Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

Mkuu Nguruvi3 na wengineo

Tatizo kubwa linalotukabili Tanzania sasa hivi ni kuangalia kila jambo kwa mizani ya kisiasa ya SISI vs WAO, CCM vs UKAWA n.k.

Inawezekana kabisa Mheshimiwa Rais anaona kwamba Makonda amevurunda lakini akiangalia wapiga filimbi wakubwa ni kina Gwajima, Tundu Lissu na Mange Kimambi! Hapo ndipo kigugumizi kinapoanza kwamba akimtumbua Makonda itaonekana amefanya kwa shinikizo la wapinzani wake... kitu ambacho hayuko tayari kukubali! Shida kubwa iko hapo... EGO!

Moja ya madhaifu makubwa ya mheshimiwa ni kujawa na roho ya kiburi, pride, ego na kumchukulia kila anayempinga ama kumkosoa kuwa ni adui na anamkwamisha kutekeleza kazi yake. Kila mwenye mawazo tofauti na yeye moja kwa moja anachukuliwa kwamba ni adui. Ndio maana kwa mfano aliwatamkia wanasheria wanaotetea watuhumiwa kuwa nao watashughulikiwa!

Ndio maana jana amesema kwamba hafanyi kazi kwa kushinikizwa na "mitandao"... sio kwamba hajui kwamba kuna tatizo la hasha! Bali ni "pride" na "ego" iliyopo kuona kwamba atakuwa anajishusha kwa kusikiza ushauri kutoka kwa malofa wa mitandaoni. Ingawa kwa upande mwingine yeye mwenyewe ameonesha kuwa ni mshabiki wa mambo hayo hayo ya udaku (shilawadu)!
Nilishawahi kusema humu kuwa, Huu si Wakati wa Mivutano isiyokuwa ya lazima, aina ya serikali iliyopo ni Mtaji bora kuwahi kupata, ila tu Akili kubwa inahitajika.
 
Baada ya Rais kutamka kuwa hashinikizwi ili kutoa maamuzi na kwamba RC aendelee kuchapa kazi, RC aliinuka na kutoa heshima, baada ya hapo Waziri Simbachawene akampongeza. Pale kuna tafsiri mbali mbali zaweza kujijenga. Wengine wanaweza kusema RC ni untouchable (I don't believe this), pili ni kwamba maamuzi yanaweza kufanyika baadaye na kwa uhakika.

Ni kweli, si vema kumshinikiza Rais, kwani vyombo vyake vinafanya kazi kwa mujibu wa sheria na ndio vitakavyomshauri. Tumeona Waziri wa habari akichukua hatua, tuamini pia kwamba na vyombo vingine vinachukua hatua kwani ndio kazi zao.

In my opinion, Rais alikuwa sahihi kwa wakati wake kusema alivyosema kwani inawezekana kabisa taarifa kamili na rasmi za ushauri hazijamfikia, mbali ya kwamba yeye ni mpenda matukio ya papo kwa papo na kufanya maamuzi. Maamuzi ya aina hiyo huko nyuma yalileta ukakasi kwa baadhi ya maafisa serikalini wengine wakaumwa, wengine walipoteza maisha na wengine ni vigumu kuajiriwa kwa sababu ya maamuzi ambayo yalikuwa magumu lakini ni ya papo kwa papo.

Rais ni taasisi kubwa, na Rais bado (kama mmeona) anajifunza baadhi ya mambo. Wengi wanaolifuatilia suala hili bado hata hawajaweza kuleta taarifa iliyokamilika....tuhuma zipo nyingi...taarifa zilizopo ni za kuungaunga na nyingi bado zina maswali mbali mbali ukiondoa hili la kuvamia kituo cha habari (Clouds), jambo ambalo wamiliki wamethibitisha na hawakulifurahia na wame-demand apology from RC...again hili nalo ripoti yake (kutoka serikalini) itatolewa....kama alivyosema Waziri wa habari na mapendekezo yatapelekwa mezani kwa mwenye Mamlaka juu ya RC

Tumpe muda Rais,....nina hakika atachukua hatua. Mfano mzuri ni kwenye issue ya madawa ya Kulevya....RC alipoanza mikikimikiki yake ya kutangaza watu na kuwaweka rumande, ni jambo lililomfadhaisha kidogo (ingawaje asingeweza kulisema hili hadharani....mbali ya ku-support vita)......Mh Rais na alichukua hatua haraka sana ya kuteua Kamishna na kuifanya ile Mamlaka ifanye kazi zake immediately....kwa kuwa taarifa za mapendekezo ya uteuzi na ufanyaji kazi wa Mamlaka ile ulikuwepo mezani kwake na ilikuwa ikusubiri tu uteuzi rasmi....hakusita kufanya hivyo.....Rais anaudhika pale anapopata mashinikizo kama vile yeye hajui cha kufanya....na wala sidhani kama ni ego/insecurity...inawezekana kabisa uzoefu wa kuumba maneno yatakayowa-please wengi hana....na tukubali huyu ndio Rais wetu...ndivyo alivyo katika kuongea
 
Shida kubwa ni kwamba Rais alishatengeneza standards kwenye suala zima la utumbuaji kwa kutokuwa na simile wala masihara. Wengi wametumbuliwa tena kwa makosa ambayo ni mepesi kulingana na anachutuhumiwa Makonda. Hawa hawakupewa muda wa kujieleza wala kujitetea wakatumbuliwa on the spot. Wengine walitumbuliwa hadharani kama marehemu Kabwe baada ya kutuhumiwa na Makonda huyu huyu! Mama Kilango akatumbuliwa kwa kutoa taarifa isiyo sahihi ambayo inawezekana alikuwa mislead na walio chini yake. Dr Malecela akatumbuliwa kwa kutofuata itifaki kwenye utoaji ripoti ya NIMR... na wengineo wengi.

