Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
17,040
2,000

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
11,762
2,000
Uzi huu umekuwa mchungu kweli!!!
Kwa bahati mbaya sana uzi huu umevamiwa na watu wasioijua Marekani. Marekani ni nchi ya wahamiaji na sababu kubwa ya watu kuhamia Marekani ilikuwa ni kuzikimbia tawala za kiimla. Hakuna taifa duniani lenye watu wa kutoka kila pembe ya dunia (hadi Tanzania) na kila kabila, rangi na jinsia inapatikana Marekani. Kila desturi, kila lugha, kila tamaduni, kila tabia inapatikana Marekani na ni rhuksa. Bila Marekani fikiria dunia ingekuwaje, ingekuwa tofauti kabisa na i!ivyo hivi sasa.

Trump yupo leo na jitithada zake za kuitawala Marekani kiimla nakuapia hazitafanikiwa. Wewe, TUJITEGEMEE, ni kama mnywa gongo au fisi anayesubiri mkono wa binadamu udondoke. Marekani ni polisi wa dunia kwa sababu moja tu, ni kimbilio la watu wanaotafuta maisha huru na mazuri zaidi kihali, kimali, kiafya, kijamii...Wako watu walijipenyeza Marekani kwa malengo tofauti na kweli hali hii ya kila mtu kuwa huru haiwapendezi, wanataka ziwepo tofauti waweze kuabudiwa.

Hapana, si Marekani. Mrusi mmarekani, Mtanzania mmarekani, Mchina mmarekani, Mwingereza mmarekani, Mdengereko mmarekani, Muitaliano mmarekani, Mhindi mmarekani, Muarabu mmarekani, Muajemi mmarekani...hawa wote walizikimbia nchi zao, wakawaacha ndugu zao, familia zao, rafiki zao, jirani zao na wapenzi wao wakahamia nchi mpya kwa nini? Halafu leo atokee mtu moja anataka kuzima ndoto zao za kuishi maisha waliyoyatafuta, hapana TUJITEGEMEE huijui Marekani!

Acha ulevi wa gongo wa kusoma RT news, ziko nchi zingependa Marekani isambaratike waweze kuitawala dunia kwa mabavu lakini Marekani inawapiga stop. Hawalali, kucha wanapanga namna ya kuisambaratisha Marekani wanashindwa. Mara moja moja wanapata watu wa kuwatumia kama Trump lakini mwisho wa siku ndoto zao zinazimwa. Kama ulitaka kujua kwa nini Marekani inaitwa Sanctuary Nation ya dunia, tulia ufuatilie gharama za uhuru zilivyo kubwa.
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
17,040
2,000
Acha ulevi wa gongo wa kusoma RT news, ziko nchi zingependa Marekani isambaratike waweze kuitawala dunia kwa mabavu lakini Marekani inawapiga stop.
====
Khaaa!!! Mkuu Mag3 Ha ha haaaa
Yaani Mkuu, hutaki kabisa kusikia Second opinion!!! Sasa uhuru upo wapi sasa hapo!? Nimesoma post yako yote neno kwa neno. Kuna mahali ilibidi niwe nasimama kusoma ili niweze kucheka kidogo...!
 
Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
11,762
2,000
Khaaa!!! Mkuu Mag3 Ha ha haaaa
Yaani Mkuu, hutaki kabisa kusikia Second opinion!!! Sasa uhuru upo wapi sasa hapo!? Nimesoma post yako yote neno kwa neno. Kuna mahali ilibidi niwe nasimama kusoma ili niweze kucheka kidogo...!
Yawezekana umesoma kila neno nililoandika lakini kama kawaida umetoka kapa bila kuambulia chochote wala kuelewa chochote. Sijui hukubaliani na lipi...kwamba hakuna Msukuma mmarekani? Hakuna Mchina mmarekani? Hakuna Muarabu mmarekani? Kuna miji Marekani ukiingia utadhani uko Beijing au Mumbai...si lugha tu bali tamaduni, mila na desturi.

