Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani | Page 21 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Discussion in 'Great Thinkers' started by Nguruvi3, Nov 7, 2016.

 1. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #1
  Nov 7, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  ELECTION NIGHT IN AMERICA

  Ref: Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

  H.CLINTON (DEM) VS D.TRUMP (GOP)

  Wanajamvi
  Miaka , miezi, siku na ni masaa machache tu uchaguzi wa Marekani utakamilika.

  Macho ya dunia yapo Marekani kujua nani atakuwa Rais ajaye wa Taifa hilo lenye nguvu

  Uchaguzi wa Marekani unaathari kubwa kwa dunia. Ni taifa lenye nguvu za kiuchumi, kijeshi, kisiasa na kijamii zinazoathiri mataifa mengine. Kwa hali yoyote ni tukio linalogusa dunia

  Hatua zote za uchaguzi zimefanyika na upigaji kura wa awali umeshamalizika

  Kesho ni siku ya kupiga kura ambapo state zilizokuwa na uchaguzi wa awali zitamalizia na zile zinazofanya kea siku moja zitamaliza.

  Itakapofika saa 3.0 usiku saa za Marekani sawa na saa 11 saa za Tanzania vituo vya mashariki vitafungwa. Vituo vya Marekani kati na magharibi vitafunga kwa muda huo kwa nyakati zao

  Kwa kuangalia ramani ya uchaguzi na umuhimu wa Mjaimbo, matokeo yanaweza kukamilika ikifika saa 4 au 5 za Marekani kama hakutakuwa na tatizo ambazo ni sawa na saa 12 au 1 za Tz

  Uzi huu utakuwa maalumu na endelevu ukiwaletea hali halisi ya matokeo kwa muda (real time)

  Kutakuwa na uchambuzi wa kila tukio linalohusiana na uchaguzi kwa wakati

  Nyote mnakaribishwa na uzi huu utakuwa 'active' kesho Jumanne saa 2 za usiku za Marekani sawa na saa 10 usiku Tz na kuendelea hadi matokeo ya mwisho

  Hadi wakati huo endelea kuwa nasi Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

  Kaa mkao wa habari
   
 2. El Jefe

  El Jefe JF-Expert Member

  #401
  Jan 3, 2017
  Joined: Sep 13, 2016
  Messages: 225
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 80
  Huu ndio ushahidi unaouzungumzia?

  [​IMG]

  [​IMG]

  Je USIC wametoa ushahidi wa kuhusisha Russia au serikali ya Russia mojamoja?

  Kilichotolewa mpaka sasa ni ushahidi wa kudhaniwa tu na hii inatuonesha kuwa US hawana ushahidi wa kuhusisha Russia kwenye hiyo hacking iliyotokea kwa DNC au John Podesta.

  Then USIC wanakuja wanatoa untraceable Tor IP addresses 876, hivi huo ni ushahidi ambao ni beyond reasonable doubt? IP addresses ambazo zinaweza kuwa 'spoofed' ndio ushahidi?.

  Kwani ni uongo? Au kisa amesema Trump?

  Sir, unasubiri mpaka Trump akutafunie na hilo?

  Hivi unafahamu kuna taarifa kwamba hiyo malware iliyotumika na huyo aliyewa-hack DNC na John Podesta unaweza kui-download hata wewe hapo ulipo tena bure na kuitumia?.

  Ina maana kuwa mtu yeyote anaweza kui-download hiyo malware na kuitumia kutoka katika nchi yoyote duniani.

  Kama watu wa nje ya USIC waliweza kupatia huku USIC wakikosea huko nyuma, hiyo inatakiwa ikufanye ufikiri kuwa sio kila wanachokisema ni cha ukweli hasa katika mazingira kama haya ambapo kabla ya Presidential debates walisema kitu hicho hicho then serikali ika-ignore.

  Hapa ni kuzungumza Facts tu maana USIC leaders walioteuliwa na Rais Obama wanafikiri huo mtego ni mgumu kwa Trump ambaye anasifika na kuaminika kwa kuzungumza ukweli. Ndio maana aliwataka USIC kuwa na uhakika na wanachozungumza kwa sababu mpaka sasa hivi hamna cha maana walichoonyesha.

