Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa anapambanishwa na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa kupata mwanasiasa bora anayekubalika zaidi kwa ajili ya kuwania TUZO YA JAMII.
Shirika la Tanzania International Awards ndilo linaratibu shindano hilo.Wapo pia wanasiasa wengine pia wanaowania tuzo hiyo kama Mizengo Pinda,James Mbatia,Ibrahim Lipumba,Bernard Membe na wengineo ingawa mchuano zaidi unaonekana ni kati ya Dr Slaa na Lowassa
Pia kuna tuzo kwa ajili ya vijana na wanapambanishwa John Mnyika,Halima Mdee,David Kafulila,Mwigulu Nchemba,Saada Mkuya na wengineo.
Mpambano huo unafanyika kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa mfano kumchagua Dr Slaa unaandika ujumbe MM03 kwenda 15522.