama vyote?
  3. Kwanini walitoa emails za Dem peke yake?
  5. Je, Russia walifanya hivyo kujifurahisha au walikuwa na sababu?
  6. Malalamiko ya Ujerumani na Poland kama ya US ni ya kweli au ni uzushi?
  7. Kwanini Trump hatoi evidence nyingine ku refute taarifa ya IC
  8. Kwanini Trump anaamini Assenge na Russia kuliko vyombo vyake tarehe 20?
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #431
  Jan 9, 2017
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Yatasemwa mengi sana lakini ukweli ni kwamba:

  [1] Hillary alikuwa ni mgombea mbovu. Zaidi ya jinsia yake hakuwa na jingine lolote lile la kutia hamasa. Shabaha yake kubwa ilikuwa ni kuvunja lile 'dari la kioo' na kuwa mwanamke wa kwanza kuwa rais wa Marekani. Hakuwa na jingine zaidi ya hapo.

  [2] Huu ulikuwa ni uchaguzi wa mabadiliko [change election]. Mara nyingi Wamarekani huwa hawatoi mihula mitatu kwa chama kimoja. Ni jambo gumu sana. Hata Al Gore alishindwa licha ya uchumi kuwa katika hali nzuri ile mwaka 2000. Aliweza George H.W. Bush lakini matokeo yake akaja kuja kuwa rais wa muhula mmoja tu. Bush alibahatika tu kusafiria nyota ya Ronald Reagan. Hillary nafasi yake nzuri ya kushinda ilikuwa mwaka 2008. Lakini watu wa chama chake wakamkataa na kumpa uteuzi Obama ambaye hata hakuwa na tajiriba kama ya Hillary. 2016 haukuwa mwaka wa Democrats.

  [3] Kwa hiyo haya mambo ya sijui udukuzi na blah blah nyingine kama hizo yamejawa na siasa mno. Dems wanayatumia kwa manufaa yao ya kisiasa katika kuyaunganisha na ushindi wa Trump na yeye anajibu mapigo. Halafu utadhani wao hawana hiyo dhambi ya kujiingiza katika mambo ya nchi zingine....Haiti, Congo, Honduras, Vietnam, na kwingineko.
   
 13. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #432
  Jan 9, 2017
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Nafikiri huu ndio unapaswa kuwa ndio msingi wa mjadala bila kujali nia halisi ya waliohusika na udukuzi ilikuwa ni kumnufaisha nani. Trump kwa nafasi yake hawezi kukubali 100% kinachosemwa na intelligence agencies wake sababu atakuwa anajikaanga mwenyewe pia.

  Nilishasema kabla kwamba unless mheshimiwa Trump aje na uchunguzi mbadala utakaobaini wahusika udukuzi kuwa sio warusi basi tuhuma zilizotolewa na CIA & FBI zitaendelea kusimama. Suala la kukubaliana/kutokubaliana nao ni juu yake, pia ikiwa atachukua hatua zozote au atapotezea pia ni juu yake... lakini mwisho wa siku suala hili litaendelea kumuandama kisiasa asipochukua hatua zozote na akiendelea kupingana na intelligence agencies.

  Obama ameitwa majina mengi kwamba anaunga mkono magaidi wa kiislamu, mjamaa etc kutokana na sera zake juu ya Iran, Cuba n.k. Hivyo tusishangae sana Trump naye akiandamwa na tuhuma kwamba ni puppet wa Urusi... Ndio siasa hizo!
   
 14. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #433
  Jan 9, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Mkuu, Trump ame miss opportunity. Tulisema hapa kuwa alichopaswa kufanya ni kukaa kimya au kuungana na wenzake kuwa kulikuwa na cyber attack na hilo ataliangalia
  Jana baada ya kupata briefing za Intel community, akasema ataunda tume ya cyber security

  Yaani alimalizia pale alipopaswa kuanzia. Tulijadili hili na NN.

  Kinyume chake Trump akaanza malumbano na Intel community akiwa hana evidence yoyote ya ku back up madai yake.

  Alichokifanya ni spinning kwamba hacking haikubadili matokeo

  Hoja hiyo ilipoteza mashiko pale ambao Dem, Rep, media na Intel comm zote ziliposema ameshinda kwa kura na hakuna wizi katika upigaji.

