Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri... | Page 13 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri...

Discussion in 'Great Thinkers' started by Nguruvi3, Dec 30, 2015.

 1. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #1
  Dec 30, 2015
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  MWANZO

  HAPA KAZI, MATARAJIO NA MATUMAINI YA WANANCHI

  DHANA YA 'MABADILIKO' DHIDI YA KIU YA WANANCHI

  Awamu ya 5 na miezi 2. Ni muda mfupi kutathmini utendaji/ufanisi ikizingatiwa changamoto nyingi za Taifa. Pamoja na ukweli huo, tunaweza kuipima serikali kwa uundwaji, uelekeo na vipaumbele vyake

  Mengi yamejitokeza na kuamsha hisia tofauti miongoni mwa wananchi. Wapo wenye matumaini na wenye mshangao kuhusu mwelekeo na kiu ya mabadiliko

  Hoja ya mabadiliko ilitumiwa na wapinzani , Rais Magufuli akaunga mkono kutokana na haja ya wakati.

  Tunasema Magufuli, kwasababu hakuna rekodi za CCM kuzungumzia mabadiliko

  Hata hivyo, mabadiliko hayakuelezwa kwa undani na pande zote mbili

  Wapinzani wakisema ni namna tunavyofanya mambo, CCM wakisema ni mabadiliko ndani yake na serikali

  Mbele ya fikra za wananchi, mabadiliko ni matumaini na kukidhi haja na matarajio. Ni kubadili yanayogusa maisha yao, kujenga utamaduni mpya na kuweka misingi ya kudumu

  Dhahiri, wamechoshwa na hali ya uchumi, utendaji , uongozi na maono ya siku za baadaye. Uchovu huo hauna chama wala itikadi, kwa pamoja wanakubaliana kuhusu hilo

  ''Makubaliano'' hayo ndicho chanzo cha uchaguzi uliokaribiana sana. Pengine kungalikuwepo na taratibu nzuri za uchaguzi, huenda hali ingalikuwa tofauti

  Kukaribiana kwa uchaguzi kulizaa kampeni zisizo za kistaarabu. Wanasiasa wakaacha hoja na kuhamia katika kejeli, matusi na kashfa, ukabila, udini na kuvikipaliliwa

  Mbegu zilizopandwa zinachanua na kuweka ufa usio na ulazima katika Taifa. Wanasiasa hutanguliza masilahi yao zaidi ya umma. Kwao athari za kauli si nzito kama za kukosa uongozi.

  Tutaangalia awamu ya tano kwa muda uliopo, tukijadili mwelekeo unaonekana na nini tutarajie

  Mabandiko yatajadili nini matarajio na matumaini ya wananchi katika zama za #HapaKaziTu, na kama tupo katika mwelekeo au mwendelezo

  Inaendelea.....
   
 2. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #241
  Dec 6, 2016
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Hivi IGP anampigia salute CDF? Ninaomba jibu ili niweze kujenga hoja juu ya hotuba ya Rais alipoongea na jeshi la magereza!
   
 3. General Mangi

  General Mangi JF-Expert Member

  #242
  Dec 6, 2016
  Joined: Dec 21, 2013
  Messages: 7,074
  Likes Received: 7,089
  Trophy Points: 280
  Yes anampigiaa,
  Hujui katika masuala ya ulinzi baada ya Rais ni CDF?
   
 4. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #243
  Dec 6, 2016
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Asante sana!
   
 5. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #244
  Dec 6, 2016
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280


  Sidhani kama aliwahi kuwepo CDF aliyetoka kwenye majeshi mengine zaidi ya JWTZ. Kama ndiyo hivyo, kwa mawazo yangu, kusema mfano koplo wa JW ni sawa na wa Magereza kuna changamoto hapo. Msisitizo ulitakiwa kuwa kwenye kuheshimiana na kupendana.Halafu hii hotuba nadhani hakitakiwa kuwa public!!Raia hatukupaswa kuiona hii kitu. Hii inaathiri uaminifu wa wananchi kwa majeshi yetu. Niko tayari kukosolewa kwa maoni yangu haya.
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #245
  Dec 6, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Mkuu, CDF ni mkuu wa majeshi ya ulinzi yanayokusanya majeshi yote.