  Wala hata sio mwanzo wa kutoaminiana na vyombo vya ulinzi na usalama bali ni muendelezo.

  Naamini hata Hillary Clinton haamini sana USIC kwa sababu walimfanya akapiga kura kuunga mkono vita ya Iraq, kura iliyom-cost kwenye uchaguzi miaka 16 baadae.

  They have to be sure.

  Trump ameshaona haja ya kufanya mabadiliko kwenye nafasi za juu kwenye US Intel. Agencies, alianza na CIA na naamini atabadilisha wengi.

  Kwani USIC wametoa ushahidi usio na shaka? Hebu tuambie namna ushahidi walioutoa ulivyo wa uhakika.

  Mbona Trump anatweet karibu kila siku na mda mwingine mara nyingi kwa siku na kila akitweet anaamsha mazungumzo. Trump anapenda kutoa reaction yake kwenye Twitter kutokana na habari ambazo zinatengeneza headlines. Katika hiyo Tweet ni wazi alikuwa anampa taarifa Kim wa N. Korea.

  Sasa utasema alivyo-tweet kuhusu China kufaidika zaidi ya US kwenye biashara baina ya nchi hizo mbili ni juhudi zake za kubadili mazungumzo? Angekuwa na nia ya kubadili mazungumzo angetuma tweets nne (4) baada ya hiyo ya North Korea chini ya masaa 13?

  Vyombo vya habari kufanya speculations ni kitu cha kawaida, hawajaanza kufanya leo. Hata kipindi hiki cha Rais Obama wamefanya sana.

  Kuhusu kuelezea hatua akakazochukua, Trump alishasema anaamini China inaweza kusaidia ku-deal na tatizo la North Korea na hakuwa na ulazima wa kutangaza hatua specifically akazochukua jana, au leo au hata kesho.

  Ni kweli utatuhabarisha, maana unachukua huko kwenye liberal sources bila kuzichuja na kutuletea huku.

  Hivi huoni kuwa hizi drama zitaisha within the next two weeks?
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #402
  Jan 3, 2017
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Ukweli ni kwamba 'internet' ni chaka.

  Na kwenye chaka mtu au kitu chochote chaweza jificha popote pale.

  Kwa hiyo hackers wa Kimarekani wanaweza wakapozi kama vile ni Warusi ili kupoteza lengo.

  Au yawezekana ikawa ni Waisrael lakini waliopozi kama vile ni Warusi.

  Na ndo maana hakuna ushahidi wa uhakika kwamba kweli Warusi ndo waliofanya huo udukuzi.

  Nyie jiulizeni tu...mdukuzi gani huyo adukue halafu aache nyayo zake waziwazi hivyo?
   
 4. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #403
  Jan 3, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  Mkuu , hawa jamaa wa US kuna nyakati nawashangaa kidogo.
  Inapofikia mahalli wanafanyiwa hacking huwa kuna kauzumbe.

  Nasema hivyo kwasababu mambo mengi magumu wanakuwa na majibu
  Katika tech wao wanafunguo zote na wanaweza kutenda tu wakiamua

  Hili suala tatizo lake ni moja, ile 'denial' ndiyo inalikuza

  Trump anakuwa Rais in two weeks time, kama kuna upikaji wa habari anayo nafasi ya kuonyesha hilo kwasababu atakuwa top.

  Kama aliwahi kusema atatafuta private investigator kuhusu emails, kuna tatizo gani akatafuta mwingine kuhusu hacking na kuwa prove wrong?

  Kwasasa anapokuwa tofauti na kila mmoja katika rank za uongozi , inatia shaka isiyo na ulazima. Kuna uwezekano wakawa Waisrael au wengine, hilo nakubaliana nalo kabisa.