  Akabadili na kusema wanataka ku delgitimize urais wake

  Hoja ikafa kwamba, ameshinda ndiye pres elect na hakuna wizi ni legit pres elect

  Mwisho akaanza tweets za ku denigrate intel community.

  Hapo ndipo walipokaa sawa kwani walijua kosa moja tu atalitumia vema.

  Wamempa hadi go between wa Russia na Assenge anaowaamini

  Bado ana tweet wanaotaka mahusiano mabaya ni stupid hata baada ya evidence zote

  Sasa hivi ana 'vita' na intel community, Republican achilia mbali adversary wake Dem

  Unaweza kuona alivyo drag na poor handling itakavyo mgharimu siku zijazo
  Uchunguzi mbadala alisema Jumatano au Alhamisi. Kumbe alisubiri mahojiano ya Assenge na Fox akidhani atapata mahali.
  Hana evidence ya kukabiliana na hoja za 16 security agencies ambazo unanimously zimeafiki kuwa ipo hacking na ilitoka Russia na imefanyika sehemu nyingine pia.
  Obama ni smart sana.

  Kila alichofanya alikuwa na majibu tayari

  Iran, aliuliza wenye mbadala wauweke hadharani.

  Hakuna aliyekuwa nao na in fact wengine wanakubaliana naye.

  Kilichotokea na hasa Trump alisema deal ya Iran Obama alitoa pesa cash

  Ukweli ni kuwa pesa za Iran zilikuwa zimezuiliwa na suala hilo lilifika mahakama za dunia

  Kuendelea kukaa nazo ni kuongeza interest kwasababu mwisho wa siku watalipa

  Akatumia nafasi kuibana Iran, kwa kamba waliyokuwa nao Iran na kuwatia kitanzi

  Cuba: Obama ameeleza sanction zipo miaka 50 na ushee, nini kipya kimetokea?

  Uhusiano wake na Cuba ni approach mpya ya kuingia Cuba na kufanya instigation
  Ndivyo US walivyofanya mataifa mengi.

  Obama hatakuwepo lakini 20 yrs to come outcome itaonekana. USSR haikuanguka na Reagan,ilianza mika mingi Ronald akamalizia tu

  Ujamaa: Walimtuhumu sana, akuliza ni nchi gani ya kibepari iliyofanya tofauti na yeye

  Obamacare: Hadi jana aliuliza, kama Obamacare ni mbaya mbadala upo wapi?
  Sote tunajua Trump hana na Republican wanahangaika kutengeneza sasa hivi

  Kwahiyo kuna tofauti ya u-smart kati ya wawili hao katika hatua za mwanzo tu.

  Tofauti zitaendelea kujadiliwa kutokana na maamuzi ya Trump , anaweza kufanya vizuri au vibaya hilo ni suala lisiloweza kujadilika akiwa hana power.

  So far bado anajifunza. Vita na intel community itamweka pagumu

  Maamuzi yote yataangaliwa kwa jicho la shaka sana na hilo litakuwa tatizo
  Wiki hii wanaanza confirmation ya cabinet.
   
 15. General Mangi

  General Mangi JF-Expert Member

  #434
  Jan 9, 2017
  Joined: Dec 21, 2013
  Messages: 7,098
  Likes Received: 7,161
  Trophy Points: 280
  Trump Akubali Urusi Ilifanya Udukuzi.

  Rais Mteule wa marekani Donald Trump ameikubali ripoti ya ujasusi kwamba Urusi ilihusika katika mashambulizi ya mitandao yaliyolenga kuvuruga uchaguzi wa Marekani.

  Mkuu mtarajiwa wa shughuli za ikulu katika serikali ya Trump Reince Priebus amesema na kuongeza huenda hatua zikachukuliwa.

  Akizungumza na shirika la habari la FOX siku ya Jumapili, Priebus amesema Trump anakubali kuwa kuhusu hoja hii, ni taasisi za Urusi ambazo zilihusika na uingiliaji huo wa mpangilio na shughuli katika chama cha Democratic.

  Priebus amesema Trump anapanga kuziagiza taasisi za ujasusi kutoa mapendekezo ya kuhusu kile kinachostahili kufanywa. Kwa kutegemea mapendekezo hayo, hatua zinaweza kuchukuliwa.