  Kwa uelewa tu ni kama ilivyo katika sekta ya afya kwamba popote, Daktari ndiye anakuwa kiongozi ingawa kuna Nurse, Pharmacist, Lab tech n.k.

  Hivyo CDF kwa mafunzo na majukumu ya JWTZ anatoka huko.

  Hapa haina maana wengine hawana mafunzo, la hasha, Magereza wana mafunzo yanayowiana na kazi yao kama ilivyo Polisi, Zimamoto n.k. yaani specialized

  JW wanaweza kufanya majukumu ya wengine, lakini si kinyume chake

  Kuhusu hoja kuwa koplo wa Magereza halingani na wa JW , kinadharia inaonekana hivyo, kikazi si hivyo wote wana hadhi sawa. Tofauti yao ni hiyo niliyokueleza katika makukumu

  Kama unadhani koplo wa Magereza hana hadhi sawa na JW, vipi wa JKT?
  Utambue kuwa wapo chini ya Amir Jeshi mkuu mmoja na CDF mmoja.
  Huiwezekani kuwa na koplo kidogo na koplo saana

  Kuhusu namna alivyoongea, nadhani tatizo ni namna anavyofikisha ujumbe na si ujumbe wenyewe
  Lugha inabeba mantiki sana katika kufikisha message across the intended audience

  Mfano, alipo ongelea matumizi ya wafungwa, ni kweli. Kuna wafungwa wataalam na vibarua.
  Magereza wanaweza kujenga nyumba zao kwa gharama ndogo sana kwasababu wana labor
  Kama wanajenga kwa maafisa nyumba binafsi, wanashindwaje kuwatumia kujenga nyumba zao?

  Lakini message ya 'wamenyeke kweli' inalenga kuwapa askari fursa ya 'abuse' na hilo si sahihi
  Kumfunga mtu ni kumchukulia uhuru katika mazingira magumu sana.

  Hiyo ni adhabu hahitaji kubebeshwa matofali 10 kichwani ili amenyeke
  Lengo la kifungo ni kumrekebisha mtu si kumuumiza.

  Hili ni pamoja na kuhakikisha wafungwa mafundi wanatumika iwakitoka kujielewa na pengine kujiajiri

  Wafungwa wapo wenye utaalam sana, hawa wangepewa incentive kwasababu ni cheap labor

  Likewise, hakupaswa kuonyesha kuna tofauti.
  Alipaswa kuonyesha usawa ili kutoleta picha tofauti kwa jamii.
  Angeongea nao kama askari tu ilitosha, lakini kuwaweka katika mizani haikuwa sawa

  Message yake ilikuwa nzuri tatizo ni lugha inayobeba ujumbe inakuwa na 'ukakasi' na mara nyingi kupoteza maana iliyokusudiwa
   
 7. General Mangi

  General Mangi JF-Expert Member

  #246
  Dec 7, 2016
  Joined: Dec 21, 2013
  Messages: 7,074
  Likes Received: 7,089
  Trophy Points: 280
  Mkuu CDF ni Mkuu wa majeshi yote ya ulinzi. Katika majeshi hayo sio polisi wala magereza bali ni majeshi yote ya JWTZ.

  Kumbuka kwamba ktk JWTZ kuna majeshi Manne ambayo ni Jeshi la Anga, jeshi la ardhi, jeshi la majini na JKT.

  Tunapozungumzia JKT sio kwamba ni jeshi jingine tofauti na JW. JKT ni kitengo cha JW ambayo inaendesha mafunzo ya kijeshi na ukakamavu kwa ajili ya vijana ambao wanaweza kutumika katika majeshi mengine kama polisi, JW, magereza, uhamiaji na hata mgambo au makampuni ya ulinzi.

  Hivyo JKT ni hawa hawa JW, na ndio maana Mkuu wa JKT anaweza teuliwa na Rais kuwa CDF. Au Mkuu wa JKT anaweza toka JW baada ya kupandishwa cheo.
  Koplo wa JKT ni sawa na JW kwani wote hupata mafunzo ya Ukoplo sehemu moja.