Sasa iweje inapofikia mkuu wa mkoa anatuhumiwa kwa idendity theft, kufoji vyeti n.k. Na kubwa zaidi kuvamia ofisi ya chombo cha habari na askari wenye silaha kushinikiza habari fulani irushwe hewani kuwe na kigugumizi kuhusu kumtumbua? Ni kwa sababu tuhuma zimetolewa na Gwajima? Ndio maana nimesema tatizo ni "ego" na kutotaka kuonekana umefanya jambo kutokana na shinikizo la mtu haijalishi kwamba jambo hilo ni sahihi.

Kwa hili Mheshimiwa anatengeneza precedence ambayo mwisho wa siku itaishia kuwa mtego kwake. Ataweza vipi kutumbua watendaji wengine wabovu ikiwa huyu amegoma kumtumbua?
 
"Ogah, post: 20274818, member: 121"]Baada ya Rais kutamka kuwa hashinikizwi ili kutoa maamuzi na kwamba RC aendelee kuchapa kazi,Wengine wanaweza kusema RC ni untouchable (I don't believe this)
Mkuu Ogah ni ngumu sana kukataa hii hoja kwa wanaodhani ni hivyo.

Historia yake si njema kama kiongozi. Unakumbuka aliwahi kumtumbua'kamanda' hadharani? Akamwendea kombo marehemu Kabwe. Akaagiza watu wapigwe, achilia mbali kuongoza fujo kwa Mzee Warioba kama zilivyojirudia Clouds.
Haya yanatosha, kulikoni kukingiwa kifua?
In my opinion, Rais alikuwa sahihi kwa wakati wake kusema alivyosema kwani inawezekana kabisa taarifa kamili na rasmi za ushauri hazijamfikia
Hili ni tukio kubwa lililohusisha usalama, kama hakuwa na habari kwa siku nzima, kuna tatizo jingine
Tumpe muda Rais,....nina hakika atachukua hatua.
Kwanza, ni kweli katiba na sheria haziruhusu apokee shinikizo.

Vita ya matumizi fake ya vyeti inatuhitaji tumuunge mkono.
Sasa anaungwaje mkono huku kukiwa na double std?

Pili, tukio la ''kuvamia'' kituo cha TV na Radio si la kawaida nchini.

Kwa matumizi ya dola katika mambo mambo binafsi tunawezaje kusema ni tukio la kawaida linahitaji muda?

Tatu, ingekuwa vema angeliacha kulizungumzia. Aliposema 'chapa kazi' sehemu kubwa ya jamii imehisi tofauti. Katika mazingira hayo, impression ni wapo walioonewa na wapo wanaolindwa. Kuna hisia zoezi zima la vyeti feki, uhakiki wa elimu hqlina credibility.

Hapa ndipo tatizo lilipo maana kuondoa fikra hizo si kazi rahisi
 
"Mwalimu, post: 20280068, member: 11689"]Shida kubwa ni kwamba Rais alishatengeneza std katika utumbuaji kwa kutokuwa na simile wala masihara.

Wengi wametumbuliwa tena kwa makosa ambayo ni mepesi hawakupewa muda wa kujieleza wala kujitetea wakatumbuliwa on the spot.

Wengine walitumbuliwa hadharani kama marehemu Kabwe, Mama Kilango akatumbuliwa Dr Malecela
Na Kitwanga aliokuwa na 'kiroba'.
Makonda alimtumbua Kabwe, akamsema kamanda Sirro na orodha inaendelea

Kwanini ikifika kwake ambako si suala la vyeti bali 'uvamizi' kwa kutumia madaraka ionekane ni jambogumu linalohitaji muda?

Kwa hili Mheshimiwa anatengeneza precedence ambayo mwisho wa siku itaishia kuwa mtego kwake.
Utakuwa mtego mbaya na mgumu kwake

Akimtumbua mtu watu wataanza kuangalia kwanini haraka haraka.

Hapo ndipo utasikia zile hoja nyepesi na za kijinga na za kipuuzi kwavile tayari kila jambo litaangaliwa kwa jicho la Mkaonda. Na hapo ni ngumu kukanushwa
 
KWA HILI NAPE APONGEZWE

Baada ya tukio la uvamizi wa Clouds lililofanywa na RC Mh Nape Nnauye alitembelea ofisi hizo akiambatana na wajumbe kadhaa wa makundi tofauti

Kauli yake ya kwanza ilikuwa kulaani tukio bila kujali lilitokea katika mazingira gani
Kwa maneno mengine hakukuwepo na sababu za kuvamia kituo kwa silaha usiku

Kauli yake ya pili ni kuundwa kwa tume ili kusikiliza hoja za pande zote na mazingira ya tukio. Tume iliyopewa masaa 24 kukamilisha kazi

Ilidhaniwa kuwa Nape ameunda tume kama sehemu ya kuua tukio kama ilivyozoeleka
Awamu ya nne ilitumia sana mbinu hiyo katika kutuliza tafrani bila matokeo kamili

Leo tunafahamu masaa 24 yamepita bila taarifa kwasababu mbali mbali zikiwemo jitihada za kutaka RC.Taarifa inasema RC hakutaka kuhojiwa kama haki ya msingi ya kusikilizwa

Taarifa ya tume imetoka katika muda takribani uliokadiriwa.
Ilieleweka taarifa pengine itapitia 'mahali' kuchujwa kwanza na kucheleweshwa
Tunajua kwanini ilichelewa na sababu za msingi kabisa

Mambo kadhaa yamejitokeza. Kwanza, unyeti wa suala una gharama, lakini basi japo waziri alisimama na kusema haikuwa sahihi siku ya kwanza,akaomba radhi leo

Kuomba radhi si udhaifu ni uungwana na ukomavu

Taarifa inayomhusu RC anayeonekana kuwa na sheria tofauti na wananchi ni nzito

Tume aliyounda ilikuwa balanced na matokeo yake yanaweza kujieleza

Matokeo yamewekwa wazi hata kama yupo asiyekubaliana nayo, lakini yapo wazi

Mh Nape katimiza wajibu wake kwa uchache wa kusema.

