Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

TWAWEZA NA 'UTAFITI'

Kwa kawaida utafiti hupingwa kwa tafiti. Hivyo hatujafanya tafiti hatuwezi kupinga tafiti za Twaweza. Hii ni kanuni ya kawaida. Pamoja na ukweli huo hatuwezi kuzuia akili zkutafakari yanayotokana na tafiti kwa kiwango cha binadamu.

Tukishindwa kufanya hivyo tutakuwa robot na tafiti hazitatusaidia

Shaka za rafiti za Twaweza zinajengwa na ukweli kuwa zipo taasisi nyingine zilizowahi kutumika katika tafiti ambazo leo tunajua hazikuwa na nia njema

Kuna tafiti za taasi moja ya chuo kikuu DSM zilizoongozwa na msomi mmoja.
Imebainika msomi huyo ni kada wa kisiasa, tafiti zake zilikuwa na mikono mirefu ya chama na serikali

Tumeona wasomi wanavyosita kusimama na kusema ukweli hata kama ukweli huo upo 'uchi'. Wasomi wetu wamegundua njia rahisi ya kutoka kimaisha ni kuungana nao '...you can't beat join them'

Tumeona walivyomiminika Bungeni, wanavyozawadiwa teuzi za kisiasa n.k.

Hilo linaenda mbali na kugusa taasisi zote,kuna kila sababu za kuamini hivyo.

Hoja yetu ni kuwa taasisi zetu na wasomi wetu wamepoteza imani na hadhi ya usomi na ni haki kutilia shaka kila wanalofanya.

Kwa nchi za wenzetu kila jambo hufanywa kwa nyakati maalumu.

Ijumaa wiki hii kule Marekani idara ya twakwimu itatoa mwelekeo wa ajira.
Hili hufanyika kila ijumaa ya kwanza ya mwezi.

Kuna kalenda maalumu ya shughuli za biashara na uchumi.
Kwa mfano, leo wanajua 'Reserve bank' itakaa lini na tutegemee nini.

Makampuni yana muda wa kutoa mapato yao kwa quarter n.k.

Hii ni tofauti na haya tunayoona hapa nchini. Taarifa za benki kuu, idara ya takwimu na hizi za Twaweza hazina kalenda! Kuna kila shaka

Taarifa hizo kama ile ya BoT zina element za kisiasa.

Itaendelea
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Inaendelea..
TAARIFA ZA BOT, NBS, TWAWEZA

Tukiziangalia kwa wepesi taarifa hizo kuna mambo yanahitaji ufafanuzi

Twaweza wanasema utafiti umeonyesha hakuna Udikteta Tanzania
Kwanza, hatudhani suala la udikteta ambalo ni dhana ni muhimu.

Kuna wasi wasi kuhusu uchumi n.k kuliko dhana tu ya udikteta

Kuna hoja za umoja wa Taifa kwa wakati huu, mwelekeo wa nchi na mipango ya muda mrefu na mfupi inayogusa wananchi.

Hatudhani udikteta ilikuwa ni hoja nzito, ingawa ina uzito kwa Twaweza kiasi cha kufanyia tafiti kubwa kama hii

Twaweza wanasema 'Watanzani hawadhani kuna udikteta nchini'.
Takwimu zinaonyesha asilimia zilizohojiwa, 31% ilisema haijui

31% ni 'statistically significant'. Dhana ya 'Watanzani wanasema hakuna udikteta' haina maana. Watanzania wapi ikiwa 1/3 inasema haijui

Na hiyo asilimia 60, je,wana uelewa wa dhana ya udikteta kwa ukamilifu?

Kwa upande wa Idara ya Takwimu, nao wametoa maelezo kwa ujumla
Hakuna mchanganuo wa takwimu kuhusu mambo waliyosema

Kwa BoT, pamoja na mengine 'headline' ni serikali kulipa deni la ndani baada ya muda mrefu wa kutofanya hivyo.

Gavana hakuteueleza deni hilo ni kiasi gani, limekuwepo kwa muda gani

Bilioni 90 au 100 ni kiasi kikubwa,kwa deni la Trilioni 1 ni sehemu kidogo.

Tumeeleza mifano hiyo kirahisi tu ili kupata wazo kama haya yanafanyika kwa maana ya wajibu au yana motivation nyingine

Mpangilio wa matukio una mtiririko unaojenga shaka katika mambo ya uchumi

Uchumi ni namba, wakati ukifika hakUtakuwa na namna.

Bandari walIkana ''ukame wa mel', mwisho wa siku wakakubali tatizo

Ni wakati sasa taasisi kama BoT na NBS ziwe na kalenda za ku update umma

Hizi habari za kukutana na waandishi kama matukio, zinatia shaka

Twaweza, kuna mambo muhimu sana nchini kuliko kushughulikia dhana

Neno udikteta linaathiri gani kuliko huduma za afya, shule na hali ya uchumi?

Tusemezane
 
HILI LA UJAMBAZI NA VIBAKA LINATIA HOFU
AMANI NA UTULIVU NI KAULI PANA

Matukio ya vibaka na ujambazi kwa kutumia mapanga, visu na silaha kali yamejitokeza sana

Rais akiwa katika viwanja vya Biafra na mikutano mingine ameliongelea kwa undani

Hii maana yake ,tatizo hili si kuwa 'limeanza' bali linajulikana.

Kuna nyakati Rais alisema hata mama wana hofu ya kutembea na pochi achilia mbali maisha yao

Tunapozungumzia Amani na utulivu nchini tunazungumzia maana pana.

Kwa mtazamo wa wengi, Amani na utulivu ni kutokuwepo kwa mitafarauku ya kisiasa au uwepo tu wa ukimya

Amani na utulivu ina maana pana sana, kwa uchache tu wa hoja ya msingi, hakuna Amani katika mtaa , kata, tarafa hadi ngazi ya taifa kama hakuna Amani na utulivu kwa kuanzia nafsi ya mtu ,familia na ndugu

Na wala hakuna Amani na kwa mtu, bila kuwepo Amani ya Taifa katika ngazi zote.

Kwa mantiki hii hatuwezi na ni akosa kudhani mitafaruku ya siasa ndicho chanzo au ndilo tatizo la Amani na utulivu

Kuna taarifa za watu kuporwa na vibaka wakitumia mapanga na visu.

Wapo waliojeruhiwa na wengine kupoteza mali zao mbali na hatari dhidi ya maisha yao.

Hawa hawawezi kuwa na Amani na utulivu kwasasa, hawana Amani wakiwa katika vitanda au baada ya kunusurika. Kisaikolojia hawana Amani na wala hawana utulivu

Tunakumbuka matukio ya silaha yaliyogharimu wananchi na watumishi wa vyombo vya dola kwa nyakati mbali mbali mbali.

