Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri...

Discussion in 'Great Thinkers' started by Nguruvi3, Dec 30, 2015.

 1. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #1
  Dec 30, 2015
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,176
  Likes Received: 4,736
  Trophy Points: 280
  MWANZO

  HAPA KAZI, MATARAJIO NA MATUMAINI YA WANANCHI

  DHANA YA 'MABADILIKO' DHIDI YA KIU YA WANANCHI

  Awamu ya 5 na miezi 2. Ni muda mfupi kutathmini utendaji/ufanisi ikizingatiwa changamoto nyingi za Taifa. Pamoja na ukweli huo, tunaweza kuipima serikali kwa uundwaji, uelekeo na vipaumbele vyake

  Mengi yamejitokeza na kuamsha hisia tofauti miongoni mwa wananchi. Wapo wenye matumaini na wenye mshangao kuhusu mwelekeo na kiu ya mabadiliko

  Hoja ya mabadiliko ilitumiwa na wapinzani , Rais Magufuli akaunga mkono kutokana na haja ya wakati.

  Tunasema Magufuli, kwasababu hakuna rekodi za CCM kuzungumzia mabadiliko

  Hata hivyo, mabadiliko hayakuelezwa kwa undani na pande zote mbili

  Wapinzani wakisema ni namna tunavyofanya mambo, CCM wakisema ni mabadiliko ndani yake na serikali

  Mbele ya fikra za wananchi, mabadiliko ni matumaini na kukidhi haja na matarajio. Ni kubadili yanayogusa maisha yao, kujenga utamaduni mpya na kuweka misingi ya kudumu

  Dhahiri, wamechoshwa na hali ya uchumi, utendaji , uongozi na maono ya siku za baadaye. Uchovu huo hauna chama wala itikadi, kwa pamoja wanakubaliana kuhusu hilo

  ''Makubaliano'' hayo ndicho chanzo cha uchaguzi uliokaribiana sana. Pengine kungalikuwepo na taratibu nzuri za uchaguzi, huenda hali ingalikuwa tofauti

  Kukaribiana kwa uchaguzi kulizaa kampeni zisizo za kistaarabu. Wanasiasa wakaacha hoja na kuhamia katika kejeli, matusi na kashfa, ukabila, udini na kuvikipaliliwa

  Mbegu zilizopandwa zinachanua na kuweka ufa usio na ulazima katika Taifa. Wanasiasa hutanguliza masilahi yao zaidi ya umma. Kwao athari za kauli si nzito kama za kukosa uongozi.

  Tutaangalia awamu ya tano kwa muda uliopo, tukijadili mwelekeo unaonekana na nini tutarajie

  Mabandiko yatajadili nini matarajio na matumaini ya wananchi katika zama za #HapaKaziTu, na kama tupo katika mwelekeo au mwendelezo

  Inaendelea.....
   
 2. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #261
  Jan 3, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,176
  Likes Received: 4,736
  Trophy Points: 280
  Bandiko hili #69 na #52 tumeongeelea tatizo la mfumo wa elimu analokumbana nalo Waziri wa elimu Mh Ndalichako

  Jambo moja tunalikubaliana kama taifa ni kuwa mfumo wetu wa elimu una matatizo
  Ukubwa wa tatizo umeongezeka awamu ya nne ambapo mambo mengi yamefanyika kienyeji

  Bila shaka kazi aliyo nayo waziri wa elimu ni kubwa na ngumu na huenda inapelea yeye kuwa kiongozi wa hoja zenye utata 'controversy' kila mara

  Waziri Ndalichako'anashambuliwa' bila kuonyeshwa mbadala au mapungufu ya hoja zake

  Sehemu ya tatizo analitengeneza mwenyewe hasa kwa matamko yake kama amri

  Akiwa waziri ana nafasi ya kutoa amri, lakini asisahau nafasi yake ya kiongozi wa umma

  Sifa ya kiongozi wa umma ni kusikiliza, kujadiliana, kutoa hoja kwa facts na si matamko

  Tatizo la pili linalomkumba Mh waziri ni kuvutika katika migogoro ya kisiasa

  Ni mwanataaluma akiwa na nafasi ya siasa. Zipo sehemu siasa haichukui nafasi ya taaluma

  Tunasema haya kwasababu kuu mbili.