Unajua majanga yanayotokea Marekani kila mwaka na hasara inayosababishwa na majanga hayo? Je umewahi kusikia China imepeleka msaada Marekani? Umewahi kusikia Urusi imepeleka msaada Marekani? Sasa subiri janga kubwa lizikumbe nchi hizo, Marekani huyo keshatia kambi. Juzi tu Australia imepokea misaada ya hali na mali kutoka taifa kubwa, Marekani!

Ukifika Marekani, umeiona dunia nzima. Ukifika Marekani lazima utakutana ama na mtoto wako, ndugu yako, kaka yako, dada yako, mzazi wako, baba mdogo wako, mama mdogo wako, mjomba wako, shemeji yako, shangazi yako, babu yako au bibi yako. Huwezi ukakosa kabisa usiye na uhusiano wowote naye. Hakuna nchi nyingine duniani utakuta hali kama hiyo.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
Uzi huu umekuwa mchungu kweli!!!
Nivunje hekima zangu za kutojihusisha au kujishughulisha na maandishi yako.

Uzi huu upo kwa ajili mahususi, kutanabahisha , kuyaangalia, kuyachambua mambo kwa namna rahisi ambayo kila msomaji wa lugha ya kiswahili ataelewa na kuelewa wenzetu katika dunia ya Marekani wanafanya nini.

Lengo la uzi si malumbano ya uchungu au utamu, huko siko walipo wasomaji .
Ni kwa msingi huo wengine hujitenga ili sote tusiwe wale.
Watu wakikaa kimya au kukuachia jamvi kuna busara hapo, ni vema ukaitafakari

Una hiari ya kuchangia au kutochangia(Kwa siasa za Marekani sidhani kama unauelewa ).
Mchango wako kama utakuwepo ulenge kusaidia wasomaji.

Lakini pia una hiari ya kufuata busara njema, kwenda mahali ambapo malumbano ' low'' yana nafasi.

Nakunahisi, kama una kitu cha kuandika, basi lenga kusaidia wasomaji wengI tu wanaotusoma.

Endapo unasuburi wengine waandike, basi subira yako iwe na hekma

Kwa wasomaji wa Duru, kuna uzi wa '' Uchaguzi wa Democrats 2020'' utaanza pindi tukimudu majukumu yanayotukabili na kujaaliwa nafasi.
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
17,040
2,000
Lakini pia una hiari ya kufuata busara njema, kwenda mahali ambapo malumbano ' low'' yana nafasi.
===
Hii ni hatari. Kama 'fikra pevu' inafikia hatua ya kutoweza kukubali kukosolewa ama kuelezwa kile ambacho haikutarajia kukisikia. With 'my lowness' nitajitahidi hivyo hivyo kupenyeza maoni mbadala ambayo baadhi yenu yaweza kuwa yanawakera lakini hii itakuwa ni faida kwa wengine ambao hawakubali 'kulishwa' habari za upendeleo wa upande mmoja tu.

Nikirejea kwa Mkuu, Mag3 (nakupongeza kwa kueleza unachokiamini bila kificho na moja kwa moja), ni kweli kabisa Marekani ni Taifa kubwa kiuchumi na kiteknolojia. Bahati mbaya ukubwa huu wa Marekani umejengwa katika 'hila', lakini bahati nzuri hila za US zimeanza kushughulikiwa na washindani wake. Na kama US hatafanya unyama kama alioufanya Iroshima na Nagasaki huko Japan (kuua wajapan kwa bomu la nyuklia), Nawapa Marekani miaka 20, watakuwa wamepitwa na washindani wao katika 'ukubwa' niliotangulia kuuleza. Ushahidi wa dalili hizi huu hapa chini, ingawa chanzo cha ushahidi kinaweza kuwa kero kwa baadhi yenu lakini huo ndiyo ukweli.