Hili linaonyesha ukubwa wa tatizo hata kama hatukubali uwepo au ukubwa wake

Katika mkoa ipo kamati ya ulinzi na usalama. Kitaifa tuna viongozi kuanzia Waziri, mkuu wa Polisi, wakuu wa polisi wa maeneo, maafisa usalama kabla ya kutaja viongozi wengine wa kitaifa

Huko nyuma tumeona matukio kama ya siasa yakisimamiwa kwa nguvu zote ili kulinda Amani na utulivu.

Haionekani kama zipo jitihada za dhati za kukabiliana na tatizo hili la vibaka ambalo halina uhusiano na siasa

Hoja ya upungufu wa watumishi katika vyombo vya umma haina mashiko.

Haiwezekani tuwe na watumishi na zana zote kwa baadhi ya nyakati na baadhi ya nyakati rasilimali zote ikiwemo rasilimali watu inakuwa tatizo.

Kwanini iwe hivyo sasa na si kwa baadhi ya nyakati?

Inakuwaje intelejensia inafanya kazi kwa mambo ya kisiasa lakini intelejensia isiweze kubaini wahalifu hawa wachache wanaotishia maisha na mali za wananchi?

Na inawezekanaje kutumia rasilimali kukamata watu waliosema hovyo tu mitandaoni bila kuhatarisha lolote na isiwezekane kukamata vibaka tunaojua mitaa yao wanaojeruhi na kuua watu?

Kiongozi mmoja amedai wanajipanga kukabiliana na tatizo a ujambazi na vibaka.

Ni kauli ya kusikitisha, wananchi hawahitaji kusikia kauli za kisiasa, wanataka matokeo ya kazi

Na wala hawahitaji kujua mikakati na mengine yanayohusiana na hayo.

Wananchi wanataka matokeo ya kazi za waliopewa dhamana. Wanataka kuishi kwa Amani ili utulivu uwepo

Tunaposisitiza Amani na utulivu kwa 'jicho la siasa' tu hatutawatendea haki wananchi

Hili la vibaka linahitaji kipaumbele, endapo limeshindikana wananchi wataarifiwe ili kujua wanawezaje kuleta Amani na utulivu katika maeneo yao.

Tatizo la kuacha suala hili kwa wananchi, ni kutoa fursa ya uvunjaji wa sheria, na haki za binadamu

Tunadhani tatizo ni la viongozi kutolipa suala hili mtazamo mzito au viongozi kutokuwa na mbinu za kutosha au kuelekeza nguvu katika mambo yasiyo na umuhimu.

Kwa uchache wa kusema, hili Linatia doa sana

Tusemezane
 
TAIFA LILIVYOGAWANYIKA

'UCHAGUZI UMEKWISHA SASA WATU WAFANYE KAZI''

Mwanzoni mwa mbandiko haya tulisema, kazi ya kwanza ya Rais ni kuliunganisha Taifa
Makovu ya uchaguzi/kampeni zake na yatokanyo yamelicha taifa limegawanyika mapande

Tulisema hakuna anayefanikiwa peke yake au Taifa la mtu au wachache bali la Wananchi

Tumesikia viongozi wakisema muda wa uchaguzi umekwisha watu wafanye kazi pamoja.

Ukweli usiosemwa ni kuwa Taifa letu limegawanyika hasa kiitikadi za kisiasa.

Kuna kundi linaloona lina haki 'miliki' ya nchi na makundi mengine hayastahili heshima

Hata katika 80% au 90 za ushindi, kiongozi wa Taifa anatakiwa kulileta pamoja kwanza

Kugawanyika katika misingi ya kisiasa kunapanda mbegu ya migawanyiko mingine hatari

Ni ukweli kauli na matendo ya viongozi wa ngazi mbali mbali kwa kujua at kutojua yanana matatizo makubwa.

Kwamba, masilahi ya wananchi si muhimu kuliko masilahi ya baadhi ya watu

Mfano mzuri ni wa aibu iliyotokea Arusha katika uzinduzi wa jengo la akina mama,watoto.

Jengo limelenga kuhudumia sehemu muhimu ya jamii yetu ambayo kwa kiasi kikubwa haijapewa umuhimu

Ni Hospitali itakayomtibu mwananchi yoyote kama ilivyo hospitali nyingine nchini.

Haibagui wa Arusha au maeneo mengine,viongozi wangekuja pamoja katika jambo la kheri

Ni ukweli pia kuwa , mradi huo umekuwa ni sehemu ya ahadi za Mbunge wa Arusha kwa muda mrefu.

Uchaguzi uliopita mradi ulitumika kama kuonyesha kushindwa kwake kutimiza ahadi

Hatu ya jana ilikuwa ni nzuri si kwa mbunge bali ushindi kwa wananchi wa Taifa hili.

Tunajua siasa za Arusha za Minyukano ambazo zenye zinachangiwa na nguvu kutoka nje

Hivi kwanini tukio hilo limegeuka kuwa la siasa badala ya tukio la maendeleo?

Mradhi wa Arusha hata kama umefanywa na mpinzani na si mtu wa CCM ni muhimu ukaungwa mkono na viongozi wa nchi ambao siyo CCM tena bali viongozi wa Taifa.

Kitendo cha kufanya siasa majitaka kwa mradi huu kimedhalilisha Taifa na viongozi wanaodai wananchi wapelekewe maendeleo na atakayekwamisha achukuliwe hatua

Tunadhani ni wakati Rais akaliunganisha Taifa kwa hali iliyopo.

Hii ni pamoja na kuchukua hatua dhidi ya viongozi wasioweza majukumu yao. Kushindwa majukumu ni pamoja na kushindwa kufanya kazi pamoja

Haiwezekani kila siku kukawa na malalamiko juu ya kiongozi mmoja anayeleta matatizo na kiongozi huyo kubaki na nyadhifa. Hatudhani kama kuna kiongozi aliyechaguliwa kupambana na wapinzani au serikali

Tunachojua viongozi wanaomkwamisha Rais kama anavyosema hawafai, waondolewe mapema

Tukio la jana si aibu kwa wahusika, bali nchi na uongozi wa nchi kwa ujumla.

