Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

TOOL LITLLE,TOO LATE

YA LEMA NA MAHAKAMA

Wazungu wana msemo huo wakimaanisha ''kinachofanyika hakitoshi na kimechelewa''

Mahakama imekaripia suala la kunyimwa dhamana la Mbunge wa Arusha
Serikali ikiondoa hoja zake dakika za mwisho

Kinachoonekana hakina maelezo bali ulikuwa utashi tu binafsi kutenda kinyume

Miezi 4 bila uhuru ni muda mrefu,sababu zilizotolewa zikizondolewa mwishoni inaeleza jambo. Kwamba, hakukuwa na sababu za kisheria bali nyingine nje ya hizo

Karipio la mahakama limekuja likiwa limechelewa na 'uharibifu' ukiwa umeshafanyika
Mahakama ilipaswa kuliona hili mapema kabisa na 'sensitivity' yake

Kwanini mahakama za chini hazikuweza kuliona hili?
Pengine ni kutokana na mamlaka ilizo nazo, inatosha kusema hatua zimechelewa

Zile hisia za mihimili kupoteza nguvu zilizozagaa vichwani mwa watu zinazidi kupata nguvu kutokana na kauli ya mahakama

Mambo kama haya yanajenga hisia kuhusu mihimili yetu na mamlaka zake

Yanajenga hisia zisizo za lazima kuhusu utawala wa sheria
Yanatugawa kama taifa na yanajenga hisia za ''uonevu'' zinazoweza kujengewa sababu

Miezi 4 magereza bila huru na bila hukumu nani atafaidia muda huo?
Na sababu gani zinazoweza kutolewa ku justify hali hiyo? Ilikuwa kukomoana?

Yes kwa mahakama lakini ni too little too late

Tusemezane
 
TOOL LITLLE,TOO LATE

YA LEMA NA MAHAKAMA

Wazungu wana msemo huo wakimaanisha ''kinachofanyika hakitoshi na kimechelewa''

Mahakama imekaripia suala la kunyimwa dhamana la Mbunge wa Arusha
Serikali ikiondoa hoja zake dakika za mwisho

Kinachoonekana hakina maelezo bali ulikuwa utashi tu binafsi kutenda kinyume

Miezi 4 bila uhuru ni muda mrefu,sababu zilizotolewa zikizondolewa mwishoni inaeleza jambo. Kwamba, hakukuwa na sababu za kisheria bali nyingine nje ya hizo

Karipio la mahakama limekuja likiwa limechelewa na 'uharibifu' ukiwa umeshafanyika
Mahakama ilipaswa kuliona hili mapema kabisa na 'sensitivity' yake

Kwanini mahakama za chini hazikuweza kuliona hili?
Pengine ni kutokana na mamlaka ilizo nazo, inatosha kusema hatua zimechelewa

Zile hisia za mihimili kupoteza nguvu zilizozagaa vichwani mwa watu zinazidi kupata nguvu kutokana na kauli ya mahakama

Mambo kama haya yanajenga hisia kuhusu mihimili yetu na mamlaka zake

Yanajenga hisia zisizo za lazima kuhusu utawala wa sheria
Yanatugawa kama taifa na yanajenga hisia za ''uonevu'' zinazoweza kujengewa sababu

Miezi 4 magereza bila huru na bila hukumu nani atafaidia muda huo?
Na sababu gani zinazoweza kutolewa ku justify hali hiyo? Ilikuwa kukomoana?

Yes kwa mahakama lakini ni too little too late

Tusemezane
Wameamua kuondoa zuio la dhamana sasa hivi sababu lengo lao limetimia, kumshikisha Lema adabu. Baada ya Lema kuachiwa hutasikia tena kesi hii ikipewa uzito tena. Na huu ndio mtindo wa kesi zote zenye mwelekeo wa kukomoana na kwa bahati mbaya sana mhimili wa sheria umekuwa ukitumika vibaya kufanikisha malengo haya maovu.

Natamani mahakama pia itoe karipio kali kwa wakuu wa mikoa na wilaya kwa matumizi mabaya ya madaraka kwa kuamuru watu wawekwe ndani masaa 48 kwa makosa ambayo hayahusiani kabisa na sheria husika. Wamekuwa waki-abuse madaraka yao kwa kutoa amri za kukamatwa kwa makosa ya kushughulikiwa kiutumishi au kutokana na chuki binafsi tu!
 
"Mwalimu, post: 19917022, member: 11689"]Wameamua kuondoa zuio la dhamana sasa hivi sababu lengo lao limetimia, kumshikisha Lema adabu.
Imechafua sura ya Taifa. Imetuondoa katika utawala wa sheria. Kila jambo sasa linaangaliwa kwa mtazamo wa 'kukomoana' hata kama lina ukweli.
Baada ya Lema kuachiwa hutasikia tena kesi hii ikipewa uzito tena. Na huu ndio mtindo wa kesi zote zenye mwelekeo wa kukomoana na kwa bahati mbaya sana mhimili wa sheria umekuwa ukitumika vibaya kufanikisha malengo haya maovu.
Mhimili wa sheria unatia shaka na kwa hili la Lema , mhimili umechafuka sana.
Nilishangaa wakati mawakili wanaambiwa 'wawekwe mahabusu'

Wanasheria walikuwa wanacheka kana kwamba lilikuwa jambo jema
Hakuna aliyeonyesha mshangao, walikuwa wanachekea tu kwa raha kabisa

Kuna sehemu nilisikia ' Jaji anaona mbona hutumii kifungu fulani'?
Hapa ilieleza kuwa kazi ya Jaji ni kuegemea upande wa wakili wa serikali
Wanasheria walikuwa kimya tu bila kutetea wajibu wao kama watenda na watoa haki

Katika kuhakikisha mhimili unadhibitiwa, uchaguzi wa chama cha taaluma sasa unapigwa mkwara. Ile kauli ya 'sitamchagua Jaji mwenye uelekeo wa siasa' ilimaanisha wasichaguliwe watu fulani. Waziri naye kasema atafuta chama hicho ikiwa....

