Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri...

Discussion in 'Great Thinkers' started by Nguruvi3, Dec 30, 2015.

 1. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #1
  Dec 30, 2015
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  MWANZO

  HAPA KAZI, MATARAJIO NA MATUMAINI YA WANANCHI

  DHANA YA 'MABADILIKO' DHIDI YA KIU YA WANANCHI

  Awamu ya 5 na miezi 2. Ni muda mfupi kutathmini utendaji/ufanisi ikizingatiwa changamoto nyingi za Taifa. Pamoja na ukweli huo, tunaweza kuipima serikali kwa uundwaji, uelekeo na vipaumbele vyake

  Mengi yamejitokeza na kuamsha hisia tofauti miongoni mwa wananchi. Wapo wenye matumaini na wenye mshangao kuhusu mwelekeo na kiu ya mabadiliko

  Hoja ya mabadiliko ilitumiwa na wapinzani , Rais Magufuli akaunga mkono kutokana na haja ya wakati.

  Tunasema Magufuli, kwasababu hakuna rekodi za CCM kuzungumzia mabadiliko

  Hata hivyo, mabadiliko hayakuelezwa kwa undani na pande zote mbili

  Wapinzani wakisema ni namna tunavyofanya mambo, CCM wakisema ni mabadiliko ndani yake na serikali

  Mbele ya fikra za wananchi, mabadiliko ni matumaini na kukidhi haja na matarajio. Ni kubadili yanayogusa maisha yao, kujenga utamaduni mpya na kuweka misingi ya kudumu

  Dhahiri, wamechoshwa na hali ya uchumi, utendaji , uongozi na maono ya siku za baadaye. Uchovu huo hauna chama wala itikadi, kwa pamoja wanakubaliana kuhusu hilo

  ''Makubaliano'' hayo ndicho chanzo cha uchaguzi uliokaribiana sana. Pengine kungalikuwepo na taratibu nzuri za uchaguzi, huenda hali ingalikuwa tofauti

  Kukaribiana kwa uchaguzi kulizaa kampeni zisizo za kistaarabu. Wanasiasa wakaacha hoja na kuhamia katika kejeli, matusi na kashfa, ukabila, udini na kuvikipaliliwa

  Mbegu zilizopandwa zinachanua na kuweka ufa usio na ulazima katika Taifa. Wanasiasa hutanguliza masilahi yao zaidi ya umma. Kwao athari za kauli si nzito kama za kukosa uongozi.

  Tutaangalia awamu ya tano kwa muda uliopo, tukijadili mwelekeo unaonekana na nini tutarajie

  Mabandiko yatajadili nini matarajio na matumaini ya wananchi katika zama za #HapaKaziTu, na kama tupo katika mwelekeo au mwendelezo

  Inaendelea.....
   
 2. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #2
  Dec 30, 2015
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  WANANCHI WANA KIU GANI?
  Wana kiu ya kutaka kubadili mwendo katika Nyanja za siasa, uchumi na utamaduni. Miaka 50 ya kujitawala ni mingi kuweza kujitathmini

  Utaratibu tuliojiwekea miaka 50 ulikidhi haja na matakwa ya wakati huo.

  Mkoloni alipotoa uhuru miaka 50 iliyopita, tulijiandikia utaratibu wa kujitawala

  Miaka ya 1950/60 ilitawaliwa na harakati za ukombozi. Miaka ya 1970 siasa ilitawala nguvu za dunia.

  Miaka ya 80, mabadiliko yakaikumba dunia kutoka sehemu mbambali. Hilo likalazimisha jiografia na siasa za dunia kubadilika(geopolitical landscape)

  Miaka ya 1990 ikatawaliwa na mataifa kuungana ili kujenga nguvu za kiuchumi na kisiasa. Siasa za dunia zikachukua mkondo mpya kabisa

  Miaka ya 2000+, uchumi ukawa nguvu kubwa kiusalama.Katika mabadiliko hatukubaki kama kisiwa.

  Tulibadilika kuendana na wakati. Kwasababu za kisiasa,mabadiliko yetu hayakuambatana na mabadiliko ya taratibu kulingana na wakati. Tunajitawala kwa taratibu za zamani katika dunia mpya.

  Hili limepekelea kilio cha kukaa chini na kujiandikia utaratibu wetu(katiba)

  Tofauti na inavyodhaniwa, katiba ni suala linalogusa taratibuza maisha, kiuchumi, usalama, utamaduni

  Kwa kutambua utaratibu tunaoutumia ni wa zamani, uliolenga ujenzi wa umoja wa Taifa n.k. haja yake kwa wakati tulio nao haikidhi tena

  Tulikuwa na katiba yenye mrengo wa kijamaa ikitumika na chama kimoja. Kwasasa tuna mfumo wa soko huria na ubepari katika siasa za vyama vingi.