Tulipofikia Watanzania tunahitaji kujitathmini, tumegawanyika si wamoja tena! Tupo mapande pande

Tusemezane
 
KWA HILI SERIKALI IKAE MBALI

Katika mabandiko tumezungumzia dhana ya serikali kutokuwa na dini lakini watu wana dini
Upo msemo maarufu wa kutchanganya dini na siasa, ingawa msemo huo hauna kuchanganya siasa na dini

Hii ni kwasababu wanasiasa wanafahamu zipo nyakati wanawahitaji viongozi na waumini kwa malengo yao

Kwa mfano, ikitokea viongozi wa dini wakamwalika mwanasiasa hilo litalaaniwa kwa nguvu zote

Na mwanasiasa huyo atakapoingia katika kusadia iwe jamii au chama cha siasa hali inakuwa mbaya Zaidi

Kwa upande mwingine, wanasiasa wanaweza kuwaalika viongozi wa dini na kuahidi kuwasaidia

Hilo halionekani kuwa tatizo kwasababu kuna imekubalika 'kuchanganya siasa na dini'

Dini ziachwe zijiendeshe kwa misingi na waumini wake, zisiwe katika mambo ya kisiasa
Pale itakapohijika msaada, hilo liwe katika hali inayoeleweka

Katika hali ya mwelekeo mpya, serikali inaonekana kuwa karibu na dini kwa maana ya kusaidia

Tumeona viongozi wakichangisha na kutoa misaada kujenga nyumba za ibada.

Nyumba za ibada ni maeneo ya waumini wa dini na ndio wenye dhima ya kupanga nini wafanye

Kutokana na mahusiano yaliyopitiliza, viongozi wa dini wame abuse system katika kodi

Jambo hili limetokea kwa serikali kuwa na ukaribu usiohitijika katika mambo ya dini

Haionekani kama viongozi wanaona tatizo mbele ya safari.

Serikali inaweza ku facilitate dini kufikia malengo na si kujiingiza katika shughuli za dini moja kwa moja.

Ugeni uliotufikia na kuahidi kujenga majengo ya ibada na kutangazwa na wanasiasa, inatia wasi wasi isiyo na ulazima

Wageni wangewezeshwa kukutana na dini kujadiliana namna ya ushirikiano

Serikali ingekuwa ime faciliatate na si kujiingiza katika shughuli kama ujenzi wa majengo

Rai yetu, sisi tukiwa Taifa moja lenye watu wenye Imani , wasiomini na wagani tunatakiwa tuishi kwa upendo na umoja.

Jambo hilo litawezekana pale ambapo hakutakuwa na minong'ono isiyo ya lazima

Tunashauri serikali ikae mbali, haina dini bali wananchi wake wana dini , hawana, au hawaamini

Wote ni Raia wa Taifa moja, na hawapaswi kuhisi tofauti. Serikali ikae mbali na mambo ya dini

Tusemezane
 
MATUKIO YA WIKI

HATUFANIKIWI KWA KUFANYA KAZI ZA 'ZIMAMOTO'

MBONA KUNA KUYUMBA YUMBA?

Katika wiki mbili au tatu kumekuwepo na matukio yanayofikirisha katika Taifa letu

1. BUNGENI
Kiongozi wa upinzani bungeni aliuliza swali kwa madai kuwa viongozi wakuu wa serikali walishiriki kikao alichosema kilitoa milioni 10 kwa wabunge wa chama

Hoja yake pamoja na majibu ya kisheria na kisera ilipingwa na naibu Spika.
Swali alilomuuliza Waziri mkuu lilikuwa na viashiria vya 'tuhuma'

Busara zinaeleza, panapokuwa na mjadala wa tuhuma pande husika hupewa fursa ya kujieleza. Ndivyo mfumo wa kutoa haki mahakamani unavyofanya kazi

Swali hilo la 'tuhuma' limebaki bila majibu.Kila mtu atapaswa kutafuta majibu.
Jibu lolote litakalopatikana kichwani kwa mtu yoyote litakuwa sahihi

Watakaosema haikuwa rushwa bali posho watakuwa sahihi, na watakaosema ni rushwa watakuwa sahihi. Swali hilo limeachwa kwa wananchi watafakari wenyewe

2. BUNGENI
Kamati ya PAC imeundwa kufuatilia tuhuma dhidi ya majengo ya NSSF Kigamboni.
Nazo ni tuhuma, lakini kwa namna fulani zimepewa uzito na kutafutiwa majibu bungeni

Maswali ya kujiuliza kwa hoja 1 na 2 ni kuwa rushwa inapimwa kwa kigezo gani?
Kwanini kuna kuchagua lipi la kushughulikia na lipi liachwe hewani?

3. MISIBA
Kumetokea misiba miwili ya watumishi wa umma na wazee wetu.
Ni watu waliotumikia taifa kwa muda mrefu.Pole kwa wafiwa na mungu awarehemu

Bunge liliahirisha shughuli kumuenzi Mzee Sitta na keshokutwa ataagwa ndani ya Bunge

Heshima hii ni kubwa na wala si haja ya safu hii kuhoji ukubwa wake au sababu zake

Katika msiba mmoja siku na masaa kadhaa yamepotea kwa shughuli ambayo ingeweza kufanywa kwa kuratibiwa vema na bado ikabeba uzito ule ule

Kwanini Bunge lisiendee na shughuli zake hadi Alhamisi litakapomuezi mzee Sitta?

Kuna mantiki gani ya kuwa siku tofauti na maeneo tofauti ya shughuli ile ile?
Kwanini kusiwe na uratibu wa shughuli hapa Dar au Dodoma na wahusika kujumuika?

Kinachojitokeza ni kutokuwa na utaratibu unaojulikana wa mazishi.
Kuna itifaki za kiutawala na uongozi serikalini hadi katika vyama.

Tunadhani ni wakati uwepo utaratibu namna gani watumishi na viongozi wataenziwe

Msiba wa Mzee Sitta na Mzee Mungai kama ilivyo kwa mingine huamuliwa na watu kwa matakwa bila kanuni. Ni muhimu ukawepo utaratibu wa kitaifa wa mazishi ya viongozi

Inaendelea
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Inaendelea

4.MSAJILI WA VYAMA

Msajili wa vyama amefuta usajili wa baadhi ya vyama vya siasa kwa kutozingatia sheria

Moja ya sababu zilizotolewa ni vyama husika kutokuwa na ofisi bara au visiwani
Nyingine ni kutowakilisha hesabu na mali za vyama hivyo na hivyo kukiuka sheria

Vyama hivi vimekuwepo kwa muda mrefu sasa. Inakuwaje basi viliweza siasa na chaguzi bila kujulikana kwa muda mrefu? Kwanini hakukuwepo ukaguzi wa maendeleo ya vyama?

Ofisi ya masjili wa vyama ipo kisheria na hufanya kazi zake kila siku kama ofisi nyingine.