  Kazi ya kujenga mfumo mbovu ni ngumu na hatutegemewi awe malaika kwa usahihi.

  Lakini pia yapo anayosimamia ambayo kwa mtazamo ni sahihi na anayopotoka

  Ni kwa msingi huo, tutapitia hoja na matamko yake kwa ukaribu

  MITIHANI YA BAADHI YA TAASISI BINAFSI NA UMMA KURATIBIWA NA NECTA

  Moja ya hatua nzuri za Mh Waziri ni kuahakikisha mitihani kwa baadhi ya taasisi inaratibiwa na chombo kimoja.

  Kwamba NECT itapima watahaminiwa wa taasisi binafasi na zile za umma

  Tukumbuke, soko huria lilifungua milango na elimu ni sehemu mojawapo.

  Kwa muda mfupi kulizuka vyuo na taasisi zinazotahini wanafunzi kisha kutunuku vyeti

  Taasisi binafsi zinatoa elimu kwa utaratibu wa biashara.

  Ubora ambalo ni la kwanza, hupewa umuhimu wa pili baada ya biashara kufanyika.

  Tumekuwa na matatizo ya watahiniwa waliopata vyeti katika mazingira ya kusikitisha

  Kitendo cha kuamua watahaniwa wapimwe kwa chombo kimoja kama NECT ni kizuri sana

  Hili linapima ubora na kupora nguvu za ''biashara'' kwa wafanyabishara ya elimu

  Ingawa baadhi ya watu hawakufurahia, jambo hili ni la kuungwa mkono na kupongezwa.

  Tunahitaji ubora katika elimu si mchezo wa biashara katika suala nyeti na muhimu kama elimu kwa Taifa

  Inaendelea...
   
 3. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #262
  Jan 3, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,176
  Likes Received: 4,736
  Trophy Points: 280
  ''KUSHAMIRI'' KWA VYUO VIKUU

  Katika kipindi cha miaka 10 Taifa limekuwa na vyuo kuliko awamu tatu kwa mfululizo

  Katika kipindi hicho idadi ilifikia 50 kwa vile vya umma na binafsi

  Kama tulivyoeleza awali, mfumo wa soko huria ulichukuliwa huria katika maeneo nyeti

  Awamu ya pili iliyofungua soko huria ilikuwa makini, kama ilivyokuwa awamu ya tatu

  Vyuo holela vilishamiri awamu ya 4, na kushindwa kutofauti high school na University

  Ubora wa baadhi ya vyuo hasa binafsi ni wa kutilia shaka kila eneo

  Tatizo lilianzia wapi?

  1. Serikali:
  Haikuwa na mipango madhubuti ya elimu kuanzia ngazi za chini.
  Kukawa na ongezeko la wanafunzi wanaohitaji elimu ya juu kwavile hakukuwa na maandalizi ya muda mfupi na mrefu. Kilichotokea ni mambo ya zimamoto

  Tatizo hii lilitengenezwa na siasa kutawala utaalam.
  Kwamba, wanasiasa walichotaka ni idadi ya vyuo na wanafunzi ili kujenga hoja ya maendeleo bila kujali ubora wa elimu na wahitimu wake

  2. TCU:
  Tume ya vyuo yenye jukumu la kutathmini/kusimamia ubora wa elimu ikawa njia panda

  Kwanza, inaongozwa na maamuzi ya wanasiasa, utaalam haukuwa sifa au muhimu tena

  Pili, wahadhari wa vyuo vikongwe wakaona huo ni mradi wa kupata part time
  Wakasimama kidete dhidi ya tume na serikali ili mradi wao wa 'pembeni' uwe endelevu

  Kwa pamoja, wanasiasa na wahadhiri wakapoka nguvu za TCU kusimamia uanzishwaji na ubora wa elimu inayotolewa.