Yote hayo ni katika kudhibiti mhimili wa sheria, na kwa bahati mbaya wanasheria wamekuwa 'kondoo' watiifu wakisubiri appointment. Mhimili huu umejichafua
Natamani mahakama pia itoe karipio kali kwa wakuu wa mikoa na wilaya kwa matumizi mabaya ya madaraka kwa kuamuru watu wawekwe ndani masaa 48 kwa makosa ambayo hayahusiani kabisa na sheria husika. Wamekuwa waki-abuse madaraka yao kwa kutoa amri za kukamatwa kwa makosa ya kushughulikiwa kiutumishi au kutokana na chuki binafsi tu!
Mkuu mhimili wa sheria sidhani kama utaweza
Ikiwa hawawezi kuzungumzia nafsi zao watawaezaje kuzungumzia umma?

Tuliwahi kusema hizi amri za kufunga watu kwa makosa ya ajira ni kinyume cha sheria
Tatizo ni kuwa wanaopaswa kutafsiri sheria sasa wapo taabani, wameshakuwa tawi
 
KIPI KIMEPATIKANA BAADA YA MIEZI 4?

Nakumbuka Mh Rais aliposimamishwa ziarani na mama mmoja akimlilia kunyimwa haki za baada ya kifo cha mumewe. Rais alitoa maagizo ya wahusika kushughulikia suala hilo

Ndivyo ilivyotokea Dar, mama akililia kuongea na Rais, akiwataja wahusika walioshindwa kumsiadia hasa vyombo na idara za sheria, usalama na haki

Kila kona ya nchi watu wananyimwa haki zao au kucheleweshewa
Mh Rais ameliongelea mara nyingi akisisitiza vyombo husika kutimiza wajibu wake

Tunachotaka kusema, kuna matatizo mengi yanayohitaji nguvu na utendaji wa serikali kuanzia eneo la mahakama, mwanasheria mkuu, DPP, DCI n.k.

Tunafahamu rasilimali hazitoshi, chache zilizopo zitumike kwa busara

Kwa miezi 4 ya Mbunge kanyimwa dhamana kwa dana dana tu.
Tunaweza kueleza nini hasa kimepatikana kwa ustawi wa jamii kwa dana dana hizo?
Muda wa kutengeneza dana dana ulitumia gharama kwa walioajiriwa na kulipwa

Sababu za kunyimwa dhamana zilionekana kubwa kutokana na aina ya kosa!
Mahakama ya Rufaa ikashangazwa na kukemea kilichoendelea

Serikali ikaondoa pingamizi na kurudisha suala mahakama kuu
Mahakama kuu imetoa dhama kwa mbunge

Katika mzunguko wote huo kuna maswali ya kujiuliza

1. Kulikuwa na sababu zozote za msingi za kumyima dhamana?
Je, sababu hizo sasa hivi zimepoteza umuhimu wake?

2. Katika miezi minne, nini kimepatikana tunachoweza kusema ni kwa faida ya umma?

3. Je wahusika ikiwemo mahakama ya mwanzo walitimiza wajibu wao kusaidia Taifa?

4. Sura ya Serikali na mtazamo wa jamii kuhusu haki upo katika mizani gani sasa hivi?

Tunauliza kwasababu nguvu zinatumika wakati makubwa yakikosa msukumo inasikitisha

Yapo yanayohitaji kushughulikiwa katika jamii yetu, hili halikuwa moja yao

Utendaji wa namna hii unamlazimu Mh Rais kupokea malalamiko ya watu mitaani?

Hiyo ni dalili kuwa wasaidizi wake ima hawatimizi wajibu, hawana mwongozo n.k.

Ndiyo maana tunauliza, miezi 4 imetoa nini tofauti na siku ya leo?

Tumepata kitu gani zaidi ya gharama tulizotumia kama Taifa?

Tusemezane
 
ALICHOSEMA KAMISHNA SIANGA NA MANTIKI ZAKE

Katika hotuba, kamishna Sianga alisema mambo kadhaa kuonyesha uelekeo.
Kwa maana alipanga safu yake, akatoa dira ya mapambano

1. Kamisha aliwatambulisha wakuu wawili, Intelejensia na Oparesheni
Hii ni kuwa na habari za uhakika ili kuwezesha operesheni kufanyika

2. Bw. Sianga akazungumzia matumizi ya sheria katika mapambano
Alimaanisha kuepuka ukiukwaji wa haki za watu(intelejensia na oparesheni)

3. Sianga akagusia hatua kwa maafisa wa serikali wanaozembea madawa kuingia nchini.
Sianga ana maanisha kama dawa hazitaingia, hakutakuwa na wateja

Na kwamba, dawa inawezaje kufika Morogoro, Manzese au Mbagala bila kuingizwa?

Hoja ya Sianga ni kuwa tatizo si watumiaji, bali watumiaji wanapata kutoka wap?
Kitaalam Sianga anajaribu kuziba mianya ya kuingiza madawa (conduit)

4. Akazungumzia mahakimu na mawakili wa serikali wanaovuruga kesi
Alilimaaminisha pesa inatumika, hivyo mapapa yanaendelea kuwepo

5. Kamishna akasema mapambao ikibidi yatafika Zanzibar
Hoja, huwezi kupambana na madawa kwa mkoa ni vita ya kila kona ya nchi

6. Akasema, walioathirika watapata msaada wa matatibu.
Ni katika kuonyesha kuwa waathirika ni 'victims' na siyo criminals

Criminals ni 'supply chain' mzigo unapotoka hadi unapomfikia mtumiaji (conspiracy)

Kwa hoja hizo tunaona mkakati unavyotofautiana na harakati

Vita ya madawa ni watu wenye uwezo, hatutegemei matokeo ya haraka, lakini kuna jambo moja tukubaliane, kwamba, ni vita ya fikra na si maguvu

Vyovyote iwavyo tunarudia kusema kwa dhati, Kamishna Sianga anajua anachofanya

Changamoto inayomkabili ni kupewa ushirikiano bila kuingiliwa kisiasa

Changamoto ya pili ni mfumo unaoweza kum 'frustrate' kutimiza majukumu

Tusemezane
Five drug kingpins nabbed in 3 weeks

New approach to war on drugs: controlling Supply

Wakati trunaliongelea suala la madawa [HASHTAG]#275[/HASHTAG] na kuendelea, tulieleza ni kwanini vita inapigwanwa bila maarifa. Tulisema hii si vita ya mkoa bali ya mataifa na kwamba lazima kuwe na ushirikishaji wa vyombo mbali mbali na si kauli za mtu mmoja au wawili