Nini kilitokea vyama hivyo vikiwa vimekiuka sheria na bado vikaendelea kuwepo?

Lakini pia kuna swali kuhusiana na matumizi.
Je, msajili anakagua vyama kuhakiki matumizi ya fedha ikiwemo ruzuku za vyama hivyo?


Tunaunga mkono kufuta vyama vya briefcase hata hivyo hayo yawe mambo endelevu
Ukaguzi wa vyama isiwe kazi ya msimu au tukio

Bila kufanya hivyo na kwa vyama vyote, bila kujali ukubwa au udogo, uwezekano wa viongozi kugawana mali unaweza kuwa sehemu ya maisha ya kawaida

Viongozi 2 ,10,100 au 200 wanaweza kukaa na kugawana mamilioni au mabilioni ya fedha za wananchi kwa kisingizio cha fedha za chama au mambo ya ndani ya vyama

Jambo kama hilo likitokea si kuwa linadhulumu fedha za wanachama au wananchi wanatoa ruzuku kupitia kodi,pia litafungua mianya ya rushwa kwa visingizio mbali mbali

Rai yetu, ukaguzi ufanywe kuhakiki mali na raslimali za vyama ili kuzuia vyama vya siasa kutengeneza mifumo ya kifisadi au kuwa vichaka vya ufisadi, rushwa na maovu mengine

Tusemezane
 
  • Thanks
Reactions: BAK
POLITICAL STABILITY OR INSTABILITY

KAMA TAIFA TUMESIMAMA WAPI KISERA?

Tuongelee dhana ndogo sana ya kile kinachoitwa Political stability.
Dhana hii imechukuliwa kiurahisi kama kutokuwa na vurugu, migomo au tafrani katika Taifa.

Imekuwa ni rahisi viongozi kusema taifa letu lina political stability.Pengine ni kweli

Kuna kitu kinachoitwa integrity ambacho ni sehemu muhimu ya stability.
Integrity inaelezwa ni kuaminiwa kwa kile nchi au serikali inachosimamia

Integrity inaeleza tunasimiaje thamani zatu (values).
Na values hulindwa na sera(policy) tulizojiwekea. Ndiyo maana sote bila kujali itikadi zetu tunaamini binadamu wote ni sawa na wanastahili utu na heshima.

Ni kwa msingi huo, serikali yetu iliamini katika sera ya uswa, utu na heshima
Ilichukua misimamo kadhaa mingine michungu katika kulinda values zetu kama Taifa

Tulikuwa wananchama wa nchi zisizofungamana na upande wowote(NAM) ili kuwa huru kuunga mkono eneo lolote linalosimamia thamani zetu za uhuru, usawa, utu na heshima.

Tuliunga mkono harakati za ukombozi kusini hadi Magharibi. Palestina, Nigeria na kwingeneko ambapo wananchi walisimamia haki zao zinazolingana na thamani zetu

Taifa letu lilikuwa na sera bila kujali nani ataongoza kutoka wapi
Miaka ya karibuni sera za Taifa zimegeuka kuwa za vyama na kutuyumbisha

Hivi leo tuna sera ipi kuhusu uhuru, usawa, utu na heshima ya mwanadamu?

Ziara ya mfalme wa Morocco inatuweka wapi tukiiingalia Sahara , Plestina na kwingine kwenye madhila yanayofanana na hayo yayonakinzana na values zetu?

Je, bado tuna integrity katika jumuiya ya kimataifa?
Na je integrity yetu inaeleza nini kuhusu policy zetu kama Taifa na stability yetu?

Integrity yetu haiishia katika eneo hilo la Kimataifa. Hata katika local level upo wasi wasi

Awamu ya nne ilisimama kuhakikisha Watanzania popote walipo wanatoa mchango kwa Taifa.
Na kwamba uwepo wao nje iwe sehemu ya mafanikio na si usaliti.

Hilo ndilo liliunda 'idara' ya diaspora ili kuhakikisha wanachangia maendeleo ya nchi waliko

Tangazo la serikali kuhusu umilikiwa ardhi kwa diaspora limekuja na vishindo.
Kwanza, serikali ya chama kile kile haina sera na wala haiminiki. Pili kama nchi hatuna sera za Taifa

Mifano miwili awali inaeleza integrity ya serikali. Kwa mwekezaji au wawekezaji tunaowakaribisha, mifano ni mingi inatosha kuwaeleza political stability ya nchi yetu

Investors hawapendi mashaka 'uncertainty' na hali ilivyo, hata wazawa wanaona uncertainty nyingi kimataifa hadi kitaifa.

Mwekezaji ana kila sababu ya kuogopa!

Tusijidanganye kwa kauli mbiu ya political stability, tujiulize tuna integrity? Tuna sera kama nchi?

Tusemezane
 
HATUNA SERA ZA NCHI, TUNAZO SERA ZA 'WATU'

Bandiko la juu tumezungumzia political stability/instability na athari za taswira ya nchi zetu

Mataifa yaliyoendelea zipo sera za nchi, na za vyama hotofautiana utekelezaji

Kwa bahati mbaya hata sera za vyama wananchi wetu hawawezi kuzihoji
Hii imepeleka mabadiliko ya kila mara ya sera kutokana na watu na si wananchi

Hali inachanganya wananchi au wageni, inatia hasara zisizo na ulazima

Kwa mfano, suala la katiba

Hili lilikuwa takwa la wananchi lililofanywa sera za wapinzani.
Lengo lilikuwa kuboresha katiba yetu kwa kulingana na nyakati tulizo nao

Hoja ya katiba 'ikatekwa' na Rais kwa kuanzisha machakato si wananchi

Ikawa tena si ya wananchi bali takwa la kiongozi aliyekuwa madarakani

Kwa kukosa muafaka, na hoja kuporwa kutoka kwa wananchi , katiba ikawa suala la kikundi cha watu kikitaka kuamua kwa niaba ya Taifa. Tulifeli

Pesa kwa mabilioni zilitumika bila matokeo chanya.
Katika uchaguzi mkuu, katiba haikuzungumziwa kwasababu ilionekana mtego

Awamu ya tano inasema katiba si kipaumbele cha serikali iliyopo madarakani
Kwamba, kila kiongozi madarakani ana sera zake na si nchi kuwa na sera

Katiba ni suala la kitaifa ingawa kunaweza kuwepo tofauti za nini katiba ibebe
Iweje serikali ya chama kile kile iwe na sura mbili? moja ikitaka na nyingine ikikataa?

