Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

TUNARUDI KULE KULE, AJIRA ZA MUUNGANO!
AJIRA NI GHARAMA, MCHANGO WA ZNZ UPO WAPI?

Habari hii ni kwa hisani ya gazeti la Mwananchi katika makala hii

Mwandishi anajitambulisha kama Salim Said Salim.
Bw Salim ''amekusanya' maoni ya Wazanzibar kuhusu ajira za muungano

Ni vigumu kutofautisha kama ni maoni yake kwa kutumia neno wznz au ni maoni ya kutoka katika vyanzo alivyosema. Jambo moja linaloonekana wazi ni weledi na upotoshaji

Kwanza, mwandishi ameeleza Wazanzibar kunyimwa ajira katika serikali ya muungano
Hakueleza ni eneo au taasisi gani wala kufafanua ajira za muungano ni zipi anazoongelea

Inaeleweka, asilimia '21' ya ajira za muungano kwa Zanzibar katika taasisi za muungano
Kwa makusudi na nia ya kupotosha umma wa wznz, Bw Salim hakueleza ukweli huo

Mwandishi aelewe ajira za taasisi nje ya zile za muungano si haki ni fadhila na hisani

Kuna idadi ya Wazanzibar wameajiriwa halmashauri za miji za Bara na taasisi zisizo za muungano. Ndiyo maana soko kubwa la ajira kwa Wazanzibar ni Tanzania bara,ni ukweli

Katika kuchanganya umma au weledi hafifu ameongelea ajira za muungano kwa ujumla
Ameongelea taasisi bila kutofautisha akidhani kila taasisi zote za bara ni ya muungano

Pili, Salim anasema kuna taasisi za muungano ambazo hazijaongozwa na Mzanzibar tangu muungano uasisiwe. Bw Said atambue ajira haziangalii eneo au sura bali uwezo na weledi

Tatu, anasema tume ya kuangalia ajira inapaswa kuwa na uwiano sawa wa wajumbe
Salim anapaswa kutambua usawa anaousema hauji tu kama mvua bali kuna wajibu

Kwamba, gharama za muungano ni za Tanganyika na hilo halijawahi kupingwa.
Hakuna mzanzibar anayeeleza kwa miaka 10 au 20 Zanzibar imechangia nini katika muungano unaotoa ajira wanazodai

Mawazo ya Salim ndiyo waliyo nayo viongozi wengi kutoka Zanzibar
Ajira ni gharama ni wajibu kueleza mchango wa Zanzibar kabla ya kudai 'haki'

Salim anapotosha kwa kusema uwepo wa serikali 3 utasaidia ZNZ katika ajira
Ni muhimu atambue ajira za taasisi za muungano na zile zisizo za muungano zinazotoka Tanganyika au Tanzania bara zinatoa ni nyingi kuliko ajira za SMZ kwa ujumla wake

Lakini pia Salim atambue ''taasisi muungano'' kama tulivyoeleza nyuma zina mbadala znz

Hakuna sababu ya Mzanzibar kuajiriwa TFDA , HESLB, TBS, SUMATRA, MARITIME, TANESCO n.k. akidhani ni taasisi za muungano.Ikitokea ni hisani na fadhila si haki

Kwa taasisi ambazo Zanzibar imeanzisha mbadala, zile za Bara ni za watu wa bara tu
Ikitokea Mzanzibar kuajiriwa ni fadhila si haki kama Bwana Said pengine asivyoelewa

Ni wakati Wazanzibar waeleze mchango katika kuendesha muungano kabla ya madai. Tunasema hivi kwasababu 'ukiona vyaelea ujue vimeundwa'

Viongozi na waandishi kama Salim waeleze ukweli wa gharama za muungano na si kuorodhesha madai na waweze kutofautisha kati ya hisani na haki, wajibu na madai

Hakuna madai ya ZNZ yatakayobeba uzito ikiwa hayatasimama katika kuonyesha mchango wa Zanzibar katika kuendesha muungano ni upi au kiasi gani

Hiki ni chombo chenye gharama kubwa na madai yao yajengwe katika mchango



Tusemezane
 
UDHAIFU WA HOJA ZA MWANDISHI KUHUSU AJIRA ZA MUUNGANO

Hoja zipo hapa

Mwandishi anasema kuna Wazanzibar wanaokerwa na tatizo la ajira za muungano na kushauri uwepo wa serikali tatu, ya Bara, SMZ na Muungano

Hoja ya mwandishi Salim au uchukuzi wa maoni haukuzingatia hali halisi na ukweli

Kwa kigezo cha asilimia 21 za ajira za muungano, muungano unajiri Waznz wengi kuliko SMZ.