Tukasema kutaja 'mateja' hakuwezi kutoa suluhu kama supply chain haitaangaliwa

Ukisoma taarifa hizo, utakubaliana nasi tuliposema kamashna wa madawa ya kulevya anajua anachofanya labda tu akwaze na wananasisa

Alichoeleza kamishna ndicho tumezungumzia kila siku tukikosa nguvu za mtu au mkoa mmoja kuwa nguvu za Taifa. Vita ya madawa ni vita kubwa iunayohitaji maarifa na weledi

Tusemezane
 
Nguruvi3 habari za siku nyingi mkuu.
pole na hongera kwa kazi ya kuleta mijadala mizuri na yenye tija kwenye jukwaa hili.

mie nina mambo makubwa mawili ambayo nataka niyaomngelee

hayana uhusiano ila nayaweka pamoja lakini kwa aya ili wote waelewe.

Hoja 1: hivi kweli uhalali wa serikali kuzuia TLS kufanya uchaguzi wake kwa demokrasia ni sahihi? Mbona jamani kama demokrasia yetu inabakwa? hivi vyama vya kitaaluma vinamahusiano gani na uendeshwaji wa serikali kiasi kwamba serikali inakataza mwanasiasa kutokugombea? Nauliza hivi inamaana hata viongozi wa CWT, hawaruhusiwi kuwa wabunge wala wanasiasa? kama ndio ipi ndio sababu? nijuavyo mimi vyama hivi vya kitumish vyaweza kabisa kujianzishia chama chao cha siasa na kikaruhusiwa kusajiliwa manake kwenye katiba yetu hakuna mahali ilipo sema memba wa vyama vya kitumish asiwe mwanasiasa. Hivi mtu kama ni mwanachama wa kundi fulan la kiutumisha tena lililosajiliwa kwa katiba waliyoiandika wenyewe ambayo hukuwa nayo before leo hii unapata wapi courage ya kusema usishiriki siasa? je inamaanisha waaalimu wote wanasiasa wanakosea? ama ni kwa sababu ya mtu fulani tu ndio maana hili limekuwa hivi?

je huu sio mwendelezo wa kubaka demokrasia nchini?


Hoja 2: nimemskiliza kwa makini sana DR. Shein akisema hatishi na TANESCO kumtishia kukata umeme Zbar.
kwa mtazamo wangu sioni kama anayesemwa hapa ni Tanesco bali ni serikali iliyoko madarakani na hapa nanusa harufu mpasuko mkubwa sana.

sijawah kumsikia Shein ametamka maneno makali kama ya leo na kwa ile kauli unaona kabisa ni mtu aliyechoshwa na aina fulani ya maisha. na hapa lazima CCM iwe makini sana manake wakuu wa nchi kwenye level kubwa kama hii wakianza kutoleana maneno ya aina hii ni hatari.
mie ninachokitafakari kwa kauli "yake ya mtu asilete fyoko fyoko mkikata umeme tutatumia vibatari" nanusa hali ya sintofahamu ndani ya chama tawala na muungano kwa ujumla.
 
gfsonwin za siku njema, mkuu umetoweka kabisa.
Kulikuwa na tetesi 'u-DC' ulikuwa unasubiri uhakiki wa vyeti vyako teh teh

Anyways back to the topic

Kuhusu la vyama vya kitaaluma, hii ni aibu nyingine kwa Taifa

Vyama vipo kulinda masilahi ya taaluma. Havimlazimishi awaye kuwa mwanachama

Kanuni zinatengenezwa na wanachama katika kusimamia misingi na maadili ya taaluma

Nimepitia baadhi ya katiba za vyama, havina panapozuia wanachama kuwa wanasiasa

Jukumu la serikali ni kuhakikisha vyama vinasajiliwa kisheria na kufanya kazi kisheria

Kusajiliwa kuna lenga kutambua chama husika kama mwakilishi wa wanataluma

Kufanya kazi kisheria ni kuhakikisha hakuna matumizi mabaya ya vyama nje ya malengo

Vyama vya taaluma vina kalenda na taratibu ambazo serikali haina mkono wa aina yoyote

Waziri wa sheria ni mwanachama, hakuna kipengele kianchomzuia kuwa kiongozi

Hisia za chama kitakuwa cha siasa hazina uthibitisho wa kimazingira wala kisheria. Ni hisia tu

Hivyo kuingilia uchaguzi wa TLC si jambo la kawaida wala la kubezwa, ipo sababu kubwa
Ni 'ushahidi' wa kutaka kuminya taaluma ya sheria kutimiza majukumu ya taaluma na jamii

Kama unavyoona mihimili mingine imebaki kuwa kama ilivyo isipokuwa uliotitia chini

Katika kuhakikisha kazi ya udhibiti inakamilika, ni lazima eneo lenye ukorofi lidhibitiwe

TLS kina jukumu la kulinda masilahi yao na ya jamii kwa ujumla
Pengine ndilo linapelekea kiwewe, kwani mengi yanayofanyika yatahojiwa, kanushwa au kupingwa

Kitendo cha wanasiasa hasa wa upinzani kuingia katika kinyang'anyiro ni tishio kwao

Kinachoshangaza mbona huko nyuma hatkuona haya?
Lini Tanganyika medical society iliwahi kuamuliwa nani aongoze?

Lini Tanzania Registered Nurse iliwahi kupewa mwongozo?

Lini CWT kiliwahi kusimamiwa na serikali? Lini Eng waliahi kupewa nani aongoze nani asiongoze

Kwanini TLS?

Inakuwaje askari mstaafu chini ya mwaka anaingia katika siasa,kupewa nafasi za siasa?

Kwanini haikuhojiwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na Jaji mkuu mstaafu alipochukua fomu za Urais? Lini alijiunga na chama cha siasa ?

