Chatanda awataka Wanawake kujitokeza kugombea nafasi za uongozi katika maeneo yao

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda amewataka Wanawake nchini kuendelea kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi katika Maeneo yao kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu mwakani 2025.

Akizungumza katika Semina ya mafunzo kwa viongozi wanawake wa mikoa ya Kanda ya Ziwa iliyofanyika jana Machi 27, 2024 katika ukumbi wa Winterfell jijini Mwanza Mwenyekiti Chatanda ametoa hamasa kwa wanawake hao kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi.

"Niwaombe wanawake wote Nchini tunaimani kubwa na nyie wanawake kwa kuwa ndio waaminifu ,waadilifu na wenye uwezo mkubwa wa kuwatumikia wananchi katika maeneo mengi ya Nchi yetu"

🗓️ 27/3/2024


#UWTImara
#JeshiLaMamaSamia
#KaziIendelee

IMG-20240328-WA0011.jpg
IMG-20240328-WA0012.jpg
IMG-20240328-WA0010.jpg
 
kwenye mikono ya Mama madhubuti na shupavu Dr. Samia Suluhu Hassan, Tanzania ni Imara na, iko Salama.

viva Marry Chatanda na UWT viva....

Kidumu Chama Cha Mapinduzi 🐒
 
Back
Top Bottom