Dr Slaa na Kuhalalisha Gongo: Kwanini Yupo Sahihi

Status
Not open for further replies.
Imeruhusu pombe zipi ambazo ni Salama? wajua Gongo haina tofauti na Konyagi? na konyagi ukinywa nyingi unakufa! ndio na gongo vile vile nyingi una ndei

Huwezi fananisha mtu aliyekunywa Konyagi nusu lita na aliyekunywa GONGO nusu lita!
 
Kabla ya sijajibu swali lako, je unakubali kwamba hilo ndilo alilosema dr slaa?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Hiyo ni sehemu ndogo ya mengi aliyosema Dr. Slaa na haibebi dhumuni kuu la sababu ya Slaa kutaka gongo ihalalishwa. DHumuni kuu ni kuondoa bughudha ya polisi.
 
Nakupongeza sana Mchambuzi kwa mjadala huu na uchambuzi ulioufanya kwa mtazamo wa kitaifa zaidi badala ya kiitikadi.

Tumejifunza historia jinsi mengi ambayo yalishaasisiwa na wazee wetu yamekuja kupigwa vita na wakoloni kwa kuhalalisha bidhaa zao ambazo zilichukua nafasi ya soko mbadala, jitihada za wazee wetu zilitokana na mianzo hali kadhalika njia hizo hizo, iwe imani, uundwaji wa vitu mbalimbali na utamaduni.

Narejea kwenye uchambuzi wa
Mchambuzi kwamba alichokisema Dr. Slaa ndio uzalendo ambao utatufikisha kuwa na uwezekano wa kubuni kinywaji hicho ambacho kwa sasa tunavyo vingi vya kiwango cha alcohol hiyo kinachozalishwa toka nje au kuzalishwa nchini na makampuni ya nje. Kwa nini sisi wenyewe tusiendeleze kile ambacho tayari kinafanyika na kinachotakiwa ni tu kuboresha mazingira, vitendea kazi na nafasi ya soko? Hivi vinywaji vya kutoka nje vilianza kwa njia za kienyeji hivi hivi, nimeshuhudia mwenyewe nilipotembelea maonyesho ya makampuni yao yalivyoanza huko kwao.

Naweza kutamka wazi kwamba ni ujinga tunapopinga kila kitu hata kiwe chema kwa manufaa ya watanzania kwa vile tu kimetoka upande wa upinzani, hayo ndiyo yanayotuangusha na kudidimiza juhudi za kujenga misingi ya maendeleo nchini.

Kweli siasa inatupeleka kubaya.

Imefikia wakati vijana wa Bavicha mnadiriki kusema kutetea biashara ya gongo ndio kutetea maslahi ya taifa, just because kasema Dr. Slaa!!!

Labda nikuulize maswali ya kizushi tu.

Unadhani watanzania wangapi ni wanywaji wa gongo regularly? na je, unadhani familia ngapi zinategemea gongo kama chanzo kikuu cha mapato?
 
Labda swali lako linajibika ukienda kwenye biashara za vileo ambako ukifanya utafiti niambie kama utakosa biashara ya vinywaji vikali kama whisky, Konyaji, nk. Kama utakuta bidhaa hizo ndilo jibu la sisi tutengeneze zetu na kwa vile kimapokeo tunazo tunahitaji tu kuziboresha. Kama hutazikuta basi nitakubaliana nawe kwamba hakuna watanzania wanaotumia vileo hivyo kwa maana hiyo hakuna sababu ya kuhalalisha uboreshaji wa kileo hicho kwa vile hakuna watumiaji.

CC; Mchambuzi, ZeMarcopolo, MSALANI
 
Hapa naona uko off point.

Kwani Konyagi inatengenezwa wapi?

Kwani kuna mtu amekatazwa kutengeneza kinywaji kikali kilicho salama kwa watumiaji?

Kinachokataliwa ni kinywaji kinachohatarisha maisha ya watumiaji.
 
