Duh! Rais Samia amkataa mama mnyonge aliyetaka kumlilia kama Magufuli. Nenda kakae…

Kwa hili maza nakupa tano, utasikiliza wangapi? mtindo huu ulioasisiwa na marehemu haukuwa mzuri, tuna watendaji kibao kila ngazi, kuna wawakilishi wa Rais kibao - kama kweli wananchi wana matatizo hadi wanataka kumwona Rais pekee yake basi tukubali watanzania kwamba tuna mfumo mbovu wa utawala - na sisi tunaodai KATIBA MPYA nikweli tuna hoja ya msingi.
 
Je hapo katoa maelekezo kwa wasaidizi wake wamsaidie au kumsikiliza huyo mama?
Raisi wa watu 65m sio kazi yake iwe kutatua individual cases, wele ambao hawana access kwake itakua je?,.....hiyo ni tabia mbaya alianzisha mwendazake kupata umaarufu wa kisiasa, na kulaghai wanyonge, kumbe mwenyewe ndo alikua adui wa watu wachini kuliko raisi mgine, Mama hongera kwa precedent hiyo, usikubali huo ujinga kwahiyo wote tunyanyuke tjkifuate uko ulipo kuna mtazania asio onewa au kudhlumia na watumishi wa ummah hususani police mahakamani aridhi nk.
 
Mama mmoja amesikika akimuomba Msheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassani kuwa anaomba atendewe haki, mama huyo amerudia mara 3 kusema anaomba atendewe haki, Lakini Rais Samia alimjibu kuwa hawa hapa wapo umeshatuandikia litanifikia nenda kakae. Rais Samia Aliendelea kusema kuwa ona yanajitokeza hata hapa. Hivyo kusisitiza mahakama zitende haki kwa kuangalia utu wa mtu.
Wanasiasa (ccm) ndio wanazibaka hizi kesi kabla hata hazijaanza kusikilizwa mahakamani!
Mnaanza kuwapangia mahakimu/majaji aina ya hukumu mnazotaka nyie kwa kuwaonea watu wasio na hatia!
Haki hapo itapatikana wapi. acheni kutuzuga kabisa!
 
Sasa kama hawasaidiwi waende kwa nani. Acheni kupwekesha jukumu la Rais.

Ukisema hawezi kusimamia mambo utapungukiwa na nini?
Kila jambo ulishughulikie wewe kisa ni rais. Utapata matatizo ya moyo kwa binadamu wasio na shukrani hata kidogo.

JPM alikuwa anataka kushughulika na kila tatizo, amefariki na ni kama wema wake ulipotea bure tu, anatukanwa na wengi humu jukwaani.
 
Kwahyo unataka Rais akawe hakimu ama Judge kwa muda huo huo mfupi hapo na atoe maamuz!!?
Sasa hamuoni kama atakuwa ameingilia muhimili mwingine!?! Halafu kesho muanze tena kumsema vibaya
Kwani kusikiliza ndio kuamua?

Mtu kaamua kufika pale baada ya kukosa msaada. Rais anauwezo wa kuchunguza jambo lolote kupitia vyombo vyake kisha akaamua. lakini pia anaweza akaomba mwanasheria wa serikali amsaidie huyo mtu.
 
Kwani kusikiliza ndio kuamua?

Mtu kaamua kufika pale baada ya kukosa msaada. Rais anauwezo wa kuchunguza jambo lolote kupitia vyombo vyake kisha akaamua. lakini pia anaweza akaomba mwanasheria wa serikali amsaidie huyo mtu.
Umenena vyema! Ila kuna kundi kila madahaifu ya Rais wanapiga mapambio! Yaani Rais anaonesha hadharani hawezi kujali masrahi ya mwananchi wa chini Wasaidizi wake si ndo itakuwa balaa!
 
Watu wamekula Hadi kupitiliza urefu wa kamba, sasa wanatukamua wanyonge

Aliye waruhusu kula urefu wa kamba nae hataki sema kitu anatwambia nenda huko huko kapambane nao (tunawezaje pambana nao )

Mama aache porojo, asikilize watu huku chini hakuna haki
 
Back
Top Bottom