Kaahidi ,kaomba radhi na kakubali matokeo na kasema atayafikisha panapohusika

Kiongozi au awaye anapofanya jambo jema apongezwe, na kwa hili Nape amefanya
 
NAPE AMELIPA GHARAMA KUBWA

Mh Nape Nnauye amepoteza nafasi yake ya uwazi wa habari , utamaduni na michezo
Hilo ni kufuatilia mabadiliko ya baraza la mawaziri yanaoyoonekana kuwa na malengo

Nape analipa gharama kama tulivyosema bandiko 306.
Ilikuwa ni wazi atazilipa kama ambavyo Mkwayembe ''amelipa''kwa kauli za siku za nyuma

Nape alikuwa mwenezi wa CCM akipigana bega na katibu mkuu kinana kukinusuru chama.

Nape ana uzoefu wa kubabaisha maneno, na sakata la clouds angeweza kubabaisha

Katika hali ya kukomaa kisiasa, kujitambua na kutambua taifa amebadilika kimtazamo
Aliamua kulitanguliza Taifa kwanza kabla ya mengine

Nafsi ilimsuta ndio maana alisimama katika ukweli. Nape alijua gharama kubwa atakayolipa kwa kugusa mtu wa karibu kuliko viongozi wengine wakuu wa nchi

Pamoja na hayo, Nape aliamua kusimama katika ukweli licha ya gharama anazolipa

Kuondolewa kwake katika nafasi si kuonewa, ni hiari ya mteuzi wake, ingawa hatua zimechukuliwa haraka kuliko hatua dhidi ya wahalifu kama waliovamia kituo cha Clouds

Ndivyo waziri wa sheria ambaye siku za nyuma alitoa kauli za ''kupingana'' na wakubwa
Na hivi karibuni akikaripiwa hadharani kwa tangazo lililohusu vyeti vya ndoa

Nape kaondoka ili kumlinda mwana wa mfalme, hapa ndipo watu wanauliza kulikoni?

Kuna nini nyuma ya kijana? Kwanini analindwa kwa gharama kubwa hata anapofanya ''uhalifu''? Maswali hayo na mengine yatazidi kuwatesa wahusika kwa muda mrefu

Ushauri kwa Nape, inafuata
 
USHAURI KWA Mh Nape Nnauye

Sakata la kupoteza nafasi ya uwaziri itakuletea taharuki, mkanganyiko na mfadhaiko
Taharuki si kutokana na kupoteza nafasi, bali mazingira yaliyopelekea kupoteza mafasi

Taharuki ni jambo la kawaida kwa manadamu yanapomsibu maswahibu ya ghafla
Uwaziri ni nafasi ya kuteuliwa na kutenguliwa, lakini katika hali ipi ndilo swali ulilonalo

Hakuna anayekataa mapungufu yako wakati unatumikia nafasi ya chama na uwaziri

Yapo mengi uliyofanya tusiyokubaliana nawe kwa kila hali. Historia ni shahidi

Ulipoamua kufuatilia sakata la RC ulifanya hivyo kwa nafasi yako katika jamii na taifa

Ulitambua gharama kubwa unayoweza kulipa kutokana na uamuzi wako

Pamoja na hayo, nafsi ilikusuta kati ya masilahi ya Taifa na nchi na masilahi yako

Ukaamua kusimama na Taifa ukitambua fika kuna gharama za kufanya hivyo

Kusimama huko kumekugharimu, lakini kuna jambo nyuma ya gharama unayolipa
Tukio limeonyesha upande mwingine wa wewe ni nani, uliokuwa haujulikani

Upande huo unakufungua na kukuweka huru, hata mbele ya mizani ni rahisi mapungufu yako ya nyuma kufunikwa na ukweli wa leo. Hilo ni baraka si balaa

Taharuki imepelekea kuitisha mkutano uliozuiliwa. Ni taharuki tu ndiyo imechukua nafasi kubwa kuliko busara za siku mbili. Bado hujachelewa kurekebisha upungufu huo

Katika kipindi hiki cha taharuki ni rahisi kuingia katika mtego wa kauli na majibishano
Huu si wakati wake kwani linaweza kuzua jambo la kufunika ukweli uliosimamia

Tuna kunasihi, utulie kwanza, ujiepushe na kauli au jambo linaloweza kuathiri taathira ya kile ulichokifanya ambacho Taifa linakuunga mkono kwa wingi wake

Hivyo basi rejea nyumbani, tulia upate 'cooling effect' itakayoweza kufungua busara

Katika wakati huu, busara , hakima na utulivu vinahitajika sana kuliko matukio yaliyotokea siku 3 ikiwemo hili la kupoteza nafasi yako. Busara zitakueleza zaidi na zitajieleza

Hili limetokea kukukweka huru, kusahaulisha mapungufu yako na kuweka rekodi sawa

Usifikirie wizara uliyosimamia, fikiria haki na umma ulio nyuma ya kitendo chako

Upe 'wakati' nafasi ya kujieleza na utajieleza wenyewe na si wewe kuueleza

Tusemezane
 
1. Mwalimu wangu umejiridhisha kuwa kulitokea uvamizi!? Hivi ukivamiwa si lazima uende polisi kuripoti?
2. Mwalimu unakubali kweli kuwa tume iliyoundwa ilikuwa na vigezo vyote vya kufanya kazi iliyopewa?
3. Ni kweli wakati Mh. Nape anajiunga CCM, chama hicho kilikuwa shimoni na yeye ndiye kakitoa huko?
 