>>> China beats US in key patents to secure technological dominance – report

*****
Ndugu wasomaji, si kusudio langu hata kidogo kuvuruga mjadala huu. Lakini pale upotoshaji wa wazi unapofanywa (na nikadhibitisha ni kweli ni upotoshaji) , mtaniwia radhi, nitalazimika na nitajitahidi kuupinga. Habari za upande mmoja hazijengi ndiyo maana hata hapa nchini kwetu hatufurahii kuwa na maoni ya upande mmoja lakini na upande wa pili ujitahidi kuwa na hoja za kujenga si kubomoa na zisiwe za hila. Tusijivunie kuwa taifa la kupokea maharamia (ill-dissidents) wa kwenda Kudhuru nchi za wenzetu kama Taifa fulani linavyosifiwa kwa kulinda maharamia wa Kudhuru tamaduni, desturi, umoja, amani na utengamano wa nchi nyingine. Hilo "taifa fulani" kupitia kazi za Dr Shiro Ishii( Mjapan katili na bingwa wa silaha za maangamiza za kibailojia) limefanya mambo mabaya yasiyofikirika( rejea link hapa chini)

>>>The Geopolitical Deployment of Biological Weapons - Part II
Maeleze ya andiko hilo juu ya silaha za maangamizi za kibailojia yanaisha kwa aya hii:

"The Western mass media have ignored all of this, censoring this entire portion of history, and even the Internet has been scrubbed with Google and Bing unable to find the truth which is out there. Once again, freedom of speech depends entirely on who controls the microphone"

Asante kwa kusoma maoni yangu.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
Ushahidi wa dalili hizi huu hapa chini, ingawa chanzo cha ushahidi kinaweza kuwa kero kwa baadhi yenu lakini huo ndiyo ukweli.

>>> China beats US in key patents to secure technological dominance – report
Labda nirejee, naona huelewi tatizo lako na nini tunachosema hapa.

Hakuna tatizo kujadili kwa mtazamo tofauti. Hakuna mtu anaye miliki ''facts'' na ni haki kupinga kwa hoja zenye mantiki na weledi na si kupinga tu kwa kuokota unachodhani ni sahihi bila kuchambua, ilimradi kinakupendeza.

Mfano mzuri ni wa bandiko lako ambapo unachukua ''analysis' ya mtu na kuiita ushahidi.
Kwamba, yoyote anayeandika kwako ni facts na ni ushahidi.

Pili, ungelijua siasa za dunia hii usingevamia tu vitu.
Katika kitu kinachoitwa geopolitics Russia ni adversary and Foe kwa United states.

Tangu Trump ameingia madarakani Russia kwa kupitia vyombo vyake kama RT vimefanya kazi nzuri kwa Taifa lao kwa kugeuza propaganda kiasi cha Rais wa Marekani kuvidharau vyombo vyake kama ilivotokea ''Helsinki'

Kwahiyo, unaposoama habari za RT lazima uelewe zinatoka wapi, zinalenga nini na kwanini.

Russia ndiyo waliogeuza suala la Ukraine kwamba ni Ukraine iliyoingilia uchaguzi 2016 na server ya DNC ilikuwa Ukraine. Intelligence za US zimekataa ujinga huo isipokuwa mtu mmoja .

Katika sakata la Impeachment wateuliwa wa Trump walisimama na kukanusha kuhusu Ukraine, ilikuwa wazi.

Hivi tunavyoandika jitihada za AG Barr kuhusu uchuguzi wa Wachunguzi wa ''Russian'' unaongozwa na Jaji aliyeteuliwa na Barr , Jaji Durham unapingwa na Intel community na kwamba ni njama chafu tu.

RT wanasubiri habari ya Durham ili waweze kufanya spinning zao. Hayo sijui kama unayajua

Ili kuhakikisha wanakwepa ukweli wa Intel community, Barr amemteua prosecutor kuchunguza waliochunguza Russia. Hii nayo sijui kama umewahi kuiona kupitia RT ambao kwao ni habari kubwa.