Zaidi ya hapo ni kupitia muungano Wazanzibar wengi wanajiriwa maeneo nje ya muungano katika sekta binafsi, za umma na hata ajira na ujasiriamali

Kwamba, serikali 3 zitasaidia ajira Zanzibar ni ukosefu wa waledi.

Rasimu ya Warioba iliyopendekeza serikali ilionyesha mambo 7 tu mengine kila mshirika atashughulika. Serikali ya muungano itakuwa ndogo na 'kivuli cha ajira asilimia 21' hakitakuwepo

Tanganyika ni soko la ajira kwa Zanzibar, kupunguza ajira za muungano hakuna athari zozote

Pili, mwandishi Salim anasema kuna taasisi hazijawahi kuongozwa na Mzanzibar kwa miaka 50

Haieleweki anamaanisha nini, kwamba mtu mmoja kuongoza taasisi ni ukombozi wa Zanzibar!

Hoja hii ni butu kwa kuzingatia ukweli kuwa wapo Wazanzibar walioajiriwa na kuongoza taasisi nyingi ndani na nje ya muungano

Taasisi kubwa kama ya Urais imengozwa na Mzanzibar kwa miaka 10 (Mwinyi)
Ndani ya taasisi hizo kuna matawi kama vice president kwa takribani miaka 30+
Wizara kama ya mambo ya nje imeongozwa na Wazanzibar
Waziri mkuu wa Tanzania ambaye ni wa ''Bara'' amewahi kuwa Mzanzibar
Wizara kama ya fedha imeongozwa na Mzanzibar
Wizara ya mambo ya ndani imeongozwa na Mzanzibar
Wizara ya mawasiliano imeongozwa na Mzanzibar
Wizara ya mambo ya nje imeongozwa na Wazanzibar
Wizara ya mifugo na maji ambayo ni ya bara imeongozwa na Mzanzibar

Orodha ni ndefu kuanzia taasisi ndogo hadi kubwa.

Hatuna uhakika ni taasisi gani anayoongelea kwasababu ya kukosa ithbati ya kile alichokiandika na kukiamini bila kuwa na facts bali hisia zilizomjia

Mwandishi asidhani taasisi ambazo Znz imejitenga na kuanzisha zao zitabaki za muungano.

Kinyume chake hata ajira za kawaida zinapaswa kuwa za Watangayika kwanza.
Mfano, TBS ni ya Tanganyika na ZBS ni ya Znz n.k. Kwanini mznz aongoze au ajiriwe TBS?

Taasisi ya Bunge inashughulikia mambo ya Tanganyika kwa asilimia zaidi ya 80
Vipi leo mwandishi adhani ni busara kuwa na kiongozi kutoka Zanzibar?

Upotofu wa hoja unajengwa kwa hisia na si uhalisia. Wajenzi wa hoja potofu hatuwasikii wakizungumzia namna taasisi hizo za muungano zinavyoendeshwa

Ni muhimu kwa Viongozi na wajenga hoja za kero za muungano au uonevu wa muungano wasiishie hapo. Kabla ya ujenzi wa hoja zao tungependa wajenge hoja ya mchango wa Zanzibar katika muungano ili hoja zao zisimame kwa miguu na si kuelea hewani

Wakati umefika wa Wznz kujenga hoja za mchango katika muungano kwanza.

Tungependa kusikia Zanzibar inachukua dhamana ipi katika gharama za muungano.
Pengine wangeomba kuendesha wizara ya mambo ya ndani tu ingeeleweka

Bila kueleza mchango za Zanzibar katika muungano, ipo siku Watanganyika wataiorodhesha kama kero ya muungano!

Kabla ya kufika huko, Wazanzibar kama walivyo wepesi wa kuorodhesha kero, watumie wepesi huo kuuleza umma nini mchango wa Zanzibar katika kuendesha taasisi na mashirika ya muungano kwanza

Tusemezane
 
MAKALA HII INAELEZA KITU ZAIDI
JE, UJAMBAZI UNA UHUSIANO 'NA MUUNGANO'

Kuna makala hii hapa inazunguka katika mitandao. Kwa namna inavyosambaa kuna kitu kinaelezwa kwa njia isiyo rasmi. Kusambaa kwake nako pia kuna maana iliyokusudiwa

Ni makala ya kawaida ambayo kimtazamo inaweza kuonekana haina lolote bali taarifa tu. Kiuandishi na kusambazwa kwake kumebeba ujumbe.Tuangalie aya moja hadi nyingine