1. Mwalimu wangu umejiridhisha kuwa kulitokea uvamizi!? Hivi ukivamiwa si lazima uende polisi kuripoti?
2. Mwalimu unakubali kweli kuwa tume iliyoundwa ilikuwa na vigezo vyote vya kufanya kazi iliyopewa?
3. Ni kweli wakati Mh. Nape anajiunga CCM, chama hicho kilikuwa shimoni na yeye ndiye kakitoa huko?
Tunaposema 'uvamizi' ni kwa mujibu wa taarifa zilizopo

Hakuna taarifa nyingine ya serikali zaidi ya ile ya Nape aliyekuwa waziri

Hatujasikia upande wa RC ambaye kwa mujibu wa tume amekataa kutoa ushirikiano

Lakini kama si 'uvamizi' ilikuwaje Clouds wakalalamika watu kuingia na silaha, kushurutisha kupewa nyaraka za habari? Labda neno 'uvamizi' lina maana nyingine

Pili, kuhusu tume iliyoundwa, kama jambo lilifanywa na waziri wa serikali mwenye dhamana basi kuna mwongozo alioufuata.

Pengine unaweza kutusaidia mapungufu ya vigezo.
Hata hivyo, Nape akiwa waziri alitoa masaa 24 kwa tume kufanya kazi

Katika muda huo mamlaka za juu zingeweza kusahihisha mapungufu ya tume kama yalikuuwepo. Hakuna masahihisho na hivyo kilichopo ndicho tunajadili

Lakini ukisoma mabandiko ya nyuma, tumesema wakati wa kumpongeza Nape kuwa suala si tume, si tukio. Alichokifanya kwenda eneo kwa wakati na kulaani tukio ilikuwa sahihi

Hakuna shaka, kuingia katika nyumba ya mtu na mwenye nyumba kulalamika ni tukio lisilo la kawaida, tena kukiwa na silaha zingeweza kuamsha tafrani kati ya wageni na walinzi.

Kuunda tume na kuipa masaa si miezi lilikuwa jambo sahihi.

Kuweka matokeo ya tume wazi kwa muda aliosema ilikuwa jambo sahihi

Kunaweza kuwepo mapungufu lakini hayaondoi ukweli,alisimama kuhesabiwa kwa wakati

Kuhusu CCM, hatuwezi kukataa ukweli chama kilikuwa kinayumba sana
Jitihada za Katibu mkuu Kinana akishirikiana na Nape zilisaidia sana uhai wake

Huu ni ukweli, unaweza kupingwa kwa maoni lakini si kwa ukweli. CCM wanajua hilo
 
NAPE AMELIPA GHARAMA KUBWA

Mh Nape Nnauye amepoteza nafasi yake ya uwazi wa habari , utamaduni na michezo
Hilo ni kufuatilia mabadiliko ya baraza la mawaziri yanaoyoonekana kuwa na malengo

Nape analipa gharama kama tulivyosema bandiko 306.
Ilikuwa ni wazi atazilipa kama ambavyo Mkwayembe ''amelipa''kwa kauli za siku za nyuma

Nape alikuwa mwenezi wa CCM akipigana bega na katibu mkuu kinana kukinusuru chama.

Nape ana uzoefu wa kubabaisha maneno, na sakata la clouds angeweza kubabaisha

Katika hali ya kukomaa kisiasa, kujitambua na kutambua taifa amebadilika kimtazamo
Aliamua kulitanguliza Taifa kwanza kabla ya mengine

Nafsi ilimsuta ndio maana alisimama katika ukweli. Nape alijua gharama kubwa atakayolipa kwa kugusa mtu wa karibu kuliko viongozi wengine wakuu wa nchi

Pamoja na hayo, Nape aliamua kusimama katika ukweli licha ya gharama anazolipa

Kuondolewa kwake katika nafasi si kuonewa, ni hiari ya mteuzi wake, ingawa hatua zimechukuliwa haraka kuliko hatua dhidi ya wahalifu kama waliovamia kituo cha Clouds

Ndivyo waziri wa sheria ambaye siku za nyuma alitoa kauli za ''kupingana'' na wakubwa
Na hivi karibuni akikaripiwa hadharani kwa tangazo lililohusu vyeti vya ndoa

Nape kaondoka ili kumlinda mwana wa mfalme, hapa ndipo watu wanauliza kulikoni?

Kuna nini nyuma ya kijana? Kwanini analindwa kwa gharama kubwa hata anapofanya ''uhalifu''? Maswali hayo na mengine yatazidi kuwatesa wahusika kwa muda mrefu

Ushauri kwa Nape, inafuata

Mkuu Heshima mbele..

maoni yangu ni kama ifuatavyo

Ilikuwa ni mapema sana kwa Mh Nape.....kuita press...busara za kiuongozi zilimshinda, angetulia tu kimya asubiri muda muafaka wakati wa kukabidhi ofisi
Nape amenasa kwenye mtego wa state kwa kutoa yale matamko...Chama chake pia kinaweza kumuadhibu kwa utovu wa nidhamu...alipopewa taarifa kuwa asifanye press meeting...angeacha na kuondoka zake. Kama unakumbuka Mh Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa alitaka kufanya mkutano, alipokuwa almost ready ku-address wananchi Polisi wakamzuia na wala hakuleta ubishi akaondoka zake....hizo ndio tunaziita busara za uongozi
Chochote kingeweza kutokea na kuvunja amani, ukizingatia pale ni karibu na sehemu ya kuabudu, hoteli ambayo kuna watalii, shule, na HQ ya Usalama....