  Niliwahi ku doubt sana kuhusu Bernie Sanders na habari alizokuwa nazo
  Kama unafuatilia Sanders alikuwa na mkono nyuma ingawa haikutakiwa kuonekana hivyo. Hivyo ni possible kabisa, kosa ni kukataa bila kuwa na proof
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #404
  Jan 3, 2017
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa kuwa denial ya Trump inalipa kiki suala zima.

  Ila mimi naamini kabisa kuwa suala zima liko politically motivated pia.

  Na hiyo ni kwa pande zote mbili.

  Dems kukomalia koo hizo habari kunawanufaisha kisiasa. Kunawanufaisha kwa sababu kunamjengea taswira rais mteule kuwa kasaidiwa na Urusi na hivyo ni kibaraka wa Putin.

  Na zile kauli zake kuhusu Putin na ile perceived 'bromance' iliyopo kati yao [Trump na Putin] ina play vizuri sana katika hiyo narrative ya kwamba Urusi ili hack ili kumsaidia Trump ashinde.

  Mwisho wa siku, mimi naamini, hakutakuwa na lolote lile la maana hapa. Ni kama tu ilivokuwa kwenye zile recounts za Jill Stein na zile juhudi za kuwa lobby wale electors wamtose Trump. Nothing will come of it kwa sababu suala zima liko politically motivated.

  Hivi mazee wewe huoni kama ni ajabu kidogo kama ingekuwa ni kweli kabisa Russia ndo imefanya hiyo hacking na Marekani kukiri hadharani?

  Manake kukiri hadharani ni kukiri madhaifu yenu. Na tena si kukiri tu madhaifu yenu...ni kukiri kuwa mmezidiwa kete na hasimu wenu mkuu.

  Mimi hapo ndo panaponifanya nitilie shaka.

  Nijuavyo mimi, suala kama hilo si la kukiri hadharani. Nitakupa mfano wa kivita....mara nyingi kwa mfano nchi ambazo ziko vitani ikitokea moja ya hizo nchi kuitungua ndege ya kivita ya adui....wale ambao ndege yao imetunguliwa huwa hawakiri kuwa ndege yao imetunguliwa.

  Huwa wanasema kuwa ndege yao ilidondoka kutokana hitilafu za kiufundi au hali mbaya ya hewa huku wale walioitungua wakijipongeza kwa kufanikiwa kuitungua.

  Ni suala la kipropaganda zaidi. Maana wakikiri kuwa ndege yao imetunguliwa ni sawa na kumpa adui ushindi flani hivi.

  Sasa kweli wewe huoni kama ni ajabu kidogo kwa Marekani kukiri hadharani kuwa mifumo yao ilidukuliwa na Warusi?

  Ina maana Warusi wanawazidi ujanja Wamarekani ikija kwenye hayo mambo ya makompyuta?

  Aisee mimi hilo bado haliingiii kabisa akilini kwamba Wamarekani wauanike udhaifu wao hadharani hivyo.
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #405
  Jan 3, 2017
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  WikiLeaks founder reveals a 'bombshell' about Russian hacking, Kellyanne Conway says

  Americans should listen to WikiLeaks founder Julian Assange 's denials that Russia was the source of hacked Democratic emails released by his group over the summer, said Kellyanne Conway, a senior advisor to President-elect Donald Trump .

  "This was the information that [Assange] put forward. I think that's a bombshell," Conway told CNBC's "Squawk Box" on Tuesday, referring to excerpts from a transcript released by Fox News of Assange's interview with Sean Hannity.

  Assange told Hannity that his source was not the Russian government, and "not a state party," adding President Barack Obama is trying to "delegitimize the Trump administration" with accusations that Russia engaged in hacking to help Trump beat Democrat Hillary Clinton .
   
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #406
  Jan 3, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  Angecheza kisiasa kwa kukaa kimya au kuwaambia hakubaliana na suala la kuingiliwa uchaguzi na uchunguzi uendelee ili achukue hatua akiingia madarakani.