  Tukafika mahali ambapo mwanafunzi aliyemaliza chuko kikuu ni mhadhiri katika majengo yaliyopakwa rangi na maua na mti wa bendera nje. Ni chuo kikuu!

  3. Mashirika na wafanya biashara wakatumia udhaifu wa serikali na wanataaluma kuanzisha vyuo hata kupanga namna gani wanataka wanafunzi wafaulu biashara iwe endelevu

  Hatua za Mh Waziri kufunga vyuo visivyo na sifa ni ya kuungwa mkono
  Hatuhitaji lundo la wenye degree zisizo na ubora.

  Tunahitaji wahitimu watakaoshindina katika soko la dunia katika mazingira yetu kwa ubora ule ule unaopatikana kwingine.

  Tunahitaji vyuo kama centre for excellence na si mkusanyiko wa wanafunzi

  Zoezi halifurahiwi na baadhi yakiwemo mashirika , wafanyabiashara na wahadhiri

  Ni zoezi la maana kwa muskabali wa taifa letu, inasikitisha waziri akipingwa kwa hili

  Je wapi waziri amekosea?

  Na nini mbadala wake kwa haya tunayoona ambapo chuo kikuu cha afya hakiwezi kutunza afya za wananchi kwa kutupa 'vitu nyeti' hovyo kama tulivyoona kule Mbezi?

  Kwanini chuo kama hicho kiendelee kuwepo? Chuo hicho kinatoa elimu gani?

  Inaendelea
   
 4. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #263
  Jan 4, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,176
  Likes Received: 4,736
  Trophy Points: 280
  'UTATA' WA WAZIRI WA ELIMU

  Pamoja na mazuri mengi na ugumu anaokutana nao, waziri wa elimu amekuwa na mambo tata

  ADA ELEKEZI
  Waziri amekuwa katikati ya mgogoro wa shule moja binafsi kuhusu madai ya wazazi ya ada kubwa
  Hilo nalo limekuwa na utata kwingine, shule binafsi zikiwa na ada 'elekezi'

  Kama tulivyoeleza, soko huria lilifungua elimu katika huria kama masoko ya huduma na bidhaa nyingine
  Elimu ikawa huduma inayolipiwa kama huduma za afya, bima , benki n.k.

  Wajibu wa serikali ni kuweka mitaala, kusimamia utoaji wa elimu pamoja na kutathmini

  Kwanini mzazi anapeleka mtoto shule ya kulipia, hilo linabaki kuwa tatizo la mzazi na si serikali

  Mzazi asiymudu gharama za elimu ana wajibu wa kutafuta eneo jingine litakalokidhi haja yake

  Kulalamika ada ni ya juu ni sawa na kulalamika bima ya magari au huduma za afya ni za juu

  Kwa upande wa waziri, suala si kutoa ada elekezi bali kujiuliza kwanini shule binafsi zinakithiri.

  Jibu jepesi ni kuwa elimu katika shule za sekondari imeshuka.

  Idadi ya wanafunzi, vitendea kazi duni, walimu hakuna au waliopo ni duni n.k.

  Kuimarisha shule za umma kutaleta ushindani kwa shule binafsi
  Ushindani utakwenda sambamba na utoaji wa huduma zinazolingana na ubora na gharama halisi

  Njia ya pili ni kuacha bei ya soko iamue.
  Ushindani utatokea miongoni mwa wamiliki wa shule binafsi na hiyo iTasaidia kupunguza gharama

  Fikiria wakati wa Mobitel inaanza, simu ya mkononi ilikuwa kitu cha watu wenye uwezo.
  Serikali haikupanga bei elekezi, iliacha other players kuingia.