Kwa upande mwingine, na wale Law enforcers hawakutakiwa kuonyesha mitutu katika hali ambayo ilikuwa kawaida mno, unapotoa silaha kuna mawili, watu kuumia/kuuawa au hasira za watu kumvamia Officer aliyetoa silaha na kumshambulia. Hivi yule askari alitoa silaha ili iweje wakati aliwa yeye na Mh Nape?

Tumefikaje huku?
Kukosa uvumilivu kwa pande zote, na kila mtu kusahau (kwa makusudi au kutokujua) majukumu yake kisheria
Ukosefu wa busara ili kutumia njia muafaka wa kutatua matatizo yaliyojitokeza

Tunahitaji nini?
Leadership ili kuweza kumaliza haya matatizo....Walau Waziri Mkuu (baada ya kujadiliana na wakubwa zake) asimame na kutoa muongozo....kwani matukio haya ni vizuri yakawa solved once and for all


tusemezane...hahaha
 
Mkuu Ogah

Kuna kitu kinaitwa 'knee jerk reactions' nadhani unakitambua
Kwamba, kuna mambo mtu anafanya hata kama hakupenda lakini inatokea

Hali hiyo hutokea hasa panapokuwa na taharuki inayoleta msongo wa mawazo

Natambua Nape ana msongo si kwa nafasi ya uwaziri bali kwa namna ilivyotokea

Alichosimamia kilikuwa kwa masilahi ya chama chake na katika misingi yake
Lakini pia ilikuwa kwa masilahi ya serikali yake ambayo ilionekana ndivyo sivyo
Na mwisho ni kwa masilahi ya Taifa na nchi hasa suala zima la Usalama

Nchi nyingi zimeingia katika machafuko kutokana na vyombo vya habari
Kuliacha suala hilo bila kulitolea kauli ili kupunguza jazba na munkari ni hatari

Tulimwelewa Nape, alituliza hali wakati suluhu ya kudumu inatafutwa

Hivyo anapoangalia wapi alikosea na kwanini 'aadhibiwe' kwa usahihi na si mkosaji kwakweli inamsumbua. Kama unavyoona ''ganzi'' katika nchi ndivyo ilivyo kwake

Katika wakati alio nao, marafiki wa kweli na wakaribu ni muhimu sana
Hawa walitakiwa kuwa naye mapema iwezekanavyo kumsaidia katika tafakuri

Kwa bahati mbaya hilo halikutokea ndio maana tukasema busara na hekma ni muhimu kuliko uwaziri na matukio. Tukachukua nafasi ya kumshauri kama anatusoma

Kwamba hayupo sawa na anahitaji muda wa kutafakari.

Wasiomtaki mema watatumia kauli kumpa mashtaka, kumhukumu na kumwadhibu.

Hapaswi kuwa na mikutano wala tweet , atulie kwanza

Kuhusu Polisi kutoa silaha kwakweli tumefika mahali tofauti.
Huyu ni waziri, IGP angempigia simu tu nadhani Nape angemsikiliza

Hata hivyo bado halijaribika jambo, Nape atafute mahali apunzike na familia ili kutafakari jinsi ya kuwahudumia watu wa Mtama

Ni psychological issue iliyohitaji psychotherapy mapema sana

Tusemazane
 
Mkuu Ogah

Kuna kitu kinaitwa 'knee jerk reactions' nadhani unakitambua
Kwamba, kuna mambo mtu anafanya hata kama hakupenda lakini inatokea

Hali hiyo hutokea hasa panapokuwa na taharuki inayoleta msongo wa mawazo

Natambua Nape ana msongo si kwa nafasi ya uwaziri bali kwa namna ilivyotokea

Alichosimamia kilikuwa kwa masilahi ya chama chake na katika misingi yake
Lakini pia ilikuwa kwa masilahi ya serikali yake ambayo ilionekana ndivyo sivyo
Na mwisho ni kwa masilahi ya Taifa na nchi hasa suala zima la Usalama

Nchi nyingi zimeingia katika machafuko kutokana na vyombo vya habari
Kuliacha suala hilo bila kulitolea kauli ili kupunguza jazba na munkari ni hatari

Tulimwelewa Nape, alituliza hali wakati suluhu ya kudumu inatafutwa

Hivyo anapoangalia wapi alikosea na kwanini 'aadhibiwe' kwa usahihi na si mkosaji kwakweli inamsumbua. Kama unavyoona ''ganzi'' katika nchi ndivyo ilivyo kwake

Katika wakati alio nao, marafiki wa kweli na wakaribu ni muhimu sana
Hawa walitakiwa kuwa naye mapema iwezekanavyo kumsaidia katika tafakuri

Kwa bahati mbaya hilo halikutokea ndio maana tukasema busara na hekma ni muhimu kuliko uwaziri na matukio. Tukachukua nafasi ya kumshauri kama anatusoma

Kwamba hayupo sawa na anahitaji muda wa kutafakari.

Wasiomtaki mema watatumia kauli kumpa mashtaka, kumhukumu na kumwadhibu.

Hapaswi kuwa na mikutano wala tweet , atulie kwanza

Kuhusu Polisi kutoa silaha kwakweli tumefika mahali tofauti.
Huyu ni waziri, IGP angempigia simu tu nadhani Nape angemsikiliza

Hata hivyo bado halijaribika jambo, Nape atafute mahali apunzike na familia ili kutafakari jinsi ya kuwahudumia watu wa Mtama

Ni psychological issue iliyohitaji psychotherapy mapema sana

Tusemazane

I couldn't agree with you more Sir...heshima mbele Mkuu

Nape yumo humu JF, I wish angekuwa anasoma...atleast kwenye hii forum ya....Great Thinkers
 
Ogah, post: 20312497, member: 121"] Tumefikaje huku?
Kukosa uvumilivu kwa pande zote, na kila mtu kusahau (kwa makusudi au kutokujua) majukumu yake kisheria.Ukosefu wa busara ili kutumia njia muafaka wa kutatua matatizo yaliyojitokeza
Tumefika huku kwasababu utamaduni wa kuvumiliana, kusikilizana na kuelezana ukweli umetoweka

Tumejenga utamaduni mpya kama ambavyo tuliona askari aliyemzuia Nape.
Ukisikiliza, askari alifika na kumwambia Nape arudi ndani ya gari.