Aya ya kwanza ya makala mwandishi ameitaka SMZ na ya muungano kufanya jitihada za kukabliana na majambazi waliofanya 'hujuma' Tanzania bara na kukimbilia Zanzibar-Tunguu a

Hoja yetu:
Mwandishi ameshafanya 'utafiti' na hitimisho kwamba majambazi wametoka bara kwavile Zanzibar haina majambazi hadi watoke bara, anaminisha magereza ya znz si kwa ujambazi

Kuitaka SMZ na Muungano kuingilia kati suala linalohusu wizara ya mambo ya ndani kuna ujumbe muhimu, tatizo linaanza na Muungano

Aya ya tatu, anasema eneo limekuwa salama kwa majambazi kufikiwa na vyombo vya dola

Hoja yetu:
Mwanzo amesema majambazi yanatoka Tanzania bara.
Ikiwa anajua hilo nini kinazuia raia na yeye kutoa taarifa katika vyombo vya usalama?

Aya ya nne,anasema kuna kesi zilizoripotiwa zikihusisha uuzaji wa madawa ya kulevya, ujambazi na uporaji wakati wa usiku

Hoja:
Anachozungumzia mwandishi ni ujambazi. Katika kushadidia hoja, ametumbukiza madawa ya kulevya kuaminisha Watu kutoka bara' wanasambaza madawa hayo.
Mwandishi angeangalia tatizo la madawa kwa upana wake angeona haya hata kuandika

Aya ya Tano, mwandishi anasema kuna tatizo la wanawake kujiuza nyakati za usiku pia

Hoja:
Kama ilivyo kwa madawa, hili la wanawake kuaminisha Wanatoka Tanzania bara.
Mwandishi aelewe katika taasisi kongwe na za zamani dunia ndoa ni ya kwanza

Lakini pia ajishughulishe kutafuta maana ya umalaya, ulianza lini na unazungumzwaje katika maandiko matakatifu yenye karne dahari.

Kuna uwezekano malaya wakatoka bara, lakini je Zanzibar haina malaya?
Hao malaya wanapata wapi wateja huko visiwani?
Nani ni malaya, yule anayejiuza au yule anayenunua pengine akiwa ndani ya ndoa?

Katika nchi zenye adhabu kali kama Saudia Arabia zipo sheria zinazotawala suala la umalaya. Adhabu zipo na zinatekelezwa kila siku. Hakuna Taifa au mkusanyiko wa watu uliokosa watu wenye tabia tofauti wakiwemo wezi, majambazi, malaya , wabakaji n.k.

Aya ya sita, mwandishi anasema vitendo hivyo vimelazimishi wakazi kuhama maeneo yao jambo ambalo si utamaduni wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla

Hoja:
Hakuna nchi yenye utamaduni wa uhalifu. Kuna tofauti ya sheria na aina ya uhalifu
Ujambazi na madawa ya kulevya si tamaduni za taifa lolote.

Kusema si utamaduni wa Zanzibar ni kutaka kuaminisha mambo hayo hayapo katika jamii ya Zanzibar bali yanaletwa pengine na hao majambazi kutoka Tanzania bara

Aya ya mwisho anasema, kwa wenye kuwapa maeneo au kuruhusu kuhamia watu wasiowajua ni vema wakafanya uhakiki na kuripoti katika vyombo husika

Hoja:
Tayari katika aya ya kwanza mwandishi amehitimisha ni majambazi kutoka Tanzania bara, hivyo hakuna haja ya kufanya uhakiki.

Anachoeleza ni Wabara wasipewe maeneo au kupangishwa, na kwa vile 'hawawajui' wasiwapangishe

Tuangalie majumuisho ya hoja hizo bandiko linalofuata

Inaendelea....
 
(UJAMBAZI NA MUUNGANO)

Sehemu ya II

Kuna wimbi la makala zikilenga kuonyesha ubaya na si matatizo ya muungano

Kama tulivyojadili mara zote hakuna muungano uliokamilika kwa asilimia 100
Matatizo ya muungano yapo kila upande,muhimu ni kujadili katika ukweli na uwazi

Ukweli na uwazi si kutaka muungano au kuukataa.Ni kueleza na mtazamo mpana
Ni Bahati mbaya kuna upotoshaji ukijengwa na hoja hisia badala ya kujenga fikra.
Ikiwa kuna kero , je tunaziangalia kwa pande zote na upana wake?

Mfano, kueleza Zanzibar inanyimwa ajira bila kuangalia namba halisi ni upotoshaji.
Kuongelea ajira bila kueleza mchango wa Zanzibar katika kuhudumia ajira ni upotoshaji.