  Mnapo anza mafunzo ya kijeshi ya JW, wote hamjui mtakuww kitengo gani.
  Baada ya mafunzo eidha ya uafisa au askari ndipo mnaanza kugawanywa wengine wanaenda JKT, wengine Ardhi, anga na majini.
  Huko mnaenda kupata mafunzo mengine ya kijeshi kutokana na nafasi hizo.

  Hivyo JKT ni kitengo cha JW kama kitengo kingine cha JW. Na unaposema JWTZ basi jua ni muunganiko wa majeshi hayo manne.

  Tofauti ya JW na majeshi kama polisi na magereza ni kwamba JW yeye anafundishwa kuua tu. Hii ndio sababu JW hawawezi tumika kutuliza vurugu za maandamani na kama wakitumika eidha polisi wamezidiwa basi ikitokea wameua huwezi kumshitaki, lakini kwa polisi anaweza shitakiwa.
   
 8. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #247
  Dec 8, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Ahsante, mkuu naomba nichangie hoja hii kwa mara nyingine

  Kama nilivyosemaCDF ni mkuu wa majeshi yote. Hilo halina tatizo

  Majeshi tuliyo nayo ni JW, Magereza, Polisi, JKT

  JW ina matawi kama Anga(Air force), majini( Navy), na nchi kavu (infantry) at least kwa muundo wa commonwealth na nchi kama US zina utaratibu wao wa kutaja ingawa kwa maana ile ile

  Hivyo matawi si jeshi tofauti bali sehemu ya jeshi la wananchi (JW)
  Hapa ieleweke tuna JW yenye mgawanyiko wa anga, nchi kavu, majini

  Matawi hayo nayo yana matawi. Kwa mfano infantry (nchi kavu) wana tawi la mizinga( artillery), wana miundo mbinu (logistic), na mbinu (tactics) kwa uchache wa kutaja ambayo si majeshi bali matawi ya tawi la infantry linalounda JW likiwa na matawi mengine ya Navy na anga

  Pili, kwamba jeshi limefunzwa kuua, hiyo ni sehemu tu ya majukumu yao.

  Kama ulivyosema, kuna sheria za nchi zinawasamehe wanapokuwa katika majukumu kwasababu interactions yao na civilians ni limited.

  Lakini hoja ya kwamba wamefunzwa kuua ina mapungufu kwa mtazamo mpana.

  Kwa wale waliowahi kupitia majeshini mtakubaliana nami kuwa jeshini kama JW kuna nidhamu ya hali ya juu ya majukumu yao,ni kimbilio la Taifa kama ilivyo sehemu zote duniani

  Katika dharura ya nchi majeshi huwa tayari kuliko sehemu nyingine yoyote.

  Utashangaa daraja linajengwa kwa masaa kama ilivyotokea wakati wa mvua pale msoga.
  Kama ilivyokuwa Kagera wakati wa vita.

  Katika uokozi wao ni namba moja na kila jambo unalofikiri

  Idd Amin alivunja daraja lililoonekana kuwa tayari kujengwa kwa miezi kama si miaka. Guess what, akapokea kichapo huku daraja linajengwa, vifaa vinapita kazi inaendelea

  Anga wanafanya yao, navy wapo victoria , infantry wanavusha askari, architect wana design daraja, structural Eng wapo kazini, civil eng wanatenda , madaktari wanatibu majeruhi. watu wa logistic wanaendelea na kazi n.k.
  kwa muda mfupi katika mazingira magumu sana, walifanikiwa

  Kwa ufupi ikitokea janga sehemu zote duniani, kitengo cha kwanza na mwisho kutumika ni jeshi.

  Si kutokana na mafunzo ya 'kuua tu', bali nidhamu na utayari wakiwa na wataalam 'the best'

  Hivyo jeshi liangaliwe katika mambo kadhaa, kwanza, lina wataalam waliobobea, pili, lina nidhamu ya utendaji, tatu, lina utayari wa rasilimali na rasilimali watu ambao wameandaliwa vizuri
   
 9. General Mangi

  General Mangi JF-Expert Member

  #248
  Dec 8, 2016
  Joined: Dec 21, 2013
  Messages: 7,074
  Likes Received: 7,089
  Trophy Points: 280
  Mkuu Nguruvi3
  Tunapozungumzia CDF tunamaanisha Chief of defence Forces katika Tanzania People defence forces.(Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania).