Nape akauliza wapi kitambulisho chako?

Ni kweli mwananchi ana haki ya kuonyeshwa kitambulisho na Polisi hasa ''askari kanzu''

Ukitazama mavazi ya askari waliokuwepo, kuna tshirt zinazofanana na chama kimoja cha siasa

Nape kama mwananchi mwingine ana haki ya kuonyeshwa kitambulisho na mtu aliyemzuia

Badala ya kutoa kitambulisho askari akatoa bastola!! Yaani jibu la kitambulisho ni bastola

Askari alizuiwa na mwenzake wa vazi jekundu akimwambia'utaharibu mambo'

Ni baada ya askari wa bastola kuondoka, ndipo hali ikatulia

Unaweza kuona tulipofika, kwamba utamaduni wa kuongea kiswahili na kusikilizana umekwisha, sasa ni rungu , bastola, makonde ilimradi tu kauli za kiungwana na matendo sahihi zimekwisha

Ubabe haushii hapo upo hadi bungeni ambako kauli za kibabe ni sehemu ya uongozi
Bungeni ni mahali pa kuunganisha wananchi ili kuisukuma serikali kutimiza majukumu yake

Kwasasa lugha ya bunge hakuna, baada ya kauli mbili tatu utaona askari wakiingia na kuzoa waheshimiwa mzobe mzobe, ukitafuta mkasa , jibu ni ubabe ubabe tu. Lugha ya staraha hakuna

Kwa bahati mabya haionekani kama tuna mwongozo wa wazee au viongozi, tumepoteza !!!

Katika mazingira hayo, wananchi wamechanganyikiwa kwani wapo kipindi cha mpito.

Hawajui ima waache utamaduni wa kitanzania waliozoea na kukumbatia utamaduni wa kibabe, au waukane wa kibabe wakumbatie ule wa kitanzania. Wapo katika mtanziko mkubwa
Tunahitaji nini?Leadership ili kuweza kumaliza haya matatizo....Walau Waziri Mkuu (baada ya kujadiliana na wakubwa zake) asimame na kutoa muongozo....kwani matukio haya ni vizuri yakawa solved once and for all
Hatuna tatizo na leadership, wapo na wanaongoza .

Tuna tatizo na kupata matokeo ya leadership. Kazi ya kuongoza ni ngumu .

Inahitaji hekima na busara kuliko uwezo wa akili,hapo tuna ombwe, chanzo cha hali iliyopo

Kuna tafsiri kuwa kuongoza ni kutangulia na wajao wafuate kama shurti

Kuongoza ni kuratibu shughuli au maoni ya watu.

Na si kuratibu ili watu wakubaliane, lakini pia wakubaliane hata wasipokubaliana.

Kuwe na lugha stara, kuvumiliana, kuambizana ukweli, kusifiana, kukosoana na kupongezana

Ukiongoza watu milioni milioni 10, 25 au 45 usitegemee kuwa na mtazamo sawa.

Kama utataka hao mamilioni waende pamoja, lazima utumie mjeledi.

kwa binadamu mjeledi hauwezekani, ni viumbe wenye akili na fahamu

Kinachotakiwa ni kusikiliza, wale walioamua kwenda, na wanaopiga kona au kurudi nyuma

Ukielewa kwanini tofauti, ukatafuta njia ya uelekeo sahihi bila kujali wengi au wachache, utafanya kazi ya uratibu na ndiko kuongoza

Nilishangaa RC alipoingia katika mtafaruku na Bunge, bosi wake waziri mkuu alikuwa kimya ingawa naye ni mmoja wa watu wa mjengoni waliodhihakiwa.

Hili la Clouds nalo kakaa kimya. Pengine katenda kupitia mtu au kakaa kimya, hatujui! tunachojua kunq ombwe, Nape alijaribu njia ya haraka akisubiri ya muda mrefu, imemgharimu

Gharama aliyolipa Nape inaonekana ni yake, lakini tufikiri zaidi

Hivi nani atasimama ili naye alipe gharama kama Nape huko serikalini?

Makapuku nani atanena kwa niaba ikiwa midomo imefungwa kwa makufuli au gundi ya mbao?

Hatujui tunaelekea wapi, lakini moja tulilo na uhakika nalo, kuna tatizo tukae kitako kwanza

Tusemezane
 
RAIS NA VYOMBO VYA HABARI

Rais ameongelea uzalendo na 'kuonya' na kuelekeza media katika kutoa habari

Amesema hakuna habari za maendeleo isipokuwa zenye 'uelekeo' wa kichochezi

Alitolea mfano uwepo wa Rais wa Bank ya dunia na kilichopatika bila kuandikwa

Akasema Media imezuia kuandika 'habari za mtu' zikiandika matusi yake
Mwisho alisema vyombo vya habari visidhani vina uhuru huo, viangalie!