Mchambuzi,

Umeitendea haki sana hii hoja na Dr Slaa kwa kuifanyia uchambuzi sawia. Kwa bahati mbaya wengi waliiangalia kwa jicho la siasa nyepesi nyepesi kama ambavyo tumeshudia.

Hoja ya Dr Slaa kuhusu gongo inaweza kuangaliwa katika sehemu kuu tatu: Afya ya mnywaji, uchumi, na ubunifu wa kibiashara.

1. Afya ya mnywaji (pamoja na uhai wake)

Mapambano dhidi ya gongo yamekuwepo kwa miaka yote tangu tupate uhuru. Na mara nyingi hutumika maneno 'pombe haramu'. Kwa kuangalia hayo maneno mawali tu unaona kuwa, kwanza kuna 'pombe' ikimaania gongo inakuwa kwenye jamii ya pombe (kilevi) lakini inakuwa qualified kwa kuongeza neno 'haramu. Kwa maana hiyo pombe inakuwa ama 'nzuri' au 'haramu'.

Sasa ni kitu gani kinachoifanya pombe kuwa kwenye mojawapo ya hilo kundi, ni mchakato mzima pamoja na ingridients zinatumika. Na pombe inakuwa 'nzuri' kwa sababu imepitia kwenye mchakato ambao umehakikiwa - kisheria na kiutaalam - na kuridhika kuwa product haina madhara kwa mtumiaji. Ndio maana leo (kwa mfano) wanywaji wa bia ya safari au Heineken wakilalamika kuwa wanapatwa na matatizo ya kiafya kila wananywapo pia hizo, kwa hakika mamlaka husika zitachukuwa hatua stahiki kugundua ni wapi wamekosea - kwa kukagua mchakato wote wa uaandaji vinywaji hivyo.

Tukiangalia Gongo -pombe haramu- mamlaka zinazohusika na vinywaji wanajua vyema gongo inatengezwa na nini na katika mazingira gani? Lakini pia, wanajua ni kitu gani kinaweza kufanyika ili kuindoa gongo toka kwenye kundi haramu na kuwa kwenye 'zuri'. Kwa sababu ambazo hazijawahi kuwekwa wazi, hakuna juhudi zozote zilizochukuliwa ili kuboresha uandaaji wa gongo. Badala yake serikali imechukuwa njia za mkato -kukataza gongo all together.

Lakini je, ni kweli watu wameacha kutengeneza na kunywa gongo kwa sababu serikali imekataza? Na je, ni kweli gongo haiwezi kusafishwa na kuwa kama spirit nyingine? Kwanini hili halijanyika? Na kama serikali ya chama X inaona haiwezi kufanya, wengine wanye nia na uelewa wa namna ya kurekebisha waendelee kukaa kimya huku maelfu ya watanzania wanaendelea kunywa mafichoni na kuhatarisha afya zao? Kwa kiingereza tunaweza kusema, just because you cannot do it, does not mean it cannnot be done.

Sababu za kuitoa gongo toka mafichoni na kuiweka kwenye mchakato unaleweka kisheria zipo. Na uwezo wa kufanya hivyo upo, tena ndani ya taasisi za Kitanzania. Shinda ni nini? Kwanini serikali haitaki kuweka utaratibu utaowezesha utengezaji gongo bora ili afya za watanzania ziimirike?

Dr Slaa alitaja baadhi ya taasisi ambazo zinaweza kusaidia kwenye hili zoezi, lakini watu wamebakia na fikra mgando kuwa gongo ni haramu! Haramu ni fikra mgando zinazoshindwa kuona uhumimu kwa kuweka mchakato wa kuboresha gongo. Haramu ni tabia ya kutokuwa na maono. Haramu ni mtindo wa kuingiza siasa nyepesi kwa mambo ya msingi.

