Sasa Da' Faiza hao Dubai wamefuata vipi msimamo wa Magufuli wakati mikakati ya Dubai na ya Magufuli ni tofauti?!
Wakati Magufuli alisema watu waendelee kulundikana misikitini na makanisani, Dubai misikiti mingi ilifungwa, na Sala ya Ijumaa ilisimamishwa.
Wakati Magufuli amesema wazi kwamba kupulizia dawa ni upuuzi, Dubai, nakumbuka ilikuwa around March 25-28 walikuwa wanapuliza dawa kwenye barabara na mitaani!!
But all in all, HAKUNA nchi hata moja ambayo ilitangaza inaweka permanent lockdown! Hata Msikiti wetu wa Ngazija pale City Center wakati wanafunga walisema wazi kwamba wanaufunga kwa muda ili kuweka mambo sawa ikiwa ni pamoja na kunyunyuzia dawa!!
Sasa kama Dubai wameshaona mambo yamekaa sawa, na zile possible threats zimeshakuwa controlled, sasa ulitarajia waendelee na lockdown?!
Kote duniani wanakolegeza lockdown hawafanyi kwa kuangalia msimamo wa Magufuli bali wanafanya hivyo kwa sababu kuna mazingira wameshaya-control!
Hata Wuhan ilikotokea COVID-19 na wenyewe wameshaondoa lockdown baada ya "evrything" kuwa under control!!
Siku nitakayosikia kuna kiongozi kutoka taifa linalojitambua ametangaza "hizi barakoa ni upuuzi mtupu kwa sababu ni matambaa ya puani tu na wala hazisaidii",
Au atakayesema disinfection ni upuuzi mtupu...
Au atakayesema watu waendelee kujazana makanisani na misikini kwa sababu huko coronavirus haiwezi kuingia,
Au atakayesema "piga ua hatuwezi kufunga viwanja vya ndege kwa sababu tutaharibu utalii"
Au "piga ua hatuwezi kufunga miapaka kwa sababu nchi hii inategemewa na majirani " Siku nikisikia habari kama hizo ndipo nitakubali kwamba huyo wamemuiga "Jembe Magufuli" lakini mengine yote kila mmoja anafanya kutokana na situation ya wakati husika nchini kwake.