  Kukataa kuwa si Russia akiwa hana ushahidi kunaipa 'kick' hili suala.
  Mbaya zaidi anajikuta hapambani na Dem bali IC na Congress

  Unakumbuka suala la IRS na Obama. Alichokifanya ilikuwa kuwahi na kusema uchunguzi ufanyike na ikibainika wote waliohusika wachukuliwe hatua. Moto ukapungua
  Na hasa yeye kuwa 'mtetezi' wa Russia ndiyo kabisa siasa inapata miguu

  Na hapa anaingia sec of state kwa ku insinuate kuwa wote wawili wana masilahi.

  Lakini mbaya ni pale anapohusishwa na suala la tax return, makampuni yake na uhusiano wake na Russia. Hapa ndipo patamsumbua kama si leo ni down the road
  Whatever the outcome, hili litakuwa 'strings' mbele ya safari.

  Hillary na emails ilikuwa hivi hivi, likarudi kwa kasi sana wakati wa uchaguzi

  Ni kweli lina sura ya kisiasa kama ilivyokuwa kwa emails za Clinton.

  Marekani ndivyo siasa zilivyo watakumbuka kura iliyopigwa miaka 30 na ikaleta tatizo

  Emails zilitumiwa kisiasa na Trump hadi Comey alipobadilisha mwelekeo wa uchaguzi kabisa na kuwa sehemu ya anguko la Hillary.

  Trump anasema anakwenda Washington to drain the swamp ikiwemo makosa kama ya Hillary. Watu wanapoangalia na kuona hataki uchunguzi,wanaomwamini wanaanza kupata shaka na anakaribisha curiosity hata kwa waliokuwa na doubt

  Emails za Clinton the same will happen to Trump kama hatafanya damage control mapema. Hizi tweets zinabaki kama kumbu kumbu
  Kukiri hadharani ni katika kutafuta kuungwa mkono na hilo limefanikiwa.

  Republican ndio wamekomalia kuliko Dem
  Hapa ni ku insinuate jambo litakaloanzisha hisia za 'inferiority' na US hawakubali hilo

  Sidhani washauri wa Trump wanakubaliana na tweets zake na jinsi anavyo handle suala . Kwasasa it's OK lakini linaacha alama.

  Nakuhakikishia miaka 4 baadaye litakuwa silaha dhidi yake.
  Unakumbuka TPP ya Clinton ilivyogeuka silaha ya Bernie na Trump dhidi ya Hillary.

  Unakumbuka Seccession na suala la ujaji .
  Atakuwa confirmed lakini hana uhuru wa kazi kwasababu kuna prejudice dhidi yake

  Unakumbuka kauli ya 'Najua zaidi ya majenerali' inavyomsumbua.
  Kwasasa haipo obvious lakini failure of any military mission itakuwa associated

  Katika hali inayoonyesha tatizo, Trump anasema ana habari zaidi ya watu wanazojua
  Tayari kuna swali, ni kutoka source zipi? Na anaweka wapi IC zake?

  Tatizo ana 'drag' na kulifanya story kila uchao mwenyewe
   
 8. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #407
  Jan 3, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  NN Kellyanne amekuwa katika denial kama Boss wake
  Assange alifanya kazi dhidi ya Democrat

  Ni ngumu sana kuamini hao wanaweza kuwa na credible info

  Lakini tuki assume kuwa ni kweli, je, IC zinabaki katika hali gani?

  Na Trump atakubaliana na briefing ya IC au ata dismiss kukubaliana na Assange?
  Hilo litaashiria nini mbele ya safari maana IC ndiyo source reliable kwake

  Kwahiyo kama ni ku delgitimize ushindi wa Trump, it should be Obama na IC zake
  Pia Republican kama hawatabadili msimamo wao wa sasa

  Hili suala wanalikuza bila sababu na litazidi ku deligimize hata kama si kweli

  Kwasasa media zitawaandama IC na mwisho watatoa habari zaidi
  Kisha kutatokea uchonganishi kati ya IC na Trump
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #408
  Jan 3, 2017
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Lakini Trump si mwanasiasa hivyo mambo ya kucheza kisiasa kwake hayapo.

  Jamaa hajawahi hata kuwa diwani...sasa kweli huyo unamtegemea awe na political savvy ya career politicians?

  Mimi nimeshaacha ku-bet dhidi ya Trump.