2. Uchumi
Kwa record za bunge, Makampuni yanayoongoza kwa kulipa kodi ni ya pombe. Chibuku wanalipa kodi kushinda makampuni ya madini, na hata ya simu (Hotuba ya waziri mkuu bungeni). Ndio maana mwaka hadi mwaka Hazina imekuwa inahemea kwenye kodi itakanayo na mauzo ya pombe. TBL wao ndio kabisa, na sasa wamekuwa kimbilio la wanasiasa kwenye miradi ya majimbo yao mfano gharama za miradi ya maji.

Sasa kama sekta ya pombe ndio tegemeo la bajeti ya serikali, kwanini hawajaona umuhimu wa kuboresha gongo ili nayo ichangie kwenye pato la taifa?

3. Ubinifu wa kibiashara
Kwenye hili ningeomba niunganishe na ubunifu wa viongozi wetu. Viongozi wengi si wabunifu kabisa. Tuna tatizo kubwa sana la ajira, na sasa imefikia hatua tunaita vijana ‘bomu linalosubiri kupasuka’. Watanzania wamejifunza namna ya kutengeza pombe, badala ya viongozi kuangalia ni nini cha kufanya ili hii pombe iingie kwenye kundi safi, wao wanazuia!

Ingeeleweka kama serikali wangejaribu kuboresha gongo na ikaonekana kuwa kweli haiwezekani (kiutalaam) basi wangekuwa na haki ya kusema kinywaji hiki hakifai. Lakini hawajafanya chochote zaidi ya kukamata watu.

Na hii si kwenye gongo tu, kuna mambo mengi sana watanzania wanafanya kwa jitahada zao binafsi, lakini hakuna mfumo unaoeleweka ili kuinuia vipaji vyao. Na anapojitokeza mtu na kuongelea nini cha kufanya kama alivofanya Dr Slaa, watu wanaibuka na hoja za kipuuzi. Kwa nini tunakuwa kama jamii semi-illiterate?
 
Mchambuzi Jibu swali lifuatalo:
JE MITAMBO HIYO YA SIDO IKITENGENEZWA, IKATOKEA BAADHI WAKAITUMIA KUTENGENEZEA GONGO "HALALI", JE WALE AMBAO WATAENDELEA KUTENGENEZA GONGO "ILE ILE" YA ZAMANI KWA KIFICHO SHERIA ISEMEJE KUHUSU GONGO HIYO?

NI MATUMAINI YANGU UTANIJIBU!
 
Mchambuzi,

Umeitendea haki sana hii hoja na Dr Slaa kwa kuifanyia uchambuzi sawia. Kwa bahati mbaya wengi waliiangalia kwa jicho la siasa nyepesi nyepesi kama ambavyo tumeshudia.

Hoja ya Dr Slaa kuhusu gongo inaweza kuangaliwa katika sehemu kuu tatu: Afya ya mnywaji, uchumi, na ubunifu wa kibiashara.

1. Afya ya mnywaji (pamoja na uhai wake)

Mapambano dhidi ya gongo yamekuwepo kwa miaka yote tangu tupate uhuru. Na mara nyingi hutumika maneno 'pombe haramu'. Kwa kuangalia hayo maneno mawali tu unaona kuwa, kwanza kuna 'pombe' ikimaania gongo inakuwa kwenye jamii ya pombe (kilevi) lakini inakuwa qualified kwa kuongeza neno 'haramu. Kwa maana hiyo pombe inakuwa ama 'nzuri' au 'haramu'.

Sasa ni kitu gani kinachoifanya pombe kuwa kwenye mojawapo ya hilo kundi, ni mchakato mzima pamoja na ingridients zinatumika. Na pombe inakuwa 'nzuri' kwa sababu imepitia kwenye mchakato ambao umehakikiwa - kisheria na kiutaalam - na kuridhika kuwa product haina madhara kwa mtumiaji. Ndio maana leo (kwa mfano) wanywaji wa bia ya safari au Heineken wakilalamika kuwa wanapatwa na matatizo ya kiafya kila wananywapo pia hizo, kwa hakika mamlaka husika zitachukuwa hatua stahiki kugundua ni wapi wamekosea - kwa kukagua mchakato wote wa uaandaji vinywaji hivyo.

