Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,629
2,000
ELECTION NIGHT IN AMERICA

Ref: Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

H.CLINTON (DEM) VS D.TRUMP (GOP)

Wanajamvi
Miaka , miezi, siku na ni masaa machache tu uchaguzi wa Marekani utakamilika.

Macho ya dunia yapo Marekani kujua nani atakuwa Rais ajaye wa Taifa hilo lenye nguvu

Uchaguzi wa Marekani unaathari kubwa kwa dunia. Ni taifa lenye nguvu za kiuchumi, kijeshi, kisiasa na kijamii zinazoathiri mataifa mengine. Kwa hali yoyote ni tukio linalogusa dunia

Hatua zote za uchaguzi zimefanyika na upigaji kura wa awali umeshamalizika

Kesho ni siku ya kupiga kura ambapo state zilizokuwa na uchaguzi wa awali zitamalizia na zile zinazofanya kea siku moja zitamaliza.

Itakapofika saa 3.0 usiku saa za Marekani sawa na saa 11 saa za Tanzania vituo vya mashariki vitafungwa. Vituo vya Marekani kati na magharibi vitafunga kwa muda huo kwa nyakati zao

Kwa kuangalia ramani ya uchaguzi na umuhimu wa Mjaimbo, matokeo yanaweza kukamilika ikifika saa 4 au 5 za Marekani kama hakutakuwa na tatizo ambazo ni sawa na saa 12 au 1 za Tz

Uzi huu utakuwa maalumu na endelevu ukiwaletea hali halisi ya matokeo kwa muda (real time)

Kutakuwa na uchambuzi wa kila tukio linalohusiana na uchaguzi kwa wakati

Nyote mnakaribishwa na uzi huu utakuwa 'active' kesho Jumanne saa 2 za usiku za Marekani sawa na saa 10 usiku Tz na kuendelea hadi matokeo ya mwisho

Hadi wakati huo endelea kuwa nasi Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Kaa mkao wa habari
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,011
2,000
Asante Nguruvi3, tumekaa tayari na tutafuatilia kwa makini kweli kweli uchaguzi wa Marekani...tumaini la dunia na kimbilio pekee la all the politically, socially, economically handicapped/persecuted.
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,011
2,000
Kura ya kwanza kabisa imepigwa katika kituo cha Dixville Notch, New Hampshire ambapo hadi kufikia saa tano mchana kwa saa za Tanzania Clinton anaongoza kwa kura 4 dhidi ya Trump kura mbili. Ni kawaida kwa kituo hiki kuwa cha kwanza kufungua milango ya kupigia kura toka mwaka 1960.


Voter Clay Smith smiles as he looks over the final tally on the board after voting in the U.S. presidential election at midnight in tiny Dixville Notch, N.H., on Nov. 8, 2016. (Mary Schwalm/Reuters)
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,629
2,000
Kura ya kwanza kabisa imepigwa katika kituo cha Dixville Notch, New Hampshire ambapo hadi kufikia saa tano mchana kwa saa za Tanzania Clinton anaongoza kwa kura 4 dhidi ya Trump kura mbili. Ni kawaida kwa kituo hiki kuwa cha kwanza kufungua milango ya kupigia kura toka mwaka 1960.

Voter Clay Smith smiles as he looks over the final tally on the board after voting in the U.S. presidential election at midnight in tiny Dixville Notch, N.H., on Nov. 8, 2016. (Mary Schwalm/Reuters)
Mkuu Mag3 ahsante kwa hili. Kilichotokea ni kuwa kituo hicho kilifungua milango ya kupiga kura saa 6.01 kwa saa za Marekani ikiwa ni tarehe 8 tayari

Waandishi walialikwa na walikuwa wengi kuliko wapiga kura.
Matokeo yametangazwa hapo hapo baada ya kura kupigwa.

Hili lina maana sana kwa kujifunza. Wenzetu kura zinapigwa saa 6 usiku hakuna askari, kila mtu yupo ameshuhudia upigaji kura na matangazo yametangazwa pale pale.