RT wakasema kuhusu Iran na US jambo ulilolileta hapa jamvini. Tulikaa kimya tukiendelea kusoma ''low''

Ulisema hivi '' US walizima radar baada ya kubaini Iran inajiandaa kurusha makombora''

Hii ni crap! hivi kama walijua hilo walikuwa na sababu gani za kuzima radar? Logic tu bila kusubiri maelezo inatosha kukupa picha. Kwavile siasa za dunia bado ni changa, uliona ni jambo la maana sana kulileta hapa

Ni hivi, lazima uzielewe siasa na kujua maana ya 'opinion, analysis na facts''

Tukirudi kwa hoja ulizoelekeza kwa Mag3 , kwamba Marekani itazidiwa baada ya miaka 20, sina uhakika kama unaijua historia ya Taifa hilo.

Marekani imepita vipindi vingi vigumu ndani na nje.
Kuanzishwa kwa Bretton woods na uwepo wa new world order na NATO ulitokana na upinzani dhidi ya US

Ilichukua miaka 40 kwa US kumaliza cold War na hakuna aliyejua. Wakati huo akina Brezhnev na Gorbachev walikuwa wakiona ukaribu wao kiushindani na US. Mwisho wa siku wakajikuta hawana USSR

Nimalizie kwa kusema, sote tunasoma habari na kuzitafakari, tatizo ni pale unapovuruga mjadala kwa u 'simba na u-Yanga'' badala ya kusaidia wasomaji kuelewa mambo ambayo si kawaida kuyasikia katika mijadala

Ni pale unaposoma habari na kutafuta ''spelling error'' ukiwa huna lolote la kueleza kama mbadala

Hata hivyo u-simba na u-yanga huo kama unatoa tija si tatizo, lakini unapofikia kiwango 'low'' inatia kinyaa

Kiwango low kama hadithi za mitaani za US kuzima radar isione makombora ya Iran, it is unfortunate!
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
17,040
2,000
Ni hivi, lazima uzielewe siasa na kujua maana ya 'opinion, analysis na facts''
Nikiri wazi kabisa hapa kuwa Nguruvi3 Mag3 Mchambuzi Elungata El Jefe Pascal Mayalla Mzee Mwanakijiji Chige Malcom Lumumba na wengine wengi wa namna hiyo, mmetoa mchango mkubwa sana kwangu katika kuwa na jitihada za kutafuta taarifa sahihi na kujiongezea maarifa. Bado nina 'spirit' hiyo ya kutafuta maarifa kwa njia zilizopo. Nina washukuru sana.

Mkuu, uwenda ukawa kweli kwamba bado sijaelewa siasa na kujua maana ya 'opinion', analysis, na facts. Hii naipokea kama changamoto kwangu na nitaendelea kuifanyia kazi. Mara kadhaa siku za nyuma niliwahi kueleza katika jamvi hili kuwa ninafurahi sana ninapokosolewa katika minajiri ya kunijenga niwe bora kwa jambo ninalofanya ama ninalojihusisha nalo kwa namna moja ama nyingine. Kusifiwa hakunipi hamasa kubwa ya kuwa bora kama kunikosoa kwa kunijenga. Hiki ndicho chanzo cha kupenda kukosolewa. Mwanzoni nilikuwa nakereka kukosolewa kwa kebehi lakini kwa sasa taratibu nimeanza kumudu kuupokea ukosoaji wa namna hiyo kwa utulivu hata kama ukosoaji huo umefungwa kwenye kebehi, dharau, simango na mengine kama hayo hili mradi tu nigundue ukosoaji huo una 'substance'!
Kwa mara nyingine nakushukuru kipekee kwa hili.