Tukiangalia Gongo -pombe haramu- mamlaka zinazohusika na vinywaji wanajua vyema gongo inatengezwa na nini na katika mazingira gani? Lakini pia, wanajua ni kitu gani kinaweza kufanyika ili kuindoa gongo toka kwenye kundi haramu na kuwa kwenye 'zuri'. Kwa sababu ambazo hazijawahi kuwekwa wazi, hakuna juhudi zozote zilizochukuliwa ili kuboresha uandaaji wa gongo. Badala yake serikali imechukuwa njia za mkato -kukataza gongo all together.

Lakini je, ni kweli watu wameacha kutengeneza na kunywa gongo kwa sababu serikali imekataza? Na je, ni kweli gongo haiwezi kusafishwa na kuwa kama spirit nyingine? Kwanini hili halijanyika? Na kama serikali ya chama X inaona haiwezi kufanya, wengine wanye nia na uelewa wa namna ya kurekebisha waendelee kukaa kimya huku maelfu ya watanzania wanaendelea kunywa mafichoni na kuhatarisha afya zao? Kwa kiingereza tunaweza kusema, just because you cannot do it, does not mean it cannnot be done.

Sababu za kuitoa gongo toka mafichoni na kuiweka kwenye mchakato unaleweka kisheria zipo. Na uwezo wa kufanya hivyo upo, tena ndani ya taasisi za Kitanzania. Shinda ni nini? Kwanini serikali haitaki kuweka utaratibu utaowezesha utengezaji gongo bora ili afya za watanzania ziimirike?

Dr Slaa alitaja baadhi ya taasisi ambazo zinaweza kusaidia kwenye hili zoezi, lakini watu wamebakia na fikra mgando kuwa gongo ni haramu! Haramu ni fikra mgando zinazoshindwa kuona uhumimu kwa kuweka mchakato wa kuboresha gongo. Haramu ni tabia ya kutokuwa na maono. Haramu ni mtindo wa kuingiza siasa nyepesi kwa mambo ya msingi.

2. Uchumi
Kwa record za bunge, Makampuni yanayoongoza kwa kulipa kodi ni ya pombe. Chibuku wanalipa kodi kushinda makampuni ya madini, na hata ya simu (Hotuba ya waziri mkuu bungeni). Ndio maana mwaka hadi mwaka Hazina imekuwa inahemea kwenye kodi itakanayo na mauzo ya pombe. TBL wao ndio kabisa, na sasa wamekuwa kimbilio la wanasiasa kwenye miradi ya majimbo yao mfano gharama za miradi ya maji.

Sasa kama sekta ya pombe ndio tegemeo la bajeti ya serikali, kwanini hawajaona umuhimu wa kuboresha gongo ili nayo ichangie kwenye pato la taifa?

3. Ubinifu wa kibiashara
Kwenye hili ningeomba niunganishe na ubunifu wa viongozi wetu. Viongozi wengi si wabunifu kabisa. Tuna tatizo kubwa sana la ajira, na sasa imefikia hatua tunaita vijana ‘bomu linalosubiri kupasuka'. Watanzania wamejifunza namna ya kutengeza pombe, badala ya viongozi kuangalia ni nini cha kufanya ili hii pombe iingie kwenye kundi safi, wao wanazuia!

Ingeeleweka kama serikali wangejaribu kuboresha gongo na ikaonekana kuwa kweli haiwezekani (kiutalaam) basi wangekuwa na haki ya kusema kinywaji hiki hakifai. Lakini hawajafanya chochote zaidi ya kukamata watu.