Mkusanyiko wa yote hayo unaweza kukueleza kwanini TLS, na lengo ni kitu gani

TLS watafanya kosa la kihistoria watakaposimama na wanasiasa na si katiba yao

Chama cha taaluma hakina mwongozo wowote mwingine isipokuwa katiba yao

Tusemezane
 
gfsonwin

Hili suala la umeme linafanywa kisiasa kama 'bargaining chip'
Ndivyo Zanzibar imekuwa inafanya kwa muda mrefu katika kukwepa wajibu

Rais Magufuli yupo sahihi kabisa katika kulizungumzia.
Tumesikia mara nyingi akiongelea kuhusu taasisi kusimama na kujiendesha.

Tanesco imekuwa ni taasisi inayotegemea ruzuku badala ya kuchangia pato la Taifa

Bandari inachangia uchumi, kwanini Tanesco iwe tegemezi wa mapato ya bandari?

Kuna mauza uza ndani ya Tanesco, ukweli wa madeni ya muda mrefu yasiyolipwa upo
Madeni si ya wananchi bali taasisi na mamlaka za serikali.

Si mara ya kwanza, Rais kukemea wizara kulipa bill zao.
Hili ni kuhakikisha mashirika kama ya maji na umeme yanajiendesha na kujipanua

Ndio kauli aliyosema kuhusu Zanzibar juzi.
Kwamba, kwa muda ZNZ imeshindwa kulipa Bilioni takribani 120 za bill za umeme.

Kiasi hicho ni kikubwa sana kwa shirika kama Tanesco katika mipango yake
Hivyo Rais haku target znz , alichosema ni watumiaji wa huduma hiyo walipe

Fikiria hivi, mkurugenzi wa Tanesco anapoomba hazina B100 wakati Bilioni 120 hajakusanya, je ina mantiki ya aina yoyote?

Hoja ya ZNZ ni kuwa wananchi wanalipa ZECO ambayo inapaswa kupewa bei ya 'jumla'

Kama ni hivyo, kwanini kwa miaka nenda rudi ZECO hawajahakikisha linafanyika?

Tofauti ya bei wanayokusanya (ZECO) na bei ya jumla ndiyo inatengeneza 120B?
Sheria inasemaje kuhusu kuuziana umeme?

ZECO walitakiwa kujadiliana na mtoa huduma ili waweze kulipa bill yao.

Kama kuna tofauti hiyo inajadiliwa na si kusubiri deni lifike Bilioni 120
Kusubiri bila kutenda ni kukataa kulipa, ni kukwep wajibu wa deni

Kama ZECO hawajalipa kwa miaka mingi, Tanesco wana haki ya kuweka interest kwa kiwango chochote watakachoafikiana.

Ukweli unabaki kuwa ZECO hawakujishughulisha kulipa deni lao

Marehemu Sitta aliwahi kusema walisamehewa deni wakati fulani katika mabilioni.

ZECO wanatumia siasa kama 'bargaining chip' kwamba suala si kulipa bali muungano

Ni jambo la kushangaza ikiwa Rais atafuatilia mita za mafuta bandarini, atafanya jitihada viwanja vya ndege, atabana matumizi yasiyo ya lazima wakati huo huo akitoa pesa kwa Tanesco iliyoshindwa kukusanya madeni yake. Deni moja ni hili la Zanzibar

Kauli zinazotolewa ni za kuondoa au kuficha ukweli kuwa ZNZ ilipaswa kujadili Bill zake kabla ya kufikia hapo. Haikufanya hivyo kwasababu haidhani ni wajibu.

Hili la umeme linaeleza 'fatique' kwa upande mwingine.

Vyovyote iwavyo Rais yupo sahihi, kila mwanachi alipe bili,taasisi ilipe bili,serikali zilipe bill

Ni ukweli mchungu lakini ni ukweli na ubaki kuwa hivyo .

Tusemezane
 
Nguruvi3 nianze na bandiko [HASHTAG]#287[/HASHTAG],
bwana wee mie nani anikumbuke hata kwa ubalozi wa nyumba kumi? achilia mbali u -DC?

mie ukweli naungana na TLS kuona kwamba wanasimamia sheria na taratibu zao kama walivyo ziweka na si kwasababu kuna influence ya serikali kwa namna yyte ile.

serikali na viongozi wake wanakosea hasa waziri wa sheria hawez kuwa na maamuzi juu ya chombo ambacho kwanza yeye sio mwanachama, na hata kama ni mwanachama hawez kulazimisha jambo kwa matakwa yake pekee.

sijui lini ukombozi utafika wa demokrasia utafika kwetu manake TLS kama chama cha kitaaluma kinachoundwa na wanaotafsiri sheria wanakuwa na hofu ya kusimamia tafsiri ya sheria na kukubali mashinikizo nini kitamkomboa mwalimu ambaye kila siku hubezwa na kukashifiwa?

mie nashauri TLS watupe matumaini kuwa watasimama imara kwa mujibu ya taratibu zao. hao wanaopandikizwa hapo sio muda wao na nia yao sio njema. mamluki hao wapo ili kuvunja mabawa ya TLS kiutendaji. wakitaka kuamini haya wajiulize lini CWT wameweza kuwa na msimamo wao? hii ni kwasababu wameruhusu siasa za chama tawala zikaingilia umoja huu.

wakiongea jambo leo wakikubaliana, wakitoka hapo taarifa zinakwenda next thing unakuta tayari vitu vimebadilika. Hata viongozi wa juu wanachaguliwa na chama tawala kwa jinsi wanavyojua wao. TLS ikiruhusu hii makucha yao yatakuwa yamefika mwisho.

karibu
 
Nguruvi3
mie ukweli naungana na TLS kuona kwamba wanasimamia sheria na taratibu zao kama walivyo ziweka na si kwasababu kuna influence ya serikali kwa namna yyte ile.

serikali na viongozi wake wanakosea hasa waziri wa sheria hawez kuwa na maamuzi juu ya chombo ambacho kwanza yeye sio mwanachama, na hata kama ni mwanachama hawez kulazimisha jambo kwa matakwa yake pekee.

sijui lini ukombozi utafika wa demokrasia utafika kwetu manake TLS kama chama cha kitaaluma kinachoundwa na wanaotafsiri sheria wanakuwa na hofu ya kusimamia tafsiri ya sheria na kukubali mashinikizo nini kitamkomboa mwalimu ambaye kila siku hubezwa na kukashifiwa?

