Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Asante sana , Mkuu, kwa kusoma post yangu na kupitia hiyo posti umenipa changamoto ya kupata majibu ya maswali kadhaa uliyouliza. Nakujibu kadri nilivyopata uzoefu kwenye ujukwaa hili, Mkuu wewe ukiwa mshiriki muhimu kwa kunipa uzoefu huo.

Karibu kwa majibu.
===
Zinawapotosha kina nani?
Wale wote wanaosubiri Main Stream Media (MSD) 'wanazozitaka' zitoe habari kisha wao kuzitafsiri kama zilivyo kisha kuzisambaza kama maoni yao na mara nyingi bila hata kutuonyesha kuwa 'wamechanganya za kwao'.
Nani hao wasiojifunza?
Democrat na wapambe wao ambao inaelekea wameshindwa kusoma alama za nyakati hata baada ya kutahadharishwa hapo kabla.
(a) HR Clinton alivimbishwa kichwa? (b)We mpuuzi kweli kweli. (c) Kwa taarifa yako alishinda kura kwa idadi ya wapiga kura milioni tatu.
(a) Ndiyo.

(b) Haya maneno nimeyazoea sana, nimeishawekwa kwenye 'ignore list' na bado hilo halijanikatisha taama ya kutaka
kuelendea kujifunza ili nijitambue. Hivyo, kama maneno ya namna hii yanakusaidia kuimarisha hoja yako kwa
wahusika, endelea tu kuyatumia. Ha ha haaa!

(c) Kuna uzi kwenye jukwaa hili kuhusu uchaguzi wa Marekani, wakuu akina Nguruvi3, na wengine ukiwemo wewe
mkuu mwenyewe, mlitufafanulia kinagaubaga juu ya utaratibu wa upigaji kura na upatikanaji wa ushindi kwa kura
za urais. Na hapa nakiri pia kuwa ni kupitia elimu yenu niliweza kuelewa namna mshindi wa urais wa Marekani
anapatika. Nina imani pia HR Clinton anajua utaratibu huo ndiyo maana wala hakukata rufaa kupinga matokeo.
Zaidi timu yake HRC iliibuka na tuhuma za kughushi za 'Russiagate'. Ili uwe rais wa US lazima ushinde "kura za
Majimbo". Sasa kuendelea kusema HRC alishinda uchaguzi wa US kwa kura milioni tatu, unajua tunakushangaa
hata sisi wanafunzi wako kwenye mambo haya.