Hoja:
Kazi za media ni kutafuta habari na kuzitoa katika malengo mengi.
Media huandika habari za mwelekeo kadhaa na nyingine tofauti

Zama za media za serikali zimekwisha baada ya mfumo wa soko huria
Soko huria linaambatana na ushindani katika soko lililokuwepo nyakati hizo

Ushindani ni mbinu, kujua watumiaji au walaji wanahitaji nini na kwa wakati gani

Pili, kazi ya habari si kugundua habari bali kueleza habari zinazotokea au kutotokea
Asilia ya media ni curiosity na kupitia hilo tunahabarika, tunajifunza na tunaburudika

Uwepo wa habari unategemea vyanzo vya habari na nyakati.
Mfano, kitendo cha Polisi kuulizwa kitambulisho badala yake kutoa bastola ni habari

Ni habari inayotueleza jinsi gani tatizo linaweza kutokea pasipo na tatizo

Linatufunza weledi wa watu walioaminiwa kumiliki silaha na matumizi yake
Linatufundisha ni kinaendelea katika suala la haki, sheria , maadili n.k.

Lakini pia ni habari kwasababu kitendo kimetokea kwa waziri masaa machache, mbunge na kada maarufu wa chama. Ni habari kabla ya kuwa habari

Je, media zinapaswa kupuuza hilo?
Kama hilo ni la kupuuzwa, vipi lile la mtu kueleza mafanikio binafsi katika media?

Inaendelea....
 
Na vyombo vya habari
Inaendelea....

Vyombo vya habari vinaandika habari za maendeleo kama habari hizo zipo
Ndivyo tulivyoona suala la madawa ya kulevya, na vita dhidi ya rushwa

Inapotokea habari mbaya, hatupaswi kuvilaumu kwasababu ndizo habari za siku
Kitendo kilichotokea clouds na kuleta taharuki ni habari kwasababu nyingi
1. Kilitanguliwa na habari iliyoachwa kuendelea kwa muda mrefu
2. Kilikuwa cha kuingilia uhuru wa habari kwa matumizi ya nguvu
3. Kilifanywa na nani na kwa wakati gani na kwasababu gani

Kuna msemo usemao habari si ya mbwa kumuuma mtu bali mtu kuuma mbwa

Hilo lazima watendaji wa serikali walielewe, ni la asili na ndivyo ilivyo popote

Tukiangalia tukio la wiki na kauli ya leo, kuna mvutano kati ya serikali na media.
Tunaweza kuwa na mitazamo tofauti, hata hivyo ukweli wa mvutano upo wazi

Serikali imeonya mitandao na kutishia kuifuta. Mitandao ipo duniani na inaandika kila uchao.
Hata kama itafungwa, mitandao ipo katika 'space' kwa maana inaongozwa na satellite.

Kuifungia Tanzania hakuwezi kuwa jibu zaidi ya kuchochoea tu mivutano

Hoja yetu ni kuwa media ni 'fourth state'' hata kama hatukubali kwa maandishi

Kupitia media kila mmoja anapata chakula cha akili ambacho ni maarifa

Hoja si media zinaandika nini bali nini kinatokea hadi media zikaandika.

Njia rahisi ya kukabliana na media ni kuondoa urasimu na kuwa tayari kushirikiana navyo

Ni kuhakikisha viongozi wanatenda yale jamii inayotaraji kwa maendeleo.

Lakini pia media haziwezi kukaa kimya kunapotokea uchechefu wa kutisha

Rai, serikali na media zifanye kazi pamoja kwa manufaa ya nchi
Zifanye kazi penye matatizo na penye mafanikio bila kuonea au kuoneana

Tusilaumu media kwa kuzipa habari, tuzilaumu kama hatuna habari za kuzipa
Tusizilaumu tunapozipa habari mbaya, tujilaumu kwanini kuna habari mbaya

Jukumu la habari ipi ni nzuri na ipi ni mbaya lipo kwa 'mlaji'

Mvutano na media hauna mafanikio, kalamu ina nguvu zaidi ya silaha nyingi tunazojua.
Nguvu ya kalamu ni inapopenya ''ghala la silaha'' ikatoka na kitu silaha zikiwa salama.

Tutafute chazo cha matatizo, tusitafute njia ya kuficha matatizo.
Tutafakari wapi tumejikwaa na kwanini, tusitafute wachawi wasiokuwepo

Tusemezane
 
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI

HILI LINASHANGAZA, LINASIKITISHA

LITAKUCHAFUA BILA SABABU

Waziri wa Mamabo ya ndani ameagiza mtu aliyechomoa bastola kumuonyesha Mh Nape atafutwe, akamatwe kwasababu kitendo si cha kiaskari, kimungu na Nape si mhalifu

Tukio lilinaswa mbele ya Kamera likionyesha aliyemfikia Waziri na kisha mtafaruku kidogo
Walikuwepo askari kanzu na muda si mrefu gari iliyopiga honi ilifika eneo hilo

Mtu aliyetoa bastola alibaki eneo , ikieleza, alimiliki silha kihalali na hakuna shaka

Askari walifika eneo hilo wa ngazi zote hakuna taarifa za mtu asiye askari kumtisha Mh Nape

Itakuwa jambo la kushangaza sana kama umma utaamini aliyemwambia Nape arudi ndani ya gari alikuwa jambazi ambaye hakutaka Nape ahutubie bali aondoke

Waziri anaposema atafutwe inashangaza. Hivi kweli Mh Waziri anaamini ni mtu asiyejulikana?
Mh Waziri anaamini yule hakuwa askari? Kweli

Kauli ya waziri ya 'atafutwe' inaeleza hajulikani alipo.
Kwanini waziri asiagize polisi kumkamata waliyemtuma na wanayejua yupo wapi kwa sasa.

