Mwalimu
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 1,581
- 1,069
Dr. Tulia Ackson Mwansasu, ingawa anaitwa daktari wa sheria, liko jambo moja tu la msingi kabisa ambalo hata bila kukanyaga milango ya shule alitakiwa alijue...
Shughuli zote za Mamlaka ya nchi zinatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo vitatu navyo ni;
Mamlaka yote hayo yaliyotajwa yanasimamiwa na Katiba ambayo kwenye utangulizi wake imeandikwa, "Kwa kuwa SISI, Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani..."
- Serikali...yenye mamlaka ya utendaji ikiongozwa na Rais.
- Mahakama...yenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki ikiongozwa na Jaji Mkuu.
- Bunge...lenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma likiongozwa na Spika.
Hakuna hata sehemu moja inasema, "kwa kuwa mimi Rais nimeamua...", hapana, badala yake Rais kabla ya kuchukua madaraka anatakiwa aape kwa jina la Muumba kuwa atailinda na kuitetea Katiba ya wananchi iliyomweka madarakani. Je Dr. Tulia Ackson iwapo Rais atashindwa kuilinda na kuitetea katiba, amejipangaje?
Swali hili linanisumbua sana si kwa Spika peke yake bali hata kwa wakuu wa mihimili mingine ya mamlaka ya nchi kama Mahakama. Ni wazi Rais Magufuli kashindwa kuheshimu Katiba na kila siku kwa vitendo na matamko anaonekana kama vile yuko juu ya Katiba lakini linalotia hofu zaidi ni swali kwamba imekuwaje wananchi tuko kimya?
Shida kubwa ya nchi zetu hizi inapofika kwa Viongozi kuheshimu KATIBA ya nchi inachukuliwa kuwa ni suala la UTASHI BINAFSI zaidi na sio suala la ULAZIMA au UMUHIMU. Matokeo yake mhimili wa kwanza SERIKALI uko huru kwenda kinyume na katiba uliyoapa kuilinda kutokana na maneno na matendo ya viongozi wake. Na ugonjwa huu umewakumba pia wale wenye wajibu wa kusimamia katiba kwa upande wa mihimili mingine (Bunge & Mahakama) ambao wameshindwa kusimama kwenye nafasi yao pale wanapoona Mhimili wa kwanza unakiuka katiba... hawa kwa namna moja au nyingine wamejiweka kwenye kundi moja lenye jukumu la KUTII mhimili wa SERIKALI.