Nani alimshauri nani? Hata Trump mwenyewe alijua anashindwa. Wengi hawakusumbuka kujitokeza kupiga kura kwa sababu walijua Trump hawezi kushinda kwa idadi ya wapiga kura na kweli alishindwa kwa kura milioni tatu.
Ukweli Democrat ilionyesha udhaifu mkubwa na hasa tukirejea aliyofanyiwa Ben Sanders. Hivyo, ni kwa wale wenye macho ya ziada waliweza kuona Ushindi wa Trump kipindi hicho. Sasa kama Democrat kilishindwa hata kuhamasisha upigaji kura wa wafuasi wake katika majimbo yote muhimu ya kuwapa ushindi unaendeleaje kuzibwa macho kuwa HRC alishinda kwa kura milioni tatu. Ndiyo maana nasema, hii si kawaida. 'Mag3' siye yule niliyemzoea, huyu kabadilika. Kwa maelezo ya ziada rejea pointi (c) hapo juu.
Ndio maana mimi nasema it was a mistake. Mwaka 2016, watu walipuuza kujitokeza kupiga kura na hivyo Rais akapatikana kwa utaratibu mwingine na hata matokeo ya mwaka 2018 yalikuja kuthibitisha ukweli huo.
Halikuwa kosa bali nikuwa wakati huo Democrat hawakuwa na ushawishi halisi waliokuwa wameaminishishwa na 'kura za maoni' zilizopigiwa debe na vyombo vyao pendwa vya habari a.k.a MSM. Mkuu jitahidi kuliona hilo la upotoshaji wa 'kura za maoni'. Matokeo ya 2018 yalipatika wakati wingu zito la tuhuma za kughushi na kudhalilisha dhidi ya Trump mfano wa tuhuma ni 'Russiagate', 'Me too', nakadhalika ili kuficha sura za aibu za Democrat. Yale matokeo hayakuwa ya kuonyesha udhaifu wa Trump kuendesha serikali bali yalikuwa ya kuonyesha ubora wa kughushi tuhuma dhidi ya POTUS. Pia na hili unalifumbia macho; Mkuu unajua sikuelewi ujue! Ha ha haaa!
@TUJITEGEMEE, (i) sisi wengine hapa si wapiga kura wa Marekani na (ii) nakuomba sana uache kukurupuka kwa hoja za kipuuzi. (iii) Yawezekana ndani ya hilo jiwe lenu mnauona Utrump lakini kaa ukijua huko kuna sheria na hakuna aliye juu ya sheria. (iv) Ndio maana nasema acheni kujadili mambo ya Marekani kwa jicho la Kitanzania. (v) Siasa za Bongo mwisho mpakani.
(i) Asante kwa kutujuza kuwa bado haujaanza utaratibu wa kuwa na 'uraia pacha'.
(ii) Rejea pointi (b) hapo juu.
(iii) Hakuna aliye juu ya sheria huko na ndivyo ilivyo hapa kwetu. Vinginevyo, uje na ulinganifu wa unachomaanisha
kwa mifano ya matukio na sheria zilizokiukwa.
(iv) Ni makosa sana kugeuka misimamo yenu ya 'dunia kama kijiji' kwa kuacha kulinganisha kitongoji kimoja na kingine
kwenye kijiji hicho hicho. Ni kweli, US wana misimamo yao na sisi tuna misimamo yetu lakini hilo halitufanyi
kutafakari na kujadili pande hizi mbili kwa uoga/woga wa kuzifananisha. US ni nchi huru na Tanzania ni nchi huru
kwa vipimo vya kawaida vinavujulikana, hivyo hakuna haja kuogopa kujadili nchi hizi kwa ulinganifu.
(v) Tanzania ni kubwa. Usiichukulie kirahisi rahisi hivyo, Mkuu.
Achana naye huyo, leo Chairman of the Joint Chiefs of Staff wa Marekani kampa somo conman-in-chief Trump akimwambia majadiliano lazima yafanyike kuhusu bendera za waasi (confederate flags) sanamu zao pamoja na majina yao kupewa vituo vya kijeshi na hatua kuchukuliwa kuziondoa hizo bendera, sanamu na majina kufutwa. Mambo yanazidi kuwa moto kwa huyo conman-in-chief!
Rejea post number 1117 ya uzi huu.
====
Nadhani nimejitahidi kukujibu kadri ulivyotarajia. Tuendelea na mjadala wa 'Duru za Siasa: Marekani(US) Chini ya Donald J....'

Asubuhi njema.
 
"Mlenge, post: 35977032, member: 450"]
Psychiatry 101 students are taught that every human is a mental case... mere difference is in the degree of it... kwa hiyo siyo vema wala haki kuacha kujadili matokeo ya ushiriki wa Kanye kwa vile tu unadhani ana maradhi ya akili. Hiyo pia inaweza kuwa ubaguzi. Kwa wanajitutumua kujua siasa za viungani DC watoe hoja zinazoonyesha ujuzi wao. Wait... Does Obama qualify kama anayejua siasa za viungani DC?
Mkuu, kwa wanaojua sisasa za viunga vya DC, hiyo clip ya Obama imesaidia sana kueleza jambo.
Msikilize ameanzaje halafu ameongeaje.

It was sarcasm tu, akisema ''Nasia Kanye anataka kugombea kuwa Spika wa House''
Halafu akaendelea kwa utani mkubwa, kwa wanaojua siasa za DC alikuwa anafanya mzaha mwanzo mwisho.

Hapa napo kunazuka swali jingine, je, tunaposikiliza clip tunajua semantics!!!


Kuna mwaka katika music awards Kanye alimnyang'anya microphone Tailor Swift, na Beyonce akatuliza hali.

Ndio uliokuwa mwanzo wa watu kutilia shaka afya ya Kanye. Mgazeti yaliandika sana kama habari kubwa.