  Jamaa si tu ni teflon Don....ni Houdini kabisa.

  Ni bonge moja la escape artist.

  Rules za political gravity kwake hazi apply/ hazifanyi kazi.

  Pale unapodhani ndo kapatikana mwisho wa siku hamna kitu.

  Sema ukweli...hivi pale ile tape ya 'grab them by the pussy' ilipovuja, wewe ulidhani atapona tena?

  Mimi nilidhani katika ma blunder yake yote hiyo ndo ilikuwa msumari wa mwisho kwenye jeneza lake.

  Na si mimi tu niliyedhani hivyo...hata wabobezi wa uchambuzi wa siasa za Marekani walidai hivyo.

  Jionee mwenyewe hapo chini.....   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #409
  Jan 3, 2017
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
   
 11. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #410
  Jan 3, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  But now he is a politician ''by default'
  Katika mazingira hayo anaweza kuendelea na misimamo yake mwisho wa siku akajikuta anakosana na inner circle yake kama Pence ambao ni wanasiasa. Kukosoana kutatokana na kusigishana within na hilo lilianza wakati wa kampeni. Hadi aliporejea kwenye teleprompter wenzake akiwemo Pence walishamuacha. Walikuwa wanajenga career zao

  Katika uso wa dunia akiwa kiongozi wa Taifa lenye nguvu hawezi kuepuka diplomacy ambayo ni 'twin sister' wa politics.

  Kinyume chake atakuwa mtu wa ''controversy'' kila mara na hapo atanasa.
  Atakapokwenda oval office anaweza kucheza kwa muda lakini si muda wote.

  Wanasiasa wapo katika mshangao lakini wanamsoma

  Kwa mfano, hataki kuongea na media kwa kuogopa maswali na hoja.

  Hilo litafika mwisho kuna nyakati atalazimika kusimama kama president, hatakwepa media

  Kwasasa ana leeway ya tweet, sidhani wakati wa masuala mazito ya kidunia akiwa the most powerful man in the planet anaweza kuandika maneno matatu au character 140 akaeleweka.

  Anaweza kufanya hivyo, haitachukua muda atageuka kuwa kituko
  Tatizo anafanya kazi na politicians hawezi kuwakwepa na kukwepa politics

  Kwa mfano alisema biashara zake hazizuiwi na sheria ataweza kuacha 'holding' yake.

  Taratibu wanasiasa wamemzunguka anatafuta namna ya kukwepa conflict of interest

  Mwanzoni alisema hakuna sheria, na ni kweli hakuna. Taratibu analegeza msimamo
  Ile tape haikummaliza, kuna factor nyingine.

  Kwa mfano kwanini wanawake walio offended wamepigia kura almost sawa na Hillary!!
  Au wale waliaomini tu atafuta Obamacare unawezaje kuwashawishi kwa tape?
  Au kundi la supremacist kama lililokuja Washington hadharani, utawaeleza nini kuhusu tape. Rust belt wanakota viwanda na wanaoona TPP ilikuwa mwiba kwao, tape ile iliwadhuru kwa kiasi gani kiasi cha kuifikiria!

  Ni kweli ile tape ilihitimisha safari yake kwa mujibu wa wachambuzi na hata mini nilidhani hivyo. Kilichomsaidia kushinda si kuwa ni mwanasiasa aliyeweza kubadilisha hali, bali hali ilibadilisha mazingira ya siasa .

  Angalia Obama alivyo handle issue ya Reverend na jinsi Trump alivyo handle tape, na angalia matokeo yake.

  Wote walishinda mmoja akigeuza kibao na Trump akiacha 'nature' ifanye kazi.

  Kwamba kuna watu walishakuwa na sababu za kumpigia kura au kutompigia mpinzani wake na tape haikuathiri kabisa misimamo yao
   
 12. El Jefe

  El Jefe JF-Expert Member

  #411
  Jan 4, 2017
  Joined: Sep 13, 2016
  Messages: 225
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 80
  Diplomacy sio kukubali kulishwa taarifa ambazo watu hawana uhakika nazo na kwamba Rais mteule haruhusiwi kuhoji masuala ambayo yana chembe za kisiasa yanayomu-undermine.