Hasara zinazotokana na sera za watu na si nchi, moja ni hili la katiba.
Kushindwa kuandika katiba inaeleza political instability na si stability

DIASPORA
Awamu ya nne ilishiriki vema kuhamasisha diaspora kama sehemu ya wananchi.
Tumeshuhudia diaspora wakijiunga katika makundi na serikali kuunda kitengo

Serikali yA JK ilihimiza diaspora kushiriki shughuli za nyumbani, au kuwekeza wakiwa huko na serikali itawatambua kama Raia wanaotafuta

Awamu ya tano imetoa tangazo linalowatisha na kuwasumbua diaspora waliovutika na hoja za awamu ya nne. Kwamba, wangepewa kipaumbele kama Raia na si wasaliti

Leo walionunua ardhi , majumba , viwanja, nyumba pengine kwa ndugu wanahangaika bila kujua nini hatma yao hata kama ni kidogo ''walichowekeza''

Haya yote ni kwasababu kama nchi hatuna sera za mambo ya kitaifa.
Tuna sera za watu binafsi zinazoleta hasara na usumbufu usio wa lazima

Sisi kama Taifa ni wakati sasa tuwe na sera za nchi tuzisimamie kwa 'integrity'
Tuzuie watu kutengeneza sera nje ya utaratibu kisha kuzifanya za nchi

Ya katiba na hili la diaspora hayatoshi kueleza instability na integrity yetu?

Tusemezane
 
Ni kweli Watanzani tu wapumbavu na hatua akili hata kidogo. Viongozi wetu wanatujua hivyo na ndiyo maana hawana hofu na sisi. Serikali inafanya madudu lakini ikija uchaguzi chama kilekile kilichounda serikali iliyofanya madudu inashinda. Kundi la kwanza linaloongoza ni la vyombo vya usalama. Vyombo vya usalama vinaamini kuwa tunaposema usalama wa Taifa tunamaanisha Usalama wa viongozi na CCM. Matokeo yake ukifika uchaguzi wanawalinda viongozi badala ya kulinda Taifa. Wakati mwingine hili halifanyiki kwa bahati mbaya au kwa kutokujua ni kwa sababu ya matarajio ya kupata vyeo mara baada kumalizika kwa uchaguzi.
Vyama vya upinzani ni kundi lingine la wapumbavu: Hawa nawasema hivyo kwa sababu hoja ya Tume huru ya uchaguzi hawaishikia bango vya kutosha. Huwezi kutegemea ushindi wakati muamuzi wa mchezo ni mchezaji pia. Haiwezekani mtu akuteue halafu kesho akupe maagizo ukatae, atakutoa.
CCM hawana hofu ya kushindwa uchaguzi hata wangetuburuza namna gani kwa sababu wanajua Watanzania hatuna kwa kugeukia.
Anggalieni mifano ya nchi za wenzetu- Rais aki mess wanachagua toka chama kingine. Mfano mdogo ni Marekani hata viongozi wa wa juu wa cha Dolnad Trump walimpokataa wanachama wengine wakampa kura akateuliwa kuongoza chama chao. Democrat kimeongoza kwa vipindi viwili mfululizo, hata kama mgombeo wao angekuwa mzuri namna gani wametaka kubadilisha uongozi. Hili kwa Tanzania haliwezekani. Kwa nini viongozi walioko madarakani wasituone wapumbavu? Rais anatoa maamuzi bila kufuata sheria, sisi ndiyo mzee, chama kinageuza maoni ya Rasimu ya katiba inayopendekezwa kuleta maoni ya chama chao sisi ndiyo mzee. Jambo lolote ni ndiyo tu. Kwa nini viongozi wasitufanyie chochote wanachotaka?
 
Ni kweli Watanzani tu wapumbavu na hatua akili hata kidogo. Viongozi wetu wanatujua hivyo na ndiyo maana hawana hofu na sisi. Serikali inafanya madudu lakini ikija uchaguzi chama kilekile kilichounda serikali iliyofanya madudu inashinda. Kundi la kwanza linaloongoza ni la vyombo vya usalama. Vyombo vya usalama vinaamini kuwa tunaposema usalama wa Taifa tunamaanisha Usalama wa viongozi na CCM. Matokeo yake ukifika uchaguzi wanawalinda viongozi badala ya kulinda Taifa. Wakati mwingine hili halifanyiki kwa bahati mbaya au kwa kutokujua ni kwa sababu ya matarajio ya kupata vyeo mara baada kumalizika kwa uchaguzi.
Vyama vya upinzani ni kundi lingine la wapumbavu: Hawa nawasema hivyo kwa sababu hoja ya Tume huru ya uchaguzi hawaishikia bango vya kutosha. Huwezi kutegemea ushindi wakati muamuzi wa mchezo ni mchezaji pia. Haiwezekani mtu akuteue halafu kesho akupe maagizo ukatae, atakutoa.
CCM hawana hofu ya kushindwa uchaguzi hata wangetuburuza namna gani kwa sababu wanajua Watanzania hatuna kwa kugeukia.
Anggalieni mifano ya nchi za wenzetu- Rais aki mess wanachagua toka chama kingine. Mfano mdogo ni Marekani hata viongozi wa wa juu wa cha Dolnad Trump walimpokataa wanachama wengine wakampa kura akateuliwa kuongoza chama chao. Democrat kimeongoza kwa vipindi viwili mfululizo, hata kama mgombeo wao angekuwa mzuri namna gani wametaka kubadilisha uongozi. Hili kwa Tanzania haliwezekani. Kwa nini viongozi walioko madarakani wasituone wapumbavu? Rais anatoa maamuzi bila kufuata sheria, sisi ndiyo mzee, chama kinageuza maoni ya Rasimu ya katiba inayopendekezwa kuleta maoni ya chama chao sisi ndiyo mzee. Jambo lolote ni ndiyo tu. Kwa nini viongozi wasitufanyie chochote wanachotaka?
bantulile kuna mambo yanatia uchungu kuyaeleza kama raia. Solution ya kueleza ni kuhakikisha yanaeleweka, na njia ya kueleweka ni kutafuta lugha itakayoeleweka. Lugha ya kueleweka ni ile ambayo kila mmoja atapenda kuisikia au kuisoma. Hivyo, jitahidi kupunguza jazba ili ujumbe wako ufike kwa njia njema na lugha sahihi
 
SAKATA LA DIASPORA

WALENGWA NI DISAPORA WALIOCHUKUA URAI MWINGINE

Katika sakata la Diaspora linalowasumbua na kuweka roho za wengi juu, tumeelezea serikali mbili zilivyoliangalia suala kwa mitazamo tofauti kana kwamba ni kitu kutoka nje ya nchi

Tulihoji integrity ya serikali za CCM na kama tuna sera za Kitaifa kama Taifa

Tangazo la umiliki wa ardhi ndilo limeamsha hofu na wahka

Utetezi: Kuna hoja, tangazo lililenga Watanzania wanaoishi nje ya nchi.
Ni kweli, wapo watanzania wanaomiliki hati za Tanzania na waliochukua Uraia mwingine

Mtanzania mwenye hati ya Tanzania awe anasoma au anafanya kazi nje ya nchi bado ni Mtanzania na hakukuwa na sababu ya kumweleza uhalali wake wa umiliki wa ardhi

Uhalali hauondolewi na kusafiri kwa mujibu wa sheria hata kama amekaa nje miaka 100

Ukweli, tangazo lililenga Watanzania wanaoishi nje ya nchi wenye uraia wa nchi nyingine.