  Lakini timu ya mpito ya Donald Trump imekilaumu chama cha Democratic kwa kuruhusu anwani za barua pepe zao zao kudukuliwa. Timu hiyo imepuuzilia mbali ripoti za mashirika ya ujasusi kwamba Urusi iliingilia mchakato wa uchaguzi.

  Naye Rais Barrack Obama amekiri kuwa hakutiilia uzito athari ambazo habari potofu za udukuzi zinaweza kuhujumu demokrasia ya nchi, kauli inayojiri baada ya ripoti ya ujasusi kuhusu hatua ya Urusi kuingilia kati uchaguzi wa Marekani.

  Akihojiwa na shirika la habari la ABC, Obama amemtahadharisha mrithi wake anayechukua hatamu za uongozi katika muda wa wiki mbili zijazo Donald Trump kuhusu tofauti kati ya kampeni na utawala, huku akisema rais mteule hataendesha urais kama anavyoendesha biashara ya kinyumbani.

  Mahojiano hayo ya Obama yalirekodiwa Ijumaa. Siku ambayo pia shirika la ujasusi lilitoa ripoti mpya iliyosema kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin aliagiza kampeni ya udukuzi kufanywa na kuzifichua taarifa za siri na porojo kupitia vyombo vya habari kwa lengo la kumhujumu aliyekuwa mgombea wa urais wa chama cha Democratic Hillary Clinton.

  Trump akubali Urusi ilifanya udukuzi | Matukio ya Kisiasa | DW.COM | 08.01.2017
   
 16. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #435
  Jan 9, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii taarifa umeona inavyojichanganya?
   
 17. General Mangi

  General Mangi JF-Expert Member

  #436
  Jan 10, 2017
  Joined: Dec 21, 2013
  Messages: 7,098
  Likes Received: 7,161
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nilipata walakini, kwamba Trump amekubali ripoti ya IC lakini timu ya mpiti inapinga taarifa za Urusi kuingilia uchaguzi.
  May be Mwandishi anamaanisha timu ya Trump ilipinga kabla Trump hajakutana na IC
   
 18. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #437
  Jan 10, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Mkuu ukimfahamu Trump, utaelewa kwanini anafanya hivyo

  Alisema ana ushahidi atautoa kwasababu wengi hawajui.

  Ushahidi hakuwa nao alichokuwa anasubiri ni Assenge aseme ili naye adakie
  Hapa alikwenda chini sana, kwamba, Assenge anajua zaidi ya intel comm zake!

  Hoja yake ni kuwa urusi haikuingilia wala kubadili matokeo.
  Anachotaka ni hoja ibaki hapo

  IC imemueleza wazi kuwa hakuna kura iliyobadilishwa au kuibiwa.
  Wakasema hawafanyi tathmini ya mwenendo wa siasa za Marekani

  Walichokifanya ni kutafuta ukweli ikiwa Urusi iliingilia.

  Wakampa Trump kila aina ya ushahidi alioutaka
  Huko nyuma Trump alisema mbona hawaweki ushahidi

  Baada ya briefing Trump akasema ataunda cyber security team.
  Kwa maana ya kuwa amekubaliana na Intel community.

  Transition team ikasema uchaguzi haukuvurugwa,kuondoa watu ktk hoja ya Russia

  Hapa anacheza na akili za watu na kwakweli ni mtaalam

  Ni mtaalam, jana ametangaza Kushner kuwa mshauri wa WH na Ivanka ku resign Trump org.

  Matangazo hakuyatoa kwa bahati mbaya , yalikuwa ni timing kama ambavyo tweet zimekuwa

  Alichotaka ni kuondoa media katika ''confirmation hearing'' watu wake wanatiliwa mashaka

  Yupo Secession aliyeahi kunyimwa ujaji. Yupo Tillerson ambaye uhusiano wake na Russia una utata n.k

  Hivyo alitaka kuondoa media katika hilo na alifanikiwa.Habari za jana zilikuwa juu ya Kushner na Ivanka.
   
 19. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #438
  Jan 11, 2017
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Nguruvi3, leo vyombo vingi vya habari vimejikita katika mahojiano ya mteuliwa wa Trump kwa nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jeff Sessions na Senate Judiciary Committee. Hata hivyo yaliyokuwa yakiendelea kwenye mkutano wa Senate Intelligence Committee na IC, yamezua maswali yanayoweza kuleta sintofahamu kubwa mbele ya safari. Donald Trump akae chonjo!
   