  Kama kila mtu anaruhusiwa kuhoji taarifa za USIC kwanini Trump asihoji ukizingatia hilo suala halijaanza baada ya uchaguzi.

  Viongozi na raia wengi walihoji kwanini Dems wali-support kurudiwa kuhesabu kura kwenye States tatu wakati hakukuwa na ushahidi uliowasilishwa kuwa Russia wali-hack mashine za kuhesabia kura.

  Trump alivyohoji na kusema ni upotevu wa muda na fedha akabebewa mabango lakini mwisho wa siku alikuwa sahihi.

  Sasa hivi anahoji tena, anabebewa mabango. Lakini ukimsikiliza Trump sio kwamba hakutaka kura zirudiwe au kwamba hataki uchunguzi wa hacking ufanyike bali anahitaji kuona ushahidi usio na shaka ndio maana amehitaji kuwa updated na USIC.

  Hata inner circle ya Trump inazungumza lugha hiyo hiyo. Kwahiyo hata kama kutatokea kusigishana itakuwa ni baina ya Trump na Dems + Reps ambao ni anti-Russia au Anti-Putin, hao ambao hawapo na Trump kwenye mstari mmoja kwenye suala la kuimarisha mahusiano baina ya US na Russia kwa sababu ya chuki zao kwa Putin.

  Swali ni Je, kama Trump anahoji taarifa za USIC, kwanini asipewe ushahidi usio na shaka? Kwanini watu wasubirie taarifa ambazo hajapewa na USIC?

  Kila Rais ana preference yake kuhusiana na namna ya kuwasiliana na wananchi. Twitter inampa Trump nafasi ya kutupia mawazo yake briefly kwa wananchi kwa mcha mchache.

  Trump anaweza kuwa hajahold Press conference lakini ameshahold Press Interview nyingi tu na amekutana na hoja nyingi na amezijibu kadri alivyoulizwa.

  Lakini tujiulize, Hivi Trump kweli ni mtu wa kuogopa Press? Amefanya Press conference ngapi tokea alivyoanza safari yake ya kugombea Urais?. Ni wazi Trump akianza kazi yake WH atafanya Press conference.

  Suala la conflict of interest sio suala la kisiasa na Trump anaelewa hilo na ameonekana kuelewa hilo kwa mda mrefu hata kabla ya kipindi cha kampeni na kuonyesha nia ya kuondokana nalo.

  Wanasiasa wanatofautiana naye namna anavyopaswa kulitatua kabla ya kuingia madarakani na wanatofautiana kwa sababu kesi yake sio rahisi kama za Marais waliomtangulia.

  Na hata maafisa wanao-deal na ethics wanakiri hawajawahi kukutana na kesi ya COI ngumu kama ya Trump.

  Kuna uwezekano mkubwa kuwa Trump alitaka watu waelewe kwamba sheria haimbani na kwamba anafanya hivyo kwa sababu ni tradition tu kwa sababu kuna kundi kubwa la watu walikuwa wakijibu tweets zake kumuelekeza kuwa sheria inamtaka aondokane na COI.
   
 13. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #412
  Jan 4, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  Umeona jinsi anavyotoa kiki kwa hili jambo?

  Intel community imeahirisha mkutano naye hadi Ijumaa.
  Sababu kubwa kuna clasified na non clsassified infromation.

  Of course yupo entitled kwa classified walichotaka ni kuhakikisha wasiopaswa hawana access

  Trump ka tweet ''....... pengine ili wajenge kesi' kwa maana wanataka kutengeneza kesi dhidi yake

  Kwa hali yoyote hawa atafanya nao kazi, wanaweza kukaa kimya lakini wakawa source ya habari zake

  Nimeona wapo wanao insinuate kuhusu kwanini anashikia bango Russia, wanahoji analinda masilahi yake au kuna kitu gani.