Hata hivyo u-simba na u-yanga huo kama unatoa tija si tatizo, lakini unapofikia kiwango 'low'' inatia kinyaa
Kiwango low kama hadithi za mitaani za US kuzima radar isione makombora ya Iran, it is unfortunate!
Ni kweli yawezekana kwa baadhi yenu nikaonekana 'low' kwa baadhi ya mambo kwa sababu kadhaa. Mbili kati ya hizo ni:
1. Yawezekana kuonekana 'low' kwani wakati mwingine huwa na tumia njia mbali mbali kupata taarifa za kweli kutoka kwenye chanzo lengwa kwa ku'provock' chanzo hicho na kauli 'tata'!
2.Mara nyingi TUJITEGEMEE wa 'Great Thinkers Forum' (GTF) ni tofauti kidogo na TUJITEGEMEE wa Jukwaa la Siasa, Habari Mchanganyiko na majukwaa mengine isipokuwa Jukwaa La International (JLI). Kwenye TUJITEGEMEE wa JLI anafanana sana na yule wa GTF. Hivyo kama ulimsoma TUJITEGEMEE wa jukwaa Mchanganyiko ukamlinganisha na yule wa GTF unaweza kuwa 'umepigwa chenga'.

Kuhusu suala la "US kuzima radar isione makombora ya Iran", na dhani hilo nalo tuliweke kwenye kundi la 'changamoto' uliyonipa ya kuelewa namna bora ya 'kuwasilisha' hoja zinazohusu 'opinion', 'analyis', na 'facts'.

Na kushukuru kwa mara nyingine, Mkuu Nguruvi3 kwa kujishusha hadhi kujibu hoja zangu (kama ulivyoeleza post# 1,046 ya uzi huu-sentensi ya kwanza) ili uweze 'kuniweka sana', mimi ambaye bado nina kiu ya kujifunza kutoka kwako na kwa wengine.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
AG BARR ABANWA, NI BAADA YA KUIGEUZA DOJ KUWA 'EXEC BRANCH''

Baada ya Impeachment kumalizika kwa Trump kuwa ''acquitted'' na Republican majority, Rais Trump anarudi ulingoni kwa jazba na hasira akiwatimua wote waliotoa ushahidi dhidi yake.

Republicans wengi waliamini baada ya Impeachment na kumuokoa , Rais Trump angejirudi na kuwa mwangalifu.

Tofauti na hivyo sasa ni kama ''fungulia Mbwa'' huku akimtumia AG Barr, mwanasheria mkuu kama sehemu ya kuwanasua washirika wake katika kesi zinazotokana na sakata la Russia.

'Tweet' zake ambazo huenda mbele, zimemweka AG Barr katika mazingira magumu.

Ni wazi Trump anaitumia DOJ kisiasa tofauti na 'utamaduni' wa chombo hicho kuwa 'apolitical'

Sakata la Barr kutaka hukumu ya Roger Stone, mshirika wa Trump irejewe ili mwendesha mashtaka apendekeze adhabu ndogo imewaacha watu wengi midomo wazi.

Prosecutors 4 wa kesi hiyo wamejitoa na mmoja kati yao ameacha kazi.
Duru za viungani DC zinaeleza ni suala la muda huenda wakafuata wengine.

Wanasheria wanasema DOJ haiwezi kumshtaki mtu na kuwa mtetezi wakati huo huo.

Hiyo ni kazi ya ''defensive lawyer'' na kwamba kutoa adhabu ni jukumu la hakimu na wala si lazima wafuate maelekezo ya prosecutor.

Adhabu inaweza kupendekezwa lakini hakimu au Jaji ana nafasi ya kuangalia kinachoitwa ''mitigating factor(s)'

Lakini pia Rais Trump ana nafasi ya 'commute'' kama Rais na angeweza kumsamehe Roger siku hiyo hiyo

Katika kupooza moto, AG Barr alitoa kauli ya ''kumkemea'' Trump akisema anaifanya kazi yake iwe ngumu.
Hapa ni kuwa Barr anaeleza tweet zinavoharibu mipango yake anayoratibu taratibu.