 20. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #439
  Jan 11, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Ndiyo habari hiyo niliifuatilia kwa muda kupata undani wake ili tujadiliane jamvini

  ''TIMU YA TRUMP ILISHIRIKIANA NA RUSSIA''
  Kwanza,Trump ame tweet ' hakuna lolote ni kutafuta mchawi kisiasa' kwa tafasiri isiyo rasmi

  Ni kufuatia inafuatia habari zinazovuma katika media kuwa Russia na surrogates (wa kampeni yake) walikuwa na mawasiliano

  Majuzi tuliwaeleza IC ilikuwa ina andaa taarifa mbili, declassified na classified
  Classified ilifikishwa kwa Obama na Trump. Declassified ikawa public

  Mtakumbuka tulisema ugomvi wa Trump na IC si mzuri kwani watata kum- prove wrong
  Trump aliwakejel hawana ushahidi, kisha akasema wanatengeneza kesi

  IC iliandaa taarifa ikiwa na ushahidi wa 'Russia'wakishangilia ushindi wa Trump

  Katika taarifa, waliambatanisha kurasa za ushahidi wa timuTrump 'walivyoshirikiana'

  IC wanasema kurasa kwa mujibu zimewasilishwa kwa wote wawili

  IC inafuatilia kwa undani habari hizo zinazoshabihiana sana na walizo nazo

  Ni sehemu ya classified info zilizo leak katika media.Wanasema hakuna siri Washington'

  MKASA ULIVYO

  Shirika moja la Russia lilikuwa linafanya uchunguzi wa biashara za Trump Russia

  Mmoja wa wachunguzi akakutana na habari ya uhusiano wa timu ya Trump na Russia

  Habari akazifikisha kwa mtaalam mzoefu wa M16 ya Uingereza aliyezifuatilia kwa ukaribu

  Baada ya kupata ushahidi aliwasiliana na balozi wa zamani wa Uingereza nchini Urusi

  Balozi naye akawasiliana na John McCain.
  Senta McCain aktuma mtu kuona na huyo wa M16 na taarifa za uchunguzi akaletewa.

  McCain akakutana na FBI Director Comey kwa dakika 5 na kumkabidhi

  Hii ilikuwa kabla ya uchaguzi, Comey akasema hilo litaingilia uchaguzi liachwe kwanza

  Mtakumbuka tulisema kwanini Comey alitoa taarifa za email za Clinton na kama hilo halitaingilia uchaguzi? Hapa unaweza kuona 'double standard'

  Huo ndio ukawa mwanzo wa taarifa hizo kufika IC na katika seneti na Bunge

  Wakuu wa (IC), DNI,CIA, FBIA, NSA kwa pamoja walikutana na Obama na Trump na kuwapa taarifa ya hacking ya Russia na pages

  Tuwarudishe nyuma kidogo, tuliwahi kusema McCain na Senta Graham walikuwa wanajiamini sana. Sasa tunajua, kujiamini kulikuwa na sababu za 'data' za kutosha

  Ndiyo maana Spika Ryan na VP Pence walikubali Russia walikuwa wanaingilia uchaguzi

  Majina ya wahusika wa uchunguzi yapo ingawa media zimekataa kutoa kwa usalama

  Tweet ya mstari wa kwanza ya Trump inaeleza hali ilivyo kwa upande wake.

  Katika mazingira ya kawaida Trump angeandika ya kutosha.

  Sasa anasema anatafutwa mchawi wapiga debe wakishindwa kukanusha au kutihibitisha

  Picha inaanza kujionyesha kwanini Trump hakupenda uchunguzi akisema wanataka ku delegitimize Urais wake.

  Kwa hili la timu yake kuhusika, kama litathibitishwa atakuwa ame ji legitimize mwenyewe

  Tusemezane
   
 21. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #440
  Jan 11, 2017
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mkuu Nguruvi3, hizi habari hata Seneta Reed alikuwa amezidaka na ndio maana kuna wakati aliongea kwa uchungu sana dhidi ya Trump. Katika post yangu # 427 nilidokeza tu kwamba Team Trump wengi hawajui hata kile wanachotetea lakini hii habari ni nzito kweli kweli. Kesho ni kesho labda Trump aahirishe conference yake na waandishi.
   
Loading...