  Utendaji wa shughuli ni zama hizo, leo utaratibu ule hauna nafasi katika siasa za nchi na dunia. Hilo limesababisha kukwama kwa shughuli zetu kwasababu tuna muongozo usiolingana na wakati

  Ili kwenda sambamba na dunia ya leo na wakati, ni lazima tubadili utaratibu na mfumo mzima
  Hayo ndiyo mabadiliko wananchi wanayohitaji

  Matatizo tunayoshuhudia,chanzo chake ni mifumo isiyokidhi haja

  Hivyo, kubadili mifumo ni kipaumbele na hatuwezi kufanikiwa 'kwa kusoma vitabu vya zamani ili kutekeleza ya leo'

  Ni lazima tufumue mfumo , tukae chini na tupange. Hayo ndiyo mabadiliko wanayohitaji wananchi.

  Mabadiliko si harakati au hadith, ni jinsi ya kuendesha shughuli zetu katika mtazamo mpya

  Inaendelea...
   
  Last edited: Dec 30, 2015
 3. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #3
  Dec 30, 2015
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  MADHARA YA MFUMO MBOVU YANAONEKANA

  WAHUSIKA HAWAKUBALI MDOMONI, MIOYONI WANAKUBALI NA KUTENDA


  Mabandiko mawili juu , tumebainisha vitu viwili. Kwanza, kampeni chafu za udini na ukabila, na pili mfumo mbovu uliopo

  Yote yanajitokeza katika njia mbali mbali ingawa wahusika hawakiri. Tutayajadili kwa pamoja

  Awamu ya 4 ilianza na baraza kubwa la mawaziri. Kimtazamo, ukubwa ulilenga shukrani kwa waliofanikisha safari ya magogoni.
  Mgawanyo wa nafasi kwa kuzingatia kanda na imani ulichukua nafasi. Huu haukuwa utamaduni wa viongozi waliotangulia

  Katiba haielezi kuhusiana na mgawanyo wa madaraka kwa vigezo vya ukanda au ukabila. Ni mambo yaliyobuniwa bila msingi.

  Tulikemea hapa duru kuwa, utamaduni huo utakapozoeleka utaleta matatizo mbele ya safati

  Tulisema , mfumo wetu ulihitaji marekebisho makubwa. Kauli za wapinzani zilibezwa na CCM
  Leo tunaona yote yaliyosemwa kuanza kutekelezwa tena yakionyesha ''ufanisi''

  Kuandika katiba mpya ilikuwa mwanzo mzuri wa kufumua mfumo na kuusuka upya.

  Rasimu ya Warioba ilipigwa stop na CCM kwavile tu ilitishia masilahi yao. Katiba pendekezwa ikapingwa na wananchi, tutakwama sote

  Kinachoshangaza , yale ya Rasimu ya Warioba yanaanza kutekelezwa ingawa waliyakataa hadharani

  Awamu ya 5 ya ni mfano mzuri unaotuonyesha tunavyoweza kupanga mipango,lakini kikundi cha watu kupitia siasa kikatuvuruga
  Tulidhamiria kuandika (katiba) , kundi la wanaCCM likatuvuruga. Leo Rais anayetoka CCM anatekeleza maoni waliyokataa CCM

  AWAMU YA 5 HAPA KAZI YAINGIA

  Rais akaanza kufuatilia majukumu akiwa hana watendaji wala wasaidizi.

  Kwa lugha nyingine alikuwa ana ''set tone'' kuwaamsha usingizini waliotopea katika usingizi ''business as usual''

  Hata hivyo, yote aliyofanya au kuagiza yanaangukia katika eneo lile la mfumo mbaya. Taswira nzima inawachanganya wananchi

  AUNDA BARAZA LA MAWAZIRI

  Rasimu ya Warioba ilieleza ukubwa wa baraza la mawaziri. Wapinzani walipigia kelele jambo hilo.
  Hakuna aliyejali au kuwasikiliza. Rais ameunda baraza dogo la mawaziri. Tunajiuliza, CCM walikataa nini na nini kinafanyika sasa?

  Rasimu ya Warioba ilieleza mawaziri wasitokane na wabunge. Rais ametaua mawaziri wengi kutoka nje ya wabunge wa kuteuliwa

  Rasimu ilisema, uteuzi nje ya wabunge utampa Rais nafasi ya kutafuta wasaidizi anaowataka. Itaondoa dhana ya wawakilishi kugeuka kuwa serikali na itaongeza nguvu kwa mawaziri ambao hawategemei hisani ya majimboni au ndani ya vyama vyao vya siasa na hivyo kuwajibika

  Pengine Rais Magufuli ameuona ukweli huo na akautumia kwa mujibu wa sheria. Tunauliza, CCM walikataa nini na leo wanakubali kipi?

  Tusisitize kuwa CCM ndio waliokataa Rasimu ya Warioba, wakapitisha katiba pendekezwa yao.

  Tunaona Rais anayetokana na CCM akitekeleza kwa vitendo kile walichokataa kutoka kwa Jaji Warioba.
  Huo ndio msingi wa hoja na wala hailengi kuwasuta

  Inaendelea...
   
 4. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #4
  Dec 30, 2015
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  AUNDA BARAZA inaendelea...