  Kwa muda gharama zikapungua kiasi cha watu wengi kumudu.
  Hata hivyo, kama mashirika zaidi yatarhusiwa, gharama zitakwenda chini zaidi ya sasa

  Waziri hapaswi kuwa katikati ya mgogoro wa wazazi na wamiliki.
  Anachotakiwa kufanya ni kutengeneza mazingira mazuri ya ushindani.

  Kwanza, kuimarisha shule za umma katika ubora na unafuu
  Pili, kujenga mazingira ya washindani wengine kuingia katika sekta ya elimu
  Tatu, kusimamia sera ya taifa ya elimu kuanzia ufundishaji hadi kutahini

  Kuingia katika mgogoro ni kutafuta utata usio na ulazima.

  Inaendelea...
   
 5. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #264
  Jan 4, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,176
  Likes Received: 4,736
  Trophy Points: 280
  UTATA WA WAZIRI

  VYUO VYA CHINI, KATI NA VYUO VIKUU

  Waziri alinukuliwa akisema wanaosoma kada za chini na kati hawawezi kwenda kusoma University
  Kauli ilileta utata ingawa ilifafanuliwa waziri alinukuliwa vibaya

  Kwa vyovyote itakavyokuwa kuna umuhimu wa kueleza kwanini suala hili lina utata

  1.Uwepo wa kada za kitaaluma

  Kuna sababu za msingi za kada mbali mbali kuwa na viwango vya wataalam kwa ngazi tofauti

  Hili ni suala lililopo duniani kote kuanzia nchi zilizoendelea hadi nchi masikini. Kuna sababu

  a)Mgawanyo wa kazi kulingana na kada husika

  Katika serikali, taasisi, mashirika, NGO au makampuni kuna viongozi wa juu mfano wa CEO

  Wawe ni wataalam wa fani husika au la, kazi yao ni kutengeneza mazingira ya kazi pamoja

  Kutoa maamuzi mazito yanayohusu kazi, na kuwa viungo kati ya maeneo yao na mengine

  Hapa tutoe mfano rahisi kueleweka. Kazi ya CEO wa kampuni ya ujenzi ni kutafuta fursa au kupokea fursa na kuzifanyia tathmini. Kazi hii husaidiana na wenzake katika ngazi za juu 'management'

  Hivyo kazi yaCEO ni kuhakikisha fursa iliyopo inatengenezewa mazingira mazuri na management.
  Kazi ya kuiweka management pamoja ni yake.

  kuanzia hapo management inatumia wataalam kutathmini, kupanga mikakati kwa kuwatumia wataalam

  Kwa wataalam hapo utakuta Architect, Civil Engineer, structural engineer, Energy, communication, transportation, watu wa drainage, buiding materials, accountants n.k. orodha inaendelea

  Kundi hili lina wataalam wanaoweza kutoa tathmini, kutafsiri na kutafuta njia mbadala kufikia malengo
  Wana uwezo wa kueleza na kujenga hoja za kitaalam

  Itafuta kada nyingine kama ya Technicians wenye majukumu yao wakisimamiwa na kada ya juu

  Mwisho itakuja kada ya chini ya wenye certificate nao wanawajibika kwa ngazi inayofuata

  Mpangilio huo hautokei kwa bahati mbaya, unatokea kutokana na mafunzo kutoka katika mitaala

  Kwa mfano huo tunapata vyuo vya kada mbalimbali, kama certificate, Diploma, Degree n.k.

  Utaratibu huo huonekana kila mahali, kwa mfano kuanzia karani hadi katibu mkuu, waziri na kuendelea

  Uwepo wa kada mbali mbali ni suala la ulazima na universal, si la Tanzania tu.

  Tutajadili kwa undani utata uliozuka kuhusu suala hili.