mie nashauri TLS watupe matumaini kuwa watasimama imara kwa mujibu ya taratibu zao. hao wanaopandikizwa hapo sio muda wao na nia yao sio njema. mamluki hao wapo ili kuvunja mabawa ya TLS kiutendaji. wakitaka kuamini haya wajiulize lini CWT wameweza kuwa na msimamo wao? hii ni kwasababu wameruhusu siasa za chama tawala zikaingilia umoja huu.

wakiongea jambo leo wakikubaliana, wakitoka hapo taarifa zinakwenda next thing unakuta tayari vitu vimebadilika. Hata viongozi wa juu wanachaguliwa na chama tawala kwa jinsi wanavyojua wao. TLS ikiruhusu hii makucha yao yatakuwa yamefika mwisho
Hapa kwanza tuweke mambo mawili tofauti na kisha tuonyeshe wapi TLS walipo na wanapoelekea

1. Kuna vyama vya taaluma ambavyo uanachama wake kwa baadhi si lazima ingawa ni muhimu
Kwamba, society unayoitumikia ukiwa mwanachama integrity yako katika 'entire society' inakubalika

Jukumu la vyama vya taaluma ni kusimamia masilahi ya wanachama katika kuwatete, kuwaendeleza n.k. Lakini pia vyama hivyo vinajukumu la kulinda masilahi ya umma (public interest) kwasababu wao ndio wanaojua taaluma husika

2. Kuna 'board' zinazohusika na taaluma au kada fulani ya kitaaluma. Hizi zina kazi ya kusimamia maadili, nidhamu, sifa na kulinda utukufu wa taaluma (nobility) ya taaluma

Mfano, chama cha Madaktari (TMA) kinaweza kusimama na kukemea tabia ya wanasiasa kuwaweka mahabusu madaktari kwavile kufanya hivyo ni kuidhalilisha taaluma, kudhalilisha wanataaluma na kuondoa imani ya jamii kwa wanataaluma. Hapa wanalinda masilahi ya taaluma, mwanataaluma na umma

Bodi ya madkatari itakapisikia taarifa kwa njia yoyote, itakaa na kutathmini kama kosa la Dkatari husika ni la kitaaluma, au lilifanywa kisiasa na si kitaaluma au halikuwa kosa kwa mujibu wa taaluma
Je, Dakatari husika aliji conduct vipi kabla, wakati na baada ya tukio

Baada ya kujiridhisha Board itaamua kama ni kumuonya, kumzuia ku practice au kutokuona kosa

Tukirudi kwa TLS, kwa hii iliyopo sisi wananchi tunaona mapungufu. Kuna mambo mengi yametokea TLS ikiwa kama haipo. Mawakili kutishwa, kukosekana kwa mwongozo wa kisheria kwa masuala yenye masilahi kwa taifa na hata kushindwa kusimamia taaluma ya sheria katika mambo ya msingi kabisa

TLS haijawahi kufafanua kwa umma au kuhoji, ni sahihi mhimili wa sheria kuongozwa na 'acting' na hiyo acting ni kwa dharura gani na itakamilika lini?

Hayo hayatokei kwa bahati mbaya, ni kwasababu uongozi uliopo 'ni tiifu na una kubalika'

Kuacha TLS iongozwe nje ya watu waliozoeleka ni tishio hasa tukizingatia mwenendo uliopo

Hatuwezi kusema nani anafaa, hilo ni jukumu la TLS na wanachama wake.

Tunachoweza kusema ni kuwa kama TLS hataweza kusimama na kuongozwa na sheria inayosimamia, itapoteza jukumu lake la msingi la kulinda sheria na maslahi ya wanachama wake

Hapa ndipo tutauliza, TLS italindaje masilahi yake, wanachama na ya umma?

Kesi zilizofunguliwa zita undermine nguvu ya wanachama na chama katika kuamua mambo yao
Kama yapo matatizo, je, yalizungumzwa kwa taratibu za chama kabla ya kwenda mahakamani?

Tusemezane
 
Haya mambo Nguruvi3 yana shina lake na hilo shina linalisha mti unaotoa lishe kwa watu wengi sana na kwa bahati mbaya wakitoka hapo hawana pa kwenda na wakikosa pa kwenda pia watakosa na mlo wao wa kila siku. Huko tulikotoka tuliona kama vile tupo kwenye ardhi oevu, lakini hapa tulipo ni kama tupo chini tumenasa kwenye tope ziwani tukiwa tunanyemelewa na Mamba ama Boko.
 
SAKATA LA RC MAKONDA
Serikali yaguswa, Media zaguswa, taharuki mitandaoni

Kwa wiki kadhaa sasa RC Makonda amekuwa katika sakata linalohusisha vyeti na elimu
Sakata lilihusisha viongozi wa dini ambao sasa ni sehemu ya sakata kwa upana wake

Kwa ufupi, inatuhumiwa kuwa RC ametumia majina yasiyo yake baada ya kufeli kidato 4
Madai yaliyotolewa na askofu aliyesema majina halisi ni Daudi Albert Bashite

Kuna mijadala mitandaoni ikiwagawa wanajamii katika makundi kadhaa

1. Wapo wanaosema si kweli , ni uzushi kutokana na vita ya madawa aliyoanzisha RC
2. Wapo wanaosema ni kweli kwasababu majina halisi yametolewa na hayajakanushwa
3. Wapo wanaosema kuna uwezekano wa kubadili majina na wala halijawa tatizo

Kutokana na mkanganyiko huo kuna hoja mbili zinazojitokeza kutoka makundi hayo
1. Wapo wanaotaka RC uthibitisho wa tuhuma zinazomkabili kwa kueleza hali halisi
2. Wapo wanaosema mwenye tuhuma ana wajibu wa kuweka ushahidi na si mtuhumiwa

Hoja zote zina mantiki kwa kulingana na jinsi gani mtu anaziangali kwa macho matatu

Kwanza, wanaotaka RC aweke ushahidi ni kwa ukweli, wadhifa na dhamana kwa umma na mteuzi, hakuna sababu za kutiliwa shaka.