  Rasimu ya Jaji Warioba ilisisitiza uwepo wa maadili ya viongozi ili kujenga jamii ya wazalendo na wawajibikaji.
  CCM 'walikataa' hilo. Katika katiba yao wakalitengeneza katika hali ya kupunguza nguvu za hoja
  Leo Rais Magufuli anaendelea na timua timua ya viongozi waliohusika na ufisadi au wizi au uzembe. CCM walichokataa ni kipi?

  Katika moja ya shughuli za mabunge, aliyekuwa Mbunge Bwana David Kafulila alieleza jinsi serikali tatu zinavyoweza kuendeshwa.
  Akasema mapato ya bandari tu yanaweza kuendesha serikali kuu ya muungano.

  Wabunge wa CCM wakamzogoa na kumzomea. Tunachokiona ni ushahidi Kafulila alikuwa Sahihi. Ya TRA na Bandari yanajieleza

  Rasimu ya Warioba ilizungumzia ukomo wa deni la Taifa. Wapinzani wakahoji kama deni hilo lilidhibitiwa au kuwa na maana kwa Taifa
  Waziri wa fedha wa serikali ya awamu ya 5 kasema, ataimarisha ukusanyaji wa mapato kuondokana na omba omba
  CCM walichokataa ni kipi na leo kinafanyika nini?

  Rasimu ya Warioba ikaeleza uwepo wa S3. CCM wakakataa wakidai hatua hiyo itaongeza mzigo na gharama kubwa kwa serikali

  Rais amepiga marufuku ziara za nje zinazokadiriwa kuligharimu Taifa zaidi ya bilioni 300 kama usafiri na posho tu
  Rais na waziri mkuu wameshuhudia ukwepaji wa kodi wa mara moja uliogharimu Taifa bilioni 80

  Kila uchao tunasikia madudu zaidi, magari na makontena yakipita bila kodi.
  CCM waliogopa ongezeko la gharama kwa serikali ya muungano

  Je hoja yao bado ina mashiko tukizingatia kuvuja na upotevu wa mapato tunao uona sasa?

  Lakini pia Rasimu ilitenga shughuli za nchi mbili. Leo ZNZ hakuna muafaka na hali ya kisiasa na kicuhumi imezorota sana.
  Kwa maneno mengine Tanganyika inachangia uendeshaji wa shughuli zilizokwama za SMZ na JMT

  Rasimu ya Warioba ilisema, uwepo wa S3 utakuwa na kifungu kinachosema 'nchi moja mshirika akikwama, mshirika anawajibika kusaidia kwanza' Ndivyo ilivyo sasa, kwamba Tanganyika inabeba mzigo wa muungano na ku compliment shughuli za SMZ.
  CCM walichokataa ni kipi hasa?

  Rasimu ya Warioba ikaeleza kuhusu utumishi wa umma, jinsi ya kupata viongozi n.k.
  Tunaona Magufuli akifukuza fukuza tena walioteuliwa na Rais aliyepita.

  Hii maana yake hakukuwa na vetting ya kutosha kuhusu uwezo, uadilifu na utendaji.

  Rasimu ya Warioba iliona hilo na kutaka kutengeneza mfumo sahihi. CCM walichokataa ni kipi na nini kinatokea sasa?

  Tuangalie baraza la mawaziri la awamu ya tano baada ya mifano hiyo michache inayoonyesha mfumo ulivyo na nini tulitaka kiwe na kukwamishwa na kikundi cha watu wachache

  Tungefanikiwa pengine leo tungaliongelea mambo makubwa zaidi ya kushangilia timu timua

  Rasimu isingekuwa kamili, lakini ndiyo mabadiliko ya mfumo wananchi waliyotaka!

  Hayo ndiyo mabadiliko, siyo harakati !

  Inaendelea....
   
  Last edited: Dec 31, 2015
 5. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #5
  Dec 31, 2015
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  BARAZA LA MAWAZIRI

  Rais alikabiliwa na changamoto kubwa katika kuunda baraza la mawaziri

  1. Kuhakikisha anaendeleza ule utamaduni mpya'ku-balance imani na ukanda, mambo yaliyoanza na awamu iliyopita
  Kampeni zilizojaa tuhuma na hisia zikiendeshwa na vyama vya siasa ziimelifanya suala kuwa sensitive kuliko ilivyokuwa

  2. Kuhakikisha hapati wasaidizi wenye makando kando ya tuhuma mbali mbali

  3. Kuhakikisha haudhi waliomsaidia katika safari yake, nao wakiwa na matumaini ya fadhila

  4.Kukwepa wale aliowaita wanafiki wakati wa kampeni ndani ya chama chake

  5. Kuhakikisha mawaziri wake hawana mwingiliano wa masilahi 'conflict of interest ' hasa ya kibunge

  6. Kulitazama suala la muungano ili kuleta sura inayokusudiwa

  Nia yake nzuri ya kupata kikosi kitakachomsaidia katika falsafa ya hapa kazi inakwaza na vigezo hivyo hapo juu.