Trump haonekani kukerwa na kemeo la Barr kwa sababu nzuri tu.
AG Barr ni msiri anayejua mengi na aliyezuia mengi sana , vinginevyo Trump angekuwa Mar Lago.
1. AG Barr alificha taarifa ya Mueller na kuipotosha. Hadi leo ni yeye peke na wanasheria wa Trump wanaoijua
Suala hilo lilifanya ugumu wa kumshtaki Trump kwa impeachment kwani ushahidi umefichwa na Barr

2. Suala la Ukraine lililopelekea Ukraine, Barr alitajwa na alikataa kujiuzulu. Whistle Blower alipofikisha suala mbele yake Barr alitaka kulizima lisiende mbele ya Congress. Hii ilikuwa kuzuia impeachment

3. Barr anaendesha tume ya Durham ili kumsafisha Trump na tuhuma za Russia. Barr amesafiri kutafuta ushahidi, hata hivyo Intel community zimemgome kuhusu uchunguzi wa Durham

4. Barr alitangaza kimya kimya kuhusu kusafishwa kwa Hillary Clinton kwa tuhuma kadhaa, moja, Benghaz, pili deal ya Iran na tatu emails. AG alifanya hayo kimya kimya ili kumnusuru Rais Trump na fedheha ya uzushi.

Hayo ni kwa uchache wa mengi aliyofanya kuzuia habari zinazomhusu Trump na ni wazi Rais Trump hawezi kumfanya lolote. Barr amebeba siri nyingi na nzito na fundisho la John Bolton, Gen Kelly

Jamii ya watumishi waliowahi kutumikia DOJ wakiwemo senior officer wameandika na kusaini waraka unamtaka Barr ajiuzulu. Hata hivyo, watu hao 2000 wamebainisha kuwa Barr ahatajiuzulu kwa jinsi wanavyomjua, na hivyo kuwataka maafisa wengine wa DOJ 'kusema kitu wakiona jambo''

Wakati Barr ameitwa na kamati ya House March 30, pressure inayomkuta ni kubwa sana. Kuna uwezekano pressure hiyo ikamzidi kadri siku zinavyosonga. Hata hivyo Barr ni ''loyal'' kwa Trump na anaweza kukomaa liwalo na liwe. Tatizo la viungani DC wapo wajuvi wanaoweza kumweka katika wakati asiotarajia

Tusemezane
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
88,481
2,000
Bado mpo humu?

Teh teh teh naona kila kitu kinabuma.

Mwokozi wenu Mini Mike Bloomberg naona kimemtokea puani.

Hahahahaaaaaa.
 
Mwalimu

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,543
2,000
Bado mpo humu?

Teh teh teh naona kila kitu kinabuma.

Mwokozi wenu Mini Mike Bloomberg naona kimemtokea puani.

Hahahahaaaaaa.
Bloomberg hajawahi na hatakuja kuwa mgombea tishio... ameunguza hela zake bure tu mwisho wa siku hakubaliki hata ndani ya chama chake.
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
17,040
2,000
. Kama ulitaka kujua kwa nini Marekani inaitwa Sanctuary Nation ya dunia, tulia ufuatilie gharama za uhuru zilivyo kubwa.
Weakness ya uendeshaji nchi 'kidemokrasia' kwa mising ya uhuru wa soko ( soko huria) - frèe market hata kwenye afya za watu umeanza kudhihirika kwenye ' sanctuary nation(SN) '. Hii si dalili nzuri kwa wale mara zote wanatuhimiza kuendesha nchi kwa mtindo utumiwao na SN. COVID19 ( CORONA virus) imeumbua udhaifu mkubwa wa mfumo wa utawala ambao tuliaminishwa hata punguani anaweza kundesha nchi hii iliyopewa jina la SN. Kitendo cha SN kuwazunguka hata washirika wake kukwapua nyenzo za kukabili corona virus kimenifumbua macho.