  Sasa haya yote anayataka kwasababu angenyamaza hadi Ijumaa sijui kama angepungukiwa na kitu
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #413
  Jan 4, 2017
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Sawa, yeye pamoja na mahasimu wake wote kwa pamoja wanalipa kiki hilo suala.

  Binafsi nadhani litaisha tu kama zilivyoisha zile so called recounts ambazo yeye mwenyewe Trump alizidi kupata kura na hatimaye kumfanya Jill Stein apotee kabisa.

  Litaisha tu kama suala la electors lilivoisha.

  Litaisha tu kama yale maandamano dhidi yake yalivoisha.
   
 15. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #414
  Jan 4, 2017
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Unless timu ya Trump ije na uchunguzi mbadala na kutoa matokeo tofauti kuhusiana na kashfa ya udukuzi lakini kwa yeye kupingana na CIA/FBI kuhusiana na hili inaweza kumweka mtegoni siku za usoni. Tayari matamshi yake ya mara kwa mara akimsifu Putin kuwa kiongozi mzuri na kwamba atakuwa tayari kutambua eneo la Crimea kuwa ni sehemu ya Urusi yamesababisha atazamwe kwa jicho tofauti kidogo.

  The last thing Trump would want is to be viewed as "soft" or "weak" against US arch nemesis Putin. Na kitendo cha Obama kuwatimua wale diplomats kinamweka Trump kwenye mtego zaidi manake Putin ameamua kukaa kimya akimsubiri akiingia madarakani arachukua uamuzi gani whether atatengua maamuzi ya Obama ya kuwafukuza wale maafisa ubalozi au atapotezea!
   
 16. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #415
  Jan 4, 2017
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  MWALIMU MIMI nimekuwa kimya kwa sababu moja tu, thread imeingiliwa na ushabiki wa Kitanzania. Ndugu zangu Watanzania kuna wakati najiuliza hii laana tuliitoa wapi? Ubishi uliopo kwenye thread zinazomjadili Trump wetu (Magufuli) hazina tofauti na ninaoushuhudia humu.

  Lakini tofauti na sisi ni kwamba Marekani, Rais si kila kitu na kumalizika uchaguzi hauwi mwisho wa siasa, ndio mwanzo. Obama, hata kabla ya kuapishwa mwaka 2008, Republicans waliapa kumkwamisha, lakini leo hao hao Republicans wanaomba Donald Trump apewe angalau nafasi.

  Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kama kuna mtu atapata wakati mgumu Zaidi kwenye Urais Marekani, ni Donald Trump. Urais Marekani si lelemama, unatakiwa uwe na hekima, busara, uvumilivu na utunze kumbukumbu...sifa ambazo Trump hana, naomba tuzidi kuwa watazamaji.
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #416
  Jan 4, 2017
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Mwanzo mlisema hata uteuzi wa kugombea hawezi kuupata. Alipoupata mkahamisha goli mkasema hawezi kumshinda bibi.

  Sasa kamgaragaza bibi mmehamisha tena goli na mnasema atapata wakati mgumu kwenye urais.

  Keep betting against Trump.
   
 18. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #417
  Jan 4, 2017
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Mkuu Mag3,
  Umeamua kuuendeleza huo utanzania kwa kupiga ramli chonganishi?

  Naendelea kujifunza toka kwenu nyote.
   
 19. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #418
  Jan 4, 2017
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Mlisema, mkasema, mkahamisha, mmehamisha, sasa mnasema...who are you referring to?
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #419
  Jan 4, 2017
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Team Dems aka team Hillary aka team losers aka team chockers
   
 21. magode

  magode JF-Expert Member

  #420
  Jan 5, 2017
  Joined: Oct 2, 2014
  Messages: 1,471
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  Mkuu mag3 bora hata ungeendelea kukaa kimya,maana ulichoandika umeandika kitanzania haswaa...!! Yaani mpaka leo bado mnaamini trump atakwama!!? Kweli bado tuna safari ndefu. Mpaka leo hapa jukwaani mtu akiandika tofauti na maoni yenu anaonekana adui wa jukwaa..!! Ngoja me niendelee kusoma tu...
   
Loading...