Ilikuwa ni habari kwasababu habari kwa magazeti ni ile inayouza na si uvumbuzi wa kitu .

Hapa nina maana kuvuma kwa habari kusikubebe mzobe mzobe bado una nafasi ya kufikiri kama wewe.

Kuhusu mjadala huu kuufanya ''been to' kwa mujibu wa clip yako hilo si kweli.
Huu ni mjadala huru ambao mawazo yanapingwa kwa hoja au yanaungwa mkono kwa hoja.
Sasa hapa kuna tofauti kati ya maoni ' opinion' na ignorance.

Kinachopingwa ni ignorance. Kwa mfano, Mlenge anaamini Kanye West anaweza kushiriki uchaguzi

Kwa maana ya kushiriki hilo ni kweli. Kwa maana ya uchaguzi hilo halina fallacy. Kwanini!

1. Katika mazingira ya kawaida conventions za GOP na Dem zilikuwa zifanyike mwezi huu.
Primaries zimeshakamilika na hakuna namna nyingine ya ushiriki. Kuna states zimeshafunga mjadala wa Urais

2. The Lincoln Project ilijaribu kumweka Justin Amash, pamoja na nguvu zote bado magavana wamefunga primaries na mgombea wa Republicans ni Trump. Huko Dems primaries zimekamilika hakuna nyingine tena

Arguably utasema Kanye anaingia kama independent. Well hilo lilitokea kwa Henry Ross Perot, Billionaire na liliacha historia na funzo kubwa kwa vyama.

Ni kwa msingi huo Mabilionea waliotaka kugombea kama akina Bloomberg walipitia vyama na si independent candidate. Wanajua ni ngumu katika mfumo wa siasa za DC.


Kanye West hana influence yoyote, na nakuhakikisha katika viti vya electoral college , Kanye hawezi kupata hata hata kiti kimoja kama kura zake za nchi nzima zitachanganywa.

Huu ni ukweli ambao si rahisi kuukana isipokuwa kwa kutumia vijarida na kushindwa kupambanua mambo. Watu wanaelewa ni mgonjwa na wanamchukulia hivyo kwa kauli zake, lakini pia wapo wasioelewa ni mhonjwa

Kwa mintaarafu hiyo, hakuna anayekataa mawazo au mitazamo ya mtu, lakini basi mitazamo hiyo iwe katika standard ya kufikirisha si kufifisha ili kuzuia adulteration ya mjadala na kuufanya minutia bila sababu.

Kuna wakati katika mjadala huu mpuuzi mmoja asiyejua siasa za Viungani DC na anayejitutumua tu awepo alikuwa anachangia hoja hafifu. Tuliheshimu mawazo yake hata kama ilibidi kuyapuuza.

Tulilazimika kukemea upuuzi wake pale alipoandika '' Marekani ilizima Radar zake ili isione makombora ya Iran'' na kulazimika kujibu. Think about that!

Kukaa kimya ilikuwa kukubali upuuzi na tulimkemea na kumtaka akae pembeni.
Like wise siasa za dunia si za Mataga zilizojaa upuuzi na ubutu.

Hizo zifanywe kwingine na ni huru kabisa kuwa na uzi lakini si hapa! hatuvumilii ujinga
Kuna nyuzi ya Mataga, je, uliona kuna mtu anawasumbua huko? Lakini mataga si kila mahali, kwa wene akili zao upuuzi wa mataga uachwe huko huko na tunawataka mataga wasishiriki mijadala kwani hawana la maana

Kwa hili la Kanye mimi nimejaribu kutoa elimu ya kutosha, anayeelewa ataelewa, aliyegoma kuelewa aendelee na mgomo kwa gharama za dhalili juu yake, na kwamba, sitaongelea tena suala la Kanye ili nisiende 'down the rabbit hole''
 
...

Kwa hili la Kanye mimi nimejaribu kutoa elimu ya kutosha, anayeelewa ataelewa, aliyegoma kuelewa aendelee na mgomo kwa gharama za dhalili juu yake, na kwamba, sitaongelea tena suala la Kanye ili nisiende 'down the rabbit hole''

Tutaendelea kuchangia kuhusu Kanye, au lolote lingine kwenye uzi huu. Ninyi mnaojua siasa za DC, probably the been tos, itabidi mtuvumilie tu kwa kweli. At the moment you are condescending kwa akina sisi tulio TZ, mkiwa kana kwamba mnajiona superior kwa vile tu mko / mliwahi kuwapo Marekani.
 


He is mental case. He won't actually run. He is just attention-seeker. He is about to release an album. Then, why worry?

Intention may be to just take some few votes in the key swing states that allows write-in... and that would be enough to sway the election one way or the other...
 
Tutaendelea kuchangia kuhusu Kanye, au lolote lingine kwenye uzi huu. Ninyi mnaojua siasa za DC, probably the been tos, itabidi mtuvumilie tu kwa kweli. At the moment you are condescending kwa akina sisi tulio TZ, mkiwa kana kwamba mnajiona superior kwa vile tu mko / mliwahi kuwapo Marekani.
Absolutely ! haki ya kuchangia ipo bila kikwazo chochote. Mimi ni ' been to'' kwasasa nipo nyumbani nalima magimbi. Tofauti ni kuwa nina access and well informed na habari za dunia every single minute.

Ninaweza kukueleza Trump kafanya nini au Shilole kapigwaje na uchebe wa Bongoflavor.

Simba wa Nyika waligawanyikaje na kutoa less wa Wanyika. Nini kilitokea Jamhuri Jazz ya Tanga wanatoa wimbo wa Wanyama wakali kama siyo single mpya ya Harmonize au Vanessa Mdee.

Ukinifukunyua nitakueleza siasa za kina Bibi Titi Mohamed na Lucy Lameck, kama hupo huko basi nitakurudisha kwa Zari the boss lady na ukiomba nitakupeleka Sandrigham House siyo Harry na Meghan unayosoma katika vijarida na clips za tweete. Nitakupitisha kwa Rosa Parks n.k tukiwatafuta akina Angelou

Ni suala tu la kuwa informed, ninapokushauri nimeona upotofu, lakini ushauri si shurti ni hisani

Nitakue Shinzo Abe anakabiliwa na nini, Xi Jimping anafanya nini na UN katika kuwabana Wamarekani.

Huku nyumbani nani anaunga mkono jitihada, nani ametoswa na nini kinaendelea na siasa za Zanzibar na Hussein Mwinyi kapatikanaje na kuna reaction gani kutoka Zanzibar.

Uzi huu mwanzoni, tulieleza middle east na jinsi Trump atakavyopata tabu na nuclear deal ya Iran, inatokea.

Tulieleza kuhusu North Korea na jinsi siasa za China zinavyofanya kazi na Trump atakapokwama, inatokea. Tulieleza kushindwa kwa amani kule Palestine kutokana na suala la Jerusalem na siasa za Saudia, Qatar. Hakuna tulichosema ambacho ni kipya katika habari za leo. Hatuendi na clips au vijarida.

Ngoja nikupe latest za Zanzibar. Uteuzi wa Hussein Mwinyi una tatizo. Wazanzibar wanaamini kuwa Ali Hassan Mwinyi kwao ni bara na ndiyo maana mwanawe alikuwa mbunge wa Mkuranga.

Ingawa Wazanzibar asili yao wengi ni kutoka maeneo tofauti kuna hali fulani ya chuki ilijengwa na CUF ya kwamba kama asili yako ni bara wewe si mzanzibar.
Hilo ndilo limepelekea wale wazanzibar wa Mapinduzi daima kuwaita wenzao Machotara.

Kosa la CCM Zanzibar la leo lilianza na katiba mpya. Ni Wazn waliokataa katiba itakayokuwa na Tanganyika na Zanzibar wakichelea kwamba Mapinduzi yatakuwa matatani na sultani kama si vizazi vyake vitarejea.
Leo wamepewa nafasi ya kuteua majina wakijua ndani ya NEC kuna wajumbe 129 wa Bara na wao 35

Vuai Shamsi ambaye ni waziri kiongozi wa zamani hii ilikuwa fursa yake.
Ni kiongozi anayekubalika pande zote, lakini ni tatizo kwa wahafidhina wa bara wanaomuona kama mtu anayeweza kuwageuka katika muungano.

Katika majina 30 yaliyochukua fomu Kamati maalumu ya CCM Zanzibar walijua Hussein ''huenda'' ameletwa wakampa doubt kama mtoto wa mzee Mwinyi.Wakahadaika na Mbarawa bila kujua kuwa kete ni Hussein.

Kosa lao lilikuwa moja, katika majina 30 wangechagua unpopular 2 na kuyashindanisha na Shamsi Vuai

Definite Shamsi anayekubalika sana na CCM Zanzibar angeibuka kidedea.
Katika kumpendeza Rais mstaafu wakaweka jina la Hussein wakijua Mbarawa '' keshachinjiliwa' mbali. kosa!!

Walipofika Dodoma wakapigwa na mshangao pale kura zilipogawanyika za Wazanzibar, wakati za bara zikibaki ''intact'' 129. Hilo tu linaonyesha haikuwa bure kuna namna, walizungukwa bila kujua.

Uteuzi wa Hussein Mwinyi ni kosa la kiufundi la CCM Zanzibar kuanzia katiba mpya ambayo ingewapa more autonomy hadi majina 30 na kudanganywa kuwa kete ni Mbarawa bila kujiuliza huyu Hussein Mwinyi aliyekuwa Mbunge wa Mkuranga kaenda kule kwa nguvu na msukumo gani?

Sasa nini kitatokea? Hali iliyotokea ime demoralize CCM Zanzibar.
Mbele ya macho ya Wazanzibar CCM wanaonekana wameiuza Zanzibar kwa usemi wa Rais wa visiwani anachaguliwa Dodoma.Hilo litawagawa na kuwapa Wapinzania ''ACT Wazalendo'' nguvu kubwa ya kisiasa.

ACT wataungwa mkono na Wazanzibar waliochukizwa hata kama ni CCM.
Wapo wanaoamini hilo si chaguo lao na kwamba wamechoshwa na majina ya Dodoma.

Matfaruku utafanya kampeni kuwa ngumu sana kwa CCM na kutegemea 'Jecharism'' kwa ushindi

Hata hivyo, umma unaweza kuwa na nguvu katika hali isiyotarajiwa na Jecharism inaweza kutofanikiwa. Tumeona hayo kule Iran kwa Shah na kwingineko ambako nguvu ya umma imetamalaki

Ni hayo tu duru za Bongo ninakolima magimbi, turudi kwa siasa za DC lakini Kanye nakuachia uendelee naye
 
Absolutely ! haki ya kuchangia ipo bila kikwazo chochote. Mimi ni ' been to'' kwasasa nipo nyumbani nalima magimbi. Tofauti ni kuwa nina access and well informed na habari za dunia every single minute.

We consider ourselves lucky to have you in this thread.

ukiomba nitakupeleka Sandrigham House siyo Harry na Meghan unayosoma katika vijarida na clips za tweete. Nitakupitisha kwa Rosa Parks n.k tukiwatafuta akina Angelou

Ni suala tu la kuwa informed, ninapokushauri nimeona upotofu, lakini ushauri si shurti ni hisani

Asante. You will have to make do with kuvumilia maoni unayoyaona potofu ya the ill-informed wasoma-vijarida. Unaweza kusaidia zaidi ukieleza kwa kutanabahisha sababu za upotoe unazoziona, badala ya kudismiss whatever is posted kwamba ni wrongthink, just because it is not posted by a been-to.

Ni hayo tu duru za Bongo ninakolima magimbi, turudi kwa siasa za DC lakini Kanye nakuachia uendelee naye

Doubleplus good!

Kanye is attempting to play the role of party-pooper. His name is not helping the matter either :(. He appears to not seriously wanting to win the presidency itself, or even to actually run. His extreme detractors allege he might be off his meds, but the calculated effects of his gimmick are as follows:

1. IF he actually runs, he may split the votes. In the states where the winner is determined by a small margin, he could sway the election one way or the other. It is debatable which side: Trump or Biden, will he hurt more.

2. IF he doesn't run, but remains in the election limelight and conversation, he might speak issues that sway some voters one way or the other, and hurt either Trump or Biden campaign.

According to vijarida vya kwenye mtandao, tena vile vya mrengo wa kulia, Mshauri Mmoja wa Kampeni ya Trump (Does he meet your DC-insider esoteric knowledge criterion?), kazungumzia pointi hizo mbili, lakini kama mwamba ngoma, akivutia kwake (Video iko chini). Aidha, kwenye vijarida vingine vya mijadala mtandaoni, vinatilia mashaka. Mfano:

Co-founder of Students for Trump: Kanye West "is a trojan horse into the Democrat voting bloc" - Democratic Underground (mrengo wa kushoto)

Kanye West again says he will run for president (mrengo mchanganyiko)

Video kuhusu mshauri wa kampeni ya Trump (mrengo wa kulia):
 
Ni suala tu la kuwa informed, ninapokushauri nimeona upotofu, lakini ushauri si shurti ni hisani. Ni hayo tu duru za Bongo ninakolima magimbi, turudi kwa siasa za DC lakini Kanye nakuachia uendelee naye
Mkuu Nguruvi3, kuna watu kama wangeweza kukaa kimya wangeficha ujinga wao...hebu fikiria upuuzi huu wa wenda wazimu kuendela kuitesa dunia kwa siasa za kilimbukeni na kishamba, haya sasa;
  • Kanye West Drops Out of 2020 Presidential Race!
  • Bashite achukua fomu ya Ubunge Kigamboni, kupitia CCM
  • Zaidi ya 80 kujitokeza kugombea ubunge jimbo la Kawe Dar!
Kanye West alipofilisika na kujikuta ana madeni alikimbilia kwa Trump na kumwita baba. Mkewe ambaye ni bilionea alimkatalia kabisa asiguse pesa zake, si unajua tena mambo ya prenup agreements. Ghafla baada ya kumlamba miguu huyo babake wa kambo, mambo kidogo yakamnyokea.

Hata hivyo haikuchukua muda akajikuta tena anazama kwenye lindi la madeni baada ya matumizi ya hovyo. Akamkimbilia tena baba yake wa kufikia na kumlilia. Safari hii akalamba pesa za stimulus za corona na kumuahidi Trump angegombea Urais ili kupunguza kura za weusi kwa Biden, sasa wapi!

Ujinga mtupu.
 
Kura za maoni zinawapotosha sana...! Hawajifunzi. Nakumbuka namna HR Clinton alivyovimbishwa kichwa na kura za maoni. Na kipindi hicho yeyote aliyeshauri watu wawe na kiasi katika kujihakikishia nani anakuwa Rais wa US basi alionekana 'kituko'. Naona wale wale wanataka kurudia kosa.

Kura za maoni zinaonyesha kwamba Kanye anaweza kupata asilimia mbili (02%) ya kura zote. Tayari Kanye kajiandikisha rasmi kwenye tume ya uchaguzi kama mgombea wa Urais Marekani 2020. Kwa sasa, kuingia kwa Kanye kama 'mtibuaji' kunazidi kunogesha uchaguzi, kwa vile, kama lisemavyo gazeti la Chicago Tribune, Kanye "could feasibly siphon away some votes from either Biden or Trump in what could turn out to be a tight election."

Asilimia mbili ya kura iko ndani ya wigo wa kiasi kinachoweza kuamua mshindi kwenye majimbo yenye ushindani mkali.

Kanye atakuwemo kwenye
karatasi za kura za Jimbo la Oklahoma.
 
Some Quotes:

SOURCE: https://www.newsweek.com/which-states-could-kanye-west-appear-presidential-ballot-1519731
Kanye West's 2020 presidential bid has landed him on the Oklahoma ballot, and there's also a chance that he could appear on the ballot in his home state of Illinois and 38 others if he is able to get enough signatures through August and September.

SOURCE: Analysis: Is Kanye West serious about running for president?
Justin Levitt, an American constitutional law scholar and professor at Loyola Law School in Los Angeles, agreed that West should not be ignored.

"He absolutely could make a difference," Levitt said. "In elections, there are a lot of factors -- the weather and how the local sports team performed. If there were less at stake or the result seemed inevitable, then you might see people support Kanye as a protest vote."

David J. Jackson, a political science professor at Bowling Green State University who specializes in the relationships between entertainment and politics, said that West's media presence could play a decisive role in the outcome of the race.

 
This 2020 US Presidential Election has hallmarks for an explosive post-election situation:

  1. Biden/Left supporters see the election as one and perhaps the only realistic way to consign President Trump to the dustbin of history, and therefore rescue America. They cannot imagine to what extent four more years of Trump will harm The United States.
  2. Trump/Right supporters see the election as one and perhaps the only realistic way to consign Vice-President Biden to the dustbin of history, and therefore rescue America. They cannot imagine to what extent four more years of Biden will harm The United States.
Interesting Times.
 
Kanye anaweza kupunguza kura za Biden Illinois na kuacha likachukuliwa na Trump; kumbuka yeye ni shabiki sana wa Trump. Mwaka 2000 kulikuwa na jamaa anaitwa Ralpha Nader alivuta kura nyingi za Labor Unions huko Ohio ambao tranditionally walikuwa democrats na sehemu kadhaa za Florida na kufanya majimbo hayo kuangukia kwa Bush kwa percentage ndogo sana kuliko alizopta Nader. Mwaka 2016 pia kulikuwa na mama yule Jill Stein ambaye naye alinyofoa kura nyingi sana kule Wisconsin na Pennsylvania ambazo zilikuwa traditionally za Democrats, na kufanya majimbo hayo yaanguke mikononi wa Trump kwa percentage ndogo kuliko alizopata mama Stein.
 
Kanye anaweza kupunguza kura za Biden Illinois na kuacha likachukuliwa na Trump; kumbuka yeye ni shabiki sana wa Trump. Mwaka 2000 kulikuwa na jamaa anaitwa Ralpha Nader alivuta kura nyingi za Labor Unions huko Ohio ambao tranditionally walikuwa democrats na sehemu kadhaa za Florida na kufanya majimbo hayo kuangukia kwa Bush kwa percentage ndogo sana kuliko alizopta Nader. Mwaka 2016 pia kulikuwa na mama yule Jill Stein ambaye naye alinyofoa kura nyingi sana kule Wisconsin na Pennsylvania ambazo zilikuwa traditionally za Democrats, na kufanya majimbo hayo yaanguke mikononi wa Trump kwa percentage ndogo kuliko alizopata mama Stein.

Kichuguu, kazi kubwa ya Kanye ni kupunguza kura za mgombea. Wapo wanaosema atapunguza kura za Biden, lakini wengine wanasema atapunguza kura za Trump, kwa misingi ifuatayo. Kwa vile Kanye anajulikana ni shabiki wa Trump, wapiga kura wengi anaoweza kuwachukua ni wale wa Trump. Kanye siyo mashuhuri miongoni mwa Wamarekani-Waswahili, kwa hiyo kwenye jimbo hilo hawezi kunyofoa kura nyingi. Hivyo kama kweli Kanye ana nia ya kugombea, basi ugombea wake utamnufaisha nani, hilo ni suala bado la mjadala.

Rejea:
Kanye West Filed To Appear On Five Ballots (So Far) In Unlikely Presidential Bid

Here’s Why A Kanye West Run Might Be More Likely To Hurt Trump
 
This 2020 US Presidential Election has hallmarks for an explosive post-election situation:

  1. Biden/Left supporters see the election as one and perhaps the only realistic way to consign President Trump to the dustbin of history, and therefore rescue America. They cannot imagine to what extent four more years of Trump will harm The United States.
  2. Trump/Right supporters see the election as one and perhaps the only realistic way to consign Vice-President Biden to the dustbin of history, and therefore rescue America. They cannot imagine to what extent four more years of Biden will harm The United States.
Interesting Times.
popcorn-face.jpg
 
Kiongozi Nguruvi3 ,

Tunaomba, ukiona vema na ikikupendeza, utuanzishie mada pacha wa hii... this time ikihusu utawala wa Biden-Harris Administration.
 
Back
Top Bottom