Hivi kuwa Rais ni lazima uwe na jiko? Ni matakwa ya Katiba au umeongea tu kwa kuwa jina lako linakuruhusu kutamka chochote? Ibara ya 39 ya Katiba ya JMT ya mwaka 1977 inataja sifa za mtanzania anastahili kuchaguliwa kuwa Rais wa JMT, hakuna popote panataja lazima uwe na jiko. James Buchanan alikuwa Rais wa Marekani asiekuwa na mke.... Rais Cleveland alioa baada ya kuingia Ikulu ya Marekani..... Thomas Jefferson, Andrew Jackson, Martin Van Buren na Chester Arthur kwa vipindi fulani wamekaa Ikulu bila kuwa na Wake. Ikiwa Marekani hawana tatizo na hilo inashindikana vipi kwa Tanzania ambayo Katiba yetu haitoi sharti hilo! Ian Khama amekuwa Rais wa Botswana akiwa Single. Ukiacha Mwalimu Nyerere, hao viongozi wengine waliokaa Ikulu, wake zao waliwasaidia nini Watanzania zaidi ya kuwa wafanyabiashara na pengine wakwepa kodi? Kwako kiongozi Bora ni aliye na Mke? Hata hivyo jina Msalani linakuruhusu kutamka utakavyo.