Kitendo hakikuwa cha kiungwana, ni matumizi mabaya ya mamlaka. Kuombwa kitambulisho hakumaanishi kutoa bastola na kumsota Mtanzania aliye mbunge, waziri na Raia asiye na hatia

Tunaamini kwa dhati waziri hakuzungumza kutafuta point za kisiasa bali kwa dhamira ya moyo
Tungemshauri atoe agizo la hatua dhidi ya Polisi huyo kwasababu haikuwa tukio la ujambazi

Kamera zipo waliokuwepo wapo hakuna sababu za kubabaisha umma kwa maneno matamu

Mh Waziri atambue kauli za namna hii hazitamjenga, zitambomoa kwani ataonekana 'opportunistic' akitumia matukio kupata point za siasa , tukio la hatari

Ipo siku mh waziri ataulizwa kuhusu hili, hilo linaweza kuwa 'anguko' lake katika uaminifu, ukweli, udhati na litaweka maadili yake ya kiroho eneo karibu sana na ulghai

Mh Waziri, hapana! hakuna kutafuta mtu, yupo anajulikana.

Kama zipo hatua zichukuliwe wazi
Kama ni utamaduni wa kuficha maovu kwa kauli basi liachwe tu na ondoa kauli yako

Tendo la kusema bila kutenda kwa kukwepa ukweli usiohitaji kibatari, mwezi au jua ni kuwafanya Watanzania majuha.

Ndio yale yale ya tukio la clouds kusemwa upande mwingine haujasikika
Tunajua upande ulikataa, waziri anatetea hilo bila aibu kwa kujua wananchi ni majuha

Kwamba waziri anahitaji ushahidi kuwa kulikuwa na 'uvamizi' wa clouds , hadi sasa hana taarifa

Ifike mahali viongozi wazitazame nafsi zao kwanza, wajiulize kuhusu 'moral authority' na kama wanayosema wanatenda haki kwa umma. Haya yanashangaza yanatisha

Tusemezane
 
Nguruvi3 asante sana kwa muda wako unaotumia japo kujadili hali ya siasa katika nchi yetu kwa sasa.

mimi toka last week nimejikuta nashindwa kuongea jambo.

kuna swala kubwa sana limetokea ambalo hilo lazima tulijadili kwa kina zaidi.

tuliona Mhe Nape mtu aliyetumia nguvu kubwa sana kupiga kampeni ili mhe shimiwa rais apate madaraka akiangukia pua. kwa maana nyingine tena tunaona jinsi ambavyo bao lake la mkono lilivyomtokea puani.

lakini tujiulize hivi leo hii watu wanaoona kwamba kaonewa hivi walitegemea nini?
je Nape alikuwa na uhalali wa kuunda tume ya uchunguzi wa sakata la mkuu wa mkoa kuvamia clouds ikiwa kwamba mkuu wa mkoa ndio mwakilishi wa raisi katika mkoa? tena anaunda tume kintyume na matakwa ya rais??

swala hili je linatofauti gani na lile alilolifanya Mwakyembe la kutoa tamko la serikali kwamba kuanzia sasa hakuna ndoa kufungwa bila cheti cha kuzaliwa. Halafu baada ya siku chahce rais anatoa tamko la kukataa hilo agizo?

kwanini Nape aonekane amekuwa mkosaji wakati kosa lake na la mwakyembe hayana tofauti. yote mawili hayakuwa na baraka za rais. na pia yote mawili ni maosa yaliyofanywa na watendaji wa serikali waliochaguliwa na raisi mwenyewe.

kama hilo halitoshi kwann kuwe na double standard ya jinsi ya kuhandle hii ishu? mwakyembe abadilishwe tu wizara halafu mwenzie atupwe nje?

isitoshe mawaziri wanapata wapoi guts za kauleta matamko ya serikali pasi kuongea na kukubaliana kwenye mkutano wao wa baraza la mawaziri?

Jambo jingine baya ni hili la mkuu wa mkoa wa DSM. Hivi kweli hilo swala lake yeye kutojisafisha kwa kuonyesha cheti chake ni kitu cha kupuuza na kuona tume iliypoundwa nje ya baraka za raisi ndio kosa kubwa sana?

kuna quote moje iliwah klusemwa na mfaransa mmoja kwamba "its dangerous to be right when your government is wrong"

nitarudi, subirini.....................
 
Nguruvi3 na wanaduru naomba niendElee kidogo kuandika hapaa.

kutokana na historia tumeona watu wengi sana waliojaribu kutumia kalaamu zao ili kuelimisha umma ama kupasha habari umma wakianguKIa pua kwa namna moja ama nyingine.

yapo matukio ambayo yalipelekea adi wengine kuitwa wakimbizi akina mzee Jenerali ulimwengu kisa kalamu zao. Wapo wengine tuliona wakifukuzwa hadi kazi kisa kalamu zao. Tirdo Mhando alifukuzwa kazi TBC kisa kurusha kipindi cha upinzani live.

well tumshukuru sana Mungu kwamba wahanga wote wa matukio haya bado Mungu anawapigania na hawajawah kupoteza kalamu zao.

leo hii naona media zinanyimwa uhuru kwa staili mpya kabisa, haikuishia hapo vitisho viko nje nje, sheria ya uhuru wa habari na mitandao nayo inakuwa mwiba mwingine mkali kwa watu.

haya yote tunayajua na kuyalalamikia chinichini hakuna anayeweza kumfunga paka kengele. kisa tunaogopa.

jambo la kujiuliza ni wapi ambapo sisi tunakosea katika kutekeleza haya? je kuongea jukwaani ni kosa? ama kuandika ama nini?

Hivi leo hii wanasheria wetu wabobezi pamoja na waandish wa habari wa mambo ya siasa wakitusadia kudraft statement nzuri kisha tukaenda nayo mahakamani kweli hatutasikilizwa?

mkiwaza kwa mbali mtaagundua kuwa tumekuwa hodari wa kulalamika lakin pia hatujui WAJIBU WETU PENGINE NDIO MANA HAYA YANATOKEA
 
Back
Top Bottom