  Tuangalie sababu ya pili ya uwepo wa kada hizo

  Inaendelea
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #265
  Jan 8, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,176
  Likes Received: 4,736
  Trophy Points: 280
  Inaendele

  VYUO VYA CHINI, KATI NA JUU

  Sababu ya pili ya kuwa na kada hizo ni kupata wataalam katika viwango na mahitaji tofauti
  Huwezi kumpeleka mtu wa ngazi fulani katika kijiji lakini unaweza kupata watu wa kada eneo hilo

  Hapa ina maana kuwa kazi ndogo zinazohitaji utaalam wa kiwango hicho hufanywa katika maeneo kama vijijini na watalaam wa kada za chini , na linapokuwa jambo zito wataalam hao watashauri

  Kwa mfano Clinical officer atatibu kwa kiwango alichoelekezwa.
  Ikitokea haja atafanya rufaa katika ngazi ya juu na hilo litaendelea hadi ya juu kabisa.

  Ndivyo ilivyo dunia kote na si suala la Tanzania tu

  ii) Katika nchi changa kama yetu, baada ya uhuru tulikuwa hatuna wataalam.
  Kilichofanyika ni program za kupata wataalam wa kada za chini kusaidia kwanza tukijenga uwezo

  Kwa walioishi miaka ya 60, 70 na hata 80 watakubaliana na hoja hii.
  Ndio maana tulikuwa na vyuo vingi vya kati na chini kuliko ilivyo sasa.

  Hili lilisaidia sana kupunguza tatizo la wataalam ingawa halikuwa suluhisho kamili.

  iii)Miaka 10 tu iliyopita tulikuwa na vyuo vikuu si zaidi ya vitano.
  Idadi ya wanafunzi waliomaliza kidato cha sita ilikuwa kubwa kuliko uwezo wa vyuo hivyo

  Kuwapa elimu katika vyuo vya kati ilikuwa suluhisho la tatizo

  Kutokana na sababu hizo zote zilizojadili, ni makosa kudhani kuwa waliopitia vyuo vya kati na chini wana uwezo duni na hawana haki ya kujiendeleza. Hapa ndipo mh Waziri alipopotoka

  Kwanini tunasema Mh Waziri alipotoka? Hili tunalijadili kwa kuangalia historia fupi tu ya vyuo kama Marangu(elimu), Butimba(elimu), Mlingano(Kilimo). Olmotoni( Nyuki na misitu),Mpwapwa(elimu),Kigurunyembe(elimu),Ifunda (elimu/ufundi), Bugando(Clinical officer), Machame(Clinical officer), KCMC(Clinical officer) Ifakara (Clinical officer) Dar tech(Ufundi) Arusha tech(ufundi) n.k.

  Inaendelea
   
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #266
  Jan 9, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,176
  Likes Received: 4,736
  Trophy Points: 280
  VYUO

  Vyuo tuloivyotaja bandiko la awali vilikuwa na hadhi na vimetoa wataalam katika fani mbali mbali
  Kwa mfano, chuo cha elimu Marangu kilijulikana kwa kutoa wahitimu wazuri sana katika elimu

  Chuo cha Mlingano Tanga kilifikia hatua ya kuwa taasisi ya utafiti kikiwa affiliated na SUA
  Chauo cha Olomotoni, hadi leo ni sehemu ya chuo kikuu cha SUA

  Arusha na Dar tech navyo kama vile vya afya tulivyotaja vilitoa wataalam katika viwango vizuri sana
  Wahatimu wa vyuo hivyo waliweza kujiendeleza hadi ngazi za udkatari na uprofesa

  Swali kwa mh waziri,ni kwanini iwe ni lazima kupitia kidato cha sita kuingia chuo kikuu?
  Wanafunzi wa kidato cha sita na wanaomaliza vyuo na kujiung hutahiniwa sawa

  Waziri angejiuliza, ikiwa wametahaniwa na kufaulu au kufeli kwanini liwe tatizo kwa upande wa wanaopitia vyuoni? Je, ana takwimu za kuthibitisha madai kisayansi?