Wanatambua RC hawajibiki kwao, lakini akiwa kiongozi anadhamana
Tuhuma hizo zinamgusa mteule kama zitaachwa bila kupatiwa ufafanuzi

Kundi la pili hapo juu lina hoja. Kama kuna ushahidi wa madai, wanaolalamika wanawajibu wa kutoa ushahidi huo mbele ya sheria.

'Natural justice zinasema' jukumu la kuthibitisha madai lipo kwa mlalamikaji

Kwanini suala limefika hapa lililpofika! Inaendelea...
 
SAKATA (Sehemu ya II)

Kuna ukweli unaoachwa kuhusu suala zima la RC makonda kwasababu ya jazba na hisia

RC Makonda ni m/kiti wa kamati ya usalama ya mkoa,mteuliwa wa Rais na mwanasiasa

Maisha ya mwanasiasa hayana siri (privacy) ni kanuni zilizopo duniani kote

Akiwa RC na watu milioni 5, akibeba jukumu la ulinzi na usalama, na mwakilishi wa Rais , hakuna namna anaweza kuishi akitiliwa mashaka hata kidogo

Kwa mfano, itakuwa jambo la ajabu RC yoyote akituhumiwa 'kulawiti' watoto na kukaa kimya bila kueleza, kufafanua, kukanusha au kwenda mahakamani kama anasingiziwa

RC amebeba dhamana ya Mh Rais na si vema kumhusisha Rais na makosa au tuhuma za aina yoyote. Ndiyo maana kuna sheria ya maadili ya viongozi maeneo wanayoishi

Club ya leaders ilianzishwa kama eneo viongozi wanakutana katika starehe baada ya kazi kama mabwalo ya Polisi au Jeshi katika kuwalinda na kashfa zinazoweza kugusa kazi zao

RC Makonda anawajibika kutoka na kufafanua madai anyotumiwa mbele ya umma

Hilo si kwa mujibu wa sheria,ni kanuni za asili za uongozi, maadili na kiutawala zinamtaka

Laiti RC angejitokeza kueleza, kiwe kweli au si kweli, mzigo wa tuhuma ungebaki kwake

Kwa kukataa kufafanua akiendelea na kejeli, suala limeondoka kwake na kutua kwa Rais

Limemfikia Rais kama mashtaka dhidi ya tuhuma za mtu anayemwakilisha

Kwa mantiki hiyo Mh Rais angaaliwa kama mwenye kauli itakayondoa sintofahamu

Sintofahamu ipo wapi?

Na kwanini kuna upotoshaji wa suala hili?

Inaendelea
 
SAKATA LA RC MAKONDA (Sehemu ya III)

Katika kubadilisha mjadala kuna jitihada za aina mbili zinaendelea
Kwanza, kunusuru suala hili lisitolewe maamuzi na mamlaka husika, pili kupotosha ukweli

Kubadili jina ni jambo a kawaida na hufanyika hadharani kwa kutumia mhakama na kupata affidavit

Ingelikuwa jambo rahisi RC Makonda kumpa katibu muhtasi wake afikishe nyaraka kwa media
Hakuwa na sababu za kuita mkutano,simple. Kwanini hajafanya!?

Pili, kuna tuhuma alifeli na kupata division 0 ndiyo maana akabadili jina.
Ili kuzima hoja RC aweke vyeti hadharani ukweli ujulikane. Kwanini hajafanya hivyo!

Tatu, RC ana nafasi katika na access na media kuweka rekodi sawa. Kwanini hafanyi!?

Nne, mamlaka kama zenye uwezo wa kuthibitisha uhakiki wake kwanini hazielezi !

Hoja iliyopo ni kuhusu tuhuma za elimu na vyeti ambazo zipo katika tuhuma za 'udanganyifu'

Suala si u-RC wake , Rais anaweza kumchagua mtu bila kujali elimu yake.

Hilo haliondoi ukweli kuwa mwakilishi wa Rais lazima aaminike kwake na kwa wananchi.

Kwa hili la RC kuaminika ni kuondoa mashaka ya udanganyifu si u-RC au kubadili jina

Upotoshaji unaendele kuwa vita dhidi ya madawa, u-RC na wivu wa mafanikio vinasumbua umma

Hilo si kweli. Hoja Zilizopo ni hizi

1. Alipata division 0. Ithibitishwe kweli au uongo kwa ushahidi usio na shaka

2. Alibadili jina kuficha division 0 kwa jina la mtu mwingine. Ithibitishwe kwa vidhibiti au ikanushwe

3. Alisoma elimu ya juu kwa udanganyifu. Ithibitishwe kwa vielelezo au ikanushwe kwa vielelezo

Hayo ndiyo yanahitaji kufafanuliwa na si suala la kutaka suala lipite tu.

Madhara yake ni mkaubwa kwa utawala katika siku za usoni.

Tutafafanua
 
SAKATA LA RC (Sehemu ya IV)

Mh Rais amemtaka RC kuendelea 'kuchapa kazi'yeye ndiye anajua ampange nani na wapi

Ni ukweli Rais ana mamlaka ya kisheria kabisa na katika kutekeleza anahaki ya kuchagua

Hata hivyo, Rais ni kiongozi wa umma ambao RC ni sehemu ya uwakilishi wake

Ni muhimu kusikiliza na kujibu hoja za umma hata kama hazipendezi

Rais hana sababu za kumuondoa RC katika wadhifa wake.

Kwa mamlaka yake na nafasi ya RC,Rais anasababu za kuutanabahisha umma nini kinaendelea ili aweze kuungwa mkono katika agenda zake

Moja ya agenda ni kuondoa 'wadanganyifu'' ambao umma umeonyesha shaka kwa RC

Kuliacha suala hilo na kuliita udaku, mbele ya safari kutakuwa na matatizo

1. Wananchi watavunjika moyo na kutokuwa na hamasa na wito utakaotolewa

2. Wananchi wataondoa imani (trust and credibility) kwa kauli za viongozi wao

3. RC Makonda atabaki reference . Watu wasiomtakia mafanikio Rais wataifanya agenda

a) Kila hatua atakayoifanya itaangaliwana kupimwa kwa jicho la RC.