Hili limeshadidiwa na hoja ya dual citizenship na hoja diaspora waje kama wawekezaji

Hoja ya wanaoitwa diaspora ni ndefu na tutaijadili kwa urefu wake.

Lakini kwanza tujue kwanini wanaokwenda nje huamua kuchukua urais wa nchi nyingine?

Jibu la swali hilo ni rahisi, wanataka kurahisha maisha ya huko wanakoishi

Mifano ni mingi sana, tueleze michache

Diaspora wapo wenye familia zao. Huduma za wanakoishi zinategemea aina ya Uraia.

Shule anayesoma mtoto mwenye hati ya Tanzania inaweza kulipiwa dollar 10,000
Mwenyeji au Mtanzani huyo akichukua Uraia ada hiyo inakuwa 3,000 kama Raia

Huduma za afya nazo ni katika mfano huo huo. Kwamba, kitanda cha hospitali kwa asiye raia kinaweza kuwa dollar 1000(mfano),Raia anaweza kutolipa au kulipa dollar 200

Ukiwa si raia usafiri katika shughuli za maisha utategemea kupatikana kwa visa.

Zipo nchi lazima ima urudi kupata/renew visa nyumbani au uende balozi za mbali

Hili linaathiri ajira. Waajiri hawahitaji kutafutia mtu visa kwa shughuli yenye ushindani

Moja ya masharti ni kuhakikisha muajiri anapata kibali cha kazi

Hapa ieleweke, visa haitoi kibali cha kazi inawezesha kibali cha kazi.

Hivyo umiliki wa Uraia wa Tanzania unaongeza vikwazo katika maisha ya diaspora
Kwanza, apate visa, pili kibali cha kazi, na tatu awe tayari kujihudumia elimu,afya n.k.

Kumbe matatizo yanaweza kwisha kwa Uraia na mtu akabaki na moyo wa Utanzania.
Hawa ni watu wenye ndugu,familia, marafiki n.k. katika nchi yao achilia mapenzi ya nchi

Ndiyo maana diaspora hufuatilia habari za nyumbani pengine kuliko walioko nyumbani.
Dhana kwamba kuchukua Uraia ni usaliti haina mashiko na ni ufupi tu wa fikra.

Je, tunawezaje kutengua kitendawili cha dual citizenship?

Inaendelea....
 
SAKATA LA DIASPORA
URAIA PACHA

Ipo hoja, kweli sheria zetu haziruhusu uraia pacha. Sheria inawekewa uzio 'kwa usalama'

Sheria inatumika kufunika hoja za diaspora kwa kupumbuza umma
Hoja ya msingi ni kutambuliwa kwa diaspora ili washiriki kama wananchi

Kushiriki ni kumuondolea diaspora vikwazo visivyo na ulazima kwa kumpa 'preference'

Bila kuathiri sheria za uraia pacha , hili linawezekana wenzetu hata kwa raia wasio wa nchi zao.
Mfano, kuna green card, kuna permanent resident n.k. zikiwa ni hadhi za ukazi wa kudumu

Kuna nchi Raia wa Tz anapata hadhi ya ukazi wa kudumu(permanent resident) na kumpa haki zote kama raia isipokuwa za kisiasa (kugombea, kupiga kura n.k.)

Mtanzania mwenye hadhi ya kudumu iwe UK, Canada, Australia n.k. hahitaji visa, kibali cha kazi na ana haki zote za huduma ikiwemo kumiliki ardhi mali n.k.

Utaratibu kama huo unatumiwa na baadhi ya mataifa kusaidia diaspora wao wanaporejea
Kwa maana ya kumrahishishia kushiriki shughuli za nyumbani bila vikwazo au ugumu

Kwanini Utratibu kama huo usitumike kwa diaspora wa Tanzania wa kuwapa ukazi wa kudumu?

Upotoshaji:
Hoja ya ukazi wa kudumu inapotoshwa kwa kisingizio cha sheria ya Uraia pacha

Endapo uraia pacha ni tatizo la kikatiba, bado zipo sheria chini ya sheria mama zinazoweza kufanyiwa amendment bila kuathiri sheria ndani ya katiba

Mfano, katiba inazuia uraia pacha. Regulations zinaeleza zuio hilo na impact zake

Serikali inadhamana ya kufikisha mswada wa marekebisho, mpya n.k.Bungeni
Serikali inapokwepa suala hili kwa kusema ni suala la bunge, ni kukwepa hoja bila mashiko

Hadi pale itakapokuwepo hoja binafsi, mabadiliko ya sheria ni jukumu la serikali kwa ukubwa wake

Hizi danadana za Bunge na serikali ni kukwepa hoja ya msingi ya diaspora kutambuliwa kwa njia nyingine na si lazima uraia pacha. Lakini pia kwanini suala hili halijadiliwi ili kuona kikwazo kipo wapi?

Lini tumejadili ugumu wa uwepo ukazi wa kudumu(permanent resident) kwa diaspora wa Tz?

Inaendelea...
 
DIASPORA

Ikiwa tutakubali hoja kuwa katiba ni tatizo, kuna maswali ya kujiuliza sana kuhusu ubabaishaji huu
Mabadiliko ya katiba ya znz 2010 yaliathiri ya JMT. Mbona hakukuwa na hatua za kuzuia hilo

Kuna mswada wa gesi na mafuta unaoathiri katiba ya JMT, mbona hilo haliwagusi wahusika

Kitendo cha serikali kutupia Bunge mzito wa hoja za diaspora ni kukwepa wajibu wake
Diaspora wana hoja ya msingi na ya maana sana ikiwa ni win-win situation.