Hiyo ndiyo demokrasia tunayosema kuwa ipo kiwango cha juu.
Hakuna kusubiri namba zikafanyiwe 'tathmini Dar' kisha kutangazwa

Tutaendelea kuwaleta habari kila zinapojiri
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,629
2,000
NJIA ZA KUFIKIA MAGIC NUMBER 270

TRUMP

1. Njia ya kwanza, ni kushinda Arizona,North Carolina,Florida, Ohio na Iowa
Akipoteza state moja kati ya hizo njia inakuwa ngumu

2. Ashinde Pennsylvania au Michigan. Hata akipoteza North Carolina hizo mbili zitafidia upungufu

3. Asipofanikiwa kushinda Penn na Michigan atatakiwa kushinda North Carolina, Arizona, Florida, Ohio na Iowa. Halafu ashinde New Hampshire na Nevada au ashinde Colorado, Penny na Michigan

CLINTON

1. Anachotakiwa ni kushinda blue states kwa maana asipoteze hata moja kwa Trump
Halafu ashinde ima North Carolina, Florida , Ohio.

Kwa wote wawili, ikitokea state kama Colorado, Utah, Wisconsin, Arizona, Georgia, Virginia zikabadili mwendendo wao wa kawaida wa kupiga kura kutakuwa na hali zifatazo
1. Blue state zikibadilika zita favor njia ya Trump kwenda white house kuwa rahisi
2. Red state yoyote ikibadilika, ita complicate njia ya Trump na kurahisisha njia ya Clinton

Tutaendelea
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,629
2,000
Florida kuna explosions ya Latinos kupiga kura kiasi cha 300% ya mwaka 2012

Florida ina waCuba wengi ambao ni Republican kwa msimamo wao juu ya Castro na Cuba
Wanaona ni vema kukawa na vikwazo Zaidi kushinikiza Cuba

Florida kuna Puerto Rico ambao historically ni loyal kwa Democrat

Wingi wa Latino unatafsiriwa kwa namna tofauti. Je, ni wale Cuba wanaounga mkono Republican?
Je, miongoni mwao ni wale waliochukizwa na maneno ya Trump?

Hawa Latinos ni 'sleeping giant' wataamua hatma ya uchaguzi kwa baadhi ya maeneo, FL ikiwemo.

Kule Iowa, kwa taarifa za awali kura zikiendelea zinaonyesha Trump akiwa na upper hand

Arizona, misururu ni mirefu ikiwa na Latino pia

Tutaendelea
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,629
2,000
Colorado wanapiga kura kwa mail zinazotumwa kwa wapiga kura
Takribani 2/3 ya kura za awali zimeshapigwa kabla ya siku ya leo

Kuna takribani watu milioni 1 watakaopiga leo, baadhi wakiwa independents

Pennsylvania na Michigan hazina kura za awali, kwa maana leo ndiyo siku yao
Ikifika saa 2 matokeo ya kura za leo yatapatikana

Michigan haijawahi kupigia kura Republican tangu 1988 wakati wa Reagan.

Siku za mwisho za kampeni Michigan inaonekana ''battleground'' habari zisizo njema kwa Democrat
Hii ni Blue state, kwanini kuwe na wasi wasi!
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,629
2,000
Wakati tunasubiri matokeo, tuangalie baadhi ya mambo yanayoweza kuathiri uchaguzi kwa namna moja au nyingine na pengine kuleta surprise

1. Kuna Latinos 'explosion' ambayo ni mapema kusema inaeleza nini
2. Black ambao kura za awali 'early' vote idadi yao imepungua
3. White ambao wamejitokeza kwa wingi kuliko siku za nyuma
4. Wanawake ambao wamekuwa sehemu ya mjadala wa uchaguzi
5. White color walioathiri na kufungwa kwa viwanda hasa battleground state
6. Kuna Immigrant ambao nao wamekuwa sehemu ya mjadala iwe kwa asili au dini
7.Kuna historia, kwamba si rahisi chama kushika madaraka vipindi mfululizo
8.Kuna suala la mgombea mwanamke aanayeleta utofauti kati ya wagombea kama ilivyozoeleka

9. Evangelical: Hawa hawana nguvu kutokana na aina ya wagombe. Si factor kubwa

Hizi ni baadhi ya factors zitakazoangaliwa matokeo yakianza kupokelewa
CO, NV, AZ,FL,OH,NC,PEN,VR,WS, MG,

Matokeo ya FL yatatoa picha nini kinaendelea CO
Matokeo ya Ohio yatatoa picha nini kinaendelea Iowa
Kama ilivyo NH, VR, MG

Kwa upigaji kura za awali, Iowa inaonekana kuelekea kwa Trump na likely Ohio kwasababu tulizoeleza hapo juu. Tunarudia kwataarifa na wala si usahihi, likely Iowa na Ohio kwenda GOP