Na hii si kwenye gongo tu, kuna mambo mengi sana watanzania wanafanya kwa jitahada zao binafsi, lakini hakuna mfumo unaoeleweka ili kuinuia vipaji vyao. Na anapojitokeza mtu na kuongelea nini cha kufanya kama alivofanya Dr Slaa, watu wanaibuka na hoja za kipuuzi. Kwa nini tunakuwa kama jamii semi-illiterate?

Naona mko busy kulishana matango!
 
Huwezi fananisha mtu aliyekunywa Konyagi nusu lita na aliyekunywa GONGO nusu lita!

Ni kweli kabisa na ndiyo maana Dr. Slaa kwa kuliona hilo aksisitizia viwanda vyetu kama vile SIDO vitatengeneza mitambo midogomidogo kwa ajili ya kusindika na refine (standardize) hicho kinywaji kiwe safi na bora kwa matumizi ya binadamu ili viwango vyake vithibitishwe na TBS kama vilivyo vileo vingine.
 
Nawahakikishia baada ya mwaka,hili litabebwa na viongozi wa CCM

mmesahau Kinana alivyoingia na kushusha bei ya vifaa vya ujenzi na lile la Korosho,Lowasa alivyoshadadia elimu bure kufikia kidato cha 6.yote wamechukua Ilani ya CHADEMA 2010-2015
 
Dah watu mnapoteza wakati wote huo kutetea pombe ya gongo ambayo ni haramu kisheria na hata kwa mujibu wa vitabu vya Mungu? Haya ni majanga.
 
Umeandika maneno meeeeeeeengi lakini kumbe hata hujui Dr. Slaa alisema nini!

Anza kwanza kusoma alichosema Dr. Slaa halafu kafanye correction ya kile ulichoandika.

Slaa alisema anahalalisha gongo ili wauza gongo wasikamatwe na polisi ambao huchukua rushwa kwa wauza gongo.

Gongo iwapo itaboreshwa, gharama yake lazima itaongezeka na wanywaji watashindwa kuinunua pombe ya gharama kubwa. Pombe bora zipo lakini hawazinunui kwa sababu ya gharama wanaopt kunywa gongo.

This is to say that wazalishaji wa pombe ya gongo isiyokidhi viwango lazima wataendelea kuwepo. Swali ulilopaswa kujiuliza ni je, polisi wasiwakamate hawa ambao wataendelea kuuza hii pombe isiyokidhi viwango?

Pili, fikiria kwa mapana zaidi. Gongo inasababisha magonjwa ya ini yaani cirhosis pamoja na liver cancer. Economic barden ya kumhudumia mgonjwa mmoja wa kansa ya ini haipungui shilingi milioni tano. Ukijumlisha na indirect barden ya watu wanaomuuguza kushindwa kwenda kazini, watoto wake kushindwa kuconcentrate na masomo kwa sababu baba au mama mgonjwa etc utagundua kuwa mtu anayeshabikia kuruhusu biashara ya gongo ishamiri either ana upeo mdogo au hana nia njema na nchi yetu.

Taarifa nilizopata ni kwamba Slaa alipigwa "kipapai". Lengo lake lilikuwa kuongea kuhusu katiba mpya lakini akajikuta anaongea kuhusu gongo.

Kwa kuongezea hapo kwenye red Mchambuzi anatakiwa kukumbuka kuwa Dr slaa alikuwa ana lengo la kuwa saidia hata wazalishaji wanao tegemea hiyo pombe kama chanzo cha kipato na wengi wana maisha duni na kipato kidogo sana, sasa Dr.W.Slaa alisema atawaagiza sido watengeneze mitambo na kuwauzia watengenezaji wa gongo, lakini slaa kashindwa kufikiri kuwa hawa watu wana kipato kidogo na hawatoweza kuinunua hiyo mitambo labda waiuze tsh500. na hao anao watetea lazima wataikataa hiyo mitambo.

Mchambuzi, Dr.W.Slaa Rose Mayemba WANAONGEA LUGHA TOFAUTI.
 