  Jeshi la ulinzi la wananchi wa tanzania ndio hili tunaita kwa kifupi JW.
  Jeshi letu lina muundo kama ambao kidogo unafanana na uingereza.
  Katika jeshi la marekani wao hawana kiongozi wa kijeshi mkuu zaidi ya majeshi yote bali kila jeshi lina General wake. Hapa namaanisha kwamba Navy, air force na army wana General wao. Na katika majeshi hayo yanajitegemea kiuendeshaji na kutoa mafunzo.

  Katika jeshi letu hapa tuna General mmoja ambaye anaongoza majeshi yote manne. Hivyo tunaposema majeshi ya ulinzi hatumaanushi Polisi, magereza, uhamiaji bali ni JKT, jeshi la anga, jeshi la maji na ardhi. Na viongozi wakuu wa majeshi haya manne huwa na cheo cha kuanzia Brigedia au major jererali na huripoti kwa CDF na CDF ndie huripoti moja kwa moja kwa Rais.
  Hivyo CDF ndie mkuu wa majeshi hayo Manne na wala ahusiki polisi, magereza n.k

  Sasa tukija kuangalia Mkuu wa Majeshi yote yaani JW, polisi na magereza hapa ndipo anakuwa Rais wa nchi (Commander in chief).

  Rais ndie mkuu wa majeshi yote yaani JW, polisi, magereza, uhamiaji na zima moto.
  Hivyo CDF hausiki katika uendeshaji ktk polisi wala magereza na wala hana amri yoyote kule.

  Hivyo JKT, navy, army na airforce ni Majeshi ya ulinzi ambayo kwapamoja huunda JW. Na ndio maana viongozi wao huteuliwa na Rais na sio CDF. Hii haionekani wazi lkn nchi km marekani haya ni majeshi kamili yanaojitegemea na Mageneral wao wanavyeo sawa ila hapa kwetu huongozwa na General mmoja.
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #249
  Dec 8, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Mkuu General Mangi kuna point ndogo sana ya 'contention' baina yetu

  Kama umenisoma vema mfumo wetu ni model ya commonwealth
  Mfumo wa Marekani una utofauti katika mpangilio

  Kwa mfano, Marekani kuna joint chief of staff, huyu ni kiongozi wa chief of staff wa majeshi husika na ndiyo maana kuna neno joint. Hili sina tatizo nalo

  Kwa Tanzania kuna vitu viwili vya kutofautisha

  Kuna Amri Jeshi mkuu ambaye ni Rais wa Majeshi ya Ulinzi na usalama

  Halafu kuna CDF ambaye ni mkuu wa majeshi ya ulinzi.
  Tazama ukubwa wa maneno 'ulinzi na usalama'

  Amir Jeshi atakapohitaji majeshi yote atayaita majeshi ya ulinzi na usalama.

  Majeshi ya ulinzi na usalama yanapokuwa katika 'mission' moja, mkuu wake ni CDF. Ndivyo ilivyokuwa katika vita vya Kagera.

  Unachosema kuhusu CDF kutokuwa na kauli na majeshi ya Polisi na Magereza ni sahihi, lakini logically haipo hivyo.

  Jeshi likihitajika mtaani linawajibika kwa CDF siyo mwingine.
  Umeona kitu hapo?

  Kwanini nakuambia Navy, air force, Infantry,JKT ni sehemu ya JW?
  Hata kama zina wakuu wake, kuna Chief of staff mmoja tu! Think about that

  Kwanini wakuu wa 'matawi' wanateuliwa na Amir jeshi mkuu?

  Ni swali technical nisingependa kujadili zaidi kama utanielewa

  Nikuache na kionjo tu, Rais Moi wa Kenya alinusurika jaribio la mapinduzi kwa kurudishwa na kikosi cha anga cha Nanyuki.
   
 11. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #250
  Dec 8, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Mwezi mmoja uliopita tuliongelea kuhusu stability, integrity n.k. katika mabandiko 2 hapo chini.