  Katika kuhakikisha baraza lake halina mwingiliano wa masilahi ya kibunge na wanawajibika kwake bila hofu(5)
  Kukwepa wanafiki(4) na kupata wasio na tuhuma(2)
  kuepuka tuhuma za ukanda na udini(1)
  Mwisho kuteua wabunge kukidhi haja ya muungano(6)

  Ameteua wabunge na kuwapa uwaziri kuliko mazoea ya siku zilizopita

  Mambo hayo sita yamezua ''tafrani'' nyingine kinyume na matrajio.

  Kwanza, ameudhi waliomsaidia wakitegemea ulua(3).
  Pili, ameingia katiika 'ugomvi' usioa rasmi na wabunge wa CCM wanaohisi kudhalilika

  Tatu Miongoni mwa mawaziri walio wabunge wa kuchaguliwa anapata wenye 'matatizo, makando kando, au tuhuma' (1 na 2)

  Kuweka mizani sawa kwa mambo sita tuliyosema ni changamoto. Swali ni je, amefanikiwa au tunarudi kule kule?

  Itaendelea....
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #6
  Jan 1, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  WAZIRI MKUU
  Ni mwalimu kitaaluma, ameshiriki shughuli CWT--mkoa kabla ya ukuu wa Wilaya.

  Akawa Mbunge 2010 na naibu waziri ofisi ya waziri mkuu na tawala la mikoa.

  Ana elimu ya Chuo kikuu,hana historia ndani ya CCM au bungeni. Historia ni fupi kitaaluma/kisiasa

  Anatokea kusini iliyoasi CCM kwa suala la gesi lilosumbua awamu ya JK.

  Pengine uteuzi ulikuwa wa kimtazamo zaidi ya vigezo.

  Endapo vigezo vingetumika, wapo wenye sifa - CCM, Bungeni na serikalini

  Inawezana uteuzi uizingatia timu isiyo na mazoea kukidhi falsafa ya hapa kazi

  Tunaweza kuuangaliwa kwa mtizamo ufuatao

  a)Kwamba, ni damu mpya isyo na kashfa itakayosimamia shughuli

  b)Kujenga mizania (ambayo ni mbaya na mbovu) kuhusu ukanda kiuongozi

  c)Kutazama sensitivity ya imani iliyochochewa na kampeni (upuuzi mpya)

  Vigezo vya elimu, uzoefu au sifa ya utendaji havina nafasi katika fikra.

  Kigezo(b) pengine kurudisha kuimarisha CCM, hakina mashiko pia.
  'Uasi' wa kisiasa umeikumba nchi nzima na haihitaji nguvu ya ziada kuzuia

  Kigezo (a) hakina nafasi, kutokuwa na kashfa kunatokana na kutoshika nafasi kubwa za kimaamuzi

  Sifa ya kusimamia shughuli za umma/CCM na serikali alizotumikia hazipo wazi.

  Tunabaki na kigezo kimoja . Viongozi wanapotoa kauli katika kampeni kwa hoja zenye hisia, wanajenga utamaduni unaoleta ugumu wa utendaji mbele ya safari

  Kazi ya kuliunganisha Taifa inakuwa ngumu kuliko, na kuanza kuligawa taifa

  Waziri mkuu ni msaidizi mkuu wa Rais na msimamizi wa shughuli za serikali.

  Kwasababu tulizoeleza ni mapema kueleza msimamo na uwezo katika kusimamia majukumu

  Hata hivyo, tunaweza kuzungumzia machache hasa ziara yake Bandarini na Lindi

  Itaendelea..
   
  Last edited: Jan 1, 2016
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #7
  Jan 1, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  WAZIRI MKUU NA ZIARA
  Aliingia ofisini kwa ziara za kushtukiza bandari akionekana kufahamu yanayoendelea Bandari/TRA

  Ulikuwa mwanzo mzuri kwavile ilionekana anasimamia agenda za Mh Rais

  Mh akaelekea Lindi kuwashukuru wapiga kura . Ni jema tukijua wapiga kura ndio waliomfikisha alipo.

  Ni hisani kushukuru walioshiriki uchaguzo, ndiyo misingi ya demokrasia

  Tatizo ni alipoagiza walioshindwa 'kutowashukuru' wapiga kura wao.

  Waziri mkuu ni kiongozi wa umma na siyo chama.
  Siasa haikomi uchaguzi unapoishia. na kwa uhalisia ni mwanzo wa maandalizi ya chaguzi nyingine

  Ni jambo endelevu . Vipo vyombo kisheria vinavyo hakikisha ni jambo endelevu

  Kushukuru wapiga kura iwe kwa ushindi au kushindwa haijawa kosa kisheria

  Kauli ya Mh haina mizania, ana zima ya kumsaidia Rais kuliunganisha Taifa.
  Tumeshaeleza uchaguzi umeacha makovu mengi.Taifa haliwezi kusonga mbele likiwa limegawanyika

  Kauli imeleta ufa usio wa lazima,ni kama ana sababu za kisiasa zisizo na mantiki.
  Walioshindwa wameshakubali iwe goli la mkono au halali. Serikali ipo, hofu ya nini? Nini kinafichwa?

