Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,630
2,000
Wanajamvi

Uchaguzi wa US umekamilika jana baada ya D.J Trump kuwa Rais wa 45
Leo ilikuwa siku ya kwanza kamili ya Trump kama Rais wa US

Uzi utakuwa utaangalia serikali mpya na mwelekeo wa siasa na uchumi
Siasa za Marekani , taifa lenye nguvu katika uso wa dunia zinaathari kubwa duniani

Ni kwa kuzingatia hilo, uzi utaleta kwa kadri, yanayojiri katika Taifa hilo

Tutaendelea kumalizia hotuba ya Trump baada ya kutawazwa katika uzi huu
Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Rais Trump, mfanyabiashara aliyefanikiwa katika biashara ameondoka katika utawala wa makampuni na sasa ni mtawala wa umma na Taifa la Marekani

Kuchaguliwa kwake kama mtawala wa juu wa Taifa lenye ushawishi umekuja na mshtuko kutokana na nafasi aliyopewa katika uchaguzi wa ndani ya chama cha Republican na ule mkuu

Kuna mitazamo tofauti kuhusu kuchaguliwa kwa Trump. Kwasababu zozote ambazo wachunguzi wanaendelea kuzifuatilia kisiasa , uchumi, jamii n.k. Trump ndiye Rais wa Marekani

Siku ya kwanza, Trump amekumbana na changamoto za utawala wa nchi na si kampuni binafsi

Katika historia ya miongo michache ya Marais wa US, siku ya kwanza haikuwa nzuri kwake

1. Maandamano ya wanawake duniani
2. Ziara iliyozua utata katika Intelligence community (IC)

Tutajadili mambo hayo mawili na picha ya haraka ya nini kitarajiwe kwa siku za usoni

Tusemezane
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,630
2,000
Katika mazingira haya ya covid19 kampeni za uchaguzi zitafanyika vipi? Kutakuwa na mikutano ya hadhara? Kutakuwa na midahalo baina yao?
Mwalimu hili limekuwa suala lenye utata kidogo.
Kwa wagombea , Trump anaonekana kutojali sana suala la Corona kwasababu angependa kwenye base yake awajaze upepo wa habari za kutunga.

Anajua wazi kabisa na alishawahi kusema ''base'' yake inamsikiliza
Huko vijijini ndiko kabisa huwaambii kitu chochote hasa ukizingatia ndiko 'ubaguzi' ulipobobea

Pamoja na hayo , Joe Biden anamtishia sana hasa kumega sehemu ya wapiga kura wa vijijini.
Kuna independents ambao wengi wameondoka kwa Trump kutokana na chaos ya utawala wake

Juzi kulikuwa na ruling kuhusu Obama care na suala la birth control. Washauri wa Trump hawataki kurudisha Obamacare katika mjadala, ni kitu kinachoonekana kuwa maarufu kwasasa kuliko miaka 4 iliyopita.
Kitendo cha Trump kutumia DOJ kumega Obamacare nacho kinamweka mahali pagumu, hana mbadala wake

Kuhusu uchumi nako hali si nzuri. Unemployment ipo 14% kiwango kikubwa tangu depression post WWII
Kwa hili kauli za Trump zitamgharimu kwasababu zinaeleza kutokuwa makinini na Corona na kufika ilipo ambapo Wamarekani 30 milioni wamepoteza ajira zao.

Kampeni zitafanyika kwa mikutano?
Ni suala la muda na ikifika July tutaweza kupata uelekeo.

Kuhusu kura, state zimeanza kufuata mfumo wa kupiga kura kwa njia ya Posta
Trump hataki kabisa upiga huo wa kura

Kukataa kwake ni kwasababu Republicans kwa kutumia ''Gerrymandering na vote suppression'' walifanikiwa

Mfano, waliweka vituo vya kura mbali hasa kwenye maeneo ya Democrats.
Walichelesha kufungua vituo vya kura na wengi kutoweza kupiga kwa wakati
Kubwa zaidi walilazimisha kuwa na ID wakijua hata Raia hasa weusi wengine hawana

Trump hataki kusikia hilo na sasa anatumia DOJ kutaka kuzuia upigaji kura wa namna hiyo.
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
8,945

Trump ni janga kwa demokrasi na maendeleo ya Marekani. Kweli aliyezowea vya kunyonga, vya kuchinja haviwezi kabisa. Jamaa alizowea mambo ya mkatomkato, sasa amejikuta katika mazingira yanayohitaji afanye kazi kweli na ameshindwa, amekua ni mtu wa blah-blah na kulaumu watu wengine tu. Alipokuta uchumi wa Obama unaendelea akajichukulia sifa zote kama kweli ndiye aliyeukuza wakati uchumi ulikuwa unaendelea na ile kasi ya Obama. Sasa Uchumi umeporomoka sijui kama ataujenga tena; wao wanadhani mwarobaini wa uchumi ni tax-cut tu; kumbe sivyo. Wakati janga linaanza China, alitakiwa aanze mikakati ya kujikinga nchini kama ambavyo Obama alivyoanza kujenga mikakati ya Ebola wakati bado iko Afrika na ile Avian Flu ilipokuwa bado ingali iko China. Jamaa kwa vile hakutaka mambo ya Obama, alipofika madarakani akavuruga programs zote zilizoachwa na Obama ndiyo maana janga hili limemkuta hana maandaliizi yoyote kwani ile ofisi ya maandalizi ya magonjwa ya milipuko aliyoacha Obama ilikuwa imefungwa, na hivyo serikali yake ikawa haijui la kufanya. Nikijaribu kuangalia, ameilaumu sana China, amemlaumu sana Obama, amewalaumu sana Democrats, amelaumu sana madaktari na manesi wasiokubaliana na approach zake, amewalaumu sana magavana wasiokubaliana na approach zake, amewalaumu waandishi wa habari wanaposema ukweli ambao haumfurahishi, amewalaumu sana wataalamu wanaosema wazi kuwa approach yake ni mbovu. Amebakiza kulaumu wanyama wa porini na miti tu.
 
Top Bottom