  Tunayaweka tena baada ya sakata la Dangote

  Tutajadili zaidi

   
 12. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #251
  Dec 15, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Duru wiki hii

  Baada ya Dangote
  Mili mto Ruvu na kauli ya waziri
  Kauli ya Lisu na Chadema
  Na sasa kukamatwa kwa mwanzilishi JF

  Hekima, Busara. hasara na madhara ! Tumefikaje na nini taswira yetu kwa nchi na dunia?

  Tathmini na tafakuri ya kina inafuata!
   
 13. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #252
  Dec 15, 2016
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Ndugu yangu Nguruvi,

  Pamoja na mema yote kuhusu haki na fursa ya Watanzania waishio nje ya Nchi... aka Diaspora kuhusu umiliki wa Mali na hasa ardhi, bado Mtanzania wa Maneromango hana uhakika wa ardhi yake...
   
 14. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #253
  Dec 20, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapa ndipo tatizo linapoonekana zaidi. Nilitegemea waziri angeanza na hilo la Mwaneromango, badala yake kaanza na diaspora. Hatuna dira au sera za kitaifa kila mtu anakuja na lake akiondoka mwingine anakuja jingine. Ndiyo yale ya elimu kwa wote, Kilimo kwanza na sasa viwanda ndani ya miaka 10
   
 15. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #254
  Dec 20, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  WIKI NA MWEZI WENYE UTATA

  Hekima kwa tafsiri rahisi ni namna mwanadamu anavyokiri , pembua na uyakinifu
  Busara ni namna utekelezaji wa hekma utakavyofanyika, semwa au tendwa

  Mwezi huu umekuwa na mambo mengi ya utata yenye mapungufu ya hekima na busara

  1. Dangote : Baada ya kutangazwa kufungwa kiwanda, ilitokea sintofahamu

  Mawaziri wakilieza tukio kwa hoja tofauti hata kufikia mahali pa kulikoleza
  Dangote akaja kuonana na Rais na ilibainika sababu za awali hazikuwa za kweli

  Kwa muda wote habari zilinea duniani na kuathiri taswira ya nchi kwa wawekezaji

  Viongozi na mawaziri hawakuona hekma ya kulizungumzia jambo hilo kwa busara?
  Hawakuona hekma ya kukaa pamoja kama timu na kutafuta 'common ground'

  Alichokifanya Mh Rais ni kuzuia uharibifu usiendelee ingawa umeshatokea

  Haya ni kwasababu mawaziri hawakuwa na hekma ya kutazama ukubwa wa jambo

  Hawakuwa na busara wakati wanaongea tofauti na kuchanganyana mbele ya umma

  2. Miili ya watu 7: Hii imeokotwa na taarifa za awali mitandaoni

  Waziri wa Mambo ya ndani akatoa kauli, miili hiyo ni ya wahamiaji
  Waziri hakueleza ni raia wa nchi gani, waliwatambuaje , na kwanini walifariki

  Hakueleza uchunguzi wa kitaalamu ulionyesha nini na kwanini walizikwa haraka

  Waziri hakuona hekma ya alichotaka kuongea
  Alipoongea hakujibu hoja kwasababu ya mapungufu ya busara

  Hakuna sheria za nchi zinazoeleza mauaji yanafanyiwa uchunguzi kwa raia gani.
  Ni upungufu wa busara kudhani wahamiaji haramu ni wanadamu pungufu.

  Tanzania ilihifadhi wahamiaji na wakimbizi milioni 2
  watu 7 wanakufa na waziri anazungumza bila kujali utu wa mwanadamu

  Upungufu wa busara zaidi ni vyombo husika kujikokota katika suala hilo.
  Waziri mkuu akiagiza uchunguzi kwa jambo ambalo kwa uhakika ni la muhimu

  Vyombo vya dola vinaonekana kushupalia mambo madogo yanayohusu raia mmoja , wawili au watu kwa nguvu sana kuliko maisha ya watu 7

  Hekama inatueleza sisi kama taifa tumepoteza thamani yetu ya utu.
  Busara zinasema, hatujui nini kipaumbele na kwasababu gani na tufanyaje

  Sehemu ya II inaendele
   
 16. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #255
  Dec 21, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  WIKI NA MWEZI WENYE UTATA II

  Faru John: Waziri mkuu ameshupalia Faru John aliyefariki katika mazingira tata

  Upotevu wa rasilimali za taifa limekuwa tatizo na hatua hiyo ni muhimu

  Suala la Faru imekuja wakati wavifo vya watu 7 Ruvu.
  Kinachotokea ni mapungufu makubwa ya busara na utu.