  Kauli ya PM imetia doa na shaka . Haionyeshi kuliponya Taifa na makovu ya uchaguzi

  Akiwa ziarani ,waziri mkuu alitoa maagizo daraja la Mbwemkuru limalizeki.

  Kauli ya waziri mkuu ni maagizo ya serikali. Kama mbunge, ana haki ya kusimamia maendeleo ya eneo lake akiwa mjumbe wa vikao vya jimbo/ mkoa.

  Kutoa agizo alipokwenda kuwashukuru wananchi, kunajenga hisia zisizo za lazima.

  Kwamba, anakotoka kiongozi maendeleo yatapekwa kwa amri.

  Tayari kunahisi za uongozi na upendeleo, tumezijadili katika mizani ya ukanda.
  Inapotokea hali kama hii, hisia hizo zinazidi kujengeka kwa kasi.

  Hakukuwa na uilazima wa kutoa maagizo hayo hadharani asubuhi na mapema kiasi hicho

  Waziri mkuu alikuwa na nafasi ya kuongea na viongozi wenzake wa mkoa , wilaya au jimbo.

  Haieleweki kwanini haya yametokea mapema. Ingalikuwa busara akipewa ushauri makini.

  Inawezekana ni jitihada za ku-impress Taifa/Boss au bahati mbaya au tatizo la kutomwelewa

  Kwa vyovyote iwavyo, mwanzo wake umekuwa na mashaka miongoni mwa wananchi.
  Ikizingatia hana historia ya kisiasa, macho ya wengi yatachambua kwa umakini kauli zake.

  Hapa anaweza kumsaidia Rais au anaweza kuwa kikwazo. Muda utaeleza

  Tuangalie baraza zima kwa ujumla wake baada ya kuundwa na Rais

  Itaendelea...
   
  Last edited: Jan 1, 2016
 8. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2016
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,959
  Likes Received: 1,830
  Trophy Points: 280
  Herini ya mwaka mpya wa 2016 wana duru na jf kwa ujumla.
  pia napenda kushukuru uongozi wa jf @mexence melo na wenzie kwa kuweza kuboresha jukwaa letu ngawa kwa wazee kama mie ni kama naingia tena darasan kujifunza kuitumia upya.

  nirudi kwenye mada, @nguruvi 3 tukiangalia kwa makin serikal iliyopo madarakani na diriki kusema kwamba kuna mengi sana ya kuyasemea kwan yanahitaji kufanyiwa kazi.

  kauli za baadhi ya viongozi ukianza na rais, PM hadi watendajii muda mwingine niza vitisho na ubabe kana kwamba hawa wamepokea serikal ya kuongoza wajinga, wapumbavu na wasiokuwa na utashi wa jambo lolote lile. kuna muda kabisa unaona sheria zinapindishwa na zikipindishwa hakuna pa kusema manake kila mtu ni mwoga.

  nakubali dhana kawamba tulihitaj viongozi wenye misimamo, waadilifu, wakweli na wawajibikaj na wenye uthubutu lakin sio viongozi ambao wanaamua kwa jazba, bila kufikiri kwa mapana makubwa, na wenye kutoa kauli ambazo zimejaa ubabe na umwamba.

  mie swali langu ni kwamba hivi watanzania sisi ni punda kwamba lazima twende kwa viboko? na je hii approach ya hapa kazi tu haina namna nyingine zaid ya ubabe?
   
 9. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #9
  Jan 1, 2016
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,959
  Likes Received: 1,830
  Trophy Points: 280
  @Nguruvi3 ukiwa unaendelea na mada naomba uniambie hivi kilichotookea huko Zbar ni kuficha kombe mwanaharam apite ama ni ile dhana ya kwamba katiba yetu haina kipengele linachoruhusu seriikal ya mseto hivyo ingekuwa shida sana kukubali ushindi wa Maalim. ama je ni ule mtazamo wa woga kwamba zbar lazima iwe chini ya CCM kwan kinyume chake ni muungano kuvunjika?
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #10
  Jan 2, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  gfsonwin haya ya mazingaombwe ya ZNZ tumeyadili kidogo hapa Mitazamo na tathmini ya Uchaguzi 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers
   
 11. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #11
  Jan 2, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  BARAZA LA MAWAZIRI
  Katika uundwaji wake Rais amezingatia udogo kwa kuunganisha wizara
  katika kupunguza mwingiliano wa imajukumu na gharama

  Suala la ku-balance ukanda na uwiano wa ijinsia limejitokeza k
  Tunasisitiza, tunahitaji watumishi wa umma si kwa vigezo vingine vya kisiasa

  Baraza pia limeibua hoja nyingine tuliyoijadili ya muungano.
  Halijawa na kiungo muhimu (Rais wa ZNZ) kati ya shughuli za JMT na ZNZ

  Hili kama mengine tuliyoadili yanonekana katika Rasimu ya Warioba.
  Endapo tuna serikali ya'' upande mmoja'' kimantiki, nini tatizo la S3 ili kuondoa hali inayojitokeza?

