Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,423
- 31,451
- Thread starter
- #1,081
Trump ana sura nyingi na huwachanganya watu,ndani na nje ya USUsikwepe post yako niliyojibu; ulizungumzia walioko nje ya marekani, siyo wamarekani wenyewe au wapiga kura wa marekani. Ninajua kuwa Marekani imegawanyika kiitikadi 47%:47%:6% kwa hiyo hata kwa wamamerakani wenyewe huwezi kusema wengi wanamshabikia hata kama haibadilishi matokeo lakini siyo warrant ya kujenerealize kuwa wengi wanamshabikia. Honestly!
Ni kiongozi anayejua kutumia ''madhaifu' katika kujiimarisha , na ndivyo alivyopanda ngazi za siasa
Kwa watu wa ndani, kuna kundi moja linalogawanyika mara mbili, watu wa vijijini. Hawa, kwanza uelewa wao ni mdogo (non college grad). Ni watu wanaoamini katika ubaguzi na huingalia Marekani kwa jicho la Mabwana na Watwana
Ni hao walioaminisha na Trump kwamba Obama si Raia wa Marekani hadi leo licha ya kila ushahidi wanamwamini tu
Trump anatumia udhaifu wa kundi hili kuwaaminisha 'uongo' akiurudia mara nyingi na huonekana ukweli
Ametumia udhaifu kuchomeka mbegu za kibaguzi kama anavyofanya sasa hivi
Kundi jingine ni lile linaloamini uongo kwasababu haliwezi kujishughulisha kutafuta ukweli
Kundi hili linajumuisha hata wasomi, watu wa mijini lakini zaidi ya hapo ' Watu wa mataifa ya nje kama Tanzania''
Mfano, Trump analiaminisha kundi hili kuwa ametengeneza uchumi bora haujawahi kutokea.
1. Kwa rekodi zilizopo Trump hakutengeneza uchumi, aliyetengeneza ni Obama
Obama aliingia unemployment ikiwa katika silimia kati ya 9-14 kutegemea eneo
Alipoondoka ilifikia asilimia takribani 4.5. Ndivyo takwimu nyingine zote zinavyoonyesha hata zile za masoko
Trump anasema ametengeneza unemployment ikafikia 3.1, swali la kujiuliza kutoka wapi? na kwa wakati gani?
2. Trump anasema ametengeneza ajira kuliko Obama. Ukitazama takwimu hakuna eneo ambalo amefanya vizuri kuliko nyakati za Obama. Kinachotokea ni mwendelezo wa mieizi 74 aliyoacha Obama ya kukua kwa uchumi
3. Siasa za kimataifa ndiyo basi tena maana ile hadhi ya Marekani imefifia
Orodha ya mambo ni mengi ambayo anaoboronga ikiwemo institutions , utawala wa sheria n.k ni ndefu
Kitu kimoja alichofanikiwa, ni kusema uongo, kuurudia hadi watu wanaamini kama ndio ukweli.
Sasa hali hiyo ikifika kwa wananchi wasiojishughulisha kama Watanzania, Trump ni lulu kwasababu kila asemacho ni ukweli. Hapa ndipo unaona watu hao wakishabikia tu, lakini waulize ni kwa nini! Hawana hoja
Kuna uzi mmoja ulianzishwa, wachangiaji wakimsifu Trump kwa kufanya mambo mazuri kwa weusi ''black' wa Marekani. Niliuliza tu ni kwa yapi mazuri? Hakuna aliyetoa jibu na uzi ukafa hapo hapo.
Hii ni kwasababu watu walisikia tu Trump akisema lakini hawana hoja za kutetea hoja zao na wala hawajishughulishi kutafuta ukweli au kutafakari kwa uwezo wa kawaida tu, wanameza