  Hatuna thamani ya maisha ya mwanadamu.Tunaweza kuweka thamani ya faru

  Ni rahisi kupata ukweli wa kifo cha Faru na hatuoni ugumu na danadana unatoka wapi
  Wahusika na wenye mamlaka wapo, rasilimali za kazi zipo, nini kinaendelea?

  Hekima inasema vifo vya watu 7 na Faru ni mambo muhimu ya kufuatiliwa
  Busara inaelekeza ni kipi kianze na kwasababu gani. Je, busara na hekma zinatumika?

  Kupotea kwa Mtu
  Chadema wameeleza takribani mara mbili kuhusu kupotea kwa kijana Saaanane
  Inaoenekana familia ikiwa katika taharuki

  Madai yaliyotolewa na mwanasheria CDM yanahitaji hekma na Busara
  Huyu aliyepotea ni mwanadamu bila kujali mambo mengine yanayomhusu

  Wajibu wa kulinda mali na Raia upo kikatiba na umeanishwa vema

  Serikali imekaa kimya kwa madai yanayotolewa.

  Si dhima ya duru kueleza nani yu sahihi na nani amekosea.
  Tunachosema haya ni maisha ya mwanadamu

  Kama yupo mahali ni vema ikaelezwa yupo wapi na kwasababu gani

  Kwa hali ya matukio kadhaa yanayojitokeza jambo hili linaweza kuwa na matatizo

  Tusingependa kuzungumzia zaidi bali kusisitiza, kurudi kwa kijana huyo ni jambo linaloombewa na kila mmoja.

  Na kwamba, familia ipo katika taharuki kubwa na inahitaji msaada

  Tofauti na hivyo, hili ni tatizo kwa serikali na nchi kwa ujumla.

  Hakutakuwa na maelezo yatakayojitosheleza wakati mitandaoni kila mmoja ana lake na kulifanya fact. Habari zinazozagaa bila kuwa udhibiti ni za hatari

  Udhibiti si kuzuia wanaozungumzia bali kauli ya serikali nini kinaendelea

  Kijana huyo kapotea? Yuko wapi na kwasababu zipi? uchunguzi unafanyika?

  Tunaongelea jambo hili si kwasababu ni mtu anayefahamika katika chama au mitandao

  Ni kwasababu huyu ni mwanadamu ambaye tayari familia inataharuki

  Jambo kama hili ni dogo, lakini historia ni mwalimu mzuri

  Tutafafanua kwanini historia ni mwalim mzuri
   
 17. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #256
  Dec 23, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  HISTORIA NI 'MWALIMU MZURI'

  Historia ina tabia moja nzuri, hujirudia si kwa kuhitajika bali kwa wale wasiojifunza kutoka kwake

  Moto wa nyika hauhitaji 'tanker' la petroli kuwaka, njiti ya kibiri inatosha kuangamiza nyika yote

  Tunakumbuka tatizo la dogo la Mabucha ya nguruwe Manzese na mwembe chai yalivyosumbua

  Tunakumbuka Arab spring ilivyochochewa na mtu mmoja kujimwagia mafuta tunisia

  Tunakumbuka Mchina aliyesimama mbele ya kifaru cha jeshi kimsage akiwa hai

  Tunakumbuka vurugu za Los Angels zilivyoanza na mtu mmoja

  Orodha ni ndefu sana hatuwezi kuandika hata 0.0001% ya matukio yanayoanza na jambo dogo tu

  Baada ya mwezi wa ukimya kuhusu kijana wa Chadema kupotea, hali imebadilika.
  Wananchi wanataka kusikia nini kinaendelea kuhusu alipo kijana huyo

  Mabandiko yaliyotangulia tulieleza ni kwa vipi hili litakuwa tatizo kwa wahusika.