Last edited by a moderator:
Moja ya Malighafi ya Gongo ni Mavi, kwa hiyo DKT WA UKWELI anaahidi kusafisha mavi yawe bora?
 
Ni kweli kabisa na ndiyo maana Dr. Slaa kwa kuliona hilo aksisitizia viwanda vyetu kama vile SIDO vitatengeneza mitambo midogomidogo kwa ajili ya kusindika na refine (standardize) hicho kinywaji kiwe safi na bora kwa matumizi ya binadamu ili viwango vyake vithibitishwe na TBS kama vilivyo vileo vingine.

Ukishafanya hivyo bei yake itakuwa sh. ngapi? Yule mnywaji bado ataweza kuimudu bei hiyo?

Kwani sasa hivi nini kinawazuia SIDO kutengeneza hiyo mitambo?

By the way, unajua SIDO ni nini?
 
Kwa kuongezea hapo kwenye red Mchambuzi anatakiwa kukumbuka kuwa Dr slaa alikuwa ana lengo la kuwa saidia hata wazalishaji wanao tegemea hiyo pombe kama chanzo cha kipato na wengi wana maisha duni na kipato kidogo sana, sasa Dr.W.Slaa alisema atawaagiza sido watengeneze mitambo na kuwauzia watengenezaji wa gongo, lakini slaa kashindwa kufikiri kuwa hawa watu wana kipato kidogo na hawatoweza kuinunua hiyo mitambo labda waiuze tsh500. na hao anao watetea lazima wataikataa hiyo mitambo.

Mchambuzi, Dr.W.Slaa Rose Mayemba WANAONGEA LUGHA TOFAUTI.

Slaa labda hajui maana ya SIDO.

Hakuna kiwanda kinachoitwa SIDO. SIDO ni mkusanyiko wa wajasiriamali wanaoendesha viwanda.

Je, sasa hivi SIDO kitu gani kinawakataza kutengeneza hiyo mitambo?
 
Nashauri babu angeanza kutetea mirungi ambayo haina madhara yuyote iruhusiwe kabla yakuihalisha gongo ambayo niharamu
 
Mchambuzi.
nimejinyima kusoma hii hekaya umejitahidi kufanya siasa na kupulizia kinyesi pafyumu (manukato) ili ionekane ni kitu cha thamani sana. Pole sana. Tatizo lako ni mahaba ya kupindukia kwa Dr Slaa. Siku zingine uwe objective kwenye mambo ya msingi huenda ukaja na analysis iliyoenda shule. Kwa leo umejitahidi kubwabwaja hizi non sensical stories.

Cc.
mods - unganisheni hii thred na ile original ili wasomaji na wafuatiliaji wapate mtiririko mzuri.
 
Nashauri babu angeanza kutetea mirungi ambayo haina madhara yuyote iruhusiwe kabla yakuihalisha gongo ambayo niharamu
Pamoja na ujinga ule uliosemwa na wanasiasa yet kuna wafuasi wanajitahidi kuutetea. Madhara ya mahaba
 
  • Thanks
Reactions: Voi
Slaa labda hajui maana ya SIDO.

Hakuna kiwanda kinachoitwa SIDO. SIDO ni mkusanyiko wa wajasiriamali wanaoendesha viwanda.

Je, sasa hivi SIDO kitu gani kinawakataza kutengeneza hiyo mitambo?

Mkuu, huku ni kuzeeka vibaya kwa mzee wetu. Kuna uhusiano gani kati ya SIDO ( shirika la viwanda vidogo vidogo), na kinywaji haramu cha gongo? Wanao control viwango vya ubora wa chakula na vinywaji ni TFDA - mamlaka ya chakula na dawa. ( wale wanaochoma bidhaa mbalimbali feki za vyakula ). Mchambuzi angetuma muda kidogo kuji challenge chumbani kabla hajaja jukwaani he could be so clever.
cc
marcopolo
mchambuzi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom