Donald Trump aweka rekodi ya kuwa Rais wa kwanza wa Marekani kukanyaga ardhi ya Korea Kaskazini

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Donald Trump aweka rekodi ya kuwa Rais wa kwanza wa Marekani kukanyaga ardhi ya Korea Kaskazini kwa mujibu wa ripoti ya White House.

Katika moja ya ziara aliyowahi kuifanya Donald Trump ambayo iliingia mpaka kwenye record za Marekani.

Ni ziara ya Donald Trump kuingia nchini Korea Kaskazini na kukanyaga ardhi hiyo, katika kumbukumbu za ikulu ya Marekani inaaminika Donald Trump ndio Rais wa kwanza aliyewahi kukanyaga ardhi ya Korea Kaskazini. Katika video iliyopo hapo chini anasikika Rais Donald Trump akimwambia Rais wa Korea Kaskazini

Je naweza kukanyaga kwenye ardhi yako?" na kauli ya namna hiyo ya kuomba ridhaa kukanyaga ardhi hiyo ambapo Rais wa Korea Kaskazini akamwambia "Bila shaka unaruhusiwa" napo Donald trump ndipo akaingia kwa mara ya kwanza Korea Kaskazini.

Kumbuka muda huo mkutano wa Donald Trump na Kim Jong UN walikutana kwenye mpaka wa Nchi hiyo ya Korea Kaskazini ambapo Donald Trump alionekana akiwa nje ya mpaka na Kim Jong UN akiwa ndani ya mpaka wake.


View: https://www.instagram.com/reel/CwtjRB0IWkw/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
 
Back
Top Bottom