Ni wakati sasa wabunge wenye uchungu wachukue hoja hii kama ya dharura
Kinachoatakiwa ni hadhi rahisi tu ya ukazi kwa Watz waishio nje kuondoa usumbufu

Tunawazeja kutoa Uraia kwa wasioijua Tz tukashinda ukazi wa kudumu kwa wenye uchungu na Tz?

Ukazi wa kudumu unawezekana, kwanini hakuna mjadala

Mataifa mengi yametumia diaspora kuendeleza nchi zao.
Kwanini sisi tuwaone kama watu hatari na wasio na faida katika Taifa

Tumalizie kwa kusema katika mambo yanayotatiza ni hili la kutokuwa na sera za Taifa
Kila kiongozi sasa ana sera zake, ndio msingi wa kuhoji integrity na stability yetu

Hatutafanikiwa kwa kukwepa tatizo, tutafanikiwa tukifungua akili zetu na kujadiliana

Hofu ya diaspora inaeleza instability, mitazamo tofauti ya serikali 2 za CCM inaeleza integrity

Tusemezane
 
UTAWA WA SHERIA (RULE OF LAW)

Katika uzi huu mabandiko ya awali tulizungumzia utawala wa sheria
Hapa kusiwe na kuchanganya mambo mawili yanayoonekana kufanana

Kuna utawala wa sheria, kwa maana ya utawala katika kuzingatia sheria kutawala na kuepuka matumizi matumizi mabaya ya sheria zingatiwa

Kuna utawala bora(good governance), kwa maana utawala unaofanya na kutekeleza maamuzi katika misingi iliyokubaliwa katika jamii

Katika kuhakikisha utawala wa sheria na utawala bora vinaweza kutekelezwa, mihimili mitatu ya nchi iliwekwa, utawala, Bunge na Mahakama

Rule of law si kwa watawala tu bali ni binding kwa watawala na wananchi
Kwamba kila upande utimize wajibu wake kwa mujibu wa sheria

Tangu kumalizika kwa uchaguzi wa 2015 yanakuwepo matukio yanayoonyesha hali isiyo nzuri kwa utawala wa sheria na haki za binadamu

Sheria zetu zinaanisha haki za msingi za wananchi na serikali yao
Unaeleza nani anasimamia nini na nani anatoa haki ya kisheria

Hofu ya kutokuwa na rule of law inachangiwa na mambo mengi yakiwemo
i) Nguvu za ziada katika kutawala
ii) Matumizi mabaya ya madaraka 'abuse of power'
iii) wananchi kutojua haki zao za kisheria au za kibinadamu

Haya tutayafafanua

Inaendelea..
 
Inaendelea

Tujadii vipengele vya bandiko la awali

i)Nguvu za zaida:
Hizi si kitu kibaya. Ni nguvu aliyo nayo kiongozi kisheria kuchukua hatua ndani ya sheria

Kwa mfano, tuliwahi kusikia mkuu wa Wilaya akiagiza watumishi wa umma wawekwe mahabusu kwasababu walichelewa kufika katika mkutano.

Nguvu ya ziada ni uwezo wa yeye kuamua tu mtu awekwe ndani.
Kwamba ipo sheria inayomwezesha kuamuru Polisi kumweka mahubusu mtu.

Tumesikia viongozi wakitoa amri nini kifanyike au kisifanyike kwasababu tu wana nguvu za kisheria kufanya hivyo

Tumeona maeneo kama Bungeni viongozi wakikataa hoja zisijadiliwe kwasababu tu ya uwezo wa kukataza waliopewa bila kuzingatia jambo jingine

Tunaona vyombo vya dola vikikamata watu hata kabla ya uchgunguzi kukamilika kwasababu tu kuna sheria inayowapa uwezo huo wa ziada

Matokeo ya matumizi ya nguvu za ziada huzua tatizo jingine

ii)matumizi mabaya ya madaraka 'abuse of power'

Ni jambo gumu sana kupewa nguvu za ziada na zisiweze kutumika vibaya

Mwingereza Lord Acton alisema 'absolute power corrupts absolutely'

Hili la matumizi mabaya ya madaraka limefika katika kiwango cha kutisha

Limefikia mahali watu hawazingatii sheria, utawala wa sheria au haki
Kilichopo ni matumizi ya nguvu zinazopelekea matumizi mabaya ya madaraka

Kwanini mtumishi wa umma aadhibiwe kama uhalifu bila kuzingatia sheria za ajira?

Kwa mfano, kiongozi anaamuru mtu awekwe mahabusu kwa tuhuma tu kala pes , hajatoa rsisiti au amekataa kukubaliana na kauli kadhaa

Watu wanakamatwa kwa tuhuma tu wakati uchunguzi unaendelea.

Hivi kama hakuna uchunguzi inawezekanaje kukamata mtu?

Kumweka mtu mahabusu ni kuchukua uhuru wake.

Kwasababu za kisheria zilizoanishwa si kosa, tatizo ni matumizi mabaya ya nguvu za ziada pamoja na ya madaraka kama sehemu ya adhabu

Kwamba mtuhumiwa anaadhibiwa kabla ya tuhuma kuthibitishwa na mamlaka husika

Inaendelea
 
Inaendelea

Matumizi ya nguvu na matumizi mabaya ya madaraka yanashika kasi na kutishia

Tunarudia kusema, kuchukua hatua bila kuzingatia sheria ni kukiuka haki za binadamu
Mfanyakazi ana sheria za uajiri na inapodhihirika haki inatakiwa hatua huchukuliwa nje ya ajira

Haki si kwa vyombo husika ni pamoja na mtuhumiwa kusimama katika sheria
Mtuhumiwa kupewa nafasi ya kusikilizwa, kujieleza na kujitetea ni haki si fadhila.
Hukumu ni haki bila kujali inatoa matokeo gani. Ni haki

Inapotokea kiongozi kumwadhibu mtumishi au mwanajamii bila haki ya kusikilizwa au kujitetea si ni kuvunja haki na uonevu. Mtu anabaki kutokuwa na hatia hadi itakapothibitishwa

Kuchukua uhuru wa mtu kwa kutumia nguvu za ziada au madaraka ni jambo la kusikitisha

Haki ya mtuhumiwa si kukamatwa bali kupewa nafasi ya kupata haki zake ikiwemo dhamana

Akiwa chini ya ulinzi si jukumu la mtuhumiwa kutafuta usafiri wa kufika mbele ya sheria.
Wahusika wanajukumu,kushindwa kulitekeleza ni adhabu kwa mtu asiyethibitika kuwa na hatia

Ni kumnyima mtuhumiwa haki ya msingi ya kufika mbele ya sheria
Ni kuchukua uhuru wake na kumuadhibu mtuhumiwa bila ithabati ya iuhalifu

Imetokea mara nyingi watuhumiwa kukamatwa siku za wikiendi
Hakuna siku maalum za kukamata wahalifu lakini hili hutumika kama sehemu ya 'adhabu'

Sheria zinasema mtuhumiwa atafikishwa mbele ya sheria katika muda wa masaa 24.
Sheria imelenga kulinda haki za mtuhumiwa katika haki ya kusikilizwa kwa shtaka au dhamana.