  Waziri angetafakari,wanafunzi wanaomaliza vyuo wana msingi mzuri katika fani husika na uwezo wa vitendo 'practical'

  Hii haimfanyi wa kidato cha sita kuwa hafifu, ni ukweli, kidato cha sita kinamjenga mwanafunzi uelewa wa haraka na kupambanua mambo kwa wepesi. Ni ukweli

  Hoja ya Mh Waziri waliomaliza vyuo hawapaswi kujiunga na chuo kikuu haina mantiki

  Hoja ingekuwa na mantiki kama Waziri angefuata mfumo unaotumika kwingine duniani

  Taasisi za elimu ya juu zinatoa 'accreditation' kwabaadhi ya vyuo vya kati

  Mfano, vyuo vikuu vingefanya tathmini ya mitaala ya vyuo ili kuvipa 'accreditation'

  Kama SUA watatambua Mlingano au Olmotoni hakuna sababu ya kuzuia mwanafunzi

  UDSM wakitambua mitaala ya vyuo kama Marangu, Mpwapwa, Butimba n.k.hakuna sababu ya kumzuia mwanafunzi

  Muhimbili wanatambua Diploma zinazotolewa na baadhi ya vyuo vya afya,kwanini basi vyuo vingine visitazame utaratibu huo?

  Kwa wenzetu, kabla mwanafunzi hajajiunga na chuo au taasisi ya elimu ya kati,kuna taarifa za wazi chuo husika hakitoi 'credit' ya kujiunga na elimu ya juu, au kinatoa

  Badala ya kupiga marufuku, Mh waziri angekaa na wataalam waangalie jinsi ya ku streamline utaratibu

  Nia ya Mh waziri ni njema kwa mengi tu, lakini pia kuna maeneo anapotoka. Tumsaidie

  Utitiri wa vyuo vikuu na athari zake... Inafuata
   
 8. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #267
  Jan 10, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,176
  Likes Received: 4,736
  Trophy Points: 280
  VYUO VIKUU NA VIWANGO 'DUNI'

  Katika mambo yalitikisa awamu ya tano ilipoingia madarakani ni la wanafunzi wa UDOM

  Wanafunzi walitimuliwa baada ya kubainika walikuwa na viwango duni

  Hili ni jambo jema katika jitihada za kupata watalaam walio bora na katika viwango

  Hata hivyo kuna kitu kimejitokeza, badala ya kutafuta chanzo hisia na jazba zilitawala

  Miongoni mwa waliofukuzu kwa uduni wa viwango wapo wa mwaka wa pili, tatu

  Swali, kama wanaviwango duni waliwezaje kuvuka mwaka wa kwanza au wa pili?

  Badala ya kuwafukuza viwango duni waliovuka miaka, Mh Waziri angejiuliza walivukaje?

  Pili,tume ya vyuo vikuu inayohakiki viwango ilikuwa wapi bila kubaini viwango duni?

  Tatu, Mh Waziri aliongea na wahadhiri kujua kwanini viango hafifu vilifanya vema?

  Laiti Mhe angejiuliza uchache wa maswali, kutimua kungekuwa jambo la mwisho.

  Maana yake waziri angekuwa na majibu ya kwanini anawatimu na hapo ndipo pa kuanzia

  Kuwatimua tu ilikuwa kuwaadhibu bila sababu za msingi.

  Waliomba, wakachaujwa ,wakaingia, wakatahiniwa, wakavuka mwaka. kosa lao li wapi.

  Hatua ya Mh waziri ilikuwa na lengo zuri, kwa bahati mbaya iliongozwa na jazba na siasa badala ya sayansi ya utafiti wa tatizo, chanzo na suluhisho.

  Je, kuwatimua wanafunzi wa UDOM kume solve matatizo kama hayo katika vyuo vingine na nchi kwa ujumla wake?

  Tusemezane
   
Loading...