Utenguzi wa RC Kilango ungeelezwa tofauti kama ungewekwa katika mizani na RC
b) Kutakuwa na tuhuma za upendeleo zinaweza kupata mashiko

Mbele ya safari kutakuwa na kulinganishwa hatua dhidi ya x kwa mizani ya RC Makonda

Watu wajinga ambao ni sehemu ya jamii wataingiza hisia chafu za ukabila, udini n.k.

Lakini pia kutakuwa na historia. RC aliwahi kuleta vurugu kwa tume ya Warioba.
Akaagiza watu wapigwe atajibu. Akaingia katika ugomvi na viongozi wa dini, na sasa kafanya baya la kuvamia vyombo vya habari kwa kutumia mamlaka na nguvu za dola.

Swali, kuna sheria ngapi na za akina nani ktk nchi hii? Kwanini mtu mwenye historia yenye utata anaendelea bila kuhoji busara na hekima zake? Maadili yanangaliwaje?

Clouds, inafuata
 
SAKATA LA RC (Sehemu ya V)

Katika hali isiyokawaida RC Makonda aliingia kituo cha TV kwa kuambatana na askari

Hali inayoelezwa kuwa ya kutisha na kusikitisha ikilaaniwa na Waziri, wabunge na umma

Inaelezwa RC alifuata 'video' aliyotaraji ingekwenda hewani ikimhusisha Askofu Gwajima

Kuna hoja nzito hapa

1. Kwanini RC anachagiza mkanda uonyeshwe ikiwa ni mambo binafsi ?
2. Kwanini RC anachagiza mkanda badala ya kutoa ushahidi wa nyaraka zake?
3. Kwanini RC ametumia askari na mamlaka kuingia katika kituo binafsi cha habari?

Clouds ni kituo binafsi .Hakina uhusiano na serikali ingawa kipo mkoa wa Dar

Kitendo cha kuingia kwa kutumia askari na kutisha ni matumizi mabaya ya mamlaka

Ni sawa na kitendo cha kuvamia ukumbi au kibambaza cha nyumba ya mtu kwa kutumia nguvu ili kukidhi mahitaji binasfi yasiyo na uhusiano na shughuli za umma

Ni kitendo ambacho kama kitavumiliwa kitaweza kusababisha matatizo siku za baadaye.

Kwamba RC mwingine anaweza kuingia katika nyumba, kuondoka na mali au mke wa mtu kwasababu ana askari wenye silaha.

Hili ni tendo la aibu kwa kiongozi wa umma anayemwakilisha Mh Rais

Ubaya wa tendo hilo ni pamoja na kukiuka uhuru wa vyombo vya habari.

Kuingia katika media kwa kutumia askari ni jambo geni katika nchi yetu.

RC ameweza kufanya hivyo akitumia nguvu za dola
Hii maana yake media sasa zipo katika hali ngumu ya wasi wasi na isiyo na uhakika

Je, RC alifanya hivyo kumwakilisha mh Rais kama inavyotarajiwa ?

HITIMISHO
Kwa mlolongo na mantiki tuliyojadili, kuna mambo matatu yanapaswa kutokea kuokoa hali, kurudisha iman na kunusuru taifa na mizozo inayotuondoa katika agenda muhimu

1. Mh RC Makonda ajipime kama anamwakilisha Rais na si mzigo na hivyo kujiuzulu
Iwe kwa tuhuma zinazomkabili au hili la kuingia katika media kwa kutumia dola

2. Vyombo vimsaidie Mh Rais kumwepusha na kadhia kwa kumshauri akae pembeni

3. Mh Rais achukue uamuzi mgumu kama ule aliouchukuwa kwa Kitwanga
Ni ili kuendelea kujenga heshima na imani kwa umma wa mailioni unaomtegemea.

RC ni liability kubwa kwa serikali, ni wakati wa maamuzi magumu kwa faida ya umma

Tusemezane
 
Nguruvi3 hogera sana kwa mambandiko mazuri yaliyojaa hoja zenye mashiko. mimi naomba nichangie kwa haya yafuatayo.

  1. hoja ya RC Makonda iwe ametumia cheti cha mtu, ama laa, iwe alifeli ama laa hilo halituhusu manake kwenye katiba yetu haijasema ili mtu awe RC anatakiwa awe na div one ama laa. Ninachokiona kwake ni swala la udanganyifu ambalo ni kinyume kabisa na maadili ya utumish wa UMMA. na kwa hili hata kama rais halioni hili lakini tume ya maadili ya umma inapaswa iliangalie kwa mapana yake. Inakuwaje mtu adanganye kwamba anaitwa A kumbe ni mtu B? hilo ni kosa kisheria hata kwa mtu wa kawaida tu. kuna haja ya tume ya maadili ya watumish wa umma kuingilia hili.
  2. Pia muheshimiwa rais anahitaji sana sana mtu wa kumshauri kidiplomasia. sitaki kusema kwamba awe soft hapana ila nataka ajue kwamba watanzania wanaona kila kinachoendelea na ukweli sio wote wana empty out what ever goes into their brains. some people stores up stuffs. na hawa ndio wabaya zaid as ipo siku wataakuja kuyatapika mahali ambapo hataweza kuwazuia. swala la kutumia mabavu ni lina tafsiri mbaya sana kwa watu wengine.
  3. Kuna baadhi wana litafsiri kama ni "power insecurity" na kwamba yeye anataka kuonyesha kwamba he is the ruler. but he should remember this" giraffe is the tallest animal in the wild despite the fact that giraffe has never declared it anywhere" Haitaji kupiga kelele ili tujue kwamba ni kiranja mkuu kasema. na kwani Kitwanga aliyelewa na huyu anayeongopa majina nani mwenye kosa kubwa zaidi?
 
Mkuu Nguruvi3 na wengineo

Tatizo kubwa linalotukabili Tanzania sasa hivi ni kuangalia kila jambo kwa mizani ya kisiasa ya SISI vs WAO, CCM vs UKAWA n.k.