Tutaendelea kuwajuza
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,629
2,000
North Carolina wame extend muda kwa dakika 90 kwasababu ya electronic glitch
 
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
15,209
2,000
North Carolina wame extend muda kwa dakika 90 kwasababu ya electronic glitch
electronic glitch easy way of 'rigging '. na ni kwa several states....kumbuka! ngoja baadaye tuchore ramani ya majimbo yaliyoathirika na hili!
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,629
2,000
Mag3 habari ni kuwa maafisa wa Trump kule Nevada wame file legal objections
Sababu kubwa ni ile tuliyoeleza katika uzi mwingine'

Kwamba, katika early vote kulikuwa na kufungwa vituo saa 4 badala ya saa 1
Hoja hapa ni kuwa muda ulikuwa extended kwa mujibu wao ili kutoa fursa 'kwa kundi' maalum


Hili linapingwa na ukweli kuwa wali extend muda kwasababu watu tayari walikuwa katika mstari
Sio kwamba wali extend muda kwa watu kujiunga katika foleni bali wale waliokuwepo tayari

Sijui kisheria itakuwaje

Ndani ya camp ya Trump tayari wanasema 'smell trouble' ingawa hawakusema ni kutokana na nini
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,629
2,000
electronic glitch easy way of 'rigging '. na ni kwa several states....kumbuka! ngoja baadaye tuchore ramani ya majimbo yaliyoathirika na hili!
Hawausema electronic glitch kwa sababu gani. Tusirukie conclusion kabla ya facts
Hakuna upande ulioonyesha concern kwa hili
 
S

Singo

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,062
2,000
kisiwa kidogo cha Guam nchini Marekani kimetoa ushindi kwa HC 71.63% na Trump 24.16% na mgombea mwingine Emidio Soltysik amepata 4.22% katika kura 32071 zilizopigwa.Mara nyingi matekeo ya kisiwa hiki yamekuwa yakitabiri mshindi toka 1980 .Kwa mujibu wa USA TODAY
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,629
2,000
kisiwa kidogo cha Guam nchini Marekani kimetoa ushindi kwa HC 71.63% na Trump 24.16% na mgombea mwingine Emidio Soltysik amepata 4.22% katika kura 32071 zilizopigwa.Mara nyingi matekeo ya kisiwa hiki yamekuwa yakitabiri mshindi toka 1980 .Kwa mujibu wa USA TODAY
Yes, kwa bahati mbaya hawa kama Puerto Rico na Virginia Island hawana electoral vote na hivyo impact yao ni zero katika electoral map
Hawa wanajulikana kama US territories

Hii ni kama Washington DC ambayo ni special federal district. Tofauti wao wana 3 EV lakini hawana uwakilishi katika congress. Wana delegates wasioweza kupiga kura isipokuwa kushiriki mambo ya kamati tu
 
Zogwale

Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
12,680
2,000
Tupeni msimamo wa asilimia zikoje? Azam TV hapa sasa tu wanaongea. Nataka nione machine zikichanga. Mzizi wa fitna uishe.
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,011
2,000
Ahsante, endelea kutujuza kitakachojiri nasi tunafuatilia kutoka angle tofauti
Pingamizi la timu ya Trump dhidi ya msajili wa Uchaguzi Clark County Nevada, Joe P. Gloria, kuhusu njama za kuwaruhusu wapiga kura (early voters) nje ya muda wa saa, imetupiliwa mbali na Jaji akidai halina msingi.
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,011
2,000
Tupeni msimamo wa asilimia zikoje? Azam TV hapa sasa tu wanaongea. Nataka nione machine zikichanga. Mzizi wa fitna uishe.
Vipo vituo vitaanza kufungwa saa moja kutoka sasa na mpaka wakati huo ndio tutaanza kupata picha ya matokeo na yanakoelekea. Yako majimbo kama Clinton atashinda, Rais Mteule anaweza kujulikana mapema sana kabla ya saa sita mchana Tanzania.

Mwelekeo ni kwamba wapiga kura waliojitokeza safari hii ni wengi kweli kweli...wanaweza wakafikia milioni 200 (200,000,000) sawa na mara nne ya Watanzania wote pamoja na vichanga na vikongwe.

Pamoja na hayo tayari msafara wa mgombea Hillary Clinton umeondoka kuelekea Manhattan, New York ambako anatarajia kufuatilia matokeo.
 
Top Bottom