Kulalamika bunge kukandimiza Znz ili hali kuna wabunge wa Znz ni upotoshaji.
Kuongelea teuzi za balozi bila kusema zinahudumiwaje ni upotoshaji

Kuondoa mafuta/gesi na kutaka mapato ya gesi ya upande wa pili ni upotoshaji. Kuzungumzia haki ya umiliki wa ardhi upande mmoja na si pande mbili, ni upotoshaji

Na orodha inaendelea

Hili la majambazi, malaya na wauza madawa wa bara ni kuwashawishi Wazanzibar waamini tatizo ni muungano. Kwamba, Zanzibar ni eneo salama bila muungano

Katika mambo hayo matatu, si Zanzibar tu bali katika dunia nzima hakuna nchi iliyokwepa

Kama tutachukulia matatizo ya wanajamii kama matatizo ya nchi, leo Wazanzibar wangeangaliwa kwa jicho tofauti.

Gaidi wa ulipuaji wa balozi za US Tanzania na Kenya ulifanywa na Mzanzibar.
Je, ni haki kusema Zanzibar inatoa magaidi kwa ujumla na kwamba ni utamaduni?

Majambazi na waporaji wamejaa magereza ya Zanzibar.
Kuaminisha umma yanatoka bara ni umma uelewe majambazi ya chuo cha mafunzo znz ni bora kuliko yanayotoka Bara.Ni upotoshaji wa kujenga hisia dhidi ya muungano

Malaya wapo duniani tangu dunia iumbwe.
Kusema wanatoka bara ni kuumanisha umma wateja wao wanapatikana Zanzibar!
Kwamba kuuza mwili ni haramu, kununua mwili ni halali na ni dhambi ya muungano!!!

Hivi bila wateja, malaya na wauza madawa wangefanya nini huko uadilifuni Zanzibar?
Kwanini malaya wa' kike kutoka Bara' bila kuangalia kushamiri kwa matendo ya ushoga?

Madawa ya kulevya ni tatizo la Dunia si bara au Zanzibar.
Mitandao ya wauzaji imezagaa duniani, hakuna anayeweza kusema chanzo ni Tanz bara

Makala iliyotumwa ina lengo moja, kuonyesha muungano umekuwa tatizo kwa Zanzibar na unapeleka uwepo wa majambazi, waporaji, malaya na wauza madawa

Kwamba Wazanzibar wajitihada kuzuia Wabara kama inavyosomeka aya ya mwisho

Katika mazingira ya kuonana hawa na wale, hatudhani Wazanzibar wanajitendea haki.

Katika miaka ya 70 kulikuwa na sheria ya Wabara kuingia ZNZ kwa Passport
Wabara walipotaka ZNZ waje na passport, Zanzibar waliondoa sharti hilo kwa hiari yao

Wazanzibar wakitaka Wabara wasipewe maeneo au wasipangishwe,ni kwa gharama zao.
Nchi iliyobeba Wazanzibar wengi duniani ni Tanzania bara.

Huko wanapata huduma za ardhi bila masharti, elimu na afya bila masharti, ajira za umma na sekta binafsi bila masharti na kila aina ya faida ambayo muungano unaleta

Jitihada za makala za chuki na hisia zinasomwa si na Wazanzibar tu bali Tanzania bara.
Wanadamu wote walioumbwa wana viwango na kiwango kinapopita kadri, tatizo hutokea.

Ndani au nje ya muungano jamii zetu zitaishi pamoja. Ni asili kwamba Tanganyika na Zanzibar ni maeneo jirani ya kudumu. Jamii itaendelea kuishi kwa utangamano

Tukianza kuangaliana kwa jicho la Bara na utamaduni wa umalaya, ujambazi na madawa, na sisi Zanzibar ni wema na waadilifu, jicho hilo hilo litaona kinyume chake

Muungano na kero au matatizo yake yazungumzwe kwa muktadha huo.
Muungano usitumike kutoa hisia au kupanda mbegu za chuki ktk jamii

Kama muungano ni tatizo, Wazanzibar wanavyombo kama BLW,Wabunge na SMZ
Kwanini wasivitumie badala yake wanatumia njia zinazojenga chuki katika jamii?

Kwa upande mwingine, malalamiko tuhuma au chuki zinazopandwa zinabaraka ?
Kama sivyo kwanini hatusikii kauli ima za kufafanua, kukanusha au kukemea upotoshaji?

Tusemezane
 
Back
Top Bottom