Inawezekana kabisa Mheshimiwa Rais anaona kwamba Makonda amevurunda lakini akiangalia wapiga filimbi wakubwa ni kina Gwajima, Tundu Lissu na Mange Kimambi! Hapo ndipo kigugumizi kinapoanza kwamba akimtumbua Makonda itaonekana amefanya kwa shinikizo la wapinzani wake... kitu ambacho hayuko tayari kukubali! Shida kubwa iko hapo... EGO!

Moja ya madhaifu makubwa ya mheshimiwa ni kujawa na roho ya kiburi, pride, ego na kumchukulia kila anayempinga ama kumkosoa kuwa ni adui na anamkwamisha kutekeleza kazi yake. Kila mwenye mawazo tofauti na yeye moja kwa moja anachukuliwa kwamba ni adui. Ndio maana kwa mfano aliwatamkia wanasheria wanaotetea watuhumiwa kuwa nao watashughulikiwa!

Ndio maana jana amesema kwamba hafanyi kazi kwa kushinikizwa na "mitandao"... sio kwamba hajui kwamba kuna tatizo la hasha! Bali ni "pride" na "ego" iliyopo kuona kwamba atakuwa anajishusha kwa kusikiza ushauri kutoka kwa malofa wa mitandaoni. Ingawa kwa upande mwingine yeye mwenyewe ameonesha kuwa ni mshabiki wa mambo hayo hayo ya udaku (shilawadu)!
 
Mkuu Nguruvi3 na wengineo

Tatizo kubwa linalotukabili Tanzania sasa hivi ni kuangalia kila jambo kwa mizani ya kisiasa ya SISI vs WAO, CCM vs UKAWA n.k.

Inawezekana kabisa Mheshimiwa Rais anaona kwamba Makonda amevurunda lakini akiangalia wapiga filimbi wakubwa ni kina Gwajima, Tundu Lissu na Mange Kimambi! Hapo ndipo kigugumizi kinapoanza kwamba akimtumbua Makonda itaonekana amefanya kwa shinikizo la wapinzani wake... kitu ambacho hayuko tayari kukubali! Shida kubwa iko hapo... EGO!

Moja ya madhaifu makubwa ya mheshimiwa ni kujawa na roho ya kiburi, pride, ego na kumchukulia kila anayempinga ama kumkosoa kuwa ni adui na anamkwamisha kutekeleza kazi yake. Kila mwenye mawazo tofauti na yeye moja kwa moja anachukuliwa kwamba ni adui. Ndio maana kwa mfano aliwatamkia wanasheria wanaotetea watuhumiwa kuwa nao watashughulikiwa!

Ndio maana jana amesema kwamba hafanyi kazi kwa kushinikizwa na "mitandao"... sio kwamba hajui kwamba kuna tatizo la hasha! Bali ni "pride" na "ego" iliyopo kuona kwamba atakuwa anajishusha kwa kusikiza ushauri kutoka kwa malofa wa mitandaoni. Ingawa kwa upande mwingine yeye mwenyewe ameonesha kuwa ni mshabiki wa mambo hayo hayo ya udaku (shilawadu)!
sasa mimi iyo siiti ego tuuuu
naiita hii kama "power" ama sijui niseme "authority insecurity"

halafu sasa pia na sisi wa tanzania tujitazame wakati wa kampeni tulisema tunataka mtu mwenye maamuzi magumu. hivi tuliweka mipaka ya hayo maamuzi?? sasa haya ndio tuyapokee.
 
gfsonwin ahsante

Kuanzia awali tumesema wazi, hoja si u-RC kwasababu Rais anaweza kumchagua amtakaye, hakuna vigezo.

Wabunge wa kuteuliwa,anaweza teua wajomba, shangazi, shemeji, bila kuvunja sheria

Kama kuna watu wanaona si sahihi, wakulaumiwa si Rais ni Katiba

Hili la Makonda Div 0 si hoja hata kidogo kwani si kigezo cha kuteuliwa

Lakini kuna uhusiano wa Div 0 na kubadili majina/kutumia majina kama inavyodaiwa.
Inatakiwa uhakiki wa vyeti ili kujenga uhalali wa kubadili jina na vielelezo kama affidavit

Mwalimu ulichosema ni sahihi kabisa kuhusu uchama.
Ni bahati mbaya anayepaswa kuua mbegu ndiye anasimama kuimwagilia istawi.

Umetumia neno ego, gfsonwin akasema 'power insecurity
Nyote mumeonyesha kauli moja aliyosema gfsonwin kuhusu Twiga. Nimeipenda sana

Ukimsikiliza Rais huu ni mwaka wa pili anashukuru wapiga kura,ni dalili kutojiamini.
Lakini pia mara nyingi anasema 'Mimi JPM ndiye Rais'

Kauli hii ameirudia bila kujali athari na inavyosikika katika jamii ya watu wapole Tz
Kwamba, inaonyesha ubabe, pride,power insecurity, lack of confidence n.k.

Nimebahati kuishi nyakati za tawala zote, Nyerere alikuwa humble sana.

Sikumbuki siku aliyosema 'mimi ndiye Rais' au Nimesema , nimeamamua n.k.
Siku zote alisema 'tunasema,. tumeamua, tuliona n.k.' akimaanisha taasisi ya Urais

Sikumbuki siku Mwinyi au Mkapa waliposimama na kurudia rudia 'Mimi ndiye Rais'

Mwalimu kila mtu anajua tatizo kwa RC. Kwa mfano, RC kuvamia nyumba ya watu kwa dola kwa ugomvi wake na Gwajima ni dhalili kubwa sana

Tatizo ni kudhani kuwa kukubali maoni ya watu ni kushindwa au kushinikizwa

Rais alimwajibisha Kitwanga, alipata sifa kutoka pande zote kama Rais
Hakuna mpinzani au CCM aliyechukua credit bali Rais kwa uthubutu

Hili la RC mwenye rekodi mbovu na aliyethibitisha juzi kwa kutumia dola kuingia nyumba ya mtu (Clouds) haihitaji certificate kuchukua hatua.

Lakini, kufanya hivyo si atakuwa amekubali pressure?
Si suala la pressure ni suala la umma, mantiki, busara na hekima

Kwa bahati mbaya anavyozidi kulipa muda linazidi kuingia ofisini kwake na kuleta uchafuzi
 
Back
Top Bottom