  Wahusika sasa wanasikika wakisema suala hilo linafanyiwa uchunguzi

  Hatua hizo zimekuja kwa kuchelewa sana. Kwanza, yapo maswali yatakayohitaji majibu

  Kijana husika aliwahi kueleza jinsi alivyotumiwa message za kutishia maisha yake
  Swali; Je alitoa taarifa katika vyombo vya ulinzi na usalama?
  Hoja: Kama wahusika walifuatilia madai yake?

  Hoja hii ni nzito,mkurugenzi wa JF alikamatwa kwa tuhuma za kutoshirikiana na vyombo vya ulinzi

  Iweje basi vyombo hivyo visiweze kuwapata wahusika waliotumia simu?

  Kwanini imechukua siku 30 na kwa kelele za mitandao kwa vyombo husika kuwasiliana na umma?
  Je uchunguzi ulikwishaanza au ndio unaanza? Kama ulianza kwanini umma haukutaarifiwa? Kama ndio unaanza kwanini imechukua muda mrefu kiasi hicho?

  Kijana huyo ni mwansiasa na matukio ya kutishiwa yanahusishwa na misimamo yake katika 'mwelekeo' huo wa siasa. Hili ni jambo zito kwasababu umma unahisia tofauti kwa mitazamo tofauti

  Kila mmoja anaomba usalama wa Raia wa nchi hii kama ndugu, na sote tunatarajia mwisho mwema

  Ikumbukwe huyu ni mwanadamu anayeweza kupata matatizo ya kibinadamu pasi mkono wowote. Ikitokea isivotarajiwa , umma utaelezwa nini uamini ni jambo la asili(nature)?

  Lakini pia tatizo linaweza kuwepo bila maelezo ya kujitosheleza, swali, umma utaelezwa nini uamini?

  Tusemezane
   
 18. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #257
  Dec 30, 2016
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kweli zipo hotuba za Amiri Jeshi Mkuu ambazo hazitakiwa kuonyeshwa public for security reasons.

  Lakini kwa hotuba hii sioni jambo lolote ambalo Rais amelizungumzia linaloweza kuathiri usalama wa nchi.

  Pia sidhani kama hii hotuba itaathiri uaminifu wa wananchi kwa jeshi.

  Infact, hotuba imenisadia kujua mambo ambayo nilikuwa siyajui.

  Mfano, eti wanajeshi walikuwa wanalipia/nunua sare zao? I never thought of this?
   
 19. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #258
  Dec 30, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii inaonyesha jinsi corruption ilivyofikia kiwango cha juu

  Kwamba, Amir jeshi mkuu aliyekuwepo hakuwa na habari za askari kununua Uniform?
  Kwamba, ndani ya security organs hakuna security ya kuangalia hali ya mambo

  Kununua uniform ilikuwa 'deal' ambayo ni conduit ya wazee kupitisha mirija yao

  Ni jambo la kushangaza sana kwasababu kuna maeneo binafsi wafanyakazi wanapewa uniform bure
  Leo askari magereza walikuwa wananunua uniform! Sijui kwanini guiness book hawakuliona hili
   
 20. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #259
  Jan 3, 2017
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Au labda walikuwa wanapewa uniform replacement allowance? Kwa mfano, nimesoma kuwa kwa Marekani, wanajeshi wanapewa free uniforms mwaka wa kwanza wanapoingia jeshini ila baada ya hapo wanapewa allowance kila mwaka ku-replace uniform.
   
 21. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #260
  Jan 3, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Ingelikuwa hivyo madai yao yangekanushwa na mkuu wao pale pale.
  Ndio maana askari hawakulalamikia 'posho' kama askari wa majeshi mengine.
  Walicholalamika ni kuhusu uniform ambazo zinaonekana ilikuwa ni aina kama 'deal'

  Hata ingekuwa kama US bado hakuna duka la kununua unifrom hizo.
  Tunajua uniform za majeshi zina upekee. Kinyume chake kulikuwa na 'watu' waliofanya kazi hiyo
   
Loading...