Na sasa naanza kujikita katika kufikiria uboreshaji wa mfumo wa utawala wa nchi yetu unao kidhi matakwa ya jamii yetu nchini badala ya kuwaza zaidi kunakiri kila nukta ya mfumo wa uendeshaji nchi zingine.
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
11,101
2,000
Ina maana wote humu mpo Marekani sio
Mimi ninakaa Isevya; lakini naona kama Marekani iliingia choo cha kike kuchagua mtu kama Trump. Aliwadanganya kuwa anajua biashara kumbe hamna lolote, anaishi kwa mikopo na kukataa madeni tukwa kutumia sheria za bankruptcy. Sasa hivi nchi iko matatizoni hajui la kufanya bali kusema watu wanywe chroloquin kinyume na maoni ya madakatari. Jamaa ni mbabaishaji sana. Deni la marekani limeaongezaka kwa asilimia karibu hamsini kwa kipindikifupi alichokaa madarakani na kuijenga Marekani kama taifa linalochukiwa duniani, akiondoka ataiacha nchi ikiwa mflilisi kabisa kwa vile aitaweza kukataaa madeni hayo kama livyokuwa akifanya.
 
Drone Camera , mkuu sijui kwanini umefikia conclusion kwamba watu wanaishi Marekani na siyo China au UK. Ukisoma mabandiko na nyuzi nyingi utaona tunajadili UK, China, Balkan region, Magreb region, Middle east, Far East n.k. Ni suala la kuiangalia dunia kwa upana.

Mkuu Kichuguu Trump ni janga kwakweli. Sera za umimi na kwamba Marekani inaweza yenyewe zimefeli.
Uchumi aliopewa ukiwa unakuwa na ambao hajafanya lolote kubadili trend unaelekea kubaya sasa

Arguably watu watasema ni kwasababu ya Corona, lakini Trump alishindwa kuongoza dunia kama livyofanya Obama na Ebola. Kuna habari za uhakika intel briefing zilimweleza mapema sana ukubwa wa tatizo, akapuuzia

Ile leadership ya America imepotea kabisa. Leo anaagiza watu watibiwe na chloroquine bila utafiti, anaagiza tu

Leo US ya Trump inaagiza Mask China ! Yeye hajali watu watakaokufa anajali uchumi akijua ndio utamuondoa madarakani na anajua ilivyo ngumu kurudisha uchumi katika mstari.

Republican kimyaa kuhusu national debt hasa waliomchukia Obama kama akina Ted Cruz na Tea party

In short, huyu jamaa ni failure
 
Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
11,762
2,000
Mimi ninakaa Isevya; lakini naona kama Marekani iliingia choo cha kike kuchagua mtu kama Trump. Aliwadanganya kuwa anajua biashara kumbe hamna lolote, anaishi kwa mikopo na kukataa madeni tukwa kutumia sheria za bankruptcy. Sasa hivi nchi iko matatizoni hajui la kufanya bali kusema watu wanywe chroloquin kinyume na maoni ya madakatari. Jamaa ni mbabaishaji sana. Deni la marekani limeaongezaka kwa asilimia karibu hamsini kwa kipindikifupi alichokaa madarakani na kuijenga Marekani kama taifa linalochukiwa duniani, akiondoka ataiacha nchi ikiwa mflilisi kabisa kwa vile aitaweza kukataaa madeni hayo kama livyokuwa akifanya.

Kim-Donald.jpeg
Huyu ndiye Donald Trump...!​

Sumu haionjwi lakini katika dunia ya sasa nchi nyingi, ikiwa ni pamoja na Tanzania, ziliamua kuonja sumu na matokeo yake tunayaona.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,084
2,000
KUTOKA VIUNGA VYA DC

Habari ya gonjwa la Corona imefunika habari ya uchaguzi wa Rais wa Marekani.
Baada ya kuanza kwa kusuasua hatimaye Joe Biden sasa atakuwa mgombea kwa tiketi ya Democrats

Ushindi wake ulikuja baada ya maumivu ya chaguzi za Iowa na New Hampshire zilizowaweka Sanders na wengine katika ramani. Joe Biden alipata ushindi South Carolina na kuanzia hapo amewadunda wenzake 24 hadi kubaki mwenyewe baada ya gonjwa kukatisha chaguzi akiwa tayari kamweka Bernie Sanders katika wakati mgumu.