  WIZARA YA MAMBO YA NJE
  Kwasasa ni wizara ya mambo ya nje, ushirikiano wa kikanda na kimataifa.
  Imeondolewa wizara ya Afrika mashariki. Ushirikiano wa kikanda ni wa jumla ukihusisha SADCC n.k

  Tulipokuwa na tatizo la EAC, mawaziri wa nje na Afrika mashariki walikinzana .
  Hilo limesahihishwa, tunahitaji waziri mmoja wa shughuli za kimataifa.

  Waziri ni mh Mahiga(MB) wa kuteuliwa mwenye uzoefu wa shughuli za kimataifa.
  Tukizingatia uzoefu mdogo wa Rais kwa mambo ya kimataifa, Mahiga ni msaada

  WIZARA: OFISI YA RAIS, SERIKALI ZA MITAA, UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  Wizara hii ilikuwa chini ya waziri mkuu, sasa hivi ipo chini ya Rais

  Kwa lugha nyingine, serikali kuu na za mitaai/majiji zipo chini ya serikali kuu

  Ile dhana ya serikali za mitaa ipo wapi? Je,hapa si kuwa Rais amejiongezea mzigo mamlaka za wananchi?Hilo halipunguzi nguvu ya maana halisi ya 'local government'

  Serikali za mitaa/miji au majiji zinafanya kazi na serikali kuu,lakini mipango inaratibiwa na kutekelezwa kulingana na maeneo husika

  Huu ni ujenzi wa dhana ya kuanzia chini kwenda juu(bottom up).
  Mashirika , ahisani, wafadhili n.k. wanapendelea muundo huu ili kukwepa urasimu

  Kinachotokea sasa ni muundo wa juu kwenda chini(top-bottom).
  Mambo yatapangwa juu na kutekelezwa huko huko katika hali ya urasimu

  Pengine kilicholengwa ni kudhiibiti ubadhirifu wa local government kama inavyooyeshwa na CAG.

  Udhibiti ungefanywa kwa njia nyingine na si 'umiliki' .Tatizo ni la mfumo

  Mwaziri wa wizara walikuwemo katika awamu ya 4 iliyoacha serikali za mitaa kuwa mlango wa ufisadi, wizi na ubadhirifu kwa mujibu wa taarifa za CAG

  Inaendelea....
   
  Last edited: Jan 2, 2016
 12. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #12
  Jan 3, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  WIZARA MBILI ZILIZOBADILISHANA MAJUKUMU!

  WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA ,WAZEE NA WATOTO


  Wizara ya afya peke yake ina majukumu mengi sana.
  Kuongezewa mambo yasiyohusiana na wizara kuna mashaka ndani yake

  Jinsia haina uhusiano na afya moja kwa moja. Maendeleo ya jamii (community development ina uhusiano na serikali kuu na serikali za mitaa si sehemu ya afya

  Tofauti na hivyo, mambo yanayohusu wizara yamehamishiwa wizara isiyo husika.

  Ukiangalia, wizara moja ikongozwa na WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA,MAMBO YA BUNGE, KAZI NA AJIRA, VIJANA NA WALEMAVU chini ya waziri Mh J.Mhagama

  Walemavu ni sehemu ya ustawi wa jamii ambayo ni sehemu pia ya wizara ya Afya.
  Ilifaa wawe chini ya wizara ya Afya kutokana na husiano wa moja

  Mambo ya jinsia , wazee pamoja na maendeleo ya jamii, hayana uhusiano na wizara ya afya, pengine yangekuwa chini ya waziri ofisi ya Rais, sera, bunge, vijana kazi na ajira

  Mchanganyiko huo utaleta tatizo katika utendaji. Hivi walemavu wanawezaje kuwa chini ya ofisi ya waziri mkuu ikiwa taarifa, sera na mipango inayowahusu inatakiwa iwe katika utaalamu wa afya?

  Hivi jinsia inawaje suala la afya na si la kisera? afya inajukumu gani kuhusiana na jinsia kama jinsia

  Inakuwaje maendeleo ya jamii yawe sehemu ya afya na si mipango, sera, kazi na ajira?

  Pengine wizara ya afya ingebaki kama 'wizara ya afya na ustawi wa jamii' ikishughulikia afya, akina mama na watoto pamoja na walemavu. Makundi hayo yanatengeneza jamii katika eneo la afya

  Kuongeza majukumu ya wazee, maendeleo ya jamii hakusaidii kuweka mipango ya wizara hii nyeti

  Mawaziri wa wizara hizi mbii wametumikia awamu ya 4 katika nafasi kadhaa.

  Waziri Ummy alifahamika Zaidi wakati wa bunge la katiba lililoandika katiba pendekezwa iliyoonekana kupingwa na makundi ya jamii

  Waziri mhagama anajulikana sana kutokana na shughuli za bunge.

  Inaendelea...
   
  Last edited: Jan 3, 2016
 13. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #13
  Jan 3, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

  Hii ni wizara inayojieleza. Mipango na fedha ni mapachaNi wizara iliyo moyo wa serikali na cuhumi wa nchi, mpangilio wake hauna shaka kama unavyoonekana

  Inaongozwa na Mh Philip Mpango, MB wa kuteuliwa. Mh Mpango alikuwa Kaimu mkuu wa TRA , uteuezi alioupata baada ya kuondolewa kamishna wa TRA

  Chini ya miezi miwili, Mh Mpango akapewa jukumu zito la kupanga, kugawanya, kusimamia, kukusanya na kutafuta vyanzo vya mapato

  Mh Pango alitumikia awamu wa 4 kama mkuu wa tume ya mipango.
  Hivyo, mipango yote iliyopita ni sehemu ya kazi ya Mh Mpango

  Zaidi ya hapo, Mh Mpango hajawahi kushika nafasi nyingine ya kisiasa.

  Kupanda ngazi ghafla kwa muda mfupi kunaonyesha Imani aliyo nayo Mh Rais Hilo linaongeza pressure kwa Mh Mpango kuleta ufanisi unaotajiwa(deliver)

  Lakini pia linaleta pressure kwa Mh Rais kwani inaonekana ana Imani Mpango. Tatizo ni pale matarajio yatakaposhindwa kufikia.

  Itakuwa ngumu kumwajibisha kutokana na kuaminika' vote of confidence'

  Majukumu ya Mh Mpango ni kuliondoa Taifa katika utegemezi, kutengeneza bajeti isiyotegemea sigara na bia

  Pia kutafuta vyanzo vingine vya mapato, kuzuia uvujaji wa mapato na ukwepaji kodi, na kuhakikisha mafungu yanafikia walengwa katika wakati

  Inaendelea...
   
 14. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2016
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  So whats your point?
   
 15. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #15
  Jan 3, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Just dissecting ! Any concern ?
   
 16. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #16
  Jan 3, 2016
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Dissecting my ... ... ss.

  Yaani hapa unajifanya kama wewe ndio JPM wapi aliwaunga mkono wapinzani? Wacha kumsemea mtu.

  Sasa wewe ndio JPM, unawezaje kufahamu hisia za mtu? Wewe ni Yesu/Mungu?

  Utaangalia na nani wakati hakuna hata mmoja ambaye unawasiliana naye maana hii ni forum?


  Una uhakika wa haya uliyoandika?

  Una uhakika wa haya unayoyaandika au umeandikiwa? USA katiba yao ni ya miaka mingapi? UK katiba yao ni ya miaka mingapi? Je Nani aliandika hizo katiba? Je, huwa wanafanya nini kwenda na wakati? Just to prove unaandika uwongo ambao wewe unafikiri ndio ukweli wenyewe.

   
 17. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #17
  Jan 4, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Ndugu Wacha1 nadhani kuna namna maoni hayakupendezi, elewa kuwa uhuru wa mawazo na maoni ni haki ya kila mtu.

  Tulitegemea kama utachangia utajibu au kufafanua hoja kwa mtazamo wako. Matusi, kashfa na kejeli hazina nafasi hapa

  Kutokana na kupoteza uelekeo, umeshindwa kuelewa vitu basic kabisa.
  Kwa taarifa yako UK haina KATIBA. Hili hulielewi inakuwa ngumu kujadiliana

  Kilichopo mbele yetu ni kuiangalia serikali iliyoundwa.
  Tafsiri fupi ya demokrasia ni ' Of the people, by the people for the people' Abraham Lincoln anasema

  Hiyo ni haki yetu ikiwa na mipaka unayotuelekeza tuvuke. Huko hatuendi

  Wapinzania wameshindwa uchaguzi na hawana serikali.
  Kama ipo hoja juu yao, bado una nafasi ya kuijadili katika uzi unaona utafaa.

  Bandiko hili ni kuangalia serikali yetu bila kujali itikadi kwa mustakabali wa Taifa.
  Tutaipongeza inapodi na kuikosoa ikibidi pia.

  Hakuna ubaya , ndiyo demokrasia kwa maana ya of the people for the people

  Tunafahamu lengo lako ni kuharibu mtiririko ili mjadala uende unakotaka
  Huko hatuendi, na tunaendelea pale tulipoachia bandiko #13

  Tunataka radhi waliokwazika na kauli za maudhi za bwana Wacha1.

  Tunaomba kuvumiliana , tupo tofauti na mitazamo tofauti ingawa mingine si mizamo tunayotarajia

  Tunaendelea.. waziri ofisi ya nchi muungano
   
  Last edited: Jan 4, 2016
 18. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #18
  Jan 4, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA

  Ofisi ya makamu wa Rais imepewa jukumu la kawaida la muungano na mazingira. Ndivyo serikali zilizopita zilivyojihusisha na masuala hayo.

  Katika hali iliyopo ya changamoto za muungano, hii ni 'wizara' muhimu sana
  Makamu wa Rais alitumikia nafasi ya waziri wa nchi muungano awamu ya 4

  Busara zinahitajika kwani changamoto ya muungano ipo na huenda mambo ya Zanzibar yakifikia muafaka agenda itarudi ikisaidiwa na wapinzani

  Waziri wa nchi ni Mh Makamba aliyekuwa kiongozi wa timu ya kampeni .m Pia Mh aligombea Urais hatua za awali.Mh alikuwa naibu waziri awamu ya 4

  Kumbu kumbu zinaonyesha, mijadala mingi iliyohusisha mambo ya muungano, waziri alisimama na chama chake. Uzoefu wake kidogo katika mambo ya muungano uta weza kuzibwa na uzoefu wa makamu wa Rais.

  Kwa mtazamo wetu, mambo ya muungano huongozwa na ukomavu wa kisiasa na busara. Ni mambo tete yanayohitaji kuangaliwa kwa masilahi mapana ya nchi na busara zikitawala.

  Hii ni ''wizara'' moja inayohusu mambo ya muungano

  Itaendelea
   
  Last edited: Jan 4, 2016
 19. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #19
  Jan 4, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA

  Ni moja ya wizara za muungano yenye majukumu ya kipekee katika Taifa, inatosha kusema hivyo

  Wizara inaongozwa na Dr H. Mwinyi, mbunge wa Kwahani kutoka Zanzibar.

  Mh ni mtoto wa Rais Mstaafu Mwinyi na msomi katika fani ya udaktari wa binadamu.
  Aliwahi kuwa Mbunge wa Mkuranga -Pwani na kumfanya awe miongoni mwa wabunge wachache waliowahi kutumikia majimbo ya Bara na visiwani

  Ameshika nyadhifa kama naibu waziri wa Afya, ulinzi na Waziri kamili katika awamu ya 3 na 4

  Katika baraza la sasa la mawaziri ni mmoja wa watu walioingia vikao vyake kwa takribani miaka 15
  Kutumika katika awamu ya 3 na 4 na wizara tofauti kunampa uzoefu katika majukumu yake

  Mh Dr Mwinyi amekumbana na changamoto kadhaa katika nyakati tofauti.
  Akiwa wizara ya Afya, alipambana na mgomo wa Madaktari uliozotesha shughuli za huduma za afya na madhara makubwa kwa wananchi

  Akiwa wizara ya ulinzi, Dr alikumbana na milipuko ya Mabomu kule Mbagala na Gongola mboto, milipuko iliyosababisha upotevu wa maisha na mali

  Dr Mwinyi ni mtu aliyejijenga kisiasa mwenyewe akianzia ndani ya chama.

  Zipo hisia tu jina la mzazi lilikuwa na 'mchango' hata hivyo, kwa kutazama alivyoingia katika siasa jitihada zake zina mchango mkubwa kwa mafanikio yake

  Njia za kisiasa za Dr Mwinyi na Mzee wake zinafanana, wakiwa ni watulivu na kukubalika katika jamii.
  Tofauti zao zinajitokeza katika maamuzi yanayowagusa katika utendaji.

  Rais Mstaafu Mzee Mwinyi aliwahi kujiuzulu nyadhifa kama waziri wa mambo ya ndani kufuatia kashfa zilizotokea akiwa waziri wakati wa awamu ya kwanza

  Mzee Mwinyi alifanya hivyo kama ishara ya kuwajibika kwa yaliyotokea, na kuinusuru serikali na kadhia hiyo
  Hilo lilimjengea Mzee Mwinyi heshima kubwa, na wakati ulipofika alikuwa Rais wa ZNZ na Muungano

  Pamoja na changamoto kama za Mzee Mwinyi, Dr Mwinyi hakuwajibika kutokana na changamoto alizokumbana nazo kama zile za milIpuko ya Mabomu Mbagala na Gongo la Mboto

  Inaendelea.... wizara ya mambo ya ndani
   
  Last edited: Jan 4, 2016
 20. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2016
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280

  Mkuu wewe bure kabisa upo hapa kuongea pumba zaidi, hii ni Forum unajaza matapishi ya watu wezi kama kina EL na aliyewauzia Mbuzi kwenye gunia. Unasema UK hawana Constitution. Usilete elimu za shule za kata, kukariri bila kufahamu kwa tarifa yako how does the UK is governed:

  ''Unlike most modern states, Britain does not have a codified constitution but an unwritten one formed of Acts of Parliament, court judgments and conventions. Professor Robert Blackburn explains this system, including Magna Carta’s place within it, and asks whether the UK should now have a written constitution.''

  - See more at: Britain's unwritten constitution

  Sasa angalia hiyo magna-carta ni ya lini? BTW nini maana ya Katiba? You can call it whatever you want Wacha kuwa gwiji la kujaza server wakati hakuna anayesoma mambo ya udaku. Badilika na andika vitu ambavyo vitasaidia nchi hii kwenda mbele. Uchaguzi umekwisha subiri 2020 kama mtabahatika lakini kwa mwendo wa JPM hamtaambulia kitu.
   
Loading...