Inaendelea
 
iii) Wananchi mtambua haki zao

Kuna tatizo kwa wananchi katika kutambua haki zao.
Kutokana na hayo lolote linalofanyika hata kinyume na sheria linaonekana la kawaida

Laiti wananchi wangekuwa na ufahamu, wangeweza kushinikiza taratibu zifuatwe

Taratibu hizo ni katika sheria za ajira na zote zinazohusiana na sheria za nchi

Mathalan, kumkamata mtu ijumaa inabidi awepo hakimu wa zamu wa wikiendi ili masaa 24 yatumike na vyombo husika kutoa haki kwa wenye mashtaka na washtakiwa

Kuna watu wataliona hili kama wazo la kiwendawazimu, ukweli,nchi nyingine mtu husomewa mashtaka hata wikiendi na kama haiwezekani huachiwa na kukamatwa muda muafaka

Pili, hili suala la kukamata watu uchunguzi haujakamilika nalo lina tatizo
Inakuwaje mtu akamatwe pasi uchunguzi kukamilika?

Hata kama haujakamilika mashtaka ya awali lazima yawepo ili kutimiza takwa la masaa 24

Tatu, kwa upande wa watumishi wanaofukuzwa katika mikutano, nao walipaswa kusimama na sheria zao za ajira zinazowalinda aau kuwahukumu na kwa taratibu zilizowekwa.

Kwa ujumla wananchi hawaonekani kujua haki zao na kuridhika tu na hali ilivyo

Pengine kuna tatizo katika elimu ya umma na hapa kuna maeneo yanayohusika

1. Vyama vya kitaaluma/wafanyakazi vipo kimya tu vikusibiri mikutano ya mwisho wa mwaka

Vimesahau jukumu lao la awali la kulinda masilahi ya umma

2.Mashirika na taasisi zinazohusiana na mambo ya kijamiizimeacha majukumu yao ya asili na kujikita katika siasa badala ya masilahi mapana ya umma

Ni kutokana na nguvu za ziada , matumizi mabaya ya madaraka na uelewa mdogo wa wananchi, wanasiasa hufanya bila kuzingatia utawala wa sheria

Ni kwa msingi huo maamuzi yanayofanywa na wanasiasa ndani ya sheria, tayari kuna sura inayoonekana, kwamba, sheria hazizingatiwi kwasababu ya chuki, visasi na uonevu

Kibaya, vyombo vya kusimamia sheria na vinavyotoa haki vinaanza kutiliwa shaka.

Inaendelea....
 
HATUNA SERA ZA NCHI, TUNAZO SERA ZA 'WATU'

Bandiko la juu tumezungumzia political stability/instability na athari za taswira ya nchi zetu

Mataifa yaliyoendelea zipo sera za nchi, na za vyama hotofautiana utekelezaji

Kwa bahati mbaya hata sera za vyama wananchi wetu hawawezi kuzihoji
Hii imepeleka mabadiliko ya kila mara ya sera kutokana na watu na si wananchi

Hali inachanganya wananchi au wageni, inatia hasara zisizo na ulazima

Kwa mfano, suala la katiba

Hili lilikuwa takwa la wananchi lililofanywa sera za wapinzani.
Lengo lilikuwa kuboresha katiba yetu kwa kulingana na nyakati tulizo nao

Hoja ya katiba 'ikatekwa' na Rais kwa kuanzisha machakato si wananchi

Ikawa tena si ya wananchi bali takwa la kiongozi aliyekuwa madarakani

Kwa kukosa muafaka, na hoja kuporwa kutoka kwa wananchi , katiba ikawa suala la kikundi cha watu kikitaka kuamua kwa niaba ya Taifa. Tulifeli

Pesa kwa mabilioni zilitumika bila matokeo chanya.
Katika uchaguzi mkuu, katiba haikuzungumziwa kwasababu ilionekana mtego

Awamu ya tano inasema katiba si kipaumbele cha serikali iliyopo madarakani
Kwamba, kila kiongozi madarakani ana sera zake na si nchi kuwa na sera

Katiba ni suala la kitaifa ingawa kunaweza kuwepo tofauti za nini katiba ibebe
Iweje serikali ya chama kile kile iwe na sura mbili? moja ikitaka na nyingine ikikataa?

Hasara zinazotokana na sera za watu na si nchi, moja ni hili la katiba.
Kushindwa kuandika katiba inaeleza political instability na si stability

DIASPORA
Awamu ya nne ilishiriki vema kuhamasisha diaspora kama sehemu ya wananchi.
Tumeshuhudia diaspora wakijiunga katika makundi na serikali kuunda kitengo

Serikali yA JK ilihimiza diaspora kushiriki shughuli za nyumbani, au kuwekeza wakiwa huko na serikali itawatambua kama Raia wanaotafuta

Awamu ya tano imetoa tangazo linalowatisha na kuwasumbua diaspora waliovutika na hoja za awamu ya nne. Kwamba, wangepewa kipaumbele kama Raia na si wasaliti

Leo walionunua ardhi , majumba , viwanja, nyumba pengine kwa ndugu wanahangaika bila kujua nini hatma yao hata kama ni kidogo ''walichowekeza''

Haya yote ni kwasababu kama nchi hatuna sera za mambo ya kitaifa.
Tuna sera za watu binafsi zinazoleta hasara na usumbufu usio wa lazima

Sisi kama Taifa ni wakati sasa tuwe na sera za nchi tuzisimamie kwa 'integrity'
Tuzuie watu kutengeneza sera nje ya utaratibu kisha kuzifanya za nchi

Ya katiba na hili la diaspora hayatoshi kueleza instability na integrity yetu?

Tusemezane
 
Mkuu Nguruvi3, katika post yako [HASHTAG]#229[/HASHTAG] ni kilio kile kile tuliacho kila siku, na sisi walewale. Huna Dira ya Taifa wazalishia wapi sera za nchi? Wananchi kushindwa kusimamia sera zetu ni kushindwa kwa Top-Down, hatutaamka bado? Taifa linajengwa nje ya Uchaguzi, si kwa misingi ya uchaguzi alishinda hakushinda. Tukae chini.
 
Back
Top Bottom