Biden alipata kuungwa mkono na weusi lakini pia watu wa rika hasa wanaoishi vijijini ambako ni ngome ya Trump.

Biden alipata msaada usio rasmi kutoka ndani ya Democrats waliohofia kuhusu sera zake za kijamaa.
Lakini pia alipata usaidizi wa Hillary Clinton aliyemwelezea Sanders kama mtu aliyechangia kumnyima Urais

Tangu mwaka 2016 mahusiano ya Sanders na Clinton hayakuwa mazuri.
Wafuasi wa Sanders ambazo ni ''Russia'' waliolenga kuleta mtafaruku na kuwagawa Dems ndicho chanzo cha ugomvi baina ya wawili hao. Wafusa hao ''Russia'' walijaribu tena wakimtaka Sanders kama mgombea wa Dems

Clinton alijitokeza na kueleza 'tifu' hilo siku chache kabla ya chaguzi za Iowa akilenga kumuumiza Biden.

Msaada mkubwa sana wa Biden ulitoka kwa Trump. Kampeni ya Rais huyo wa Marekani inamuhofia sana Biden kutoka na uwezo wake wa kupenya vijijini na kwamba anaonekana kama mshindani wa dhati wa Trump.
Kampeni ikafanya makosa mawili makubwa.

1. Kumshambulia Bernie Sanders kama mjamaa anayetaka kufuta ubepari.
Hili lilifanyika kwa mtarajio kuwa Sanders atakuwa mbeba bendera wa Dems pale ilipoonekana dhahiri Biden amekwisha.Matarajio yalikuwa kuanza kumshambulia Sanders kwa kumpaka matope.

2. Kosa la pili ni Trump kutumia mikutano na hata state of union kumshambulia Sanders kwa dhana ile ile kuwa atakuwa ndiye mgombea wa Dmocrats.

Kwa kufanya hivyo, kampeni ya Trump haikujua kuwa inamsaidia Biden kama mbadala wa Sanders.

Kibao kilipobadilika kampeni ya Trump imepigwa na butwaa hesabu zote zimevurugika na mbaya wa Trump , Joe Biden ndiye atakayepambana naye.

Hayo yakiendelea gonjwa la Corona limefanya uharibifu mkubwa wa maisha ya watu na uchumi wa Marekani.

Ni uchumi ule uliojengwa na Obama na kurithiwa na Trump akijinasibu ndiye mjenzi na sasa umeanguka.
Karata kubwa ya Trump ilikuwa uchumi, kwa hili la Corona hali ni mbaya sana kiuchumi

Trump analaumiwa kwa kushindwa kudhibiti gonjwa kama alivyofanya Obama na Ebola.

Analaumiwa kwa mizaha na uongo kila uchao hata kufanya kazi za kitaalamu katika jukwaa la kisiasa
Wiki takribani tatu Trump amevurunda kiasi cha kulitia aibu Taifa hilo kubwa

Ni ngumu kueleza kila jambo lakini kuna yanayochekesha na kushangaza kama lile la Rais wa Marekani kufikiri kuwa dawa za kusafisha mazingira zinaweza kutumiwa kuua wadudu wa Corona (Disinfectant).

Hili la Corona lita define nafasi yake katika uchaguzi na Historia ya Marekani

Tutaangalia kwa undani kuhusu tatizo hilo

Katika mazingira haya ya covid19 kampeni za uchaguzi zitafanyika vipi? Kutakuwa na mikutano ya hadhara? Kutakuwa na midahalo baina yao?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom